Friday, March 31, 2017

BAADA YA RAIS ZUMA KUMTIMUA WAZIRI WA FEDHA, RAND YA AFRIKA KUSINI YASHUKA KWA KASI

Baada ya Rais Zuma kumtimua waziri wa fedha, rand ya Afrika Kusini yashuka kwa kasi

Fedha ya Afrika Kusini, rand, inaendelea kushuka thamani kwa kasi baada ya Rais Jacob Zuma kumtimua waziri wa fedha mwenye uzoefu mkubwa, Pravin Gordhan.

Zuma alitangaza uamuzi huo Alhamis hii kuwa anamuondoa Gordhan pamoja na mawaziri wengine. Wawekezaji walikuwa wameshaanza kuhofia kuwa Zuma angemtimua waziri huyo baada ya Jumatatu kumuamuru asitishe mikutano mingi na wawekezaji wa nje na kurudi nyumbani.

Hatua hiyo pia ilikuwa dhoruba kwa rand ambayo sasa imeshuka thamani yake kwa asilimia 8. Wachambuzi walionya mapema wiki hii kuwa kumuondoa Gordhan na mawaziri wengine kungekuwa na madhara.

Amekuwa waziri wa fedha kwa kipindi kirefu kuanzia mwaka 2009 hadi 2014 na kurudi tena December 2015. Zuma amteua Malusi Gigaba aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani kushika nafasi hiyo.

DO SLAA: MVUMILIENI MAGUFULI

Dk Slaa: Mvumilieni Magufuli

BAADA ya kuishi nchini Canada kwa zaidi miaka miwili sasa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa amesema anakuna kichwa ili kupima mazingira yaliyomfanya aondoke nchini na familia yake kama yapo au laa.

Septemba,2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu Dk. Slaa alijiweka kando na siasa, kwa kile alichokieleza kutofautiana na chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),Edward Lowassa.

Hata hivyo Dk. Slaa ambaye amekuwa mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, hakuweza kuainisha mazingira yaliyomfanya aondokea nchini na kwenda kuishi ughaibuni.

“Sina tabia ya kuyumbishwa…sina chuki na mtu yeyote, sipendi siasa za udanganyifu na propaganda. Nimeachana na siasa tangu Julai 28,2015, baada ya kuona misingi ya chama nilichoshiriki kukijenga imepotoshwa,”alisema Dk. Slaa siku alipotangaza kuachana na siasa.

Pamoja na mambo mengine, alisema sharti la kwanza ambalo alitaka Chadema izingatie ni kiongozi huyo wa zamani ndani ya serikali ya CCM, kujisafisha dhidi ya tuhuma ya kashfa ya sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa Waziri Mkuu.

Kurudi nchini

Akizungumza na MTANZANIA akiwa nchini Canada jana, Dk. Slaa alisema amemaliza masomo yake na baada ya kufanya tafakari atarejea nchini wakati wowote.

“Ni kweli nimemaliza masomo yangu. Bado napima mazingira yaliyonifanya niondoke na familia yangu. Baada ya hapo tutaangalia uwezekano wa kurejea,”alisema.

Alisema kuhusu matarajio yake ya kisiasa, watu wameshindwa kumwelewa siku ambayo alitangaza kustaafu siasa za vyama.

Alisema alichomaanisha ni kwamba, pamoja na kuachana na siasa za vyama,atakuwa tayari kupiga kelele pale anapoona masilahi ya Taifa yanaumia.

“Hadi sasa sijapiga kelele kwa kuwa sijaona masilahi ya Taifa yakiangamizwa, hatua mbalimbali zinazochukuliwa ni kweli zinawaumiza wasiohusika.

“Ndio maana nilitumia katika makala mojawapo mtego wa panya huwakamata wanaohusika na wasiohusika. Hivyo, makosa madogo mimi hayanisumbui kwa kuwa hakuna binadamu kamilifu ,”alisema.

Rais Magufuli

Akizungumzia utendaji wa Rais Dk. John Magufuli, alisema watu waelewe hakuna nchi hata moja ambapo kiongozi atakubalika na watu wote kwa asilimia 100.

Alisema wako watu ambao masilahi yao yataguswa kwa namna moja au nyingine hivyo lazima watapiga kelele.

Kutokana hilo, alisema Rais Dk. Magufuli katika kundi ambalo halihitaji fedha ameyatekeleza yote kwa asilimia 99.9, ikiwa ni pamoja na uwajibikaji serikalini, kuchukua hatua kali dhidi ya rushwa, uwizi wa mali za umma, uwindaji haramu na kudhibiti dawa za kulevya.

“Hatua zote zimechukuliwa,zinapaswa kuwa endelevu. Kwa bahati mbaya mchwa wengine waliopenya mpaka ndani ya Ikulu na Serikali na huwezi kufagia Serikali nzima kwa siku mmoja.

“Kwa jinsi Rais ambavyo hayumbi na wala hayumbishwi, nina hakika atafikia malengo na kurudisha Taifa kwenye misingi ya tunu za Taifa ya uwazi, ukweli, uadilifu, kuheshimiana na kuthaminiana na hasa kujali utu.

“Hii ndiyo hali ambayo JPM kila siku anaiita ‘Transition’ (kipindi cha mpito). Tutafika tu, tunatakiwa kuwa wavumilivu na wenye uzalendo wa kweli ana nia njema ya kufikisha Taifa mahali pazuri. Hii inahitaji kuweka pembeni maslahi yetu binafsi kama mtu mmoja mmoja, viongozi wa Serikali au hata wa kisiasa,”alisema Dk. Slaa.

Upinzani

Kuhusu mwenendo huo endapo utasaidia upinzani kuingia Ikulu 2020, Dk. Slaa alisema wakija na ajenda mbadala na makini yenye kuwalenga wananchi moja kwa moja itawasaidia.

Dk. Slaa ambaye pia alipata kugombea urais kupitia Chadema mwaka 2010, alisema endapo wataendelea kurukia kauli za Rais, basi upinzani utafutika kabla ya 2020. 

“Kama nilivyorejea mara kadhaa, upinzani makini utaingia Ikulu kwa ajenda mbadala. Ajenda makini yenye kuwalenga wananchi moja kwa moja katika kuwatoa kwenye kero zao mbalimbali.

“Hadi sasa ninachoona ni ‘kurukia’ kauli za JPM, lakini kauli si ajenda na hatupeani maksi kwa kuzungumzia usahihi wa lugha. Wako wanaotazama usahihi wa lugha na mahali pa kutazama usahihi huo. Kimsingi hayo ni masuala ya darasani au kwenye uandishi wa vitabu.

“Aidha kumtuhumu JPM kukiuka Katiba na sheria nayo haina tija. Wote wanaomtuhumu wanajua kuwa wakiambiwa waonyeshe kifungu mahususi alichokiuka yeye mwenyewe katika utendaji wake hawana majibu ya kuridhisha.

“Hivyo mimi sijaona mwenendo wa JPM unaosaidia kuingiza upinzani Ikulu. Isitoshe kama hawatakuja na ajenda makini na mkakati ulioandaliwa unaowatoa wananchi hapa walipo kwenda kwenye raha, upinzani unaweza kufutika kabla ya 2020,”alisema Dk. Slaa.

Thursday, March 30, 2017

MWAROBAINI KAZI YAKE KWENYE NGOZI

   Dk. Fadhili Emilly
Leo hii kupitia ukurasa wetu huu nimeona tufahamishane kuhusu faida za mti wa mwarobaini hasa katika suala zima la magonjwa ya ngozi yanayosumbua sana wanadamu.

  
   Mwarobaini (Azadirachta indica) ni mti unaofahamika kwa uwezo wake wa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali. Inaaminika kuwa mti huu asili yake ni nchini India na Burma. Mwarobaini hushamiri zaidi katika nchi za tropiki na una uwezo mkubwa wa kuhimili ukame.

 
   Hapa nchini Tanzania, mti wa mwarobaini huweza kupatikana kwa urahisi kabisa katika maeneo mengi ya mijini na vijijini pia.
Jina hili la ‘mwarobaini’ linatokana na imani kuwa mti huu una uwezo wa kutibu magonjwa yapatayo arobaini, huku majani yake na mbegu zikitumiwa kama tiba kwa miaka mingi katika nchi mbalimbali duniani.

 
     Kati ya magonjwa ambayo mti huu umetumika kutibu au kupoza ni pamoja na matatizo ya kusaga chakula tumboni, kisukari, saratani, magonjwa ya ngozi, malaria, ukungu (fungus), n.k.
 
    
      Pia matawi ya mti huu hutumiwa kama mswaki na magome yake hutumiwa kama dawa ya kusafisha meno.
Hali kadhalika mafuta ya mbegu ya mwarobaini hutumika kutengenezea vipodozi na sabuni, lakini pia mbegu au mafuta yake hutumiwa kama dawa ya kuulia wadudu wanaoharibu mimea shambani.

    Baada ya kufahamu baadhi ya faida mbalimbali za mti wa mwarobaini, leo nitakufundisha namna ya kutumia mti wa mwarobaini kujitibu magonjwa ya ngozi.

   
Mahitaji
Majani ya mti wa mwarobaini.
Sufuria
Mwiko
Jiko la gesi, mkaa au jiko la mafuta.
Hatua za kufuata
1. Chukua majani mabichi ya mti wa mwarobaini na uyaweke kwenye sufuria.

2. Chukua sufuria yako yenye majani ya mti wa mwarobaini na uiinjike kwenye jiko lenye moto wa wastani.

3. Chukua mwiko wako na uanze kuyakoroga majani yako taratibu hadi yakauke bila kuungua.

4. Majani yako yakishakauka, ipua sufuria yako, chukua majani yako yaliyokauka, yasage kisha hifadhi unga unga wako kwenye chombo cha plastiki.

Matumizi
Tumia vijiko viwili vya chai kwenye kikombe cha robo lita chenye maji ya moto, fanya hivyo mara mbili kwa siku kwa muda wa siku ishirini na moja.

RIPOTI: TANZANIA IMETAJWA KUONGOZA AFRIKA KWENYE HILI

Ripoti: Tanzania imetajwa kuongoza Afrika kwenye hili...


Tanzania imechangia asilimia 19.3 ya jumla ya wageni wa kimataifa kupitia anga (international air arrivals) ukilinganisha na asilimia 18.2 ya Kenya, asilimia 17.2 Misri na asilimia 12.1 ya Afrika Kusini katika kipindi cha kuanzia September 2016 hadi January 2017.


Takwimu hizi ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la ufuatiliaji wa masuala usafiri wa ndege, ForwardKeys ambayo hulinganisha ukataji tiketi za ndege zaidi ya milioni 16 kila siku ili kuiweka Afrika kwenye ramani ya utalii duniani.

Kwa jumla, Afrika Mashariki ina asimilia 16.4 ya ufikaji wa wageni kwa njia ya anga. Na kwa ujumla pia, kuna ongezeko la asilimia 10.3 ya ufikaji wageni Afrika. Soma zaidi ripoti hiyo hapa.

Sunday, March 26, 2017

KUPUNGUZA KIWANGO CHA CHUMVI HUZUIA KWENDA CHOONI USIKU

Watu ambao huamka usiku kwa minajili ya kuenda chooni, wanahitaji kupunguza kiwango cha chumvi katika chakula chao, kwa mujibu wa madaktari nchini Japan.

Tatizo hilo linalofahamika kama nocturia, ambapo mara nyingi huwaathiri watu walio na zaidi ya miaka 60, husababisho matatizo ya kupata usingizi na linaweza kuathiri maisha ya mtu.

Uchunguzi huo uliofanyiwa zaidi ya watu 300 wa kujitolea, uligundua kuwa kupunguza kiwango cha chumvi kwenye chakula, humwezesha mtu kupunguza safari za kuenda haja ndogo.

Watafiti kutoka chuo cha Nagasaki , waliwasilisha matokeo yao kwenye warsha moja ya sayansi mjini London.

Walichunguza wagonjwa waliokuwa wakitumia kiwango kikubwa cha chumvi pamoja na matatizo ya kulala kwa miezi mitatu baada ya kuwapa ushauri wa kupunguza kiwangi hicho kwenyeychakula chao.

Safari za kuenda chooni zilipungua kwa zaidi ya mara mbili kila siku hadi safari moja.
Hiyo pia ilishuhudiwa mchana na maisha ya watu hao pia yakaimarika.

Hitaji la kuamka usiku kwa haja ndogo huwaathiri zaidi ya nusu ya wanaume na wanawake walio na zaidi ya miaka 50.

Hali hiyo ni kawaida kwa watu wazee ambao wengi wao huamka takrban mara mbili kwa usiku.
Mtu anapofanya safari nyindgi chooni usiku, hupata matatizo ya kulala, hali ambayo husababisha pia msongo na uchovu.

MBIO ZAMFANYA HARMORAPA KUPATA DILI NONO KWENYE KINYWAJI CHA SWALA

Mbio zamfanya Harmorapa kupata dili nono kwenye kinywaji cha Swala


MSANII wa Bongo Fleva anayetrendi katika mitandao ya kijamii Bongo, ‘Hamorapa’ anatazamiwa kuwa balozi wa Kinywaji kiitwacho Swala.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, Hamorapa amefunguka kuwa yupo katika mazungumzo na kampuni inayozalisha kinywaji hicho na anatarajia kupata dili nono ya kukitangaza kinywaji hicho.

JWTZ YAILIPIA TANESCO BILLIONI 1 KATI YA BILLIONI 3 AMBAZO WANADAIWA NA SHIRIKA HILO LA UMEME

JWTZ yadaiwa na Tanesco Sh3bilioni

Dar es Salaam. Mkuu wa Majeshi nchini, Evance Mabeyo amesema Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) linadaiwa Sh3 bilioni na Shirika la Umeme nchini na kesho (Jumatatu)  watapunguza deni hilo ili wasikatiwe umeme.

Mabeyo ameyasema hayo leo wakati anazungumza na waandishi wa habari makao makuu ya jeshi (Ngome) na kueleza deni hilo limetokana na shughuli za jeshi hilo kwenye ulinzi wa Taifa pamoja na ufinyu wa bajeti.

"Baada ya kupokea maelezo ya Tanesco na kufuatia tamko la Rais, Jeshi la Wananchi limetafakari na limefanya jitihada kupata fedha za  kupunguza deni hili, tunadaiwa fedha kiasi kinachozi kidogo Sh3 bilioni, nimeagiza watendaji wetu watafute Sh1 bilioni," amesema Mabeyo.

Mabeyo amesema juhudi zinazofanywa na Jeshi hilo zinatakiwa kuonyeshwa na Taasisi nyingine ili kuweza kuiongezea Tanesco uwezo wa kutoa huduma.

ENEO AMBAPO WATOTO HUPEWA MAJINA YA KUSTAAJABISHA

Eneo ambapo watoto hupewa majina ya kustaajabisha

Katika eneo moja mashariki mwa Zambia mwandishi wa BBC Chris Haslam, anakumbana na kijana mdogo ambaye anajikakamua kusukuma baiskeli kubwa ambayo imebeba mitungi ya maji, kuni na mfuko wa mchele.

Kwa vile kijana anaisukuma baiskeli hiyo na mikono yake miwili, hana njia ya kuwafukuza nzi kutoka kwa macho yake.


Jina lake ni "Mulangani". Jina hilo ni la jamii ya Nguni linalomaanisha "niadhibu" au yule ambaye ni lazima adhibiwe. Chris Haslam alimuuliza dereva kuhusu ni nani anayeweza kumpa mtota wake jina baya kama hilo?

"Labda babu yake au chifu," dereva akajibu. Nchini Zambia na hata Zimbabwehasa mashambani , ni jambo la kawaida wazazi kuwaalika wazee wa jamii kuwapa majina watoto wanapozaliwa.

Mara nyingine chifu huwa anataka kuiadhibu familia, anasema dereva, "au anafikiri kuwa mtoto aliyezaliwa ni mzigo kwa familia."

Lakini kijana huyo si peke yake aliye na jina la kutisha. Baadaye anakutana na "Chilumba", jina linalomaansiha "kaburi la ndugu yangu"

Kisha anakutana na Balaudye - "nitaliwa" na Chakufwa- "amekufa"

Pia anakutana na Daliso linalomaanisha "baraka" na Chikondi linalomaanisa "upendo".

Kwenye utamaduni wa Afrika kuna tabia ya kuwapa watoto majina kutokana na nyakati walizozaliwa, kwa mujibu wa Clare Mulkenga afisa wa huduma za watoto nchini Zambia.

Anasema kuwa hata hivyo ni vyema kwa wale wanaozaliwa nyakati nzuri lakini pia huwa ni bahati mbaya kwa wengine.

MGOGORO MZITO UNARIPOTIWA NDANI YA CHADEMA

Mgogoro mzito unaripotiwa ndani ya CHADEMA


Chama chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kimeingia katika wingu zito na kutishia kukisambaratisha chama hicho.

Chanzo cha Mgogoro ni nafasi za Ubunge wa Africa mashariki, Uchaguzi wa kanda ya Mashariki na Hali ya kifedha ndani ya chama.

Chanzo cha ndani ya CHADEMA kinasema kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Ndugu Freeman Mbowe aliingia na majina mawili ndo akawaambia wayachague ambapo aliingia na Majina hayo ni Masha na Wenje hakukua na utaratibu sahihi wa kuwapata wagombea katika Bunge la Africa Mashariki.

Uchaguzi wa kumpata Viongozi ndani ya kanda ya Mashariki ulijaa kasoro nyingi ambapo wananchama wanaulinganisha na ule wa kanda ya Nyasa ambapo Ole Sosopi alitupwa nje ya kinyang'anyiro kwa kuwa mwenyekiti wa chama aliingia na Jina lake.

Idara ya fedha ndani ya CHADEMA haijakaa vizuri hivyo kuleta sintofahamu kwa wadhamini ambao wanataka ukaguzi wa fedha kupitia mkaguzi huru akague ili wajiridhishe wadhamini ndani ya CHADEMA wamekua wagumu kutoa fedha zao Hali ambayo inaisababishia chama ukata kwani Tajiri na Mdhamini mkubwa ndani ya CHADEMA ndugu Sabodo Alishajitoa na Kuungana na Rais Magufuli baada ya kuona Utendaji wake uliotukuka.

BASATA WAMEZUNGUMZIA WIMBO WA NAY WA MITEGO

BASATA Wamezungumzia Wimbo wa Nay Wa Mitego

Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amesema wataufungia wimbo wa 'Wapo' wa Nay wa Mitego kwani hauna maadili.


ASICHOTAKA KUKISIKIA KABISA KWENYE SOKA WAZIRI MWAKYEMBE

Asichotaka kukisikia kabisa kwenye Soka Waziri Mwakyembe


Waziri wa Mpya wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameanza kazi katika Wizara mpya. 

Lakini Dk Mwakyembe ambaye kitaalamu ni mwandishi wa habari na mwanasheria nguli, amesema hapendi kuona timu za Tanzania zinafungwafungwa tu.

 "Watanzania tumechoka na huu uteja, kusukumwa sukumwa tu kwenye soka. Ni hamu ya watanzania sasa tuonekane katika ulimwengu wa soka", amesema Waziri Dk. Mwakyembe aliyezungumza na Kamati ya Hamasa kwa Serengeti Boys alipokutana nayo kwa mara ya kwanza jana Machi 25, mwaka huu.

Waziri alikwenda mbali kwa kuiagiza Wizara yake yote ijikite kuhakikisha maandalizi ya Serengeti Boys yanakamilika kwa wakati. 

"Nataka Wizara yangu yote sasa wimbo wetu uwe Serengeti Boys," amesema Dk. Mwakyembe.

Katika hafla hiyo, Dk Mwakyembe amempongeza mtangulizi wake, Mheshimiwa Nape Nnauye kwa kuunda Kamati ya Serengeti Boys ili kutoa hamasa ya Watanzania kwa timu yao. 

Alisema Serengeti Boys ni nyota wanaoinukia (upcoming stars) na wanampa sababu ya kuanza kwenda mpirani tena. 

Waziri Dk Mwakyembe aliendelea kusema kuwa michezo ya leo inahitaji uwekezaji hivyo Wizara yake itahakikisha kuwa jukumu hilo analibeba.

"Naona kama imechelewa, lakini bado muda upo, tukimbie, nataka Wizara nzima wimbo wetu uwe Serengeti Boys", alisema kwa hamasa kubwa. 

Dk Mwakyembe amempongeza Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Serengeti Boys, Charles Hilary kwa mafanikio ya program ya mageuzi ya soka nchini. 

Naye Mkurugenzi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yussuf Singo alisema sasa imechoka kuwa kichwa cha mwenda wazimu na hivyo Taifa limeazimia kucheza Kombe la Dunia kupitia vijana wa Serengeti Boys. 

Rais wa Shirikisho la Kandanda Tanzania, Jamal Malinzi alisema kufuzu kwa Serengeti Boys kucheza fainali za AFCON ni sifa pekee na mwanzo mpya wa mageuzi makubwa ya soka la Tanzania.

Amesema maandalizi ya ushiriki wa fainali za AFCON zitahitaji takriban Shilingi bilioni moja. 

Amesema mikakati mbalimbali imeandaliwa kuchangisha kiasi hicho cha fedha, ikiwa ni pamoja na kuandaa chakula cha hisani. 

Waziri Mwakyembe amesema atahakikisha fedha hiyo inapatikana ili vijana wa Serengeti Boys waweze kufuzu kucheza kombe la dunia huko India mwishoni mwa mwaka huu.

NAY WA MITEGO ALIVYKKUWA NDANI YA KITUO CHA POLISI MOROGORO

PICHA: Nay Wa Mitego alivyokuwa ndani ya kituo cha polisi Morogoro

Hapo chini ni Picha ikimuonesha Nay wa Mitego akiwa ndani ya kituo cha Polisi Morogoro baada ya kukamatwa. (Picha kwa hisani ya Group la WhatsApp la Waandishi wa Morogoro)





HAYA NDIYO MAAJABU MENGINE YA MTI WA MWAROBAINI

Haya ndiyo majabu mengine ya mti wa mwarobaini

Mwarobaini ni mti maarufu sana na unajulikana karibu kila mahali , licha ya kujulikana kila mahali mti huu una kivuli mwanana. Lakini jina hili la mti huo limetokana na uwezo wake wa kutibu zaidi ya magonjwa arobaini. Ingawaje mti huu si majani wala mizizi ni mchungu mno kwa mtumiaji.

Lakini inasadikia kuwa mti huu asili yake imetokea nchini ondoa,  na pia ina uwezo mkubwa wa kustawi sehemu zenye ukame zaidi.  Kwa hapa Tanzania ukienda maeneo ya Dodoma utakubaliana na ukweli huu.

Labda tuangazie macho japo kwa uchache kwa kuona maajabu ya mti huu kama ifuatavyo.

1. Mwarobaini ni dawa ya kuua minyoo yote tumboni,

2. Hutubu homa, hasa zile homa za usiku

3. Mwarobaini hutibu kikohozi.

4. Mwili kuwaka moto.

5.kuharisha pamoja na tatizo la vidonda vya tumbo. Chukua majani ya mmea huu kisha yatafune bila kujali uchungu yaliyo nayo.

6.Mwarobaini hutubu matatizo ya macho.

Ili kutibu matatizo ya macho Unachotakiwa kufanya ni kufuata maelekezo kama amabayo nitaeleza hapo chini.

7.magonjwa mbalimbali ya ngozi hutibika pia kwa kutumia mti huu wa mwarobaini.

Kwa kutibu magonjwa hayo na magonjwa mengineyo unachotakiwa kufanya:

Chemsha majani ya mti wa mwarobaini kwa muda wa dakika kumi tano,  baadae acha mchanganyiko huo upoe, kisha chuja kwa ajili ya matumizi. Unaweza ukanywa mchanganyiko huu asubuhi na jioni. Kwa kiwango cha kikombe kimoja cha chai. Kikombe kimoja asubuhi na kingine jioni.

MAYAI YASIPOIVA NI HATARI

Mayai Yasipoiva Ni Hatari

Mayai ni moja ya vyakula vyenye viini lishe muhimu kwa ajili ya afya ya mwili wa binadamu. Kwa kawaida mayai kabla ya kuliwa, huandaliwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchemshwa, kukaangwa au kuchanganywa na vyakula vingine kama vipande vya viazi mviringo ambavyo ni maarufu kwa jina la chips.

Pia, kuna baadhi ya watu wanaopendelea kula mayai mabichi kama dawa ya tiba mbadala, kwa ajili ya kulainisha sauti na wengine hupendelea kula mayai ya kukaanga ambayo hayakukaushwa vizuri.
Ukitembelea migahawa mingi utabaini kuwa watu wanakuwa na mitazamo tofauti na wanavyopenda kula mayai.

Mfano kuna wanaoagiza watengenezewe mayai kwa mtindo unaojulikana kama ‘macho ya ng’ombe.’ Ukiagiza namna hiyo, mpishi atataka kuuliza kama ni ‘macho ya ng’ombe’ ya kugeuza.

Ina maana kuwa ‘macho ya ngombe’ ya kugeuzwa ni yale yanayoivishwa pande zote lakini yale ambayo siyo ya kugeuza, huwa linaiva nusu. Upande mmoja unabaki ukiwa mbichi, na ndiyo raha ya baadhi ya watu.

Hata ukienda kwa wakaanga chipsi, utakuta wanawauliza wateja wao kama wanapokaanga na mayai wakaushe au wasikaushe. Hii inaashiria kuna watu wanataka wale chipsi zikiwa na mayai ambayo halijaiva sawasawa.

Kuna watu wengine wanaamini kwamba kula mayai mabichi kunafanya sauti inakuwa nyororo, hivyo wale waimbaji huwalazimu kufanya hivyo ili kufanya nyimbo zao zivutie.

Si hivyo tu, kuna baadhi ya watu huamini pia dawa ya kikohozi ni kunywa yai bichi lililochanganywa na asali. Hizi ni imani ambazo zimejengeka kwenye jamii na watu hufanya hivyo ili kufikia malengo waliyokusudia.

Katika siku za karibuni, imevuma kuwa mayai ya kwale yanatibu magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, saratani na kifua.

Katika mpango huo, wanapendekeza wahusika kula mayai mabichi ya kwale tena kwa kutafuna hadi kaka lake, yaani ganda la nje.

Hali hii imesababisha biashara ya mayai ya kwale kuwa kubwa na hata wafugaji wameongezeka mara dufu.

Tuesday, March 21, 2017

TUMIA TANGO KWA FAIDA ZIFUATAZO

Tumia Tango Kwa faida zifuatazo

Leo katika makala hii afya tujifunze  faida za Tango katika miili yetu, ikiwa watu wengi tunakula bila kujua faida zake katika maisha ya kila siku. Hivyo nakusihi uambatane nami mwanzo mpaka mwisho wa makala haya kwani naamini utakochokisoma hapa kitakwenda kukusaidia.

Zifuatazo ndizo faida za tango:
1. Tango ni chanzo kizuri cha vitamin B. Ambayo husaidia kwa kiwango kikubwa katika kusafisha figo. Na kuondoa sumu zote zilizomo mwilini.

2. Tango husaidia kuongeza maji katika mwili wa mwanadamu, kwani asilimia 95 ya tango ni maji, huku tukizingatia ya kwamba asilimia 75 ya mwili wa mwanadamu ni maji,  ambapo maji hayo ni chanzo kikuu cha usafirishaji wa chakula na damu katika mwili wa mwanadamu. Hivyo unashauriwa utumie kwa wingi tunda hili.

3. Tango pia hutumika kwenye matunzo ya ngozi/urembo ambapo tunda hili lina kiwango kikubwa cha silicon na sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele.

4. Tango lina virutubisho kama lariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol ambavyo kulingana na tafiti mbali mbali za magonjwa ya kansa husaidia kupunguza aina mbali mbali za kansa hasa kansa ya matiti.

5. Kwa wale ambao wana matatizo ya kinywa hasa harafu wataalamu wanasema ya kwamba tango husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani.

7.Tango husaidia wagonjwa wa kisukarikwani tango lina hormone ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho (pancreatic cells) ilikuweza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari. Pia watafiti wamegundua kuwa kuna kirutubisho kiitwacho sterol kilichopo kwenye tango ambacho husaidia kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu.

8. Kutokana na maji na virutubisho vilivyopo kwenye tango, tunda hili husaidia kupunguza homa pale inapopanda.

Cha msingi na cha kuzingatia ni kwamba kula matunda mara kwa mara kwani yana saidia sana katika afya. Endelea kutembelea muugwana blog kwa makala kama hizi.

FORBES: MABILIONEA 25 MATAJIRI AFRIKA 2017

Forbes: Mabilionea 25 matajiri zaidi Afrika 2017

Mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa orodha ya mabilionea mwaka 2017 iliyoandaliwa na jarida la Forbes.

Utajiri wa Dangote unakadiriwa kuwa jumla ya $12.2 bilioni.
Kuna mabilionea (wa Dola) 25 mwaka huu barani Afrika, mmoja juu ya 24 waliokuwepo mwaka jana.

Wafanyabiasha kutoka Nigeria Femi Otedola na Abdulsamad Rabiu hawakufanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo mwaka huu.

Mtanzania Mohammed Dewji bado ndiye bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika, utajiri wake ukikadiriwa kuwa $1.09 bilioni.

Isabel dos Santos kutoka Angola na mfanyabiashara wa mafuta Folorunsho Alakija kutoka Nigeria ndiye mabilionea wanawake pekee katika orodha hiyo mwaka huu.

Bw Dangote Dangote, ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement inayoongoza kwa kuzalisha saruji Afrika. Anamiliki asilimia 90 ya hisa za kampuni hiyo.
Dangote Cement huzalisha tani 44 milioni za saruji kila mwaka na imepanga kuongeza uzalishaji kwa asilimia 33 kufikia 2020.

Dangote pia anamiliki hisa katika kampuni za chumvi, sukari na unga.
Mohammed Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970. Kampuni hiyo huhusika katika biashara ya nguo, unga, vinywaji na mafuta. Kampuni hiyo huendesha shughuli zake katika zaidi ya mataifa sita barani Afrika.

Mabilionea 25 wa Afrika mwaka 2017:

1. Aliko Dangote, Nigeria

    Utajiri: $12.2 bilioni

2. Nicky Oppenheimer, Afrika Kusini

    Utajiri: $7 bilioni

3. Mike Adenuga, Nigeria

   Utajiri: $6.1 bilioni

4. Johann Rupert, Afrika Kusini

   Utajiri: $6.3 bilioni

5. Nassef Sawiris, Misri

   Utajiri: $6.2 bilioni

6. Christoffel Wiese, Afrika Kusini

    Utajiri: $5.9 bilioni

7. Nathan Kirsch, Swaziland

    Utajiri: $3.9 bilioni

8. Naguib Sawiris, Misri

    Utajiri: $3.8 bilioni

9. Isabel dos Santos, Angola

    Utajiri: $3.1 bilioni

10. Issad Rebrab, Algeria

     Utajiri: $3 bilioni

11. Mohamed Mansour, Misri

      Utajiri: $2.7 bilioni

12. Koos Bekker, Afrika Kusini

      Utajiri: $2.1 bilioni

13. Allan Gray, Afrika Kusini

      Utajiri: $1.99 bilioni

14. Othman Benjelloun, Morocco

      Utajiri: $1.9 bilioni

15. Mohamed Al Fayed, Misri

      Utajiri: $1.82 bilioni

16. Patrice Motsepe, Afrika Kusini

      Utajiri: $1.81 bilioni

17. Yasseen Mansour, Misri

      Utajiri: $1.76 bilioni

18. Folorunsho Alakija, Nigeria

      Utajiri: $1.61 bilioni

19. Aziz Akhannouch, Morocco

     Utajiri: $1.58 bilioni

20. Mohammed Dewji, Tanzania

      Utajiri: $1.4 bilioni

21. Stephen Saad, Afrika Kusini

      Utajiri: $1.21 bilioni

22. Youssef Mansour, Misri

      Utajiri: $1.15 bilioni

23. Onsi Sawiris, Misri

      Utajiri: $1.14 bilioni

24. Anas Sefrioui, Misri

     Utajiri: $1.06 bilioni

25. Jannie Mouton, Afrika Kusini

      Utajiri: $1 bilioni


UFARANSA :WAZIRI AJIUZULU

Ufaransa:Waziri ajiuzulu

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa,Bruno Le Roux, amejiuzulu, baada ya kuibuka shutuma kuwa aliwaajiri binti zake wawili kuwa wasaidizi wa bunge wakiwa wanafunzi.

Waendesha mashtaka walifanya uchunguzi wa awali kuhusu mikataba yenye thamani ya karibu dola elfu sitini ambazo bwana Le Roux aliwapa binti zake kati ya mwaka 2009 na mwaka 2016.

Amesema hakuna sheria ya bunge iliyokiukwa na watoto wake walifanya kazi kwa uhalali, lakini hakutaka kuwa kikwazo kwa Serikali.

Wakati huohuo, uchunguzi kama huo umeendelea kufanyika dhidi ya mgombea urais kutoka chama cha Conservative Francois Fillon, ambaye anashutumiwa kufanya udanganyifu.

Fillon amekana kuajiri familia yake na kuwalipa mishahara minono, kashfa ambayo imetia dosari mchakato wake wa kuwania urais

KUNDI LA HEZBOLLAH LADAIWA KUMUUA KAMANDA WAKE

Kundi la Hezbollah ladaiwa kumuua kamanda wake

Afisa mkuu wa jeshi la Israel ameongeza uzito katika vyombo vya habari vya Kiarabu kwamba kundi la wapiganaji wa Hezbollah lilihusika katika mauaji ya kamanda wake nchini Syria 2016.

Luteni jenerali Gadi Eisenkot alisema kuwa idara ya ujasusi ya Israel pia ilibaini kwamba Mustafa Amine Badreddine aliuliwa na wapiganaji wake.

Aliuawa katika mlipuko karibu na Damscus ambapo kundi la wapiganaji la madhehebu ya kishia lililaumu wapiganaji wenye itikadi kali wa Sunni.

Badreddine aliaminika kuendesha operesheni zake nchini Syria tangu 2011.

Hezbollah linahusishwa pakubwa katika vita vya wenye kwa wenyewe nchini humo, likiwa limesambaza maelfu ya wapiganaji ili kumuunga mkono rais Bashar al-Asaad.

Mapema mwezi huu, kituo cha habari cha al-Arabia kilisema kuwa uchunguzi wake mwezi huu kuhusu mauji ya Bedraddine ulibaini kwamba kamanda huyo aliuawa kutokana na agizo la Hassan Nasrallah.

Ripoti hiyo inasema kuwa Hassan Nasrallah alishinikizwa kumuua Bedraddine na meja jenerali Qasema Soleiman,kiongozi wa walinzi wa jeshi la Iran.

Monday, March 20, 2017

HIKI NDICHO CHANZO CHA UGONJWA WA MABUSHA

Hiki ndicho chanzo cha Ugonjwa wa Mabusha

Ngiri nyingine ni ya Mshipa wa Kushuka ni hii hapa Mabusha kwa lugha ya kiswahilBusha ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa pumbu.

Hali hii hutokea kunapokuwa na mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani. Inakadiriwa kuwa karibu asilimia moja ya wanaume wote kote duniani huathiriwa na tatizo hili.

Ifahamike pia kuwa, tatizo la mabusha halitokei kwa wanaume watu wazima tu. Watoto wa kiume hususani katika mwaka wa kwanza (infants) pia ni waathirika wakuu wa tatizo hili.

Kwa kawaida busha halina maumivu na wala kuleta madhara, isipokuwa kama litapata uambukizi kwa sababu nyingine yeyote ile, hali inayowafanya wengi wa waathirika, kuwa wagumu kutafuta ufumbuzi wa tiba.

Hata hivyo, ni vyema kama mtu ana uvimbe wowote kwenye pumbu zake, kutafuta msaada wa kitabibu ili kuweza kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa magonjwa mengine ya sehemu za siri kama vile saratani ya korodani (testicular cancer) n.k.

  Busha husababishwa na nini? Sababu za kutokea kwa busha hutofautiana kati ya watoto wa kiume na wanaume watu wazima.

Kwa watoto wa kiume Kwa watoto wa kiume, busha huweza kuanza kutokea kipindi cha ujauzito.

Wakati wa ujauzito, korodani za mtoto wa kiume huwa kwenye tumbo lake kabla ya kushuka taratibu kuelekea kwenye mapumbu.

 Wakati wa ushukaji huo, kifuko kinachozunguka korodani kinachoitwa processus vaginalis hushuka sambamba na kurodani hizo na kufanya korodani kuzungukwa na maji.

Kwa kawaida, ndani ya muda wa mwaka mmoja, kifuko hiki hufunga na maji hayo yanayozunguka korodani yote hufyonzwa na kurudishwa kwenye tumbo la mtoto.

Iwapo baada ya kifuko kufunga na maji yaliyomo kushindwa kufyonzwa kurudishwa kwenye tumbo la mtoto, mtoto hupata busha lijulikanalo kitaalamu kama busha lisilo na mawasiliano (non-communicating hydrocele).

Hali kadhalika, wakati mwingine inawezekana kifuko kikashindwa kufunga na hivyo maji yakaendelea kujaa ndani ya kifuko kuzunguka korodani.

Aina hii ya busha kwa watoto ujulikana kama busha lenye mawasiliano (communicating hydrocele). Kwa wanaume watu wazima Kwa wanaume watu wazima.

Busha husababishwa na mambo makuu mawili:

1. kitendo chochote kinachochochea tando zinazozunguka korodani kuzalisha maji kwa wingi kuliko kawaida.

2. Kupungua kwa ufyonzaji wa maji yanayozunguka korodani kwa sababu ya kuziba kwa mirija ya lymph (blockage of scrotal lymphatic system) au kuziba kwa mishipa ya damu inayosafirisha damu kutoka kwenye pumbu kwenda sehemu nyingine za mwili (blockage of scrotal venous system)

Ongezeko la uzalishaji wa maji linaweza kutokana na

Maambukizi au/na majeraha katika korodani (testicular inflammation auorchitis) Maambukizi katika mshipa ujulikanao kama epididymis yanayoweza kusababishwa na kifua kikuu (tuberculosis) cha makende,Maambukizi yanayo sababishwa na vimelea wa filaria (filariasis) wanao sababishwa na kuumwa na mbu aina ya Culex.Kujinyonga kwa korodani (testicular torsion) kunakoweza kuzifanya korodani kutenda kazi zaidi ya kiwango chake (hyperactive testis).Uvimbe katika korodani (testicular tumors) ambao husababisha uzalishaji wa maji kupita kiasi.Kupungua kwa ufyonzaji wa maji hutokana na Kufanyiwa upasuaji kipindi cha siku za nyuma katika eneo la kinena, au operesheni ya upandikizaji figo ambazo zinaweza kuathiri mfumo wa lymph na vena na hivyo kupunguza ufyonzaji wa maji kutoka kwenye mapumbu. Kuwahi kufanyiwa tiba ya mionzi kipindi cha nyuma nayo uhusishwa na kutokea kwa busha. Kwa hapa kwetu Tanzania, kung’atwa na mbu aina ya Culex anayeeneza vimelea vya filaria kunaelezwa kuwa sababu kuu mojawapo inayopelekea kuwepo kwa tatizo la mabusha na matende hususani maeneo ya Pwani na mwambao. 

Dalili za busha Katika hatua za awali,

busha huwa halina dalili zozote (asymptomatic).

Hata hivyo, baada ya muda fulani, mapumbu hujaa na uvimbe huweza kuonekana hata kwa nje. Kwa kadiri uvimbe unavyozidi kuongezeka, ndivyo dalili zingine uzidi kuonekana.

JE WAJUA ASILI YA KIDUKU

JE WAJUA ASILI YA KIDUKU?

Wengi wanapenda kucheza au kuona wengine wakicheza KIDUKU! Lakini wengi wao hawafahamu asili na chimbuko la kiduku hapa Tanzania!

Kwa kifupi ni kwamba ASILI YA KIDUKU NI NIGERIA! kiduku ni aina fulani ya ngoma inayochezwa nchini Nigeria,

Hivyo kiduku kimefika Tanzania kupitia filamu za kinigeria!

Filamu ya 'Ola' ilyotoka mwaka 2006 ndo kichochezi halisi cha style ya kiduku nchini kwani baada ya filamu ya Olakusambaa nchini Tanzania ndipo kiduku kilipoibuka na kuenea nchini Tanzania!

JINSI YA KUPUNGUZA UZITO KWA KUTUMIA SALADI

Ulaji saladi ya spinachi, matunda ya apple na parachichi unaweza kumsaidia mtu kuwa na uzito unaotakiwa kiafya.

Kabla mtu hajaanza kula mlo wake wa asubuhi, mchana au usiku anashauriwa aanze na mboga za majani za spinachi au aina nyingine.  Ulaji wa aina hii unamwezesha mtu kula kidogo vyakula vyenye wanga, sukari au mafuta ambavyo vinasababisha kuongezeka uzito na unene.

Saladi ya mboga za majani hujaza tumbo na kumfanya mtu ajihisi ameshiba na hivyo kuzuia tabia ya kutamani kula hasa vyakula vya wanga au sukari.  Mboga za majani za spinachi pia, zina kirutubisho kinachoitwa thylakoids, ambacho kinachochea mwili kuzalisha homoni inayopunguza hamu ya mtu kutaka kula hasa vyakula vyenye sukari.

Kuhusu matunda ya apple, kwa siku mtu akila tunda moja ni jambo zuri.  Matunda ya apple yana maji na nyuzi lishe ambazo zinalifanya tumbo kujisikia limeshiba.  Matunda ya epo pia yana kirutubisho cha pectin, ambacho kinakifanya chakula kilichomo tumboni kusagwa kwa muda mrefu na kumfanya mtu kujisikia ameshiba.

Mtu akila tunda zima la epo (siyo juisi), kabla ya mlo atajisikia hali ya kushiba na hivyo atakula kidogo chakula cha wanga au sukari.
Kwa upande wa matunda ya parachichi, kula nusu ya tunda hilo kwa siku kunaupa mwili mafuta bora kiafya na nyuzi lishe ambazo zinamfanya mtu ajisikie ameshiba muda mwingi na kutokutamani chakula mara kwa mara.

Anachopaswa kufahamu mtu ni kwamba kula vyakula vya wanga, sukari au mafuta kwa wingi ndipo mwili unaongezeka uzito na unene kupita kiasi. 

JINSI YA KULIMA KILIMO BORA CHA MIPAPAI

Jinsi Ya Kulima Kilimo Bora Cha Mipapai

MAHITAJI
Hali ya  hewa inayofaa kwa mipapai ni ya kitropik ambayo haina baridi kali na joto kiasi . Udongo usiotuamisha maji maji yakisimama kwa masaa 48 tu mpapai unaweza kufa, wenye ruruba ya kutosha kwa sababu mipapai haina mzizi mkuu haihiyaji udongo wenye kina kirefu, kipindi cha jua kali mpapai usiachwe zaidi ya wiki 8 bila kumwagiliwa maji kama hakuna mvua ingawa wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hii huongeza ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema sokoni.

Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mwingi kwani huvunjika kirahisi, kama unashamba la mipapai itakubidi kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka shamba lako, miti kama miparachichi, migravilea, vibiriti (leucaena Spp) na miembe pia inafaa. Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai kwa mita 10 mpaka 20 juu zaidi.

Kuendelea kupanda mipapai kwenye shamba moja kunaweza kusababisha usugu wa magonjwa, nashauri baada ya miaka 3 – 5 ubadilishe zao hili angalau kwa msimu mmoja ili kuua mzunguko wa magonjwa.

Mipapai inaweza kuchanganganywa na miembe na mimea jamii ya michungwa, pia mazao ya msimu kama mahindi, mtama, ufuta , alizeti  na  mboga mboga yanaweza kulimwa.

Kwa kaida kwenye mipapai kuna mipapai dume, majike  na yenye jinsia zote (multiplesex / hermaphrodite) ambayo huwa na mapapai marefu zaidi, na pia kuna isiyoeleweka ambayo huwa na mapapai mafupi sana.

MBEGU

Kusanya mbegu toka kwenye mapai makubwa na yaliyo komaa na kuiva, kausha mbegu vizuri kbla ya kupanda, kama utapata mbegu za  kununua ni vizuri zaidi, baada ya kukausha hakikisha unazipanda ndani ya wiki moja.

KUOTESHA MBEGU

Kuna wanaopendelea kuotesha mbegu kwanza na kisha kuhamishia miche shambani, sehemu ya kuoteshea iandaliwe miezi miwili kabla, mbegu zioteshwe kwenye kina kati ya sentimeta 1 – 2 chini ya udongo wenye rutuba au pakiti za plastiki, kiwango bora cha joto ni sentigredi 21 – 27 na itachukua kati ya wiki 1 – 4 kwa mbegu kuota, kwenye kila pakiti weka mbegu 2 – 3. Panda mbegu zako kwenye kitalu kwa umbali wa sentimeta 3 toka shimo hadi shimo na sentimeta 15 kati ya mistari, hakikisha maji hayatuami kabisa, pia unaweza kupiga dawa ya copper oxychloride gramu moja katika lita moja ya maji ilikukinga miche yako na fangasi.

UOTESHAJI WA MOJA KWA MOJA

Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea ya kuku sehemu ya kupandia, mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia kukinga mipapai na magonjwa. Panda mbegu 3 – 5 kila shimo maana miche mingine inaweza kufa kwa magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota dume.

KUHAMISHA MICHE TOKA KWENYE KITALU

Miche ihamishiwe shambani ikiwa na urefu wa sentimeta 20 – 40, kama udongo unatuamisha maji panda kwenye matuta yenye urefu wa sentimeta 40 – 60 mashimo yawe na ukubwa wa sentimeta 45 upana na sentimeta 30 kina na shimo lichanganywe na udongo na samadi bila kuacha kisahani cha maji, umbali ni mita 3 kwa 3 kwani mipapai inahitaji jua la kutosha.

KUPUNGUZA MIPAPAI

Baada ya miezi 3 – 5 baada ya kupanda mipapai itatoa maua na hapo jinsia ya mipapai itajulikana na mingine itabidi ipunguzwe na hasa midume, mipapai yenye jinsi zote inatakiwa isizidi asilimia 10 – 20 na midume ibaki mmoja katika kila mijike 25, mimea yenye magonjwa pia inabidi ing’olewe.

RUTUBA YA UDONGO

Weka kiasi chakilo 2 – 5 za samadi kwenye kila mpapai kwa mwaka ili kuongeza ukuaji na uzazi, mabaki ya mimea yanaweza pia kuwekwa kama matandazo na h ii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu usipotee.

MAGUGU

Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili kuzuia uoataji wa magugu, magugu yang’olewe yakiwa machanga na epuka kuchimbua chini sana maana mizizi ya mipapai huwa juu juu, njia nzuri ni kuweka matandazo kwenye shamba lote ili kuzuia outaji wa magugu.

UANGALIZI

Mipapai iangaliwe dhidi ya magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au kufukiwa chini ikiwa itabainika kuwa na maonjwa, piga dawa dhidi ya magonjwa ya fangasi na virusi mara yanapoibuka ili kuongeza uzaaji nakipato chako.

Ondoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na hii ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.

Ondoa mapapi yote ambayo yatakuwa hayakuchavuliwa vizuri na acha yale yenye afya tu

Weka miti ya kuegemea kama mpapai utazaa matunda mengi na hasa wakati wa upepo mwingi ili kuzuia mipapai isivunjike.

Mipapai ikitunzwa inaweza kuishi mika mingi, ila kwa ajili ya mazao bora ondoa mipapai na upande mingine baada ya kila miaka mitatu (3) kwani mpapai unapo kuwa mkubwa basi rutuba yote huishia kwenye mti wenyewe.

Sunday, March 19, 2017

BUASHARA NZURI AMBAYO UNAWEZA UKAIFANYA NA KUPATA FAIDA KUBWA NI HOI HAPA

Biashara Nzuri Ambayo Unaweza Ukaifanya Na Kupata Faida Kubwa Ni Hii Hapa

Habari za leo, mpenzi msomaji wa safu hii ya biashara? Nikukaribishe kwa moyo mkunjufu ili tuweze kujifunza na elimu hii ya biashara. Andaa ubogo wako ili uweze kupokea mambo muhimu ya kukusaidi kufanikiwa.

Moja ya maswali ambayo nimekuwa nikiulizwa sana na wasomaji wetu ni kwamba je, afisa mipango Benson, nifanye biashara gani ambayo itakuwa ina faida kubwa kwangu?

Kama ambavyo nimekuwa nikiulizwa mara kadha wa kadha na swali hilo tena limekuwa likijirudia. Hivyo kwa kutumia dakika chache naomba niweze kujibu swali hilo.

Jambo la msingi sana ambalo unatakiwa kulizingatia ni kwamba kila biashara ambayo unaiona machoni mwako ina faida na hasara zake, Nimeanza kwa kusema hivyo kwani watu wengi wamekuwa wakiaangalia upande mmoja tu wa kupata faida tu.

Lakini ukweli ambao unatakiwa kuujua mapema ni kwamba kabla ya kuingia katika biashara tambua ya kwamba katika biashara hiyo kuna faida na hasara, hivyo uwe tayari kubeba mambo hayo mawili pindi yatakapojitokeza.

Biashara yenye faida huanza na wazo, wazo ambalo limekuwa likitokana na mfanyabiashara kabla ya kuanza kufanya biashara husika. Wazo hilo hujengwa na misingi ya kina ya kufanya uchunguzi yakinifu juu ya biashara hiyo.

Usipofanya uchunguzi wa kutosha juu ya biashara unayotaka kuifanya ipo siku utalalamika. Ila tunashauriwa ya kwamba katika kufanya uchunguzi wa kutosha ni lazima ujikite katika kuangalia eneo ambalo utaiendesha biashara hiyo.

Wakati unangalia eneo kwa ajili ya kufanyia biashara, angalia eneo ambalo:-

Eneo linalofikika kwa urahisi.
Angalia eneo ambalo lina uwingi wa mkusanyiko mwingi wa watu tofauti tofauti.
Tafuta eneo ambalo kuna upatikaji wa huduma za kijamii, kama vile ukaribu wa benki, umeme, maji na mengineyo mengi yatakoyokusiadia kukua kibiashara.

Angalia eneo ambalo lipo karibu na wafanyabiashara wengine. Kwa mfano, kama unafanya biashara ya mashati  basi chagua eneo ambalo kuna mfanyabiashara anauza tai. Kufanya hivi kuna msaidia mteja kutopata tabu ya kuhangaika kupata bidhaa fulani.

Lakini kubwa kuliko yote ni kwamba katika kufanya uchunguzi wa eneo la kufanyia biashara ni vyema unafanya uchunguzi kwa kuangalia hasa ni yapi mahitaji ya watu.

Kisha wewe uweze kuyasogeza mahitaji hayo karibu.
Mwisho naomba ujiulize hivi, ni wapi ambapo imepanga kufanya biashara h? Na watu wana changamoto zipi nawe umekuja suluhisho lipi? Ukipata majibu hayo huo ndio utakuwa mwanzo wa kujua biashara gani italipa eneo hilo na hatimaye kupata faida.

Hivyo niseme hivi, biashara inayolipa na kutoa faida kubwa ni ile biashara ambayo umeshaifanyia uchunguzi wa kutosha na kujua soko lake liko wapi na lina ukubwa gani. Hiyo ndiyo biashara inayolipa.

MAMBO 5 YATAKAYOKUPA HAMASA KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO

Mambo 5 Yatakayokupa Hamasa Katika Safari Yako Ya Mafanikio

Katika safari ya mafanikio ni rahisi sana kufanikiwa ikiwa ndani yako kila siku unakuwa una hamasa kubwa ya kukusaidia kufikia mafanikio hayo. Mara nyingi hamasa huwa ni kama kichocheo cha kukufanya uzidi kukazana na kuweza kuendelea hadi mwisho kwenye mafanikio yako.

Kwa kawaida hamasa inapokesekana, hapo sasa ndipo mambo huanza kufanyika kivivu na wakati mwingine kukata tamaa huanza kujitokeza. Hivyo, utaona kwamba kuwa na hamasa tena kubwa ikiwa unataka mafanikio ni kitu cha lazima sana, vinginevyo uwe hupendi kufanikiwa.

Utakapokuwa na hamasa hii, suala la kukatishwa tamaa linakuwa sio rahisi sana kwako. Sasa kutokana na umuhimu wa hamasa kwenye mafanikio ni vizuri ikiwa utafanya mambo yatakayokupa hamasa ya kufanikiwa kila siku. Kwa kusoma makala haya, utajua mambo hayo ya msingi kabisa yatakayokupa hamasa. Karibu tujifunze kwa pamoja.

1. Jikumbushe malengo yako kila wakati.
Nguvu kubwa ya kufanikiwa na kupata hamasa utakuwa unaipata ikiwa utakuwa mtu wa kujikumbusha malengo yako kila wakati. Unaweza kujikumbusha malengo yako asubuhi, mchana na hata jioni iwe kwa kuyaandika au kuyasoma. Unapojikumbusha malengo yako kila siku hiyo inakupa hamasa kubwa ya kufanya kitu cha ziada juu ya malengo yako bila kuacha.

2. Fanya kile Unachokipenda.
Mara nyingi kufanya kile unachokipenda ni njia sahihi ya kukufanya kuwa na hamasa wakati wote. Hiyo ni kwa sababu, hata ikitokea kitu hicho hakileti matokeo unayoyataka kwako halitakuwa tatizo kwa sababu ni kitu ambacho unakipenda na kipo kwenye damu. Hivyo, unalazimika sana kufanya lile jambo unalolipenda ili kuwa na hamasa ya mafanikio kila siku.

3. Weka nguvu zako kwenye jambo moja.
Kama kuna jambo umeamua kulifanya weka nguvu na mawazo yako hapo. Acha kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja hayatakusaidia sana. Lakini, unapofanya jambo moja na kuweka nguvu zote hapo kufunga hiyo ni nguvu tosha ya kukupa hamasa, kwani utajifunza mengi sana kutokana na kitu hicho kimoja na itakusadia kukupa hamasa ya kuendelea mbele.

4. Kuwa chanya wakati wote.
Huwa si jambo geni sana kukatishwa tamaa hasa pale tunapokuwa kwenye safari ya mafanikio. Hiyo huwa inatokea kwa sababu watu wengi wako hasi sana.  Sasa ili kuepuka hilo inabidi ujifunze namna unavyopokea taarifa hasi na kutafsiri matukio. Kwa kufanya hivyo itakusaidia kujenga ile hamasa ambayo ipo ndani mwako na idumu kila siku na mwisho wa siku utafanikiwa.

5. Acha kujilinganisha na wengine.
Kati ya sumu kubwa inayoweza ikakufanya ukakosa hamasa ya kuendeea mbele kimafanikio ni pamoja na kujilinganisha na wengine. Siku zote kimbia mbio zako mwenyewe. Ukijilinganisha sana, mwisho utaanza kujikosoa na kujiona hufai. Hivyo unataka kuwa na hamasa kubwa kila siku, kuwa wewe kama wewe, kwa hilo litakusidia sana.

Kwa kujua mambo hayo, yatakusaidia sana kukujengea hamasa kila siku. Fanyia kazi mambo hayo ili yawe silaha ya kukusaidia kukupa hamasa na kufanikiwa pia.
Ansante kwa kusoma makala haya na tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio.

Friday, March 17, 2017

NYUMBA YA KULALA WAGENI YAPEWA SIKU SABA KUBUNJWA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge ametoa siku saba kwa Manispaa ya Songea kuvunja nyumba ya kulala wageni ya tulivu iliyojengwa kwenye chanzo cha maji na kusababisha tatizo la maji katika mtaa wa miembeni mkoani ruvuma.

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo baada  ya Mwenyekiti wa mtaa wa Miembeni Bw. Christian Komba kulalamikia viongozi wa Manispaa ya Songea kutochukua hatua za kubomoa jengo hilo ambalo lina vibanda vya maduka na nyumba ya kulala wageni mita 20 kutoka kwenye chanzo cha maji.

Kwa upande wake mmiliki wa nyumba huyo Bw.Imani Mbugi amesema kuwa ni kweli amejenga nyumba hiyo kwenye chanzo cha maji lakini kuna nyumba zaidi ya kumi zilizojengwa kwenye chanzo hicho lakini anashangaa  anasakamwa yeye tu.

BARCELONA KUIKABILI JUVENTUS, REAL MADRID DHIDI YA BAYERN

Wachezaji wa leicester wakisherehekea ushindi wao dhidi ya Sevilla. Timu hiyo inakutana na Atletico Madrid

Leicester City itakutana na klabu ya Uhispania Atletico Madrid katika robo fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Mabingwa hao wa ligi ya Uingereza walisonga na kuingia katika robo fainali ya mchuano huo baada ya kuishangaza miamba wa Uhispania Sevilla 3-2 kwa jumla.

Leicester itacheza awamu ya kwanza ya mechi hizo nchini Uhispania mnamo tarehe 11 ama 12 ya Aprili huku mechi ya marudiano ikichezwa kati ya tarehe 18 na 19 ya Aprili.

Mabingwa watetezi Real Madrid watakutana na Bayern huku Barcelona wakimenyana na Juventus.

Borussia Dortmund kutoka Uingereza itacheza dhidi ya Monaco.

Atletico Madrid (Spain) v Leicester City (Eng)

Borussia Dortmund (Germany) v Monaco (France)

Bayern Munich (Germany) v Real Madrid (Spain)

Juventus (Italy) v Barcelona (Spain)

ALIKIBA LEO KUTUMBUIZA KWENYE SXSW C FESTIVAL, TEXAS

Hitmaker wa Aje, Alikiba, Ijumaa hii ataungana na mastaa mbalimbali kutoka pande tofauti za duniani kutumbuiza kwenye tamasha kubwa liitwalo, SXSW Music Festival.

Tamasha hilo linafanyika kwa siku kadhaa huko Austin, Texas nchini Marekani. Alikiba ni sehemu ya orodha iliyopendekezwa na tamasha jingine la Passport Experience (litafanyika Septemba 3, Atlanta, GA) lililoanzishwa na Akon pamoja na meneja wa Ludacris, Chaka Zulu.

Kwenye orodha hiyo, Kiba anaungana na mastaa wa Jamaica, Ayo Jay na Charly Black pamoja na msanii wa Nigeria, May D. Wengine ni pamoja na Karlon, Fully Focus na DJ WaxFiend.

SXSW Music Festival ni moja ya matamasha makubwa zaidi duniani ambalo hufanyika kila mwezi March huko Austin, Texas.

“Each year the SXSW Music Festival hosts a comprehensive mix of brand new, up-and-coming, international, and legendary artists performing in bars, clubs, parks, churches, hotels, and just about everywhere else you can imagine around Austin, Texas,” yanasema maelezo yake.

Katika tamasha la mwaka 2016, zaidi ya nchi 67 ziliwakilishwa na kuhusisha takriban watumbuizaji rasmi 2,200.

MWANAMITINDO AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA TRENI

Fredzania Thompson akiwa na mpenzi wake enzi za uhai wake

Mrembo wa miaka 19 aliyefahamika kwa jina la Fredzania Thompson amegongwa na treni wakati akipiga picha.

Fredzania alikuwa ni mwanafunzi wa chuo cha Blinn na alikuwa na ndoto za kuwa mwanamitindo mkubwa duniani. Mzazi wa mrembo huyo, Akamie Stevenson ameliambia shirika la habari la CNN, “Bila shaka hilo ndio jamba ambalo alilokuwa akilitaka kulifanya katika maisha yake. Ndiyo shughuli aliyoanza kuifanya siku aliyofariki dunia.”

Hata hivyo msemaji wa polisi wa Navasota, Justin Leeth amesema mpaka sasa hawajagundua tatizo lolote juu ya kifo hicho kama kilikuwa cha hila yoyote.

BREAKING NEWS : RAISI MAGUFULI AFUTA AGIZO LA CHETI CHA KUZALIWA KWA WATAKAOFUNGA NDOA

Breaking News: Rais Magufuli afuta agizo la cheti cha kuzaliwa kwa watakaofunga ndoa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelifuta agizo lililotolewa jana tarehe 16 Machi, 2017 na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe linalotoa sharti la kuwa na cheti cha kuzaliwa kwa watu wote watakaofunga ndoa kuanzia tarehe 01 Mei, 2017.

Rais Magufuli amefuta agizo hilo leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi kabla ya kuondoka katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kurejea Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Magufuli amesema Serikali haiwezi kuruhusu sharti hilo kutumika kwa kuwa litawanyima haki ya kuoa na kuolewa Watanzania wengi ambao hawana vyeti vya kuzaliwa, huku utaratibu wa kupata vyeti hivyo ukiwa bado unakabiliwa na changamoto nyingi kwa wanaohitaji.

Amesema mpaka sasa idadi ya Watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa ni chini ya asilimia 20 huku wengi wao wakiwa ni wananchi waishio vijijini ambako ni vigumu kupata vyeti hivyo, na wengine wakiwa ni waliozaliwa kabla ya kuanza kutolewa kwa vyeti vya kuzaliwa nchini mwaka 1961.

“Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania msiwe na wasiwasi wowote, endeleeni na utaratibu wenu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na kama kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na cheti cha kuzaliwa ndipo aoe ama aolewe nitamuelekeza Waziri wa Katiba na Sheria Harrison Mwakyembe apeleke Bungeni kikarekebishwe”-Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametoa wito kwa wanasheria kuziangalia vizuri sheria zinazohusiana na kuzaliwa na kifo na kuoa na kuolewa ili zisilete mkanganyiko kwa wananchi. Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kupata vyeti vyao vya kuzaliwa kama kawaida na amewataka viongozi wote kuwahamasisha wananchi kuwa na vyeti hivyo.

VIDEO: Rais Magufuli alivyotembelea eneo la ujenzi wa Ikulu Chamwino Dodoma, Bonyeza play hapa chini

Thursday, March 16, 2017

MWALIMU MBARONI KWA KUMWADHIBU MWANAFUNZI

Jeshi la Polisi mkoani Tanga linamshikilia mwalimu wa Shule ya Sekondari Mkwakwani kwa kumpiga na kumsababishia madhara ya kiafya mwanafunzi, Suleyman Mohamed (18).

Mwanafunzi huyo inadaiwa alichapwa viboko juzi asubuhi na mwalimu huyo wa zamu aliyekuwa akiwaadhibu wanafunzi waliochelewa na waliokuwa wakipiga kelele darasani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema tayari mwalimu huyo yuko mikononi mwa jeshi hilo na upelelezi wa suala hilo unaendelea.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa amewataka walimu kuwa waangalifu wakati wakiwaadhibu wanafunzi ili kukwepa madhara kwa wanafunzi.

“Tunalifuatilia kwa karibu tukio hili. Niseme kwamba tutachukua hatua stahiki ikithibitika kuwa umefanyika uzembe,” amesema Mwilapwa.

Baada ya kuchwapwa, mwanafunzi huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufani ya Bombo ikielezwa kwamba tayari amepatiwa rufaa kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

YANGA YAOTA BAO LA MAPEMA


Wachezaji wa Yanga wameondoka na lengo moja la kupata bao la mapema dhidi ya Zanaco katika mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga inahitaji ushindi au sare ya kuanzia mabao mawili katika mchezo huo ili kufuzu kucheza hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Zanaco jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita.

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro' alisema wanachokifikiria ni kufuzu kucheza hatua ya makundi katika Ligi ya mabingwa Afrika.

"Tunakwenda Zambia na mkakati wa kutoruhusu kufungwa, pia tuhakikishe tunapata bao la mapema ambalo naamini litatusaidia kuwachanganya washindani wetu," alisema Canavaro.

Mshambuliaji, Saimon Msuva aliwatoa hofu mashabiki wao na kusisitiza timu yao kutotolewa na Zanaco katika mashindano hayo.

"Mtizamo wetu ni kucheza hatua ya makundi na si vinginevyo, kama walipata bao Dar es Salaam, sisi tutashindwaje kufunga Zambia, kila kitu kinawezekana," alijinasibu winga huyo.

Kocha Juma Mwambusi alisisitiza benchi la ufundi limefanyia kazi mapungufu yaliyoonekana katika mchezo wa awali na kusisitiza kwamba wanakwenda Zambia kushinda na si vinginevyo.

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Kitwana Manara alisema ni rahisi Yanga kuitoa Zanaco endapowatatulia na kucheza kitimu.

"Bahati nzuri mechi hiyo haitakuwa na presha kubwa kwa Yanga kama itakavyokuwa kwa Zanacoambayo hiko nyumbani, watulie, wacheze mpira nafasi ya kushinda ipo," alisisitiza Manara.

MAUA SAMA :SIHITAJI KIKI KUTOA HIT



Mwanadada anayetamba na ngoma ya Main Chick, Maua Sama amesema yeye hategemei 'kiki' ili ku-'hit' bali uzuri wa kazi zake, na kuwataka wasanii wengine waache kutafuta 'kiki' ili kupata majina bali wajikite kwenye kutengeza kazi nzuri.

Akizungumza leo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Maua amesema kuwa wasanii wengi wamejikita kwenye kutafuta kiki badala ya kuwapa mashabiki ladha tofauti na kusisitiza kwamba dhana ya kiki inapaswa kufutika ili kila mtu afanye kazi nzuri.

"Ukifanya muziki mzuri lazima tu utapata jina, wala hakuna haja ya kiki, mfano mzuri mimi hapa ni msanii ambaye nimepata sapoti nzuri sana kwenye 'game' bila kuongelewa kwa mambo mabaya ya kiki, 'The real deal is good music' siyo skendo, japo mimi nina skendo ya kutoa ngoma kali siku zote". Maua aliwaambia Dullah na Jay R watangazaji wa kipindi hicho.

Sama ameongeza kwamba katika muziki wapo wasanii ambao wanafanya muziki mbaya lakini wanapewa nafasi kubwa ya kusikilizwa kutokana na kiki lakini hana chuki nao kwani pia watu wa aina hiyo wana mashabiki zao wanaopenda kuwasikiliza.

"Mimi nina wivu wa maendeleo sana, lakini sina chuki na watu wanaofanya muziki mbaya kwani hata wao wana masoko yao na wanauza ila kinachotokea kwangu nikimuona mtu katoa kazi mbaya mimi naingia kutengeneza 'hits' kali ili nipate soko zaidi". aliongeza Maua.

Hata hivyo Maua ameongeza kuwa msanii yoyote ambaye huandika nyimbo zake kipindi anapokuwa kwenye hisia yoyote ni wazi wimbo huo ukiachiwa hewani lazima uwe mkali kwa kuwa unakuwa umebeba uhalisia na hisia za kweli.

FAIDA ZA PILIPILI KICHAA KIAFYA NA KITIBA

Faida Za Pilipili Kichaa Kiafya Na Kitiba

Pilipili kichaa inaweza kustawi sehemu mbalimbali na inahitaji siku 100 za ukuwaji.

Hustawi zaidi kwenye mazingira ya joto na unyevunyevu.Mmea huu hukua kufikia urefu wa futi mbili hadi nne.

Ina wingi wa 

vitamini Apia ina vitamini B,vitamini E,vitamini C,Riboflavin,Potassium,Manganese.

- Jamii nyingi hususa Marekani na bara la Asia wana historia ya kutumia pilipili kichaa kama tiba.

Ni dawa yenye nguvu sana na matumizi mengi,

hutumika sana kwa kusafisha damu na kutoa sumu mwilini,pia hutumika kusisimua mzunguko wa damu nakuweka sawa uwiano wa tindikali(acid)mwilini.

Pilipili kichaa imetumika kwa maradhi tofauti tofauti ikiwemo moyo,

gauts,kupoozahoma,kikohozi,tonsilatis,kichefuchefu hemorhoids 
kwa miaka mingi huko Asia na mashariki ya mbali.

MAAJABU YA PILIPILI KICHAA;
1.Kutibu kidonda-Hii inaweza kuwa ni ajabu kwa walio wengi lakini ni tiba liyothibitishwa na imekuwa ikitumika miaka kadhaa iliyopita katika nchi mbalimbali.Sio tu kuzuia kutokwa na damu katika kidonda cha kujikata kama ilivyozoea kutumiwa na wengi huko majumbani kwa miaka mingi bali pia huzuia fangasi na bakteria kuingia katika uwazi wa kidonda hicho hutumika pia kuondoa sumu mwilini

2.Hufanya mwili kuweza kutumia vyema virutubisho vipatikanavyo kutokana na chakula

3.Husaidia uyeyushaji wa mafuta mwilini/Kuchoma mafuta

4.Pilipili ina antioxidants muhimu kama beta carotene,ina wingi wa vitamini A,C na K hebu tuziangalie vitamini hizo: a.Vitamini A husaidia kuweka sawa kinga ya mwili pia hutukinga na kansa na magonjwa ya moyob.Kazi ya vitamini C-ni kuzuia strock,magonjwa ya moyo,macho na kansa mbalimbali.Miili ya binadamu haiwezi kujitengenezea vitamini C,hivyo basi tunaweza kupata vitamini C kupitia chakula.c.Vitamini K-Husaidia katika ukuwaji wa mifupa,pia ni muhimu katika mzunguko wa damu.Pilipili zote huwa na Capsaicin ambayo kazi yake ni kupunguza maumivu,kuzuia kansa na magonjwa ya moyo.

5.Inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu

6.Huwasaidia watu wanene(over weight) au wanaougua ugonjwa wa kisukari.Hii ni kwa mujibu wa watafiti katika chuo kikuu cha Tasmania uliochapishwa katika American Joarnal of Clinical Neutition mwezi julai 2006.

7.Inasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa INSULIN kwa 60% baada ya kula chakula

8.Husaidia kupunguza maumivu na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa RHEMATOID na ARTHRITIS kupata nafuu

9.Husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja mwilini

10.Husaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua na kukufanya upumue kwa urahisi.

11.Husaidia kupunguza uwezekano wa kupatwa na saratani ya utumbo.

12.Husaidia kuongezeka kiwango cha METABOLIC ambayo husaidia kuchoma mafuta

13.Husaidia kuongezeka kwa kiwango cha METABOLIC kwa 23% ndani ya masaa matatu.

14.Husaidia kupunguza cholestro na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu.

Tuesday, March 14, 2017

KILIMO BORA CHA MIPAPAI

KILIMO BORA CHA MIPAPAI

MAHITAJI
Hali ya  hewa inayofaa kwa mipapai ni ya kitropik ambayo haina baridi kali na joto kiasi . Udongo usiotuamisha maji maji yakisimama kwa masaa 48 tu mpapai unaweza kufa, wenye ruruba ya kutosha kwa sababu mipapai haina mzizi mkuu haihiyaji udongo wenye kina kirefu,

 kipindi cha jua kali mpapai usiachwe zaidi ya wiki 8 bila kumwagiliwa maji kama hakuna mvua ingawa wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hii huongeza ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema sokoni

Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mwingi kwani huvunjika kirahisi, kama unashamba la mipapai itakubidi kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka shamba lako, miti kama miparachichi, migravilea, vibiriti (leucaena Spp) na miembe pia inafaa. Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai kwa mita 10 mpaka 20 juu zaidi

Kuendelea kupanda mipapai kwenye shamba moja kunaweza kusababisha usugu wa magonjwa, nashauri baada ya miaka 3 – 5 ubadilishe zao hili angalau kwa msimu mmoja ili kuua mzunguko wa magonjwa

Mipapai inaweza kuchanganganywa na miembe na mimea jamii ya michungwa, pia mazao ya msimu kama mahindi, mtama, ufuta , alizeti  na  mboga mboga yanaweza kulimwa

Kwa kaida kwenye mipapai kuna mipapai dume, majike  na yenye jinsia zote(multiplesex/hermaphrodite) ambayo huwa na mapapai marefu zaidi, na pia kuna isiyoeleweka ambayo huwa na mapapai mafupi sana

MBEGU
Kusanya mbegu toka kwenye mapai makubwa na yaliyo komaa na kuiva, kausha mbegu vizuri kbla ya kupanda, kama utapata mbegu za  kununua ni vizuri zaidi, baada ya kukausha hakikisha unazipanda ndani ya wiki moja

KUOTESHA MBEGU
Kuna wanaopendelea kuotesha mbegu kwanza na kisha kuhamishia miche shambani, sehemu ya kuoteshea iandaliwe miezi miwili kabla, mbegu zioteshwe kwenye kina kati ya sentimeta 1 – 2 chini ya udongo wenye rutuba au pakiti za plastiki,

kiwango bora cha joto ni sentigredi 21 – 27 na itachukua kati ya wiki 1 – 4 kwa mbegu kuota, kwenye kila pakiti weka mbegu 2 – 3.

 Panda mbegu zako kwenye kitalu kwa umbali wa sentimeta 3 toka shimo hadi shimo na sentimeta 15 kati ya mistari, hakikisha maji hayatuami kabisa, pia unaweza kupiga dawa ya copper oxychloride gramu moja katika lita moja ya maji ilikukinga miche yako na fangasi

UOTESHAJI WA MOJA KWA MOJA
Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea ya kuku sehemu ya kupandia, mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia kukinga mipapai na magonjwa. Panda mbegu 3 – 5 kila shimo maana miche mingine inaweza kufa kwa magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota dume

KUHAMISHA MICHE TOKA KWENYE KITALU
Miche ihamishiwe shambani ikiwa na urefu wa sentimeta 20 – 40, kama udongo unatuamisha maji panda kwenye matuta yenye urefu wa sentimeta 40 – 60 mashimo yawe na ukubwa wa sentimeta 45 upana na sentimeta 30 kina na shimo lichanganywe na udongo na samadi bila kuacha kisahani cha maji, umbali ni mita 3 kwa 3 kwani mipapai inahitaji jua la kutosha

KUPUNGUZA MIPAPAI
Baada ya miezi 3 – 5 baada ya kupanda mipapai itatoa maua na hapo jinsia ya mipapai itajulikana na mingine itabidi ipunguzwe na hasa midume, mipapai yenye jinsi zote inatakiwa isizidi asilimia 10 – 20 na midume ibaki mmoja katika kila mijike 25, mimea yenye magonjwa pia inabidi ing’olewe

RUTUBA YA UDONGO
Weka kiasi chakilo 2 – 5 za samadi kwenye kila mpapai kwa mwaka ili kuongeza ukuaji na uzazi, mabaki ya mimea yanaweza pia kuwekwa kama matandazo na h ii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu usipotee.

MAGUGU
Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili kuzuia uoataji wa magugu, magugu yang’olewe yakiwa machanga na epuka kuchimbua chini sana maana mizizi ya mipapai huwa juu juu, njia nzuri ni kuweka matandazo kwenye shamba lote ili kuzuia outaji wa magugu

UANGALIZI

Mipapai iangaliwe dhidi ya magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au kufukiwa chini ikiwa itabainika kuwa na maonjwa, piga dawa dhidi ya magonjwa ya fangasi na virusi mara yanapoibuka ili kuongeza uzaaji nakipato chakoOndoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na hii ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.Ondoa mapapi yote ambayo yatakuwa hayakuchavuliwa vizuri na acha yale yenye afya tuWeka miti ya kuegemea kama mpapai utazaa matunda mengi na hasa wakati wa upepo mwingi ili kuzuia mipapai isivunjikeMipapai ikitunzwa inaweza kuishi mika mingi, ila kwa ajili ya mazao bora ondoa mipapai na upande mingine baada ya kila miaka mitatu (3) kwani mpapai unapo kuwa mkubwa basi rutuba yote huishia kwenye mti wenyewe

HISTORIA YA JESHI LA POLISI LA TANZANIA

HISTORIA YA JESHI LA POLISI LA TANZANIA

MUUNGWANA BLOG / 10 hours ago


HISTORIA YA JESHI LA POLISI – TANZANIA

1885; Wajerumani walifika Tanganyika ili kutawala, waliunda kikundi cha watu kilichofanya kazi ya Polisi.

1916;  Vita kuu ya kwanza ikiendelea Ulaya na Afrika, kundi la Maafisa 31 (NCO) kutoka Afrika Kusini wakiwa na silaha (Rifle) walifika Tanganyika kufanya kazi za Polisi.

1919; Tarehe 25 August 1919 Serikali ya Kiingereza ilitangaza katika Gazeti la Serikali No.Vol.1 No.21-2583 kuwa Jeshi la Polisi Tanganyika limeanzishwa rasmi. Makao Makuu ya Jeshi hilo yalikuwa Wilayani Lushoto chini ya uongozi wa Major S.T DAVIS.

1921; Kundi lingine la Wakaguzi kutoka Ulaya lilifika nchini Tanganyika kuanzisha shule ya Mafunzo ya Polisi huko Morogoro.

1925; Kituo cha kwanza rasmi cha Polisi nchini kilifunguliwa huko Lupa Tingatinga kwenye machimbo ya dhahabu Chunya.

1930; Makao Makuu ya Polisi yalihamishwa kutoka Lushoto kuja Dar es Salaam.

1949; Motorized Company sasa Field Force Unit (F.F.U) kilianzishwa nchini kurejesha amani penye vurugu.

1949; Vijana mbalimbali wa Kiafrika toka shule mbalimbali za Sekondari Nchini walichaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi na kuwa Wakaguzi chini ya uangalizi (Probation Inspectors).

1952; Kikosi cha Mawasiliano (Signals Branch) kilianzishwa katika Polisi bila kutumia nyaya za simu.

1958; Askari wa Polisi wa Kikie (Women Police) walijiunga na Jeshi la Polisi chini ya uongozi wa Miss. Payee.

1961; Tarehe 9 Desemba, 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake. Baada ya uhuru, Jeshi la Polisi lilianza kubadili mwelekeo toka katika kutumikia Wakoloni na Walengwa wakawa ni Wananchi kwa mujibu wa sera za Serikali ya Wananchi.

1962; Kwa mara ya kwanza nafasi ya Kamishna wa Polisi aliyekuwa Mzungu Mr. M.S Wilson – C.P, ilichukuliwa na Mwafrika
Mr. Elangwa Shaidi – C.P.

1962; Maafisa 10 Waafrika waliteuliwa kuchukua nafasi za wakuu wa Polisi wa Mikoa (Regional Police Commanders).

1964; Tarehe 26/04/1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana na hivyo kuunda Tanzania. Kwa hiyo Mr. Elangwa Shaidi alipandishwa cheo nakuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IJP).

Alisaidiwa na Makamishna watatu wa Polisi ambao ni:-
 1.  Mr Edington Kisasi  Kamishna wa Polisi Zanzibar
 2.  Mr. Hamza Azizi  Kamishna wa Polisi Bara.
 3.  Mr. Akena  Kamishna wa Polisi CID.

 
VIONGOZI WA JESHI LA POLISI WAKATI WA UKOLONI HADI UHURU.
1916 – 1920 Major S.T. Davis.
1920 – 1929  E.F. Brown.
1929 – 1933  G.H. Kiram.
1933 – 1942  F.A.B. Nicholl
1942 – 1949  E.B. Birthray.
1949 – 1951  W.A. Muller.
1951 – 1958  R.E. Fouler.
1958 – 1962  G.S. Wilson.
1962 – 1964  E.N. Shaidi.

 MAINSPEKTA JENERALI WA JESHI LA POLISI TANGU MUUNGANO HADI LEO.

1964 – 1970

Elangwa N. Shaidi

1970 – 1973

Hamza Azizi.

7/8/1973 – Aug 1975

Samweli H. Pundugu.

8/8/1975 – Nov 1980

Philemon N. Mgaya.

2/11/1980 – 30/11/1984

Solomoni Liani.  

1/12/1984 – 3/5/1996

Harun G. Mahundi.

4/5/1996 – 2/3/2006

Omar I. Mahita.  

3/3/2006 - 30/12/2013

Saidi A. Mwema.

 

01/01/2014-Hadi Sasa  

Ernest J. Mangu

WAKURUGENZI WA IDARA YA UPELELEZI (CID) TANGU 1960 HADI LEO.

17/9/1960 - 1/9/1961     M. J. McKinlay ACP.1/9/1961 - 19/7/1962     K.F.J. Flood SSP.19/7/1962 - 6/12/196      R. T. L. Egan ACP.6/12/1962 - 2/8/1967     E. E. Akena ACP.2/81967 - 13/11/1967     R.S. Kaswende ACP.13/11/1967 - 4/6/1968    N.G.M. Sawaya SACP.4/6/1968 - 2/9/1968     A.R.Shungu SACP.2/9/1968 - 23/9/1970     N.G.M. Sawaya SACP.23/9/1970 - 21/5/1973    S.H.Pundugu CP.21/5/1973 - 28/5/1975    B.M. Omari CP.28/5/1975 - 14/8/1975    F.M. Mtono SACP.14/8/1975 - 15/2/1977    H.M.Lyimo CP.12/2/1977 - 21/5/1981    M.Mwingira CP.21/5/1981 - 6/3/1985     J.M.Lemomo CP.7/3/1985 - 30/6/1992     A.A.B.Mwaitenda CP.22/10/1992 - 3/5/1996    E.A.Man CP.4/5/1996 - 2/3/2006     Adadi Rajab CP.3/3/2006 - 14/07/2013    R.S. Manumba  CP.15/07/2013 - 2014         I.N. Mngulu  CP SASA                       Diwan  Athuman   CP



MUHONGO: MNAOPATA UMEME REA MSAIDIE FIDIA

Muhongo: Mnaopata umeme REA msidai fidia

WANANCHI wanaoishi maeneo yanayopitishwa miundombinu ya umeme vijijini wametakiwa kutodai fidia ili wafikishiwe huduma hizo kwa maendeleo yao.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya mradi wa umeme vijijini chini ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA) mkoani Pwani uliofanyika Mlandizi wilayani Kibaha.

Alisema fedha zilizotengwa takribani shilingi trilioni moja kwa ajili ya mradi huo, hazitakuwa sehemu ya fidia kwa ajili ya maeneo utakapopita umeme huo.

“Bajeti iliyopangwa kutumika kwenye awamu hii (REA III) kwa nchi nzima ni mara tatu ya bajeti iliyopita; lengo ni kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma za umeme hasa vijijini. Fedha hizo ni za ndani hivyo lazima wananchi nao wajitolee pasipo kudai fidia,” alisema.

Alisema miradi ya REA ilipoanza mwaka 2007 wananchi waliokuwa wakitumia umeme walikuwa asilimia 2 na hadi kufika Desemba 2017 itakuwa imefikia asilimia 49.5 huku gharama zikibebwa na Serikali.

Alilitaka Shirika la Umeme (Tanesco) kutoa kipaumbele kwa Mkoa wa Pwani ili wawekezaji wapate umeme wa kutosha kutokana na mkoa huo kuwa na viwanda vingi vikihitaji umeme ambao ni injini ya maendeleo.

Akielezea kuhusu mradi huo mkoani Pwani, Mkurugenzi wa REA, Gisima Nyamo-Hanga alisema, utatekelezwa katika vijiji 55. Awamu iliyopita vilifikiwa vijiji 150.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema mkoa huo unakabiliwa na tatizo la wateja kuhitaji kuunganishiwa umeme, lakini vifaa kama vile nguzo, mita na nyaya ni vichache.

Aliomba mkoa huo uongezewe nguvu ya umeme kwani wanapata megawati 38 hadi 40 huku mahitaji yakiwa ni megawati 60 kwenye vituo vidogo vya Mlandizi, Chalinze na Mkuranga.

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete alisema tathimini ilifanyika katika baadhi ya vijiji kukiwa na mahitaji kidogo lakini sasa mahitaji yameongezeka.

Naye Mbunge wa Kibaha Vijijini, Abou Jumaa alisema baadhi ya vijiji vina changamoto ya ukosefu wa umeme, hivyo kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo.