Saturday, April 30, 2016

P DIDDY ATANGAZA KUSTAAFU MUZIKI NA KUHAMIA KWENYE UIGIZAJI

Rapper mkongwe kutoka Marekani, Sean John Combs maarufu kama P Diddy amesema anataka kustaafu kwenye muziki na kujikita zaidi kwenye uigizaji.

P Diddy amesema muda siyo mrefu ataachia albamu yake ya mwisho na kuachana na muziki na kufanya kazi ya filamu. Akiongea na Ace Showbiz, Diddy amesema, “I’m going to put out my last album and devote 100 percent of my time to doing films. I want to stop at a great place.

And a final album is a great place to stop. I want to take a victory lap, to do a world tour and really enjoy it one last time.” P. Diddy aliongezea kuwa, “When I’m gone, only the songs will survive. I know I’m making music that will live on. I don’t go into the studio just to be hot or to hear myself on the radio.”

Diddy ni mmiliki wa lebo ya Bad Boys Entertainment, lakini pia ni mmoja kati ya wasanii matajiri duniani akiwa mpaka sasa anautajiri wa zaidi ya dola milioni 735.

MR BLUE : SUGU AMEHATARISHA NDOA YANGU

MKALI wa Muziki wa Hip Hop, Bongo Kheri Sameer ‘Mr Blue’ ameendelea kumporomoshea lawama Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye pia ni msanii wa Muziki wa Hip Hop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’

kuwa usumbufu aliokuwa anampa ili kuiachia ngoma yake ya Freedom ulimsababishia ‘rabsha’ ndani ya ndoa yake. Shutuma hizo anazozitoa Blue ni mwendelezo wa ‘drama’ inayoendelea kati yake na Sugu ambayo kwa sasa ndiyo habari ya mjini kufuatia madai ya Blue kuwa mheshimiwa huyo alimzunguka kwa kuuchukua wimbo wake huo ambao mwanzo yeye alimshirikisha,

akaurekodi upya huku akifuta mashairi yake lakini kama haitoshi ‘akashuti’ video, jambo ambalo Blue analiona kuwa ni uonevu. “Kwanza Sugu alinisababishia matatizo ndani ya ndoa yangu mpaka nikawa sipokei simu zake.

Alikuwa ananipigia simu kila muda na kila siku akiuliza ‘project’ inatoka lini hadi mke wangu akawa anauliza kuna nini kati yetu.  

Mwanzoni nilimweleza hali halisi lakini kwa namna Sugu alivyokuwa ananisumbua ilifika hatua mke wangu akadhani kuna jambo lingine tofauti, kukawepo na rabsha za hapa na pale lakini sasa nimeweka mambo sawa,” alisema Blue.

Alipotafutwa Sugu kuhusu suala hilo, hakupokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu lolote.

ALIYEJIFANYA OFISA MSTAAFU WA USALAMA WA RAIS MSTAAFU,JAKAYA KIKWETE ATUPWA JELA MIAKA 12

Mahakama ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, imemhukumu kwenda jela miaka 12, Qasama Machibya aliyejifanya ofisa usalama wa Taifa kwenye ziara ya Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete mwaka 2013.

Kabla ya hukumu, mshtakiwa alijitetea mahakamani hapo kuwa kitambulisho alichokutwa nacho siyo chake na anashangaa kuona kuna picha yake na jina lake.

Alidai kuwa hizo ni mbinu za polisi kumminya, hivyo aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu na kwamba ana ugonjwa wa Ukimwi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Gabriel Kurwijila alisema utetezi wa mshtakiwa hauifanyi mahakama kutomtia hatiani kwa kuwa hana cheti cha ugonjwa.

Alisema kutokana na mahakama kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka uliowasilishwa inamtia hatiani kwa makosa matatu. Kurwijila alisema kosa la kwanza ni kughushi nyaraka ya Serikali hivyo, atakwenda jela miaka mitano na kosa la pili la kujifanya ofisa usalama wa Taifa kifungo chake ni miaka miwili.

Alisema katika kosa la tatu la kuudanganya umma kwa kutoa nyaraka iliyoghushiwa hivyo, atatumikia adhabu gerezani miaka mitano. Mwendesha Mashtaka wa Polisi,

Elias Mgobela alisema mshtakiwa alikamatwa wakati Kikwete alipokuwa akitarajia kuhutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara.

CHEMSHA BONGO YA LEO

Mtoto aliyekuwa karibu na marehemu aliulizwa 'ni nani kwako aliyefariki ?  akajibu 'kaka mkubwa wa mjomba wake na marehemu ni mjomba wangu'  swali 'je marehemu ni nani kwa mtoto?'.

YANGA MBELE KWA MBELE

Yanga imeendelea kushinda mechi zake za ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga Toto Africans ya jijini Mwanza kwa magoli 2-1 kwenye uwanja wa CMM Kirumba, Mwanza.

Toto walianza kupata goli la kwenye mchezo huo lililofungwa na William Kimanzi dakika ya 39 kipindi cha kwanza lakini goli hilo likasawazishwa na Amis Tambwe dakika ya 50 kipindi cha pili.

Yanga walijihakikishia pointi tatu kwenye mchezo huo kupitia beki wao wa kulia Juma Abdul dakika ya 78 na kifanya Yanga kufikisha pointi 65 baada ya kucheza michezo 26 ya VPL.

ABIRIA WANUSURIKA KUFA KATIKA AJALI YA NDEGE MJINI BUKOBA

Watu kadhaa wamenusurika  kufa baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Auric Air waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika Uwanja wa Ndege wa Manispaa ya Bukoba ilipokuwa ikitua na rubani kupoteza uelekeo  kama inavyo onekana pichani. Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Jijini Mwanza ,tukio limetokea majira ya saa nne asuhuhi ya leo Jumamosi April 30,2016.

OPERESHENI ZA VICHWA 55 ZAFANIKIWA BUGANDO

Jumla ya watoto 55 wamefanyiwa upasuaji katika kambi ya tiba ya watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi,

iliyowekwa katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza siku nne mfululizo, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa nalo, chini ya udhamini wa taasisi ya GSM Foundation.  

Zoezi litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne zinazotarajiwa kufanyika Tanzania nzima. Akiongea wakati wa kufunga kambi hiyo rasmi jioni ya leo,

Daktari Bingwa wa upasuaji na mifupa kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, Dk Othman Kiloloma(Pichani Juu) ambaye pia ni mratibu wa kambi hiyo aliishukuru taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.

Dk Kiloloma aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima,

wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu. Cha kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za matibabu.

Mpaka jioni ya leo, ambayo ni siku ya nne tangu kuanza kwa kambi hii, jumla ya watoto 55 walikuwa wameshafanyiwa upasuaji, ambapo siku ya kwanza, walifanyiwa watoto 16, siku ya pili wakafanyiwa watoto 17, siku ya tatu wakafanyiwa watoto 12, na leo wamefanyiwa watoto 10.

Mratibu huyo ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI), Dk Othman Kiloloma, amebainisha kwamba changamoto kubwa inayotokea kwa jamii linapokuja suala la watoto wenye vichwa vukubwa na mgongo wazi ni gharama za upasuaji,

ambapo gharama ya upasuaji kwa mtoto mmoja ni kati ya shilingi laki saba za kitanzania mpaka Milioni moja.
“Watoto wengi huzaliwa katika mazingira duni na wazazi wasiokuwa na nguvu ya kiuchumi, hali inayosababisha wengi wao kuwaficha ndani huku wakiwahusisha na imani za kishirikina”, alifafanua Dk Kiloloma.

Dk Kiloloma amesema zaidi ya watoto 4000 huzaliwa kila mwaka wakiwa na tatizo la kichwa kikubwa, lakini wanaorudi Hospitali kwa ajili ya tiba nhawazidi laki nne, swali kubwa ambalo jamii hujiuliza ni kuhusiana na watoto ambao hawafiki hospitalini huishia wapi? Kwa upande wake, Halfan Kiwamba, Afisa Mawasiliano wa Taasisi ya GSM Foundation ambao ndio wadhamini wakuu wa kambi hizo amesema, taasisi yake imeamua kuokoa maisha y watoto hao ambao ni nguvukazi ya taifa la kesho na inalifanya hilo ikiwa ni moja ya mikakati yake katika kurudisha fadhila kwa jamii ya kitanzania ambao ni wateja wakubwa wa bidhaa za GSM.

Kiwamba amesema taasisi yake ina lengo la kuhakikisha kwamba wananchi wa Tanzania hasa watoto ambao ni wa taifa ya kesho wanao msingi wa nguvu kazi kwa ajili ya maisha yao ambapo vitu vikubwa ni elimu boira pamoja na Afya. Kwa upande wake Meneja wa Taasisi ya GSM Shannon Kiwamba amesema wakati mwingine ni vigumu kuingia katika maisha ya kila mwananchi na kumsaidia mahitaji yake, lakini akiwa na uhakika wa Afya na elimu anaweza kwenda mbali akijumlisha na jitihada zake.

Hivyo amewaomba watanzania kujitokeza wanaposikia taasisi yake inatoa huduma ili kufaidika nayo. Kambi ya tiba ya GSM inaondoka kesho Mwanza kuelekea Shinyanga ambapo itaweka kambi kwa siku tatu.

MAKONDA ASEMA HATAKI KUONA WASANII NYUMBANI KWAKE .. KWA SABABU YA KUTOMUUNGA MKONO KWENYE KAMPENI YA USAFI

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema hataki kuwaona nyumbani kwake wasanii ambao wamekacha kuhudhuria kampeni yake ya usafi ambayo imezinduliwa Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Paul Makonda ameonesha kusikitishwa na idadi ndogo ya wasanii waliojitokeza kuunga mkogo kampeni hiyo.

“Lakini nashukuru wasanii wote ambao wamejumuika nasi, na kwa kweli hiki ni kipimo cha kuwatambua marafiki zangu wa kweli ni wapi.

Na mimi niwaambie tu, sitaki kuona msanii yoyote nyumbani kwangu ambaye hawezi kuniunga mkono kwenye mambo yangu ya maendeleo,” alisema Makonda.

“Sitaki hiyo tabia, nimemuona Steve Nyerere hapa amekuja akiwa amechelewa hilo ni onyo, ukirudia tena nakushughulikia. Huwezi kuwa rafiki yangu alafu kwenye mambo kama haya huhangaiki, wengine wanataka waombwe, eti mbona hujanipigia simu kuniomba nipost, we nani?

. Swala la usafi siyo la serikali ni swala la kila mtu,” aliongeza Makonda. Wasanii ambao walihudhuria uzinduzi huo ni, Mchizi Mox, Yamoto Band, Diamond na team ya Wasafi, Mwasiti, Queen Darleen, Salam TMK pamoja na Steve Nyerere wa bongo movies.

Katika hatua nyingine Makonda amevitaka vyombo vya usafiri jijini Dar es salaam kuwa na vifaa vya kuwekea uchafu. Pia wamewataka wafanyabiashara siku ya jumamosi, kufungua maduka yao saa 3 asubuhi ili muda wa asubuhi wautumie kwa ajili ya kufanya usafi.

MASOGANGE AKUTWA HUKO SAUZI BARABARANI SIJUI ANAFANYA NINI??

CHEMSHA BONGO YA LEO

Swali ni "Kuna neno moja ambalo limebeba jina la mnyama, ,Jina la mtu na jina la mkoa. Je, hilo ni neno gani?

LOWASSA ASIMAMISHWA NJIANI, DUMILA MORO, NA KUMWITA RAIS

EDWARD .LOWASSA aliposimamishwa na wakazi wa Dumila mkoani Morogoro akielekea jijini Dar,na kuitwa jina la rais,rais,wananchi hao walikuwa na kiu ya kutaka kumwona na kumsikia juu ya hatma yake kisiasa!

MSIKITI WAPOROMOKA NA KUWAUWA WATU 15 MOGADISHU

Msikiti uliokuwa ukikarabatiwa umeporomoka nchini Somalia na kuwaua watu 15 na kuwajeruhi wengine 40.

Kisa hicho kilitokea katika msikiti mmoja wa mjini Mogadishu wakati wa ibada ya Ijumaa. Hatahivyo maelezo yalitolewa siku ya Jumamosi.

Mamia ya watu walidaiwa kuwa ndani ya msikiti huo wakati ulipoporomoka na wengine wanaaminika kuwa chini ya vifusi vya jengo hilo la ibada.

Muhandisi mmoja aliyekuwa akiufanyia ukarabati misikiti huo alikamatwa kwa tuhuma za uzembe,vyombo vya habari vya eneo hilo vimeripoti.Mvua kubwa imenyesha katika eneo hilo katika siku chache zilizopita.

Serikali ya Somalia inadhibiti Mogadishu na miji mingine,lakini wapiganaji wa al-Qaeda wanaoshirikiana na kundi la wapiganaji wa al-Shabab wanatawala maeneo mengi ya mashambani.

Zaidi ya wanajeshi 22,000 wa Umoja wa Afrika na polisi wamepelekwa nchini humo kuilinda serikali.

URUSI NA MAREKANI ZALAUMIANA KUHUSU UCHOKOZI WA NDEGE

Urusi inasema kuwa ilikuwa na haki kuikabili ndege moja ya Marekani katika bahari ya Baltic siku ya Ijumaa.

Hatua hiyo inajiri baada ya Marekani kusema kuwa ndege ya kijeshi ya Urusi ilizua hofu ya kiusalama baada ya kuzunguka karibu na ndege yake.

Urusi inasema kuwa ndege hiyo ya Marekani ilikuwa imezima kifaa chake cha kurusha ishara zake ambazo husaidia wengine kuitambua.

Ni kisa cha pili katika bahari ya Baltic mwezi huu ambapo Marekani imezishtumu ndege za Urusi kwa kupaa kwa uchokozi. ''Ndege zetu zote za Urusi zinafuata sheria za kimataifa kuhusu utumiaji wa anga'',taarifa ya wizara ya Ulinzi nchini Urusi ilisema.

''Ndege za Marekani zina mambo mawili:Zisiruke karibu na mpaka wetu ama ziwashe ishara ili kutambulika''.

Ndege za Marekani mara kwa mara hujaribu kupaa karibu na anga ya Urusi bila taa zinazoonyesha ishara taarifa hiyo ilisema.

Katika kipindi cha miezi 18 iliopita,Urusi pia imeshtumiwa kwa kutekeleza kitendo kama hicho katika bahari ya baltic pamoja na karibu na maji ya Uingereza.

Friday, April 29, 2016

CHEMSHA BONGO YA LEO

Mtoto aliyekuwa karibu na marehemu aliulizwa 'ni nani kwako aliyefariki ?  akajibu 'kaka mkubwa wa mjomba wake na marehemu ni mjomba wangu'  swali 'je marehemu ni nani kwa mtoto?'.

MATATIZO KWA WANAUME NA JINSI YA KUYAKABILI

Viungo vya uzazi vya mwanaume vimegawanyika katika sehemu kuu mbili. Kuna viungo vya uzazi vya nje na vile vya ndani.

Viungo vya uzazi vya nje ni vile tunavyoviona kama uume na mfuko wa korodani. Viungo vya uzazi vya ndani ni mirija ya mbegu za kiume ambacho ni kifuko cha akiba cha mbegu na tezi dume au tezi ya ‘Prostate’.

Viungo hivi vyote vina umuhimu mkubwa kwa mwanaume katika kumfanikisha kuweza kufanya tendo la ndoa kwa ufanisi pamoja na uzalishaji wa mbegu za kiume.

Matatizo yakitokea katika sehemu yoyote hapo humuathiri mwanaume inategemea wapi athari ipo. Athari ni kushindwa kufanya tendo la kujamiiana na kuzalisha mbegu au manii.

Manii ni majimaji yanayolisha mbegu za kiume na kuzisafisha na huzalishwa na tezi dume.

Chanzo cha tatizo Hutegemea mahali linapoathirika. Matatizo hutokea popote katika viungo vya uzazi vya mwanaume iwe nje au ndani.

Uume Matatizo kwenye uume ni kupata maumivu katika njia ya mkojo kutokana na maambukizi au kuumia njia ya mkojo.Mwanaume mwenye tatizo hili hulalamika maumivu wakati wa kukojo, muwasho katika njia ya mkojo na mkojo kutotoka vizuri.

Kuumia kutokana na kuingiziwa mrija wa mkojo mara kwa mara katika njia ya mkojo. Maambukizi inaweza kuwa Yutiai za mara kwa mara na magonjwa ya zinaa kama kisonono na mengine.

Ugonjwa wa kaswende huathiri sehemu ya nje ya uume zaidi ambapo vipele na vidonda vyenye muwasho na maumivu  hujitokeza mara kwa mara.Tatizo hili hujitokeza kama tulivyoelezea hapo juu na huchunguzwa katika vituo vya afya.

Ni vema kuwahi hospitali endapo utahisi dalili hizo kwani ukichelewa itasababisha madhara makubwa mojawapo ni kuziba kwa njia ya mkojo, kusambaa kwa maambukizi katika viungo vingine kama kibofu cha mkojo, korodani na tezi dume.

Athari nyingine ni ugumba kwa mwanaume. Tezi dume Tezi dume ipo kwa ndani jirani na kibofu cha mkojo na mfuko wa haja kubwa. Kazi ya tezi hii ni kutengeneza na kutunza manii.Tezi dume hupatwa na matatizo mbalimbali kama maambukizi na kutanuka hadi kuwa saratani.

Kutanuka huanzia katika umri wa miaka arobaini na tano na huanza taratibu sana. Maambukizi ya tezi dume hutokana na muendelezo wa maambukizi toka katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu cha mkojo na kufika kwenye tezi dume.

Tezi dume ikitanuka huanza dalili za uhafifu katika utoaji wa mkojo ambapo mkojo hautoki vizuri au unashindwa kabisa kutoka. Tezi hii inapotanuka inabana shingo ya kibofu cha mkojo. Dalili dhahiri za ugonjwa huu hujitokeza kadiri umri unavyoongezeka, hasa zaidi ya miaka hamsini na sitini. Endapo utachelewa kupata tiba hadi umri wa zaidi ya miaka sitini, kuna hatari ya tezi hiyo kuwa kansa au saratani.

Uchunguzi wa awali wa tezi dume hufanyika kawaida katika  kliniki kubwa kwenye hospitali za mikoa na wilaya kabla dalili hazijajitokeza rasmi. Kuwa na tabia ya kufanya uchunguzi mara kwa mara hasa unapofikia umri wa miaka 45 na zaidi.

Kadiri umri unavyoongezeka ndipo dalili zinapojitokeza taratibu hadi tatizo linakuwa kubwa. Endapo utawahi kufanyiwa uchunguzi mapema , basi tezi dume inaweza kutibika au kuzuia isitanuke na ukaepuka upasuaji na saratani.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA BIASHARA

Yamkini unataka kufanya biashara, au umekwishanza kufanya ila katika biashara unayofanya mara nyingi huoni matokeo ambayo ulikuwa unategemea.

Hii ni kutoka unafananya au ulifanya biashara kwa kutokufanya uchunguzi wa kina juu ya biashara hiyo. Unajua ni kwanini  biashara yako haisongi mbele? Shusha pumzi kisha twende sawa kwani leo ndio siku ya pekee kwako kuweza kuona unapata faida endapo utaisoma Makala hii kwa umakini na kuielewa kisha kuiweka katika matendo, kwani inawezekana ukawa ni mfuatiliaji mzuri lakini sio mtendaji mzuri ila nikuombe tena kwa mara nyingine utakachokisoma hapa kiweke katika matendo na utakwenda kuona matokeo yake.

Yafuatayo ndiyo mambo ya kuzingatia katika biashara. 1. Elewa biashara yako vizuri.

Mara nyingi inawezakana unashindwa kuona unapata mafanikio hii ni kwa sababu hauifamu biashara yako vizuri. Inawezekana ukawa haujanielewa twende sawa,

kuifamu biashara hapa nina maana ya kwamba watu wengi tunafanya biashara  kutokana na kusikia kwa watu ambao wamesema kuwa biashara fulani inalipa, na baada ya kusikia hayo unakwenda moja kwa moja kwenda kuifanya matokeo yake biashara hiyo inakufa.

Hii unajua ni kwanini ni kutokana  na hukufanya utafiti wa kutosha juu biashara hiyo. Inawezekana kweli biashara fulani ikawa inalipa na wewe ukagundua hilo jambo la msingi jaribu kuchunguza ni mbinu zipi ambazo wanazutumia mpaka waseme hivyo.

Pia ukumbuke ya kwamba kusikia peke yake haitoshi, moja ya sifa kubwa ya mjasiliamali ni lazima ajue kufanya uchunguzi wa kutosha wa jambo lolote kabla hajaanza kulifanya.

Wito wangu kwako Ni kwamba itambue biashara yako vizuri hii itakusaidia kujua changamoto na jinsi ya kukabiliana nazo. Kuna mwandishi mmoja aliwahi kuandika ya kwamba usiishie kusema ndoto yangu ni kuwa hivi na vile bali anza kufanya sasa, ndoto hiyo kuwa kweli. Amini ya kwamba unaweza kuifanya ndoto kuwa kweli ndani ya muda mfupi. 2.

Simamia na thibiti biashara yako. Hili jambo la msingi zaidi kuliko hata kula anashangaa! Usishangae wala hujakosea kusoma upo sawa kabisa. Unajua kwa nini nimesema hivyo watu wengi biashara nyingi hazina Maisha marefu hii ni kutoka hatuna usimamizi wa mzuri wa shughuli zetu.

Tupo baadhi yetu tunaendesha biashara kubwa ambazo kwa siku zinaingiza pesa nyingi kwa kuwa tunakwepa kuwalipa wafanyakazi mishara mikubwa tunajikuta tunawatafuta watu wanyonge wawe wasimamizi wa biashara hizo na kuwalipa mishara midogo na kwa kuwa wafanyakazi hao wanajua wewe bosi unaingiza shilingi ngapi mwisho wa siku wanaona unawalipa mishara midogo wanaanza kukuibia.

Kitu cha msingi ni kwamba jaribu kuwajenga wafanyakazi wako waione biashara yako ni sehemu ya maisha yao. Wapo baadhi ya wafanyakazi katika biashara endapo atanunua hata nguo mpya bosi wake humuuliza hiyo nguo umeitoa wapi unashangaa huo ndio ukweli, wewe bosi ukiishi katika misingi hiyo ni lazima utaibiwa tu kila siku na biashara yako haitakuwa ikisonga mbele maana kila mfanyakazi unayemuajiri utamuona jipu tu.

Kumbuka ya kwamba kuwa biashara yako inaweza kukua kwa kumfanya mfanyakazi kwa kumfundisha mambo ambayo yataijenga biashara yako. Mfundishe mfanyakzi wako kuweza kuongea vizuri na wateja, mfundishe kuandika kumbukumbu kwa kila mzigo unao ingia na kutoka hii itakusaidi sana pia na wewe bosi ni lazima uwe daftari ya tarifa ya kumbukumbu tofauti na wafanyakazi wako.

Moja ya sababu inayopelekea biashara nyingi kufa ni kule kutokuwa na mahusiano mazuri baina ya mwajiri na mfanyakazi.

Wito wangu kwako mfanyakazi ipende kazi yako kuwa mbunifu kwa kumshauri mwajiri wako mbinu kadha wa kadha katika kupanua soko. Na wewe mwajiri Kuwa na mahusiano mazuri na mfanyakazi usimuone eti kwa sababu hana pesa na elimu ya kutosha kama wewe. Mpaka kufikia hapo sina la ziada.

Asante kwa kusoma Makala haya tukutane tena katika Makala ijayo.

TANESCO KUZINDUA HUDUMA KWA NJIA YA MTANDAO

Shirika la Umeme nchini Tanzania TANESCO kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania COSTEC imezindua mfumo uliopewa jina la TANESCO HUDUMA mfumo utakaowawezesha watumiaji wa huduma za Tanesco kuwasiliana moja kwa moja na mtoa huduma wa shirika na kutoa taarifa za matatizo ya umeme.

Shirika la Umeme nchini Tanzania TANESCO kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania COSTEC imezindua mfumo uliopewa jina la TANESCO HUDUMA mfumo utakaowawezesha watumiaji wa huduma za Tanesco kuwasiliana moja kwa moja na mtoa huduma wa shirika na kutoa taarifa za matatizo ya umeme.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa mfumo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Felichesmi Mramba amesema kuwa mfumo huo utatatua matatizo ya kimawasiliano yaliyokuwa yakilalamikiwa sana hapo awali kwani mteja ataweza kupata suluhisho la matatizo yake haraka zaidi.kupitia simu ya mkononi.

Kwa kuanzia mfumo huo utafanyiwa majaribio katika kanda ya Kinondoni Mashariki na baadae utasambaa katika maeneo mengine ya jiji la Dar es salaam na baadae kuenea Tanzania nzima.

MASHABIKI WA ARSENAL WAMKATAA WENGER

Arsene Wenger.  Mashabiki wa Arsenal wamemshambilia meneja wa timu hiyo Arsene Weger katika mtandao wa twitter na kumtaka aondoke na nafasi yake ichukuliwa na raia wa Argentina, Diego Simeone.

Wamesisitiza kuwa timu ya Arsenal chini ya Wenger haijatwaa ubingwa wa Ulaya tangu mwaka 2004 na wala haijashinda UEFA Champions League hata mara moja.
Aidha mashabiki hao walimkubali zaidi Diego Simeone baada ya kuiongoza vyema klabu yake ya Hispania Atletico Madrid na kufanikiwa kuwafunga vigogo wa Ujerumani Bayern Munich 1-0 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya UEFA.

Kambi ya Wenger msimu huu imetikisika kwa kias kikubwa kutokana na shinikizo kutoka kwa wadau wa klabu hiyo na kusababisha kuharibika kwa mbio zao za ubingwa walizoanza vyema.

NDEGE YA ABIRIA 14 YAANGUKA NORWAY

Ndege ya urusi ilioanguka Ndege moja imeanguka karibu na mji wa Norway wa Bergen huku ikiwa na abiria 14 na kuna ripoti ya watu kuonekana katika bahari.
Maafisa wa uokoaji wameviambia vyombo vya habari kwamba ndege hiyo imeharibika vibaya.

Picha kutoka katika eneo la mkasa huo zinaonyesha moshi mkubwa ukifuka katika eneo lenye mwamba mkubwa.

Gazeti la Norway Aftonbladet limeripoti kwamba ndege hiyo aina ya helikopta ilikuwa ikielekea katika eneo la mafuta la Brage kutoka Bergen.

CHEMSHA BONGO

Nguo inauzwa sh 10,000  we huna pesa ukaamuwa kukopa kwa Siz ukakopa 5000 na Bro 5000 ukapata sh.10000 ukaenda ukanunua kwa sh 9700 ukarudshwa sh.300 ukaamuwa kupunguza deni ukatoa sh.100 kwa Bro na 100 kwa Siz ukabaki na 100.

Ukabaki na deni kwa Siz sh.4900 na Bro sh 4900 Total deni ni sh.9800 ukiongeza na ile 100 yako inakuwa 9900 Je 100 nyingine imenda Wapi ?

TIGERS YATWAA TAJI NAMIBIA

Klabu kongwe ya Namibia Tigers, imemaliza ukame wa miaka 31 baada ya kutwaa ubingwa wa msimu wa 2015/2016 wa ligi kuu nchini humo.

Baada ya kulikosa mara kadhaa kombe, hatimaye klabu hiyo imetwaa taji kwa kishindo huku wakiwa wamebakiza mechi mbili na kuzima utawala wa Timu za Black Africa na African Stars,

ambazo zimekuwa zikitawala soka ya Namibia kwa miaka saba iliyopita. Licha ya kufungwa 3-2 na Citizens, lakini wamefanikiwa kutwaa ubingwa kwa kufikisha pointi 67,

sita zaidi ya Black Africa inayoshika nafasi ya pili katika ligi ya timu 16. Timu hiyo imefungwa mechi tatu tu kati ya 30 msimu huu, ikishinda 20 na sare saba.

Kwa matokeo hayo, Tigers itaiwakilisha Namibia katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

MMAREKANI AHUKUMIWA NA KAZI NGUMU KOREA

Kim alipatikana na makosa ya kufanya ujasusi Raia wa Marekani amefungwa jela miaka 10 na kazi ngumu nchini Korea Kaskazini baada ya kupatikana na makosa ya kufanya ujasusi, shirika la habari la Uchina la Xinhua limeripoti.

Kim Dong-chul, raia wa Marekani aliyezaliwa Korea Kusini, alikamatwa mwezi Oktoba mwaka jana.

Kim aliwasilishwa kwa wanahabari mjini Pyongyang mwezi jana na akaoneshwa akikiri makosa, na kusema kwamba alilipwa na Korea Kusini kufanya ujasusi.

Mwezi Machi, mwanafunzi mwingine Mmarekani alifungwa jela miaka 15 kwa kujaribu kuiba bango la propaganda. Alipatikana na makosa ya "uhalifu dhidi ya dola”.

Mhubiri wa Canada afungwa maisha Korea Kaskazini Waziri auawa kwa kusinzia mbele ya rais Kim amefungwa jela katika kipindi ambacho uhusiano baina ya Korea Kaskazini na Umoja wa Mataifa, Marekani na nchi nyingine za Magharibi umedorora.

Majuzi, Pyongyang imefanya msururu wa majaribio ya kurusha makombora baada ya kufanyia majaribio bomu ya nyuklia mwezi Januari, majaribio yote yakivunja vikwazo zilivyowekwa na UN. Pyongyang ilijaribu kurusha makombora mawili ya masafa ya wastani Alhamisi lakini yalilipuka na kuanguka baharini muda mfupi baada ya kurushwa.

Hatua hiyo ilipelekea kuitishwa kwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

TRUMP ACHEKWA KWA KUSHINDWA KULITAJA JINA LA NCHI YA TANZANIA

Mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani ambaye amekuwa akiongoza kwenye kinyang’anyiro hicho,

Donald Trump amejikuta akikosolewa vikali kuhusu upeo wake juu ya sera za nje pale aliposhindwa kulitamka bayana jina la Tanzania.

Trump ambaye Jumanne aliyopita alivuna ushindi wa kishindo kwenye majimbo yote manne yaliyopiga kura za mchujo alijikuta akitumbukia kwenye kadhia hiyo wakati akielezea vipaumbele vya Marekani kuelekea mataifa ya kigeni.

Alikuwa akigusia juu ya mashambulizi ya mabomu yaliyotokea katika ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na Kenya na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali huku watu kadhaa wakipoteza maisha.

Akiwa katika hali ya kujiamini, Trump alisema kuwa iwapo ataingia madarakani moja ya vipaumbele vyake ni kuendelea kutetea masilahi ya Marekani na kudhihirisha hilo aliamua kutolea mfano mashambulizi hayo ya kigaidi.

Lakini wakati akilitaja jina la Tanzania, mfanyabiashara huyo alijikuta akigusa hisia za wengi pale alipolitaja jina hilo kinyume na inavyotamkwa.

“ Ona mashambulizi yaliyotokea katika miaka ya 1990 katika ubalozi wetu nchini Tan-ZAY-nee-uh”. Matamshi hayo yalizusha mjadala mkubwa huku baadhi ya wakosoaji wake wakiingia kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kumuelezea kama ni mtu asiyekuwa na upeo mkubwa kuhusu siasa za kimataifa.

Baadae kambi ya kampeni ya Trump ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikisema kuwa kuteleza kwa mgombea wao katika matamshi ya jina halisi la Tanzania hakumaanishi kuwa uwezo wake kuhusu masuala ya usalama,diplomasia ya kimataifa na biashara ya kimataifa ni wa kutiliwa mashaka.

CHADEMA YATANGAZA KUTOSHIRIKI KURA YA MAONI YA KATIBA MPYA

DK. Vincent Mashinji Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema),

amesema kuwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ndiyo msingi imara pekee unaoweza kuweka mifumo na taasisi kwa ajili ya maendeleo ya kweli yatakayogusa maslahi ya Watanzania wote badala ya nchi kuongozwa na kauli za viongozi.

Kutokana na umuhimu huo wa kuzingatia maoni ya wananchi yanayobeba matakwa yao katika mchakato wa Katiba Mpya, amesema kuwa Chadema hakitashiriki kura ya maoni ya Katiba Mpya Inayopendekezwa ambayo ilipitishwa na Bunge Maalum la Katiba baada ya kubadili na kuondoa mapendekezo yaliyotolewa na wananchi kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya.

Badala yake, Chadema kitaendelea kuweka agenda ya kupigania Katiba Mpya na bora katika vipaumbele vyake, kwa sababu itatibu vidonda na kumaliza makovu yaliyoko katika jamii kutokana na matatizo mbalimbali kama vile ukosefu wa haki,

migogoro ya ardhi, wananchi kukosa huduma za msingi za kijamii zikiwemo elimu, maji na afya.

Dkt. Mashinji aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipoukaribisha ujumbe wa Chama cha Centre Party cha Norway uliofika ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutia saini makubaliano ya ushirikiano kati ya vyama hivyo kwenye Mradi wa Elimu ya Demokrasia awamu ya pili unaofanyika Wilaya ya Mtwara Vijijini. Dkt.

Mashinji pia amekishukuru chama hicho kwa kusaidia kutoa elimu ya uraia kwa Watanzania hususani maeneo ya vijijini katika mradi ambao unahusisha vyama vyote vya siasa vyenye uwakilishi ndani ya Bunge, huku akisisitiza kuwa Chadema kiko tayari kwa ushirikiano unaozingatia maslahi na matakwa ya wananchi hasa katika kukuza uelewa wa kudai haki, demokrasia na uongozi bora ndani ya nchi.

“Suala la Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi kama ilivyowasilishwa kwenye rasimu ya pili na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya ni agenda muhimu kwa Watanzania wapenda nchi yao na sisi ni kipaumbele kwa mwaka huu na kuendelea hadi hapo nchi yetu itakapopata Katiba Mpya ya Wananchi. “Jana na leo tumewasikia baadhi ya viongozi wa serikali wakisema kuwa wanajiandaa kuitisha kura ya maoni…hatutashiriki kura ya maoni ya Katiba Mpya Inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba. Tunajua Watanzania wengi wanataka Katiba Mpya iliyotokana na maoni yao, si ile iliyochakachuliwa bungeni.

“Katiba Mpya iliweka masuala kuhusu haki za wananchi, kuimarisha misingi na kuweka mifumo ya demokrasia na uongozi bora, walau kwa kuanzia. Hatuwezi kusema sasa tutatumia mikakati gani kuwahamasisha Watanzania kuidai Katiba Mpya…tutajua namna ya kuvuka tukishafika mtoni,”

Alisema Aidha, Katibu Mkuu Dkt. Mashinji alisisitiza kuwa suala la nchi kuwa na misingi na mifumo imara ya demokrasia na uongozi bora ni muhimu kwa Tanzania, katika wakati ambapo nchi inaelekea kwenye uchumi mkubwa wa nishati ya gesi na mafuta, akisema vinginevyo ni hatari iwapo taifa lenye utajiri mkubwa wa rasilimali, litaendelea kuwa na wananchi waliokata tamaa kutokana na mfumo mbovu uliopo.

Kwa upande wake ujumbe huo uliokuwa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Centre Party, Knut Olsen, ulisema kuwa chama hicho kinashukuru kwa mradi huo kuingia katika hatua ya pili kuanzia mwaka 2016-2019 huku hatua ya kwanza ikiwa na mafanikio makubwa katika jamii ya wananchi wa maeneo ya pembezoni.

“Kama unavyojua, mradi huu kupitia TCD unahusisha vyama vyote vyenye uwakilishi ndani ya bunge, na lengo letu ni kuwajengea uwezo viongozi wa vyama hasa wanawake na vijana katika ngazi ya jamii kwenye vitongoji, vijiji, kata na bunge ili waweze kushiriki mchakato wa maamuzi.

Tunatarajia kuendelea kupata ushirikiano katika hatua ya pili,” alisema Inger Bigum, ambaye ni Meneja wa Mradi hapa nchini.

Wengine waliokuwa katika ujumbe huo wa Centre Party ni pamoja na Vijana Sara Hamre Katibu Mkuu wa, Katibu Mkuu wa Wanawake, Eline Stokstad-Oslan na Kristin Madsen Katibu Mkuu wa Wazee.

Mradi huo wa Elimu ya Demokrasia katika Wilaya ya Mtwara Vijijini unaohusisha vyama vyenye uwakilishi bungeni kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) chini ya ufadhili wa chama hicho, katika awamu ya kwanza ulihusisha kata za Msangamkuu, Nanyamba, Ziwani na Mbembaleo na katika sasa awamu ya pili utakuwa katika kata za Mkunwa, Tangazo, Mayanga na Madimbwa.

MAREKANI YAITAKA URUSI KUSHINIKIZA SYRIA

Marekani imeitaka Urusi kuishinikiza Syria kusitisha kuvamia raia na badala yake kuzingatia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ametoa kauli hiyo baada ya hospitali moja iliyopo kwenye eneo la waasi kushambuliwa kwa ndege huko mjini Allepo, ambapo madaktari na watoto wameuawa.

Amesema Marekani imeshtushwa na shambulizi hilo ambalo limefanywa kwa kukusudiwa.

Zaidi ya watu sitini wameuawa mjini Aleppo lakini kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita katika maeneo yanayohodhiwa na serikali pamoja na waasi.

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa amesema hali ni ya kusikitisha. Msemaji wa ikulu ya Marekani Josh Earnest amezungumzia kuongezeka kwa vurugu hizo.

'' Tunalaani vikali wimbo jipya la mashambulizi ya anga ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu sitini katika mji wa Aleppo katika kipindi cha saa ishirini na nne pekee. Tumeshangazwa zaidi na shambulizi la anga lilipofanywa katika hospitali iliyopo mjini Aleppo ambalo limeuwa takriban wagonjwa kumi na nne na madaktari watatu- akiwemo pamoja na daktari pekee wa watoto katika mji huo''.

Maeneo ya mji wa Aleppo yamekabiliwa na mashambulizi mapya kutoka serikalini. Wanaharakati wametoa picha za video zinazoonyesha waokoaji wanavyotafuta watu waliosalimika katika tukio hilo.

LIVERPOOL YACHAPWA EUROPA

Liverpool walichapwa 1-0 Mechi za kwanza za nusu fainali za Uefa Europa League zimechezwa jana, mabingwa watetezi Sevilla wakicheza ugenini na Shakhtar Donetsk.

Matokeo ya mchezo huo ni kwamba Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 2-2 ndani ya dakika 90 za mchezo.

Sevilla ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 6 kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji Mchin Perez, na Shakhtar Donetsk kusawazisha bao hilo dakika ya 23 kupitia kwa Maros Romeo na Stepanenko kuongeza bao la pili dakika ya 35 kipindi cha kwanza.

Baadaye kelvin Gameiro akaisawazishia Shakhtar Donetsk ikasawazisha bao hilo dakika ya 82 kwa njia ya penati .

Katika mchezo mwingine Klabu ya England Liverpool ikicheza Ugenini huko Uhispania imeambulia kichapo cha bao 1-0 mikononi mwa Villarreal kwa bao la Adrian Lopez la dakika ya 90 ya mchezo.

Timu zote nne zitarejeana tena Alhamisi wiki ijayo, ikiwa ni mechi za pili hatua ya nusu fainali.

RUFAA KUPINGA KUACHIWA ABDALLAH ZOMBE

Abdallah Zombe (kushoto) akiwa na wakili wake, Richard Rweyongeza katika Mahakama ya Rufaa,

Dar es Salaam Mahakama ya Rufaa leo inatarajiwa kusikiliza rufaa ya kupinga kuachiwa huru kwa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na askari wenzake wanane waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji. Rufaa hiyo inatarajiwa kusikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Bernard Luanda, wengine ni Jaji Sauda Mjasiri na Jaji Semistocles Kaijage.

Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), alikata rufaa mwaka 2013, akipinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliyowaachia huru Zombe na wenzake, baada ya kuwaona hawana hatia katika kesi ya mauaji ya watu wanne iliyokuwa inawakabili.

Katika rufaa hiyo, DPP anadai kuwa Jaji Salum Massati alikosea kuwaachia huru washitakiwa hao kwa sababu kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani wote.

Mbali na Zombe, wajibu rufaa wengine ni ASP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, Konstebo Jane Andrew, Konstebo Emanuel Mabula, Konstebo Michael Shonza, Koplo Abeneth Salo, Koplo Rajabu Bakari na Koplo Festus Gwabisabi. Katika kesi ya msingi inadaiwa Januari 14, 2006, katika msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis, Dar es Salaam Zombe na wenzake waliwaua kwa makusudi wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Morogoro, Mathias Lunkombe, Sabinus Chigumbi na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, pamoja na dereva teksi Juma Ndugu.

Baada ya kusikiliza kesi hiyo, Agosti 17, 2009, Jaji Massati aliwaachia huru washitakiwa kwa kuwa upande wa Jamhuri ulishindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao bila kuacha shaka na Mahakama ikiwaona hawana hatia kwa makosa yaliyokuwa yanawakabili. Oktoba 6, 2009, DPP alikata rufaa Mahakama ya Rufani, akipinga hukumu hiyo kwa madai kuwa Jaji Massati alikosea kuwaachia huru washtakiwa hao,

pia kulikuwa na ushahidi wa dhahiri na wa kimazingira unaotosha kuwatia hatiani washtakiwa wote. Hata hivyo Mei 8, 2013 Mahakama ya Rufaa ilitupilia mbali rufaa hiyo kutokana na dosari za kisheria zilizobainika kwenye rufaa, lakini DPP alipeleka maombi Mahakama Kuu ili aruhusiwe kukata tena rufaa nje ya muda.

Mahamaka Kuu ilikubali maombi yake, akakata tena rufaa inayotarajiwa kusikilizwa leo.

NAFASI YA KAZI FOOD TRADE EASTERN

FOOD TRADE EAST & SOUTHERN AFRICA (ESA) EMPLOYMENT OPPORTUNITY Post Title: Monitoring and Results Measurement Specialist Reports to: Team Leader – Food Trade East & Southern Africa Duty Station: Dar-es-Salaam, Tanzania Requirements Food Trade East & Southern Africa (ESA) is a five-year UK Government funded trade enhancement and promotion program focused on staple foods. The World Food Programme, through a grant provided by the Food Trade ESA, is implementing a multi-country project to scale up the use of its Patient Procurement Platform {PPP}. The PPP project will support government efforts to build sustainable markets that link smallholder farmers to local and regional markets. The project is seeking a qualified Monitoring and Results Measurement (MRM) Specialist. The MRM Specialist will work closely with the technical team and other project stakeholders to manage an intervention MRM plan for the WFP PPP project, providing quality assessment support and improving all on-going monitoring measurement activities. Potential candidates are required to have a minimum of a university degree in any relevant field/subject, with. 5+ years' experience managing data intensive programs and designing MRM systems. Experience in integrating innovative MRM approaches in agriculture development programmes within the region is desirable. APPLICATION INSTRUCTIONS: Interested and suitably qualified candidates can send their CV and cover letter throughfoodtrade_recruitment@dsi.com. Applications should include three work-related telephone numbers'. by email only through referees and day-time Application deadline is 14 days from the date advertised. Only candidates who meet qualifications will be shortlisted and contacted. We are committed to minimizing the environmental impacts of operations related to the programme, and to ensuring our work supports social protection for everyone without bias. We encourage gender equity and diversity in our programme

Thursday, April 28, 2016

ZITTO: WAHUSIKA WA SAKATA LA ESCROW WAFIKISHWE MAHAKAMANI

MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo) ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuwafikisha mahakamani wahusika wa sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow ili sheria ichukue mkondo wake.

Zitto aliyasema hayo bungeni mjini hapa jana wakati akichangia kwenye hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, iliyowasilishwa na Waziri Angela Kairuki pamoja na ile ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),

iliyowasilishwa na Waziri wake, George Simbachawene. Alisema mwaka 2014, Takukuru waliijulisha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwamba ilikuwa inachunguza na kumaliza uchunguzi kuhusu miamala ya kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenda Benki ya Stanbic Tanzania.

Alisema katika taarifa zote ambazo Takukuru inatoa kuhusu kesi za ufisadi, hakuna mahali inapozungumzia maendeleo ya suala hilo. “Hata siku moja hakuna mahala Takukuru wanasema kuhusu uchunguzi huu na lini wahusika waliochota fedha za umma watafikishwa mahakamani. Naomba tupate kauli ya serikali kuhusu jambo hili kwani ni moja ya jipu,” alisema Zitto ambaye aligusia suala la ukiukwaji wa Sheria ya Bajeti.

Alisema kuna ukiukwaji kadhaa wa sheria ya bajeti kama vile sheria namba 11 ya mwaka 2015, ambapo kifungu cha 8 cha sheria hiyo kinaeleza namna ambavyo mfumo wa Bajeti ya Serikali unapaswa kuwa.

“Vifungu vya 8(1)(b) na 9(1)(a) na 19(1) vinaeleza namna mchakato wa bajeti unavyopaswa kuwa. Vifungu hivi vinataka mpango na miongozo ya bajeti ipitishwe na Bunge katika mkutano wake wa Mwezi Februari kila mwaka.

HII SI HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA REAL MADRID NA YEYE MWENYEWE RONALDO..

April 28, 2016 Hii sio habari njema kwa mashabiki wa Real Madrid na Cristiano .

Jina la mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo limerudi tena kwenye headlines leo Jumatano ya April 28 2016.

Ronaldo amerudi kwenye headlines baada ya Real Madrid kudaiwa kutoa ripoti ya maendeleo ya majeruhi yake. Ronaldo ambaye amekosa mechi mbili za Real Madrid huenda akakosa michezo mingine ikiwemo mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Man City utakaochezwa Santiago Bernabeu,

Ronaldo anadaiwa kupimwa na MRI Scan na kukutwa ana tatizo la msuli (muscle tear).

Cristiano Ronaldo ambaye alikosa michezo miwili iliyopita ya Real Madrid, aliumia katika mchezo walioshinda 3-0 dhidi ya Villarreal April 20 2016,
hadi sasa Ronaldo amefunga magoli 47 msimu huu katika mechi 45 alizoichezea Liverpool na kuwa mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufunga magoli mengi kwa msimu.

Insragram @Don vuitton 69
Face book @ Don vuitton

WATU 7 WAFARIKI KIBADA KIGAMBONI

Ajali imetokea Kibada Kigamboni sasa hivi, Picha iyo, Ajali imehusisha gari aina ya MAHINDRA-SCOPIO,

ilikuwa ikitokea Mji Mwema inaelekea Kibada. Imevamia matofali yaliyo pembezoni mwa barabara mbele ya nyumba ya ghorofa.

Inasemekana gari hiyo ilibeba watu wa familia moja na wamefariki watu 7 watoto 3 na watu wazima 4 katika ajali apa Kibada - Kigamboni ni

HISTORIA YA KIDUKU UNAIJUA??

Wengi wanapenda kucheza au kuona wengine wakicheza KIDUKU!

Lakini wengi wao hawafahamu asili na chimbuko la kiduku hapa Tanzania! Kwa kifupi ni kwamba ASILI YA KIDUKU NI NIGERIA!

kiduku ni aina fulani ya ngoma inayochezwa nchini Nigeria, Hivyo kiduku kimefika Tanzania kupitia filamu za kinigeria!

Filamu ya 'Ola' ilyotoka mwaka 2006 ndo kichochezi halisi cha style ya kiduku nchini kwani baada ya filamu ya Ola kusambaa nchini Tanzania ndipo kiduku kilipoibuka na kuenea nchini Tanzania!

TEKNOLIJIA INAPOELEKEA HUKU , HEBU ONA

This Smartphone Gun Is One Hell of a Concealed Weapon 380 caliber gun within the ubiquitous shape of a smartphone.

SAKHO BAADAYA YA KUSIMAMISHWA , APEWA ADHABU YA MUDA

April 28, 2016 Siku 5 baada ya Liverpool kumsimamisha Sakho, UEFA wamempa adhabu ya muda Rama Mwelondo TZA April 23 2016 uongozi wa klabu ya Liverpool ulitangaza kumsimamisha beki wa kati wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu hiyo Mamadou Sakho kutokana na kugundulika kutumia dawa za kusisimua misuli michezo, dawa ambazo ni kinyume na taratibu.

Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) leo limetangaza uamuzi au adhabu ya kumsimamisha Mamodou Sakho kwa siku 30, uamuzi ambao ni wa muda ili kuipa nafasi kamati ya maadili ya UEFA hadi itakapokaa na kutangaza adhabu rasmi.

Sakho ambaye alikuwa anachunguzwa na UEFA toka March 17 baada ya mchezo wa Europa league kati ya Man United dhidi ya Liverpool Old Trafford, amegundulika kutumia ‘Fat Burner’

kwa ajili ya kusisimua misuli, Mamadou Sakho atakumbana na adhabu kutoka UEFA baada ya kamati ya maadili kukaa na kuamua adhabu.

MLIMA KILIMANJARO ULIOPO TANZANIA UMETANGAZWA KUWA KIVUTIO KIKUU CHA UTALII KATIKA BARA LA AFRICA 2016

MLIMA Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi barani Afrika, umetangazwa kuwa kivutio kikuu cha utalii katika bara katika mwaka 2016.

Hili lilitangazwa katika hafla ya taasisi ya masuala ya utalii Afrika na eneo la Bahari ya Hindi ijulikanayo kama World Travel Awards Africa and Indian Ocean  iliyofanyika Zanzibar wiki iliyopita.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) jana ilisema hafla hiyo ilihudhuriwa na mamia ya viongozi wa masuala la utalii iliyoandaliwa na kampuni ya Diamonds La Gemma Dell’est na kufanyika huko  Nungwi, Zanzibar, Jumamosi iliyopita. “Bodi ya Utalii ya Tanzania, imepokea kwa heshima kutangazwa Mlima Kilimanjaro kuwa ndiyo kivutio kikuu cha utalii barani Afrika.

 Uteuzi huu ni dhahiri utachangia juhudi zetu za kuendeleza utalii nchini Tanzania, hususani kwa kuufanya ulimwengu ufahamu kwamba Tanzania ndiyo mmiliki wa Mlima Kilimanjaro ambalo ni kivutio kikuu barani Afrika,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

TRUMP KASHINDA TENA MAJIMBO MATANO MAREKANI

Trump amesema kwa sasa yeye ni kama "mgombea mteule" Donald Trump ameshinda mchujo wa kuteua mgombea urais wa chama cha Republican katika majimbo matano ya Marekani yaliyopiga kura Jumanne.

Mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton ameshinda majimbo manne kati ya matano yaliyoshiriki mchujo.

Baada ya matokeo kubainika, Bw Trump alijitangaza kuwa “mgombea mteule” wa Republican. Ushindi wake Connecticut, Delaware, Maryland, Pennsylvania na Rhode Island unamfanya kukaribia sana kutimiza idadi ya wajumbe inayohitajika kumhakikishia ushindi kabla ya kuandaliwa kwa mkutano mkuu wa chama hicho wa kuidhinisha mgombea Julai.

Upande wa Democratic, Bi Clinton amenyimwa ushindi kamili na Bernie Sanders ambaye ameshinda katika jimbo la Rhode Island.

WANANCHI ZAIDI YA 100 WAPATA UMEME VIJIJINI NYEMBURU NA KUONDOKANA NA GIZA

WAKAZI zaidi wa 100 katika  kijiji cha  Nyeburu  Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani waliokuwa na tatizo  la upatikanaji wa nishati ya umeme na kuishi  katika giza  kwa kipindi cha muda mrefu kwa sasa wamenufaika baada ya  kuunganishiwa umeme kutokana na  kukamilika kwa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu wa pili.

Baadhi ya wakazi hao  ambao wamenufainika  na mradi huo wakizungumza na na mwandishi wa habari hizi  akiwemo Mguya Mvuti,Tina Emmanuel pamoja na Lamia Suka   wamesema kwamba  hapo awali walikuwa wanapata kero ya umeme na kusababisha kukwamisha shughui mbali mbali za kimaendeleo.

Aidha walisema kwamba kukamilika kwa mradi huo kutaweza kuleta chachu kubwa ya kimaendeleo katika kijiji hicho kwani mwanzoni wananchi hao  walikuwa wanashindwa tutimiza malengo yao waliyojiwekea kutokana na kutokuwa na nishati hiyo ya umeme. “Kwa kweli sisi kwa upande wetu kama wananchi wa kijiji hiki cha nyeburu hapo awali tulikuwa tunapata shida kubwa sasa nah ii yote ni kutokana tulikuwa tunaishi giza kipindi chote lakini kukamilika kwa maradi huu wa umeme vijijini hata kijiji chetu kitaweza kuapata maendeleo.

Kwa upande wake Meneja wa shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani  Martin Madulu alisema kuwa kwa sasa wanatekeleza  agizo lililotolewa na serikali kuhakikisha wanawafikia wateja wao wote hususan wale wa vijijini  kwa lengo kuweza kuwaunganishia umeme kwa bei nafuu.

Aidha Madulu alisema kwamba kwa sasa watahakikisha wanafanya jitihaza za hali na mali katika kuwafikia wateja wao ili waweze kuwa na nishati ya umeme katika maeneo mbai mbali hususan kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya vijijini.

“Lengo letu kubwa kwa sasa tunatakeeza agizo lililotoewa na serikali na tumeshaanza katika maeneo ya Chalinze, Kisarawe na tutaendelea katika sehemu mbali mbali za Mkoa wetu wa Pwani na tunatarajia kufikia vijiji vipatavyo 109 vilivyopo katika Mkoa huu,”alisema Madulu.   Naye Mhandisi mkuu wa Miradi ya kupeleka umeme vijijini (REA) Mkoa wa Pwani  Leo Mwakatobe amebainisha kuwa wanakumbana na changamoto nyingi katika utekelezaji wa majukumu yao hasa wakati wanapotaka kupitisha miundomibu katika makazi ya watu.

MRADI huo wa kusambaza umeme vijijini (REA) awamu ya pili katika Mkoa wa Pwani unatarajia kuvinufaisha vijiji vipatavyo 109,sawa na wateja 11000 ambapo utakamilika mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu kwa gharama ya kiasi cha shilingi bilioni 30.

ATHLETICO MADRID YA PIGILIA MSUMALI BAYERN MUNICH

Michuano ya Kombe la Klabu Bingwa barani Ulaya hatua ya nusu fainali imeendelea tena jana,

Atletico Madrid wakipata ushindi dhidi ya Bayern Munich katika dimba la Vicente.

Atletico walichomoza na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Saul Niguez.
Timu hizo zitarudiana tena wiki ijayo ikiwa ni mchezo wa mwisho kuweza kumpata mshindi atakayecheza hatua ya fainali ya michuano.

IRAQ YAWABANA AL JAZEERA KUWA WANAKIUKA UANA HABARAI

Iraq imesema Al Jazeera imekiuka kanuni za uanahabari Serikali ya Iraq imeliamuru shirika la utangazaji la Al Jazeera kufunga afisi zake mjini Baghdad.

Wanahabari wa shirika hilo pia wamepigwa marufuku kukusanya habari nchini humo. Maafisa wa serikali wanasema shirika hilo la utangazaji limekuwa likikiuka kanuni za uanahabari, ambazo miongoni mwa mengine zinazuia mashirika ya habari kuangazia makundi ya waasi.

Shirika la Al Jazeera limesema limeshangazwa sana na hatua hiyo na limekanusha kuvunja kanuni zozote za kitaaluma.

MABASI MANNE YA MRADI WA (BRT ) YAMECHUNWA RANGI

MABASI manne ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) yamechunwa na vyombo vingine vya usafiri.

Hali hiyo imetokea kutokana na kutoheshimu taratibu kunakofanywa na madereva wa vyombo vingine vya usafiri katika kipindi hiki ambacho mabasi hayo yapo kwenye mazoezi.

Hali hiyo imetokea zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa kipindi cha mpito cha mradi huo, kitakachoanza Mei 10 mwaka huu chini ya Kampuni ya Uda Rapid Transit (UDA-RT). Msemaji wa Kampuni ya UDART, Sabri Mabruki alisema,

“Sheria za mabasi haya ni kama treni, yule aliyegongwa au kagonga basi ndiye mwenye kosa”. Alitaka vyombo vya usafiri kutotumia njia maalumu za mabasi hayo na kusisitiza wananchi kuheshimu njia hizo isaidie kuepuka ajali na kurahisisha uendeshaji wa mradi.

Alisema pamoja na kupigwa marufuku madereva kupitisha vyombo vya usafiri kwenye njia za mabasi hayo, bado kuna baadhi wanapita katika barabara hizo huku mabasi yakiwa yanafanya mazoezi.

Alisema miundombinu ya mradi huo imejengwa kulingana na mahitaji, hivyo kila chombo cha usafiri kipite na waenda kwa miguu wapite katika njia zilizotengwa. Alisema mabasi yana madereva waliofuzu, yamekatiwa bima na nauli zinatarajiwa kutangazwa hivi karibuni na Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra).

Alisema katika kudhibiti ulinzi wa vituo na mabasi, wamefunga kamera kwa ajili ya kubaini watu wenye nia mbaya ya kuhujumu miundombinu hiyo.

FACEBOOK SASA INA ZAIDI YA WATUMIAJI BILLIONI 1.65 DUNIANI

Mtandao wa kijamii wa Facebook sasa una watumiaji zaidi bilioni 1.65 duniani kote. Kati ya watumiaji hao, bilioni moja wanautumia kwa simu.

“Tumekuwa na mwanzo mzuri kwenye mwaka,” CEO na mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg alisema.

“Kwa sasa tuna zaidi ya watumiaji bilioni 1.65 na zaidi ya watumiaji bilioni moja kila siku kwenye simu.” Katika kipindi cha mwaka mmoja mtandao huo umeingiza mapato ya dola bilioni 1.51.

DIEGO SIMEON AFUNGIWA MECHI ZOTE, ZILIZO BAKI LALIGA

KOCHA Mkuu wa Atletico Madrid, Diego Simeone amefungiwa kukaa kwenye benchi kwa mechi zote tatu zilizobaki za timu yake katika Ligi Kuu ya Hispania, La Liga kumalizia msimu. Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 45 amepewa adhabu hiyo baada ya mpira kurushwa uwanjani katika mchezo wa Jumamosi, timu yake ikishinda 1-0 dhidi ya Malaga. 

 Picha za Televisheni zinaonyesha kwamba mpira huo ulipokuwa nje katika himaya ya kijana muokota mpira, ukarushwa uwanjani kutoka eneo la benchi la Atletico Madrid na kuvuruga shambulizi la Malaga. Na kwa kuwa mpira uliporushwa kutoka eneo la benchi la ufundi la Atletico - sheria zinambana kocha kwamba ndiye wa kuwajibishwa na Simeone amedhibiwa. Kocha huyo wa Atletico alipandishwa jukwaani na refa Antonio Mateu Lahoz baada ya ripoti kusema hakumtaja aliyerusha mpira uwanjani. 


 Madrid inalingana kwa pointi Barcelona kileleni mwa msimamo wa La Liga, wakati Real Madrid inazidiwa pointi moja katika nafasi ya tatu. Simeone sasa hatakaa benchi katika mechi dhidi ya Rayo Vallecano, Levante na Celta Vigo.

CPWAA AELEZA SABABU ZA KUKAA KIMYA KIMUZIKI NA KUJA NA UJIO MWINGINE

Rapper Cpwaa amesema ukimya wake haumaanishi kuwa ameacha muziki. Ameiambia Bongo5 kuwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni amekuwa akifanya shughuli zake binafsi zinazohusiana na fani ya IT aliyoisomea.

Amedai kuwa katika kipindi hicho pia amekuwa akirekodi nyimbo kibao huku sasa akijiandaa kufanya video na muongozaji wa ndani.

“Siwezi kurudi kwa style ile ile ya kizamani au kwa strategy zile zile, game imebadilika sasa hivi, watu wako vizuri, wanafanya kazi nzuri,” amesema. “Nipo kwenye hatua pia ya kuweza kurudi kwenye style ambayo itaweza kwendana na ushindani ambao upo kwa sasa,” ameongeza. Rapper huyo amesema mashabiki wake wamekuwa wakimuuliza karibu kila siku kwenye mitandao ya kijamii na sehemu zingine kuhusu ukimya wake na amekiri hilo kumsumbua.

“Ni kitu ambacho kinanikwaza sana, nakaa na watu kwenye mamall nikitoka wanauliza ‘bana vipi mbona umeacha, hebu rudi.’

Challenge ambayo nakutana nayo sasa hivi najiuliza kwenye video labda nifanye na nani. Siwezi kudanganya, siko tayari kutumia $40,000 sasa hivi niende South Africa kufanya video wakati nina majukumu mengi. Kwahiyo siwezi kuchukua hela yangu inayoniingizia mkate wangu wa kila siku kuipeleka huko,” a

mesisitiza. “Lakini I promise the industry mpaka kwamba by June watakuwa tayari wameshapata mzigo wangu mpya kabisa.”

DIAMOND PLATNUMZ KUJA NA REALITY SHOW YAKE, NI SHIDA

April 25, 2016 Diamond anaandaa reality TV show yake, P square ndani (+Audio) Newsroom TZA Kama utakuwa ni mpenzi wa kufuatilia stori za entertaiment basi hizi hapa zisikupite, millardayo.com imekurekodia stori  zote za April 25 2016  ambazo zimepata airtime kupitia 255 ya XXL na Stori ambayo imepata airtime ni hii ya P square kushoot video na Diamond Platinumz. Wasanii wakubwa Afrika ambao wanaunda kundi la P square wameonekana kwenye reality show ya Diamond Platinumz wakiwa location South Africa kwa ajili ya kushoot ngoma mpya na hii ni kauli ya Diamond Platimuz…… >>> ‘hiki sio kireality show ni reality show na sio bora reality bali ni reality bora mimi mwenyewe nilitaka nifanyage siku nyingi lakini nilikuwa nataka kuwe na production kuwe na vifaa bora,,,, hayo ni maneno ya diamond platnumz

VIDEO; RAMMY GALIS ALFAJIRI YA APRIL 27 2016 ,ALIWASILI DAR ES SALAAM