Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge ametoa siku saba kwa Manispaa ya Songea kuvunja nyumba ya kulala wageni ya tulivu iliyojengwa kwenye chanzo cha maji na kusababisha tatizo la maji katika mtaa wa miembeni mkoani ruvuma.
Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo baada ya Mwenyekiti wa mtaa wa Miembeni Bw. Christian Komba kulalamikia viongozi wa Manispaa ya Songea kutochukua hatua za kubomoa jengo hilo ambalo lina vibanda vya maduka na nyumba ya kulala wageni mita 20 kutoka kwenye chanzo cha maji.
Kwa upande wake mmiliki wa nyumba huyo Bw.Imani Mbugi amesema kuwa ni kweli amejenga nyumba hiyo kwenye chanzo cha maji lakini kuna nyumba zaidi ya kumi zilizojengwa kwenye chanzo hicho lakini anashangaa anasakamwa yeye tu.
No comments:
Post a Comment