Monday, May 16, 2016

VIONGOZI 14 WA SERIKALI WILAYANI BUNDA MKOANI WASHIKILIWA NA POLISI KWA KOSA LA UBASHILIFU WA FEDHA

Viongozi 14 wa serikali za vijiji katika halmashauri ya Bunda mkoani Mara wamekatwa na jeshi la polisi kwa amri ya mkuu wa mkoa wa Mara baada ya kutuhumiwa kuiba mamilioni ya fedha za michango ya wananchi zikiwemo fedha ambazo zilitolewa na serikali kuu kwa ajili     utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika vijiji vyao.

  Mkuu wa mkoa wa Mara Bw Magesa Mulongo, amechukua hatua hiyo kwa nyakati tofauti baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wakati wa ziara yake ya kujitambulisha katika halmashauri hiyo hivyo kubaini ubadhirifu huo mkubwa fedha za serikali na zile za   michango ya wananchi.

   Awali wananchi hao wamemueleza mkuu wa mkoa wa Mara kuwa viongozi hao wa vijiji wamekuwa wakichangisha fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo badala yake wamekuwa wakizitumia kujengea nyumba zao binafsi na kulewa pombe huku baadhi ya viongozi hao

    wakijitetea kuwa fedha hizo walizikopa na kuzitumia kwa shughuli zao za kisiasa. Katika ziara hiyo pia mkuu huyo wa mkoa amemvua uenyekiti wa serikali ya kijiji cha Igundu mtu mmoja kwa tuhuma za kushiriki katika ubadhirifu huo wakiwemo waratibu wawili wa elimu kata pia kuvuliwa nyadhifa zao kwa madai ya kushindwa kutekeleza vema majukumu yao.

No comments:

Post a Comment