Tuesday, July 25, 2017

JPM' AMTOLEA UVIVU LISSU





Rais John Magufuli amesema kuwa Serikali imetatua Changamoto mbalimbali pamoja na Madawati  kwenye Jimbo la Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu. 

"Tumetatua changamoto ya madawati...sasa hivi hata watoto wa TunduLissu wanakaa" 

Magufuli amesema kuwa kuna "Wengine mmewachagua lakini wanaongelea ya Dar es Salaam tu...Kosea kuoa unaweza kutoa talaka, lakini usikosee kuchagua"

Sunday, July 23, 2017

MISINGI BORA YA KUFUATA ILI KUJENGA AFYA YA MWILI WAKO



Katika maisha moja ya kitu cha msingi sana ambacho hutakiwi kukikosa ni afya bora. Kosa yote, lakini usikose afya bora, afya bora ina muunganiko na mambo mengi sana kwenye maisha yako ikiwa pamoja na mafanikio. 

Naomba uelewe hivi, unapokuwa hauna afya nzuri, hakuna ambacho unaweza ukakifanikisha, utashindwa kwenye mambo mengi kwa sababu ya kushindwa kuweza kuyafanya kwa ufanisi kutokana na tatizo la afya yako. 

Kwa mantiki hiyo,  mpaka hapo unaona ni kwa namna gani afya ilivyokuwa ya muhimu sana kwenye maisha yako. Sio suala la kuhoji tena ni lazima uwe na afya bora. Ni kwa namna gani utaweza kutengeneza afya bora? 

Ifuatayo Ni Misingi Bora Ya Kufuata Ili Kujenga Afya Ya Mwili Wako. 

Msingi wa kwanza,  kunywa maji kwa wingi. 
Maji mengi mwili yanasaidia mwili wako kuwa katika hali nzuri wakati wote na kusababisha baadhi ya viungo kufanya kazi kwa ufasaha. Hivyo, unalazimika kunywa maji kwa wingi kila wakati ili kuweza kulinda afya ya mwili wako ili iwe bora wakati wote, kinyume cha hapo itakuwa ni shida kwako. 

Msingi wa pili, soma kabla hujalala. 
Unaposoma kitu kipya kabala hujalala unaifanya akili yake iende kupumzika huku ikiwa na wazo jipya au kitu cha kufanyia kazi usiku wote. Ukumbuke hapa mawazo yako ya kina yanafanya kazi muda wote kwa saa 24 . Soma kitu kipya chanya angalau nusu saa kabla hujalala kila siku itakusaidia sana. 

Msingi wa tatu, fanya tahajudi (Meditation). 
Tafuta eneo lilotulia na kila siku jitahidi kufanya tahajudi ama ‘meditation.’ Hiki ni kipindi ambacho unatakiwa ukae kwa utulivu ukitafakari maisha yako na kutafakari kile unachokitaka katika maisha. Unaweza ukafanya tahajudi/meditation angalau hata kwa dakika 15 kila siku.

Msingi wanne,  fanya mazoezi. 
Unatakiwa pia ujenge tabia ya kufanya mazoezi kila siku ili kuupa mwili wako afya. Fanya mazoezi ya kukimbia, fanya mazoezi ya kuruka au fanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito. Ukifanya mazoezi kila siku na ikawa ndio kitu endelevu mwili wako utakaa katika afya nzuri sana kila wakati. 

Msingi wa tano, kula chakula bora. 
Mwili wako haujengwi kwa matofali, mwili wako unajengwa kwa chakula safi. Kwa kulijua hili kila wakati jitahidi sana kuulisha mwili wako chakula ambacho kitakusaidia wewe kuweza kuujenga mwili wako kwa  afya bora. Tafuta vyakula safi vitakavyo ulinda mwili wako na magonjwa. 

Kimsingi, afya yako haijengwi kwa kubahatisha. Afya inajengwa kwa kuzingatia msingi ya afya bora kama ilivyoainishwa katika makala haya ya leo. Usisubiri hadi uende kwa daktari, zingatia mambo haya nawe utakuwa na afya bora.

KISA CHA JUSTIN BIEBER KUPIGWA MARUFUKU CHINA


Nyota wa muziki wa Pop kutoka Canada Justin Bieber amepigwa marufuku kutumbuiza nchini China, kwa mujibu wa Wizara ya Utamaduni nchini humo.

Taarifa ya wizara hiyo imesema haifai kwa watumbuizaji ambao wamejihusisha katika "utovu wa nidhamu" kuruhusiwa kuingia nchini humo.

"Justin Bieber ni mwimbaji mwenye kipaji, lakini pia ni mwanamuziki kijana mwenye kuzua utata," amesema.

Taarifa hiyo imetolewa kujibu swali lililokuwa limeulizwa na mmoja wa watu katika tovuti ya wizara hiyo.

"Twatumai kwamba Justin Bieber atakapokomaa, anaweza kuendelea kuimarisha maneno yake na matendo, na kuwa mwanamuziki anayependwa kwa dhati na umma," taarifa hiyo imesema

Bieber aliwahi kuzuru China mwaka 2013, lakini sasa amejiunga na orodha ndefu ya wanamuziki waliopigwa marufuku nchini humo.

Wengine ni bendi ya Uingereza kwa jina Oasis na kundi la Marekani kwa jina Maroon 5, ambao wamepigwa marufuku kwa sababu ya misimamo yao ya kisiasa badala ya tabia.

Mwaka 2014, Bieber, maarufu kwa wimbo wake Sorry alizua utata baada ya kupakia picha aliyopigwa akitembelea madhabahu ya Yasukuni jijini Tokyo.

Madhabahu hayo nchini Japan yalijengwa kwa heshima ya wanajeshi waliouawa vitani pamoja na wahalifu wa kivita lakini nchini China na Korea Kusini, hutazamwa kama ishara kwamba Japan haijajutia makosa yaliyotendwa na watawala wa nchi hiyo China na Japan miaka ya nyuma.