Friday, August 26, 2016

DUDUBAYA AMFUNDISHA MWANAE KUVAA CONDOM

   Msanii Godfrey Tumaini au Dudubaya ameonesha mfano jinsi ya kuwa baba bora, kwa kuzungumza na mtoto wake kuhusu maambukizi ya magonjwa ya zinaa, na jinsi ya kujikinga na magonjwa hayo kwa kutumia condom.

      Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio, Dudubaya amesema huwa anazungumza na kijana wake kwa kuwa hataki apate magonjwa ya zinaa na kufa mapema kabla yake.

    "Mwezi wa 12 mwaka jana ndiyo nilikuwa naye alikuwa amefunga shule kwa hiyo kujiandaa kwenda form one, nilichomwambia siku moja mpaka washkaji walicheka maskani, nikamwambia dogo sikiliza, najua sasa hivi we unajisikia, sasa kama unajisikia unajua kuna kitu kinaitwa condom!? akaniambia yah, unajua kuitumia!?

       akasema hapana, nikamwambia unajua kuna magonjwa kama gono, kuna kaswende na UKIMWI, na sipendi utangulie wewe kufa mimi nikabaki, ni bora mimi nife wewe ndo uje kuwa mrithi wangu", alisema Dudubaya.

      Dudubaya aliendelea kusema kuwa wazazi wengi sasa hivi hawazungumzi na watoto wao na hatimaye watoto wanaingia kwenye mambo yasiyofaa, na mwisho wazazi huwalaum na kuwachukulia hatua watoto, kwa makosa ambayo wameyasababisha wenyewe.

   
     "Mtoto anapofikia kujisikia haina sababu ya kumfungia geti, na ndiyo maana unakuta kuna watoto wanapata maambukizi ya magonjwa kama UKIMWI, kumbe we mzazi hukuongea na mwanao, mzazi unatakiwa

     uzungumze na mwanao umwambie hivi na hivi, kwa mfano kama mjini hapa watoto kibao wanaharibika na madawa ya kulevya, kwa sababu mzazi huzungumzi na mtoto", Alisema Dudubaya.

Friday, August 19, 2016

VIGOGO WAWILI WA NIDA WAPATA DHAMANA

    VIGOGO wawili wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) wanaokabiliwa na mashitaka ya kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 1.2 wameachiwa kwa dhamana. Washitakiwa hao ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara, Avelin Momburi na Mkurugenzi wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Joseph Makani.

     Hata hivyo, washitakiwa wengine akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Dickson Maimu na wenzake watano wanaendelea kusota rumande.

      Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Respicius Mwijage alitoa uamuzi huo jana kwa kuwa washitakiwa hao wawili hawaguswi katika mashitaka yaliyofunguliwa chini ya Sheria ya Uhujumu Uchumi.

     Alisema anakubaliana na hoja za upande wa utetezi zilizowasilishwa na Wakili Johnson Jamhuri kuwa mashitaka yanayowakabili washitakiwa hao yana dhamana na hayahitaji kuombewa dhamana hiyo Mahakama Kuu.

     Hakimu Mwijage alisema, washitakiwa wanatakiwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hati ya Sh mil 200, pia wawasilishe hati zao za kusafiria na hawatakiwa kwenda nje ya Dar es Salaam bila kibali cha mahakama.

MWILI. WA MTOTO WA ALBINO WAFUKULIWA KWA UCHUNGUZI

    MWILI wa mtoto mwenye albinism aliyefariki kwa maradhi hivi karibuni na kuzikwa Jumapili iliyopita, umefukuliwa chini ya ulinzi wa polisi ili ufanyiwe uchunguzi kutokana na kuibuka maneno yenye kutatanisha kuwa wakati akiugua alikuwa akivuja damu nyingi puani na kuvimba mwili.

     Mtoto huyo, Michael Juma aliyekuwa na umri wa miaka miwili na nusu, alizikwa pembeni mwa nyumba yao Alhamisi wiki hii katika kijiji cha Bunambiyu, wilayani hapa na kuwashangaza wakazi wa eneo hilo.

  
      Katibu wa Chama cha Watu Wenye Albino Nchini (TAS), tawi la mkoa wa Shinyanga, Lazaro Anael alisema kitendo cha kuufukua mwili kimewashangaza na kwamba tangu taarifa za kifo cha mtoto huyo kujulikana, yamezuka maneno kuwa kifo hicho kina utata.

      Alisema alishiriki mazishi, lakini kabla ya kufika nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo akiambatana na Mkurugenzi wa Shirika la Under the Same Sun, Vicky Mtetema, waliukagua mwili wa mtoto huyo na kubaini haukuwa na tatizo.

     “Mimi nasema hivi maneno haya yanatoka wapi wakati mwili tuliukagua haukuwa na dosari yoyote wakati huo tulikuwa na Vicky Mtetema akiwa anaupiga mwili picha, viongozi wa kijiji na kata walikuwepo pamoja na majirani wakishuhudia kuwa salama na ndipo shughuli za maziko zilifanyika… sasa kitendo cha kufukua mwili hapo serikali inataka kuleta hofu,” alisema.

      Diwani wa Kata ya Bunambiyu, Richard Sangisangi aliyekuwa amekataa mwili huo kufukuliwa na kugoma kuwaita majirani kwa ajili ya kufukua mwili ili ufanyiwe uchunguzi aliondoka na kusema kamwe hawezi kuchuma dhambi kwa kile alichokieleza walishuhudia mwili ukiwa salama na alifariki kwa mapenzi ya Mungu sio ushirikina au kukatwa mapanga kama ilivyozoeleka maeneo mengine. Mwenyekiti wa kijiji hicho, Jonathan Katela alisema kitendo cha kufukua mwili huo sawa na kurudisha majonzi kwa jamii na familia, lakini akasisitiza ameridhia kwa kuwa serikali imetaka mwili ufukuliwe kwa uchunguzi.

     Kauli kama hiyo ilitolewa na baba wa marehemu, Juma Masudi aliyesema ametii amri ya serikali, lakini yeye binafsi hakuridhika kuufukua mwili wa mwanawe aliyedai aliugua maradhi ya kawaida na kupata matibabu kituo cha afya Bunambiyu. Hata hivyo, baada ya mvutano,

    polisi walifanikiwa kufukua mwili huku Dk Hellen Kaunda aliyekuwepo eneo la tukio akiufanyia uchunguzi na kueleza haukuwa na dosari yoyote na kwamba alifariki kwa maradhi.

..... Msafara wa Polisi, Kitengo cha Upelelezi wilayani Kishapu kupitia msemaji wake kwenye eneo la tukio, Meshack Sumuni aliwaomba radhi wananchi na wazazi huku akiwatoa hofu kwa kitendo cha kufukua kaburi kuwa ni jambo la kawaida unapotoa utata.

SUMATRA YASEMA HAKUNA USAFIRI UTAKAOSITISHWA

    MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imewatoa hofu Watanzania kuhusu taarifa za kutokuwepo kwa huduma ya usafiri wa mabasi kwenda mikoani kuanzia Jumatatu na kusema kuwa inafuatilia kuhakikisha kuwa huduma hiyo inatolewa wakati wote.

     Pia, imesema maazimio yaliyotolewa na Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa) kuhusu kufanyika kwa ukaguzi wa mabasi yote yaendayo mikoani Agosti 22, mwaka huu, usitishwe na kuwataka kutoa huduma hiyo hadi utaratibu maalumu utakapopatikana.

     Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe, alisema Taboa ilipeleka maazimio matatu yanayohusu ukaguzi wa magari unaolenga kuimarisha usalama na ubora wa huduma wanazotoa kwa jamii.

      Ngewe alisema mamlaka hiyo inakamilisha utaratibu huo wa kukagua magari pamoja na madereva na kwamba wanahitaji kuzungumza na taasisi inazoshiikiana nazo, ikwemo Kikosi cha Usalama Barabarani.

      “Maazimio haya ni mazuri na yanalenga kutoa huduma bora lakini hatuwezi kuanza ukaguzi Agosti 22 kwa kuwa tunahitaji vifaa kwa ajili ya kufanya ukaguzi huo na kujua ni mabasi yapi yataanza ukaguzi na yatakayofuata,’’ alisema Ngewe na kuongeza kuwa, wamiliki wa mabasi hayo pamoja na madereva wanatakiwa kufuata masharti ya leseni walizopewa kwa kusafirisha abiria hadi utaratibu rasmi wa ukaguzi utakapotolewa.

        Hata hivyo, alisema wananchi hawana budi kuondoa hofu ya kukosa usafiri kwakuwa hakuta utakaositishwa ili kupisha ukaguzi huo.

ARUSHA WATAKA MKUU WA MKOA AACHWE AFANYE KAZI

     WAKATI Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiapishwa jana Ikulu, Dar es Salaam, baadhi ya wananchi wa Jiji la Arusha wameshangazwa kuona viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakidai kuwa anaingilia kazi za jiji hilo.

      Mkazi wa jiji hilo, Ismail Isaac alisema tatizo ni siasa za chuki kati ya Chadema dhidi ya RC Gambo na kutaka wamuache afanye kazi kwani wananchi wanamkubali, hivyo kama chama hicho cha upinzani hakimkubali, kitajua chenyewe.

       “Wananchi wanahitaji maendeleo sasa huu ushawishi wa Chadema kwenda kwa wenyeviti wa mitaa unatoka wapi? Huyu Gambo anafanya kazi, sasa vikwazo ni vya nini?” Alihoji Isaac na kusema kuwa Chadema inapaswa kutumikia wananchi na si maneno.

      Aidha, alimpongeza Rais John Magufuli kwa kumteua Gambo. Aliwashangaa madiwani wa Chadema wanaotaka siasa za chuki ambazo wananchi hawapo tayari kuzikubali.

      Kwa upande wake, Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Arusha, Shaaban Mdoe, alisema Arusha kuna siasa nyingi hivyo ni vyema viongozi wakatimiza majukumu yao ya kikazi na kutokatishwa tamaa.

Wednesday, August 17, 2016

WABUNGE WOTE WANA HADHI SAWA-DK. TULIA ACKSON

    Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Mwansasu amesema hakuna Mbunge ambaye ana hadhi ya juu kuliko mwingine katika Bunge, bali katiba inawatambua wabunge wote wapo sawa.

     Akizungumza katika mahojiano maalumu katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha ITV, Naibu Spika amesema makundi yote ya wabunge yakishaapishwa wote ni wabunge wanaofanana katika hadhi ya kufanya kazi wanapokuwa Bungeni.

       “Katiba ilivyoyaweka makundi matano ya wabunge kuanzia wanaoteuliwa na Rais, wanaochaguliwa na wananchi, wabunge wa viti maalum na wanaotoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wote wamewekwa kwa sababu maalumu kwa sababu hiyo wabunge wote ni sawa” Amesema Dkt. Tulia Aidha Naibu Spika ameitaka jamii kubadilika kutoka katika dhana kwamba mwanamke ambaye anashika nafasi ya juu katika uongozi kwamba amebebwa.

      “Wanawake wengi ambao wamepewa nafasi ya uongozi kwa kuchaguliwa au kuteuliwa ni mara chache sana hufanya vibaya na hata akifanya vibaya jamii humhukumu kwa kuwa ni mwanamke wakati kuna wanaume katika nafasi kama hiyo ambao pia unakuta wamefanya vibaya hivyo kuna changamoto hiyo katika jamii”

    Amesema Naibu Spika Dkt. Tulia. Kwa upande mwingine Naibu Spika Dkt. Tulia amesema anaongoza Bunge bila upendeleo wowote ila anafuata sheria na kanuni za kuongoza Bunge.

ARUSHA YAONGOZA KWA WIZI WA UMEME

   Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), limefanya ukaguzi wa miundombinu yake, kwa wateja 3,523 ambapo kati ya hao 165 walibainika kuibia shirika na kusababishia hasara ya zaidi ya bilioni 1.

    Akizungumza jana katika kijiji cha Seela Sing’isi, Wilayani Arumeru wakati wa ukaguzi wa miundombinu hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi wa miundombinu Taifa, John Manyama, alisema ukaguzi huo wamefanya katika kipindi cha miezi tisa na kufanikiwa kupita mikoa 13 nchini.

      Manyama amesema katika mikoa hiyo 13, Mkoa wa Arusha unaoongoza kwa kuwa na wezi wengi wa umeme, ukifuatiwa na mkoa wa Mwanza na Mbeya ni wa tatu, hali hii inawalazimu TANESCO wafanye ukaguzi wa mara kwa mara katika mikoa hiyo ili watu waache kuibia shirika la umma.

      Amesema katika maeneo ya Mererani kwenye migodi ya madini Tanzanite, kazi yao kubwa kuiba umeme, badala ya kutumia mita wanatumia 'cable' ili kuiba umeme, jambo ambalo pia ni hatari sana kwao na wafanyakazi wao.

      Manyama amesema wizi wa umeme unamadhara mengi kama kupoteza maisha kunakosababishwa na kukanyaga nyaya zinazofungwa kienyeji na wakati mwingine kusababisha nyumba kuungua.

     Amesema hakuna sababu ya wananchi kuiba umeme kwa sasa, kwani gharama zimeshuka kwa kiwango kikubwa, tofauti na siku za nyuma, hivyo ni vema kila mwananchi akafuata sheria kupata umeme halali.

       Naye Mhandisi Mkuu Mdhibiti Mapato TANESCO Makao Makuu, Poshelee Mwasenga amesema TANESCO walipoona kuna upotevu mkubwa wa umeme, ndipo walipoamua kuunda kamati hiyo maalum ya ukaguzi wa miundombinu na kukamata wezi wa umeme.

    Amesema Mkoa wa Arusha una tatizo kubwa kwa wizi wa umeme na eneo linaloongoza kwa wizi ni Meru, Wilayani Arumeru, wakifuatiwa na Mirerani kwenye migodi, jambo ambalo wao kama kamati wataendelea kufanya ukaguzi endelevu.

WAFUASI WA UPINZANI WAKAMATWA ZAMBIA

LUSAKA,

  POLISI nchini hapa wamewakamata watu 133 wanaopinga ushindi wa Rais Edgar Lungu, baada ya mshindani wake mkuu Hakainde Hichilema, kudai kuwa kura ziliibwa katika uchaguzi wa urais.

     Maandamano yalizuka katika sehemu nyingi za Mkoa wa Kusini ukiwemo mji maaarufu kwa utalii wa Livingstone. Mkuu wa Polisi Godwin Phiri, aliliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa waandamanaji walikuwa wakiwalenga wafuasi wa chama tawala na kisha kuharibu mali zao.

    “Ni mpango uliopangwa vyema na walikuwa wakisubiri mshindi atangazwe. Utulivu sasa umerejea kutokana na kufanyika kamata kamata,” aliongeza.

     Hichilema anasema kuwa ana mpango wa kupeleka kesi mahakamani kupinga matokeo hayo. Licha ya malalamiko ya upinzani kuhusu wizi na udanganyifu wa kura, Lungu alitangazwa na Tume ya Uchaguzi kutetea urais kwa kupata asilimia 50.35 katika uchaguzi wenye ushindani mkali ambao ulifanyika Alhamisi iliyopita.

    Mpinzani wake mfanyabiashara Hichilema kutoka Chama cha United Party for National Development (UPND) alipata asilimia 47.67 ya kura. Upinzani nchini umeishutumu Tume ya Uchaguzi (ECZ) kuingia makubaliano ya kumpendelea Rais Lungu na ameapa kupinga matokeo hayo katika Mahakama ya Katiba.

     Rais wa chama cha Movement for Multiparty Democracy MMD), Dk Nevers Mumba, amesema analo mkononi pingamizi la kuzuia matokeo yasitangazwe, jambo ambalo lilipuuzwa na tume.

     “Tulienda mahakamani Jumapili na tukapewa pingamizi la kuzuia ECZ isiendelee kutangaza matokeo ya uchaguzi na wakapuuza agizo la mahakama na kuendelea kutangaza kura zenye mgogoro,” alisema.

ALIYEDAIWA KUMUUA MKEWE KWA NYUNDO AKAMATWA

Shinyanga.  

    Jeshi  la polisi mkoani  Shinyanga linamshikilia mkazi  wa Kijiji  cha  Busongo  wilayani  Kahama  anayetuhumiwa kumuua  mke wake kwa kumpiga na nyundo kichwani kisha kukimbia baada  ya kutenda unyama huo.

     Kamanda wa  polisi  mkoani  Shinyanga  Muliro  Jumanne amesema kuwa wamemkamata mtuhumiwa  huyo ambaye anadaiwa kufanya  mauaji  ya Monica  Manyabhuluba   kisha  kutoweka  kukwepa  kunaswa  na mkono wa sheria.

     Mtuhumiwa  huyo ambaye alifanya mauaji  hayo Agosti  14 mwaka huu kisha kukimbia  amekamatwa leo akiwa Kahama mjini , baada ya taarifa kusambazwa maeneo mbalimbali  na wananchi  kutoa ushirikiano kwa polisi uliofanikisha kumtia mbaroni.

WALIOJERUHIWA NA MAJAMBAZI TABORA, WAFARIKI

   Kamanda wa Mkoa wa Tabora, Khamis Issah Sulemani.

     WATU wawili waliokuwa wamejeruhiwa kwa risasi wakati wa mapambano na majambazi katika kijiji cha Isila, wilaya ya Uyui mkoa Tabora, wamefariki dunia wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora.

     Tukio hilo ambalo lilitokea usiku wa kuamkia juzi Jumapili ambapo majambazi watatu wakiwa na bunduki aina ya SMG, walivamia nyumbani kwa mfanyabiashara wa ng’ombe na kuwajeruhiwa kwa risasi watu wawili huku jambazi mmoja akiuawa wakati wa majibizano ya risasi na polisi na wengine wawili kutokomea kusikojulikana.

     Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo vya Bw. Mirija Bapa na ndugu yake Umoja Ubapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Khamis Selemani amesema kuwa watu hao walizidiwa ghafla wakati wakipata matibabu na kupeleka vifo vyao.

      Kamanda Selemani amesema kuwa Jeshi la Polisi bado linaendelea kuwasaka watuhumiwa wawili waliojeruhiwa na polisi katika tukio na kukimbia ambapo ametoa wito kujisalimisha wenyewe ili sheria ifuate mkondo wake.

SEMENYA KUSHIRIKI MBIO ZA MCHUJO LEO

   Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya, hii leo atashiriki mbio zinazosubiriwa kwa hamu za mita 800 mchujo kwa akina mama.

      Utata umekumba taaluma ya Semenya tangu anafanyiwe uchunguzi wa jinsia yake mwaka 2009, ambapo aligunduliwa kuwa na viwango vya juu vya chembe chembe za kiume.

     Kabla ya kufanyika kwa mashindano ya olimpiki ya Rio, kulikuwa na maoni tofauti ikiwa Semenya angeweza kuruhusiwa kushiriki mbio za wanawake.

     Anatarajiwa kushinda mbio hizo na hata kuvunja rekodi ya miaka 33. Watu nchini Afrika Kusini wameingia kwenye mitandao ya kijamii kumtetea Semenya na hata kufikia kiwango cha kumtungia shairi.

Thursday, August 4, 2016

EVANS AVEVA AACHIWA KWA DHAMANA

      Huku Rais wa Simba, Evans Aveva akiwa ameachiwa kwa dhamana, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) imesema ilimshikilia kwa kuwa fedha dola 300,000 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Simba katika benki moja, kwenda kwenye akaunti na benki nyingine.

     Fedha hizo ni zile za malipo ya mwanasoka Emmanuel Okwi aliyeuzwa dola 319,212 lakini fedha hizo hazikulipwa mapema baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage kufanya haraka katika mauzo hali iliyofanya uongozi wa Simba ulioingia madarakani kuanza kuhaha kupambana na Etoile hadi kufikia Fifa ili walipwe.

      Mkuu wa Uchunguzi wa Sekta ya Umma ya Takukuru, LEonard Mtalai amesema akaunti hiyo iliyohamishiwa dola 300,000 ni ya Aveva na baada ya hapo, dola 62,000 zilihamishwa kwenda Hong Kong na sasa Takukuru inashirikiana na wenzao wa nchini humo ili kujua kilichonunuliwa kupitia fedha hizo.

     Taarifa nyingine, zinaeleza fedha hizo dola 62,000 zilitumika kununua nyasi bandia ambazo tayari zimetua nchini kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa mazoezi enero la Bunju na ujenzi umeanza.

     Ofisa huyo wa Takukuru, amethibitisha kuhojiwa kwa watu kadhaa pamoja na Aveva na kusema bado wanaendelea na uchunguzi. “Tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu kuendelea na uchunguzi ili ukikamilika, kama tutagundua kuna matatizo basi mara moja sheria itafuata mkondo wake,” alisema.

     Awali, alieleza waliamua kuanza uchunguzi baada ya baada ya kupata taarifa za kiintelejensia kwamba kuna fedha nyingi zilihamishwa kutoka kwenye akaunti moja kutoka katika benki moja, kwenda akaunti nyingine katika benki tofauti.

    “Hii ilitufanya mara moja kuanza uchunguzi,” alisisitiza Mtalai.

"TIP TOP HATUISHI KIBOSI BOSI" MADEE

     Msanii Madee leo ameweka wazi mkanganyiko ambao wengi walikuwa nao kuhusu msanii anayemsimamia Dogo Janja, mbaye pia yuko chini ya Tip Top ambayo inamsimamia yeye Madee.

      Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Madee amesema ingawa Dogo Janja yupo chini yake, lakini iwapo kuna kazi anatakiwa kuifanya, lazima afanye mawasiliano na Babu Tale, na kufikia uamuzi kwa pamoja, tofauti na wengi wakivyofikiri kuwa yeye ndio ana uamuzi na Dogo Janja.

       “Mtu akitaka collabo na Dogo Janja tunawasiliana na Babu Tale, na kama ishu ya kazi hawezi kukataa, lakini lazima tujadili, kwetu hatuishi kibosi bosi, kama ni jambo la msingi linawekwa mezani kila mtu anatoa maoni yake, kama afanye au asifanye”, alisema Madee.

      Madee ambaye pia alianza kwa kumtoa msanii Raymond mpaka akachukuliwa na wasafi ambako yuko sasa, amesema anajivunia mafanikio ya msanii huyo, kwani tayari yupo kwenye historia yake.

Saturday, July 30, 2016

SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI AHAMISHIA KAMATI DODOMA

    Spika wa Bunge, Job Ndugai  Dar es Salaam.

     Spika wa Bunge, Job Ndugai ameagiza mikutano yote ya Kamati za Bunge itakayoanza Agosti 22 mpaka Septemba 4 mwaka huu ifanyikie mjini Dodoma.

     Taarifa iliyotolewa na Bunge leo Spika Ndugai ameeleza kuwa Bunge ni muhimili ambao tayari ulishatekeleza kwa vitendo kuhamia Dodoma.

Thursday, July 28, 2016

Al-shabaab WASHAMBULIA MTAMBO WA MAWASILIANO KENYA

    Wanamgambo wa al-Shabab wamekuwa wakishambulia Kenya mara kwa mara Washukiwa wa kundi la Al-Shabaab mapema leo Alhamisi wameshambulia na kulipua mtambo wa mawasiliano ulioko katika mji wa Fino, Lafey katika kaunti ndogo ya Mandera nchini Kenya.

  Afisa mkuu wa Polisi huko Lafey, Bosita Omukolongolo, amesema kuwa kisa hicho kilitokea saa nane usiku.

      Afisa huyo wa Polisi anasema kuwa walikabiliana vikali na wanamgambo hao, lakini hakuna maafa yaliyoripotiwa upande wa polisi waliokuwa wakiulinda mlingoti huo wenye vifaa vya kupeperusha mawasiliano.

     Kundi la Al- Shaabab, ambalo lina makao yake nchini Somalia, limehusika na mashambulizi ya mara kwa mara pamoja na mauaji nchini Kenya na mataifa kadhaa ya Afrika Mashariki na upembe wa Afrika.

Monday, July 25, 2016

SUMATRA KUISHTAKI UDART KUKAIDI AGIZO

    Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imesema wakati wowote kuanzia sasa itaufikisha mahakamani uongozi wa Mabasi ya Kwenda Haraka (Udart) kwa tuhuma za kuwatoza abiria nauli zaidi kinyume na matangazo yao.

      Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, mashtaka dhidi ya uongozi huo yameshaandaliwa na kilichobaki ni kuyafikisha mahakamani.

     Ngewe alisema Udart inatoza nauli ya Sh650 badala ya 400 kwa ruti ya kutoka Mbezi hadi Kimara na kuwatoza Sh650 nyingine kutoka Kimara hadi Posta.

      Akizungumzia hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Udart, David Mgwassa alisema kama wana ushahidi waendelee na hatua yao ya mahakamani.

VIJANA WADOGO WAFANYISHWA NGONO NA WANYAMA MOMBASA

    MOMBASA inafahamika kwa mambo mengi, ikiwemo madawa, ukahaba na mengineyo kibao lakini hili linalofanyika eneo la Mtwapa limetia fora. Ukahaba si jambo tena la kujificha bali ni jambo ambalo watu wanalipia kulishuhudia live.

       Kumekuwepo vitendo ambapo wanaume na wanawake hulipia kwa ajili ya kuwaangalia vijana wadogo wanaofanya ngono na wanyama. Vijana hao wadogo wa kiume na kike hupatiwa mafunzo kwa ajili ya shughuli hiyo kutokana na hali ngumu ya maisha inayosababishwa na umasikini.

        Mmoja wa mashuhuda wa vitendo hivyo vya udhalilishaji anasema vijana hao kabla ya kufanyishwa ngono na wanyama, hutumia madawa ya kulevya na baada ya kulewa hupewa dakika zisizozidi 20 kufanya ngono na wanyama na kupatiwa malipo kiduchu. Jambo linalosikitisha na baya zaidi ni kwamba vijana hawa wa kike na kiume umri wao ni kati ya miaka 8 hadi 17.

     Kila ninapofikiria jinsi wanaume na wanawake wanavyolipia kwa ajili ya kuangalia hii laana huwa nashindwa kuelewa utu wao.

    Je, ingengukwaje kama vijana hawa wangekuwa watoto wao? Nashindwa kuelewa kabisa hii ni aina gani ya biashara inayodhalilisha watoto – alisema shuhuda huyo.

     Wanyama wanaotumika sana katika vitendo hivyo ni mbwa ila sababu ya kwa nini wanawatumia wanyama hao haikufahamika. Chanzo: standardmedia.co.ke

"Riek Machar" APINDULIWA SUDAN KUSINI

     Maafisa wa serikali ya Sudan Kusini wameiambia BBC kwamba wanamtambua waziri wa madini Taban Deng Gai kuwa makamu wa kwanza wa rais akichukua mahala pake Riek Machar ambaye alitoroka mji mkuu wa Juba baada ya mapigano makali mapema mwezi huu.

     Hatahivyo msemaji wa Machar amesema kuwa wameukataa uteuzi wa Bwana Deng. Bwana Deng alikuwa mpatanishi mkuu wa Machar na hatua yake ya kuchukua wadhfa huo unaonyesha kuwa wametofautiana,

    hivyobasi kuweka mgawanyiko katika upinzani ambao unazidi kutatiza juhudi za kupata amani nchini Sudan Kusini ,kulingana na wachanganuzi.

       Takriban watu 300 walifariki katika mapigano mapema mwezi huu katika mji mkuu wa Juba,kati ya vikosi vilivyo vitiifu kwa Machar na mpinzani wake rais Salva Kiiir.

FAHAMU UMUHIMU WA KUNYWA GREEN JUICE KWA AFYA YA MWILI

    Good morning Loves, so kwa wale watu wa fitness na wanaopenda to keep their bodies healthy nadhani mtakuwa mnajua green juice ni nini na jinsi ya kuitengeneza and all that.

     Since I spend most of my time reading and writing nimekutana na sehemu mtu anauliza hii green juice inasaidia nini haswa, yaani faida zake ni nini, kwanini unywe green juice? Kwanini unywe Green Juice?

    1.Inasafisha ngozi yako. Baada ya kama wiki mbili za kunywa green juice utaanza kuona mabadiliko, ngozi yako itaanza kuwa laini na hata madoa na makovu uliyokuwa nayo yataanza kupotea. If you make a habit ya kuinywa kila siku basi ngozi yako ndio itatakata kabisa.

   2.Inakupa nguvu. Kwa wale ambao tayari mnakunywa green juice mtakuwa mnajua kuwa unatakiwa kuinywa on ana empty stomach.. kunywa ukiwa huna kitu tumboni, kaa kama nusu saa ndio unaweza kunywa au kula kitu kingine.

       Green juice ina nutrients nyingi na hivyo ni bora kama ukiinywa asubuhi kabla hujala kitu kingine chochote.

      3.Inasaidia digestion/inakupa choo Green juice inasaidia kusaga chakula tumboni, hivyo hata kama ulikuwa hupati choo just kunywa green juice for a whole day na you will feel as light as a feather siku inayofuata.

      Kwa wale wanaokunywa green juice hawapati gesi tumboni ovyo wala kuvimbiwa.

   4.Inapunguza uzito. We all know kwamba ukitaka kupungua sio mazoezi tu ndo yatakayo kusaidia, bali ni vitu unavyokula pia..Na green juice ni kitu kimoja important sana ambacho ni lazima kuweka katika diet yako ili uweze kupungua vizuri bila matatizo.

    5.Inasafisha viungo vya ndani ya mwili. Kama vile figo, mapafu, moyo nk. Kama wataka kufanya full body cleanse basi tumia Green juice.

SUDAN KUSINI YAWAUWA WANAJESHI WAKE WAWILI

   Taifa la Sudan Kusini limewaua wanajeshi wake 2 kwa kuwapiga risasi baada ya kupatikana na hatia ya kuwauwa wanandoa wawili ikiwa ni kisa cha kwanza cha mauaji kulingana na vyombo vya habari.

      Wanajeshi hao walipigwa risasi mbele ya gwaride la kijeshi katika mji wa Wau Kaskazini Magharibi,huku wakaazi na familia za wanajeshi hao zikikongamana katika eneo hilo kuona mauaji hayo.

      Mahakama ya kijeshi iliwapata na hatia wanajeshi Meja Atian Deng na Matem Ariic Mayom,kufuatia kukamatwa kwao mnamo mwezi Julai tarehe 17 katika eneo moja la wakaazi la Wau.

Rio2016: WANARIADHA WA TZ WAPATA UFADHILI

    Timu ya taifa ya Tanzania katika mchezo wa riadha itayokwenda kuiwakilisha nchini hiyo katika michuano ijayo ya Olimipiki imepata udhamini wa vifaa vya michezo pamoja na fedha za kiasi cha shilingi milioni tano.

     Udhamini huo umetolewa na shirika la hifadhi za taifa (Tanapa)kupitia kwa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo na kukabidhiwa kwa wachezaji hao.

      Ufadhili huu unalengo kuisadia timu ya taifa na kuwezesha kufanya vizuri katika michuano ya Olimpiki na pia kusaidia kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania.

     Baada ya kupata ufadhili huo .Rais wa shirikisho la riadha nchini Antony Mtaka amesema fedha hizo zitatumika kulipia kadi za bima ya afya ya wachezaji hao na familia zao kwa muda wa mwaka mmoja.

      Akizungumza kwa niaba ya wachezaji hao, Alfonce Felix amesema ufadhili huo utawaongezea chachu ya ushindi na kuitangaza nchi.

      Timu hiyo ya riadha yenye wachezaji wanne inaendelea na maandalizi ya mwisho chini ya kocha wake Francis John katika kambi yake ya West Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro.

MADRID WALIMTOSA POGBA MARA MBILI

    MADRID, HISPANIA. PAUL Pogba wakati wowote wiki hii huenda akatua Man United kwa pesa ya maana, lakini imefichuka kuwa Rais wa Real Madrid, Florentino Perez alimkataa mara mbili katika klabu yake.

      Baada ya kuona hali kuwa hivyo licha ya kocha wa Real, Zinedine Zidane kukiri anamkubali kiungo huyo, Pogba sasa mawazo yake ni kurejea Old Trafford.

       Ripoti zimefichua kwamba Pogba mara mbili tofauti alipelekewa ofa Real Madrid, lakini Perez alimkataa. Kwanza ilikuwa mwaka 2012 mkataba wake ulipofika mwisho Man United lakini Perez alijipa imani kwamba kwa kuwa United walimuachia kirahisi basi hawezi kuwa bora.

      Mara ya pili ilikuwa mwaka 2014, meneja mkuu wa Real, Jose Angel Sanchez alizungumza na Juventus na kukubaliana ada ya Euro 60 milioni lakini Perez tena akamkataa.

FABRIGAS HUMWAMBII KITU KWA MOURINHO

    LONDON, ENGLAND. KIUNGO Cesc Fabregas amekiri kwamba hakuna kipindi alichofurahia sana kucheza soka katika maisha yake kama wakati akiwa chini ya kocha Jose Mourinho.

     Kiungo huyo wa Chelsea alisema kufanya kazi chini ya kocha huyo mpya wa Manchester United, Mourinho ni raha sana. Mourinho, ndiye aliyemrudisha Fabregas kwenye Ligi Kuu England akitokea Barcelona na kutua Chelsea,

      lakini Desemba mwaka jana kocha huyo alipoteza kibarua chake Chelsea na sasa amejiunga na Man United. Fabregas alisema:

    "Kufanya kazi na Mourinho ilikuwa poa sana.

SIMU ZA NOKIA KUJA KIVINGINE NA MFUMO WA ANDROID

   Nokia imeripotiwa kuwa kwenye mipango ya kurejea kwenye soko la smartphone na simu mpya zinazotumia mfumo mpya wa Google, Android Nougat, version 7.0.

     Simu hizo zinatarajiwa kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi huu na zinatarajiwa kuzuia majina vumbi kama simu mpya za Samsung, Galaxy S7, S7 Edge na S7 Active.

     Zitakuwa na screen yenye ukubwa inchi 5.2.

Wednesday, July 20, 2016

MANENO YA DEMBA BA BAADA YA KUTEMBELEWA NA ALIYE MVUNJA MGUU

    Lilikuwa ni tukio la kusikitisha pale mshambuliaji nyota wa zamani wa Newcastle na Chelsea Demba Ba alipovunjia mguu akiwa uwanjani kutekeleza majukumu yake.

     Jina la Ba limekuwa kwenye vyombo vya habari baada ya kuvunjika mkuu wake wakati wa mchezo wa Shanghai derby. Akicheza dhidi ya Shanghai SIPG, striker huyo wa Shanghai Shenhua alishuhudia mwish wake wa msimu pale mguu wake wa kulia ulipopinda mithili ya plastic laini.

    Siku ya Jumanne, Sun Xiang alimtembelea Demba Ba hospitali ambapo pia Ba alizungumza na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza tangu alipoumia.

     Demba Ba: Nimefurahi timu imeshinda Akizungumza na kituo cha television cha Chinese TV, Demba Ba alisema: “Ilikuwa ni siku ngumu (Jumapili) kwa upande wangu na timu nzima, lakini ninafurahi tulishinda.” “Napenda kuwashukuru mashabiki wote ambao wanakuja kunijulia hali hospitalini.”

      Imeripotiwa pia na vymbo vya habari vya China kwamba, Demba Ba amemsamehe Sun Xiang kwa kusema: “Msimlaumu, mimi nae

DEMBA BA' ASEMA HATOACHA KUCHEZA SOKA

    Demba Ba ndiye mfungaji bora ligini kwa sasa Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Demba Ba amesema hataacha kucheza soka hata baada ya kuvunjika mguu akicheza.

      Ba, ambaye kwa sasa huchezea Shanghai Shenhua, alivunjika mguu baada ya kukabwa akicheza mechi ya Ligi Kuu ya Uchina. Baada ya mechi hiyo, mkufunzi wa mshambuliaji huyo wa Senegal Gregorio Manzano alisema jeraha hilo “huenda likafikisha kikomo uchezaji wake”.

     "Hili ni jeraha mbaya sana lakini ninaweza kujikwamua. Sitafikisha kikomo uchezaji wangu hapa, hilo nina uhakika nalo,” amesema Ba, mwenye umri wa miaka 31. “Msimu hapa unamalizika Novemba na kuanza Machi. Nitajizatiti kurejea kwa wakati kwa msimu utakaofuata.” Demba Ba avunjika mguu uwanjani Demba Ba alichezea West Ham, Newcastle na Chelsea katika Ligi ya Premia.

    Demba Ba akichezea klabu ya Chelsea Alijiunga na Shenhua kutoka klabu ya Besiktas ya Uturuki, akinunuliwa takriban pauni 12 milioni mwezi Julai mwaka jana. Kwa sasa, ndiye mfungaji mabao bora Ligi Kuu ya Uchina akiwa na magoli 14 kutoka mechi 18.

ALIYEMUUA MKE WAKE KUKATILI ATIWA MBARONI, KAGERA

   Jeshi la polisi mkoani Kagera limefanikiwa kumtia mbaroni Sendon Andrew mkazi wa kijiji cha Byamtemba kilichopo katika kata ya Nsunga iliyoko wilayani Misenyi

     mkoani Kagera aliyekimbilia nchi jirani ya Uganda kwa tuhuma ya kumuua  kikatili mke wake Rosemery Desdery kwa kumpigwa fimbo na mateke katika seheme mbalimbali za mwili wake.

     Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera mrakibu mwandamizi wa jeshi hilo Abel Mtagwa ambaye pia ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa mkoa huo,amesema mtuhumiwa huyo baada ya kufanya

      mauaji hayo kwenye eneo la Sebure ya nyumba yao alimburuza marehemu hadi kwenye chumba chao cha kulala na kumfunika na blanketi na wakati akitoroka aliwambia watoto wao kuwa amemuacha mama yao amelala na anaondoka atarudi kesho yake.

     Kaimu kamanda huyo akitoa wito kwa wananchi amesema jeshi hilo halitawavumilia mtu yoyote atakayejihusisha na vitendo vya mauaji kwa kuwa vitendo  hivyo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

LULU AFUNGUKA HANA TATIZO NA HAMISA MOBETO

    Msanii wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu amekanusha tetesi za kwamba ana bifu na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Dj Majay, Hamisa Mobeto.

     Muigizaji huyo ambaye kwa saa anadaiwa kutoka kimapenzi na Majay, aliingia kwenye malumbano na baadhi ya mashabiki wa Mobeto katika mitandao ya kijamii wakimtuhudi kuiba bwana. Akiongea katika kipindi cha Weekend Chart Show cha Clouds TV Ijumaa iliyopita, Lulu amesema hata tatizo na Mobeto ambaye ni mama wa mtoto mmoja aliyezaa na Majay.

     “Sipendi sana kuongelea issue ambayo nitakuwa kama nachochea, mimi ni mtu fulani very peace, very very peace, sina tatizo naye,” alisema Lulu.

      Akiongelea kama ni kweli kuna watu walikuwa wanatumwa na Mobeto ili wamtukane alisema “Siwezi kujua kwa sababu sijafuatwa direct, lakini sina tatizo naye, mtu akinipa kijembe namchukulia kama mtu kanipa kijembe” Hata hivyo, Lulu na CEO wa EFM, Dj Majay kwa sasa wapo karibu zaidi, kwani wawili hao wamekuwa wakipost picha zao katika mitandao ya kijamii wakiwa pamoja.

MKUTANO MAALUMU CCM:MADADA POA WAVAMIA

Dodoma.

   BWasichana wanaofanya shughuli ya kuuza miili, maarufu kama dada poa wameongezeka katika viunga vya mji wa Dodoma tayari kuvizia wageni watakaohudhuria Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM.

     Wasichana hao, ambao Mwananchi imebaini wanatoka katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha, Iringa na Mbeya, wameonekana kwenye maeneo mbalimbali ya starehe wakisaka wanaume nyakati za usiku.

      Madada poa ambao kwa kawaida hufurika mjini hapa wakati wa vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano, wamekuwa wakiwatoza wateja hadi Sh30,000 kwa ambaye anataka kulala naye hadi asubuhi.

      “Kama unataka madada poa nenda kwenye baa maarufu za mjini hapa nyakati za usiku. Mwanangu mbona mfuko wako tu.

     Ukitaka wa kulala naye hadi asubuhi, ukitaka wa saa kazi kwako,” alisema mmoja wa wanaume katika moja ya baa maarufu mjini hapa.

DONALD TRUMP APITISHWA RASMI NA CHAMA CHA CHAKE CHA REPUBLICAN KUWA MGOMBEA RASMI WA URAISI MAREKANI

     Donald Trump hatimaye ateuliwa sasa kuwa mgombea rasmi wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi November mwaka huu.

     Trump amepata uungwaji mkono na wajumbe kutoka majimbo na wilaya za Marekani katika kura mchujo wa kumpata mgombea wa nafasi hiyo kupitia chama chake cha Republican kupitia mkutano mkuu wa chama chake mjini Cleveland.

      Baada ya kuchaguliwa kuwa mgombea urais Donald Trump alitoa shukran zake kupitia mtandao wa twitter,na imetanabahishwa kwamba gavana wa jimbo la Indiana Mike Pence,

     ndiye mgombea mwenza .Taarifa zaidi zinasema watoto wawili wa Donald Trump wa kiume Donald na pia bintiye Tiffany wanatarajiwa kuhutubia mkutano mkuu wa wanachama wa chama hicho. Source: BBC

Tuesday, July 19, 2016

MLINZI AAMUA KUJINYONGA KWA KINACHODAIWA ALIAMBUKIZWA UKIMWI

   Mpanda. Mlinzi wa  Kampuni ya  Ulinzi ya Imara , Samwel Alcado (39) amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya chumba chake kutokana na kile kinachodaiwa ni kugundulika kuwa ana virusi vya Ukimwi (VVU).

    Mlinzi huyo ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mji wa Zamani Manispaa ya Mpanda amejinyonga kwa kutumia shati lake. Mwenyekiti wa mtaa huo, Margret John amesema tukio hilo  limetokea  leo  majira  saa kumi na moja alfajiri ndani ya   chumba alichokuwa  akiishi   Alcado.

      Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda amethibitisha kutokea kwa kifo hicho akisema uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika ili kubaini ukweli halisi wa tukio hilo.

MZEE MAJUTO ADAI FILAMU YAKE IJAYO NI ZAIDI YA ZILIZOPITA

   Msanii wa filamu za kuchekesha Bongo, King Majuto amesema kuwa filamu yake mpya ijayo ni zaidi ya filamu zake zilizopita.

    Akiongea na Times FM, “Hii ina ujumbe wa kuelimisha jamii kuachana na mambo Ambayo hayana manufaa kwa maisha ya sasa na nimewashirikisha wasanii mbalimbali maarufu.”

     Aidha Majuto amefafanua kuwa sababu ya kuchelewa kuiachia filamu hiyo kama alivyopanga ni kutokana na kuupisha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

AKAMATWA NA MIRUNGI 'AIRPORT'

      Aziza Suleiman Ally Jeshi la Polisi Viwanja vya Ndege Tanzania wakishirikiana na maafisa usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  (JNIA), wamemtia mbaroni mama mmoja aliyetambulika kwa jina la Aziza Suleiman Ally (pichani), mkazi wa Mombasa Kwamchina,  Zanzibar akiwa na mirungi.

     Imeelezwa kuwa Aziza alinaswa uwanjani hapo Julai 13, mwa huu saa nane mchana akiwa ameficha mirungi hiyo sehemu mbalimbali ya mwili wake kama vile kwapani, kwenye matiti na sehemu za siri.  Mirungi Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Viwanja vya Ndege Tanzania, ACP Maltin Otieno alisema ni kweli tukio hilo lilitokea.

    Kamanda Otieno alisema kuwa Aziza alinaswa uwanjani hapo akiwa anajiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Msumbiji kwenda nchini humo akiwa ameficha mirungi mibichi pakiti nne sehemu mbalimbali za mwili wake.

      Kamanda wa Viwanja vya Ndege Tanzania, ACP Maltin Otieno “Ni kweli sisi jeshi la polisi kwa kushirikiana na Usalama wa Taifa wa uwanjani hapa, tumemkamata Aziza Suleiman Ally (34) mkazi wa Mombasa Kwamchina Zanzibar raia wa hapa Tanzania akiwa na mirungi pakiti nne za uzito wa kilo nne akiwa amezificha sehemu mbalimbali za mwili,” alisema kamanda huyo.

    Hata hivyo, alisema kuwa thamani ya mirungi hiyo bado haijajulikana na kutoa honyo kali kwa wale ambao wanajidanganya kutaka kupitisha madawa ya kulevya uwanjani hapo kwani ni lazima watakamatwa.

SHULE 70 ZA UPILI ZATEKETEZWA KENYA

   Shule 70 za upili zateketezwa Kenya Shule 70 za upili zimeteketezwa moto na wanafunzi wenye hasira nchini Kenya. Waziri wa elimu nchini humo Fred Matiangi ameiambia kamati ya bunge iliyoundwa kupeleleza wimbi la shule kuteketezwa kuwa hakujakuwa na hata wanafunzi 20 waliohukumiwa kwa kuteketeza mali ya umma kwa sababi moja au nyingine kati ya visa 317 zilizoripotiwa kati ya mwaka wa 2007 -2016.

     Shule 317 ziliteketezwa kati ya mwaka wa 2007 -2016. ''Endapo serikali itachukua hatua dhidi ya wale watakaoteketeza mabweni yao au hata madarasa bila shaka wale wanaoiga wataogopa'' alisema bwana Matiangi.

      ''Mara nyingi tumegundua kuwa zile shule ambazo zinachunguzwa kwa sababu ya wizi wa pesa za kufadhili masomo ya bure na fedha za kununua vitabu vya wanafunzi zinateketezwa kwa sababu finyu sana''.  

 
      Walimu 15 wakuu wanachunguzwa kulingana na taasisi inayosimamia walimu nchini Kenya TSC. Walimu 15 wakuu wanachunguzwa kulingana na taasisi inayosimamia walimu nchini Kenya TSC. Wandani wa maswala ya elimu nchini Kenya akiwemo katibu mkuu wa muungano wa walimu KNUT bwana Wilson Sosion amelaumu mabadiliko ya sera yaliyotolewa na wizara ya elimu kama vile kuongeza muda wa muhula wa pili, na kupiga marufuku likizo ya kati ya muhula ujao mbali na kupiga marufuku wazazi kuwatembelea wanafunzi shuleni kama sababu zinazochochea wimbi hili la moto shuleni.

    Katibu mkuu wa muungano wa walimu KNUT bwana Wilson Sosion amelaumu mabadiliko ya sera yaliyotolewa na wizara ya elimu kwa machafuko haya yanayoshuhudiwa Hata hivyo waziri Matiang'i akijitetea aliiambia kamati hiyo ya bunge kuwa kabla ya mabadiliko hayo kutangazwa shule 90 zilikuwa zimeteketezwa tayari.

WATUMISHI SITA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA WATIMULIWE

    Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga. Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga, amewasimaisha kazi watumishi sita wa Halmashauri wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kutoa taarifa za uongo kwa kiongozi wa mbio za mwenge.

     Watumishi hao ambao wengine ni wakuu wa idara wamesimamishwa kazi baada ya kubainika kutoa taarifa za uongo kuhusu miradi iliyozinduliwa na kufunguliwa na mbio za Mwenge mkoani humo.

      Wakati wa Mbio za Mwenge Mkoani humo Kiongozi wa Mbio za Mwenge George Mbijima, alibaini kuwa mradi wa vijana wa Membe kati kuwa ni mradi hewa huku halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ikitoa hundi hewa kwa saccos ya vijana ya mjini Kigoma.

     Kufuatia matukio hayo ya Uzembe na Udanganyifu ndipo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emanuel Maganga alipochukua hatua ya kuwasimamisha viongozi hao ambao walisika na udanganyifu huo.

AINA YA WATU WANAO HARIBU UHUSIANO

   Katika mahusiano kabla hujaingia ni lazima umshirikishe rafiki au ndugu yako wa karibu lakini potelea yote moyo wako lazima ulizie kuaza mahusiano na huyo mtu ambaye unatarajia kuwa naye tukumbuke kuwa mahusiano ni ya wawili na pia hayaangalii kabila,umri.

     umbile au,kipato japo wengi husema lazima uangalie vitu kama hivyo ili kujiridhisha na nafsi yako lakini pia kati ya watu utakapokuwa una tembea naye wakushangae kuwa una tembea|kuhusiana kimahusiano na mwanamke au mwanaume mnzuri.

     Mungu ndiye mgawaridhiki,unzuri na makabila pia kwani kuna msemo unaosema mfungwa hachagui gereza laity kama mfungwa angekuwa anachagua wapi akafungwe basi wa Tanzania wangeomba kufungwa china au nchi yeyote nzuri nje ya nchi hii, ndivyo ilivyo kwenye mapenzi kuna makabila,

     maumbile au kipato cha mtu kinafanya kuwa ajute sana  kwanini alikuwa hivyo ni kwa sababu tu ya maneno ya watu juu ya kabila au vitu vingine ambavyo vinamfanya ashindwa kufurahia mahusiano..

     Watu wanaochangia mahusiano ya watu kuharibika au kutodumu bila kugombana. Marafiki Hao ni watu ambao huwa wa kwanza kuharibu mahusiano ya watu wako radhi kufanya chochote ili tu kuona hamko sawa katika mahusiano na lengo laweza kutaka kuona wapenzi hao wanaachana ni swali gumu kwa wengi je,kweli rafiki yamgu kipenzi anaweza nifanyia hivi kunigombanisha na mpenzi wangu? Ukweli ni kwamba rafiki yako anaweza kukugombanisha vizuri tu na mwandani wako kama hauko makini tunabidi kutoamini sana marafiki katika mahusiano yamkini anaweza kuwa kigeugeu kati yenu ili kuwaharibu kabisa wawili nyiye matukio mengi ya kuachana marafiki huwa wakuchochea sana ili watu waachane na pia mpe mpenzi wako nafasi katika jambo Fulani ulilolisikia juu ya mpenzi wako.

      Ndugu Hakuna maisha ambayo mtu utakosa ndugu yaweza kuwa ndugu kutoka kwa upande wa bibi mdogo babu mdogo nk, hao wote ni ndugu zetu nakuamini kuwa ndugu sio ule uliyezaliwa naye tu hawa huwa ni vichochezi nakutoa kassoro nyingi kwa mtu ambaye analetwa kutambulishwa nyumbani kwanza huaza na miguno( mmh) ndo wifi|shemeji mmh jamani aya hongera lakini mmh yani hutafuta sababu tu wa kuanzisha majabizano na ukikosea kuwapa nafasi kuuliza kuna nini utaaza kusikia kasoro watakazo

     zitoa na wakimalizia ‘kweli mapenzi ni upofu mmh ‘ kitu ambacho wengi huaza kufikiria sana na kukosea kuwapa nafasi ndugu zao kuwafanyia maamuzi katika mahusiano na kuishia kumuumiza mtu kwa faida tu ya ndugu.

      Wazazi Tunajua fika bila wazazi yamkini tusingelijua jua,mwenzi,au nyota na mbalamwenzi lakini wazazi wengi wameumiza mioyo ya watoto wao na hata wale waliowezwa kuachwa sababu ukiuliza atakuambia ‘isingelikuwa mama \baba Yake hakika angenioa’ lakini pia jibu utasikia kwa mtenda ‘kiukweli sikumpenda niliona si chaguo la mwanangu na licha ya hivyo kuna kasoro nimeona kwahiyo nisingependa awe mkwe wangu’ wazazi huacha majeraha kwa wengi na ata kusababisha wengi kujiua au kushuka thamani kwa kuharibika kisaikolojia. Mzazi,Ndugu,Rafiki kamwe usiwe chanzo cha mtu Fulani kuharibu

     mahusiano yake kumbuka chozi lake la siku moja laweza kuwa laana katika maisha yako ata kwa miaka kumi amini kuwa mahusiano ni ya watu wawili walioridhiana kwa kila jambo bila kuangalia kasoro zao wenyewe yaani wamehamua kubebana kwa kila hali wanahitaji tu Baraka zenu na

     kuwarekebisha kidogo walipokosea lakini huna haki kumwambia hakika hutakiwi kuoa|kuolewa na mtu huyu mpe nafasi ya kuchagua kwani ni mtu mzima anajua lipi baya na lipi nzuri katika maisha yake yeye mwenyewe,…

NAMTAFUTA BABA YANGU

   Naitwa Emmanuel jastin Simba namtafuta baba mzazi jastini Simba anaishi Kigoma mwanga vamia Mimi nipo kwa Dodoma kwa mawasiliano namba yangu ya simu 0759445421 

CHAMELEON ASEMA HANA TATIZO NA DIAMOND

     Msanii mkongwe wa muziki kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone amefunguka kwa kusema kuwa hana tatizo na hit maker wa wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz.

    Mitandao ya kijamii ilidai wawili hao hawakuwa sawa kwa muda mrefu kutokana na madai ya kuwa Jose Chameleone kumdengulia Diamond baada ya kuombwa kolabo, lakini hakuna aliyewai kuzungumzia tetesi hizo.

     Jumanne hii Jose amesema hakuwai kuwa na tatizo na Diamond kama baadhi ya watu wanavyozungumza. “I know how much hard work it takes to build a name and how we are all relevant to flying Africa Music to the world.

      I can see people trying to build beef lines between me and Diamond Platnumz all these years,” aliandika Jose kupitia instagrm.

     Aliongeza, “All I can say is go higher my brother the sky ain’t the limit.Stay strong and God bless you more,” Baada ya kusema hivyo, mashabiki wa Diamond pamoja na wadau mbalimbali wa muziki katika mitandao ya wamempongeza Jose Chameleone.

Wednesday, July 13, 2016

SERIKALI IMEIFUNGIA MAGAZETI 473 NCHINI

   Serikali imefuta usajili wa magazeti 473 ambayo hayajachapishwa kwa kipindi cha miaka mitatu.

     Hatua hiyo imetangazwa leo na Waziri wa Habari, Nape Nnauye katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ukumbi wa Maelezo. Amesema mtu yeyote atakayechapisha magazeti hayo kwa njia ya nakala ngumu (Hard copy) au kielektroniki atachukuliwa hatua za kisheria.

   
      “Iwapo kuna mmiliki wa gazeti ambaye angependa kuendelea na biashara hii milango iko wazi kwa ajili ya kuwasilisha maombi mapya sio kuuhuisha yaliyofutwa,” alisema Nape

Tuesday, July 12, 2016

FC BARCELONA IMEMSAJILI STAA MPYA WA NOU CAMP

    Klabu ya FC Barcelona ya Hispania leo July 12 2016 imetangaza kukamilisha usajili wa mchezaji mwingine atakayejiunga na klabu yao kuanzia msimu wa 2016/2017, Barcelona kupitia tovuti yao wametangaza kumsajili Samuel Umtiti kutoka klabu ya Olympique Lyonnais.

    V FC Barcelona imemsajili Samuel Umtiti kwa mkataba wa miaka mitano, kwa dau la uhamisho wa euro milioni 20, Umtiti atajiunga na kikosi cha Luis Enrique na atakuwa akicheza nafasi ya beki wa kushoto au beki wa kati.

      Umtiti ambaye katika mechi nyingine za Olympique Lyonnais alikuwa akicheza kama nahodha, amecheza jumla ya mechi 170 akiwa na klabu hiyo katika kipindi cha miaka mitano na amefunga jumla ya magoli matano,

     Umtiti ana umri wa miaka 22, mkataba wake na Barcelona utamuweka klabuni hapo hadi 2021.

JAY Z NA BEYONCE NDIYO COUPLE ILIYOINGIZA MKWANJA MWINGI ZAIDI DUNIANI

   Kwa mujibu wa Forbes, wawili hao ndio couple ya watu maarufu walioingiza fedha nyingi zaidi mwaka jana kwa kuweka benki dola milioni 107.5.

     Queen Bey peke yake aliingiza dola milioni 54 na kukamata nafasi ya 54 katika orodha ya mastaa 100 waliongiza fedha nyingi, huku mumewe akiingiza dola milioni 53.5 na kukamata nafasi ya 36.

    Mwaka jana Taylor Swift na Calvin Harris walichukua nafasi hiyo.

TAI NUSURA AMTWAE MTOTO AUSTRALIA

    Tai mmoja mkubwa nusura afanye kitendo cha kustaajabisha ,,, tai huyo alijaribu kumtwaa mvulana mmoja na kupaa naye nchini Australia! Umati wa watu uliokuwa katika hifadhi ya Alice Springs Desert Park ulipigwa na butwaa tai huyo alipojaribu kumbeba mtoto wakati wa kurekodi kwa onyesho moja la wanyama pori.

      Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa ''ilikuwa ni kama tai huyo aliona mnyama mdogo ambaye alitaka kumfanya mlo wake''  Mvulana huyo anayekisiwa kuwa kati ya miaka 6-8 aliepuka kwa kupiga kamsa na mwishowe ndege huyo mkubwa akapaa na kutoweka.

    Mvulana huyo alitibiwa baada ya makucha ya ndege huyo kumgwara usoni.

      Bi Christine O'Connell kutoka Horsham katika jimbo la Victoria aliyenasa tukio hilo kwa kamera anasema tai huyo alimvamia mtoto huyo akijaribu kumuinua.

   
    Hata hivyo wahudumu wa hifadhi hiyo waliingilia kati na kumfukuza tai huyo. Waandalizi wa onyesho hilo walifungasha virago vyao kwa haraka baada ya tukio hilo maarufu.

      Wasimamizi wa hifadhi hiyo wamemuondoa tai huyo kwenye onyesho hilo.

HII NDIYO SABABU YA MAENDELEO KUCHELEWESHWA AFRIKA

    Upatikanaji hafifu wa nishati kwa nchi nyingi za barani Afrika ndio chanzo kimojawapo cha kuchelewesha maendeleo barani humo nandio pia sababu kuu ya kutofikiwa kwa malengo ya milennia na kusababisha bara hilo kutofikia malengo yake ya maendeleo inayohitaji.

      Hayo yalisemwa na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais anaeshughulikia muungano na mazingira,JANUARY MAKAMBA,alipokuwa anafungua mkutano wa  upatikanaji wa nishati na tabia nchi unaoshirikisha jopo la wataalam wa nishati unaofanyika jijini DAR ES SALAAM.

     Amesema hata kama kutafanyika juhudi za kufikia malengo hayo ikiwa hakutafanyika sambamba na kurekebisha hali ya tabianchi na huduma za nishati,ni wazi juhudi za upunguzaji wa umaskini zitashindwa. Mkurugenzi mkuu wa shirika la hifadhi ya wanyama duniani WWF nchini,Dr.AMANI NGUSARU,

      amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kuja na mapendekezo ya namna ambavyo nchi inaweza kukabiliana na tabianchi kwa kuendeleza vyanzo vya nishati mbadala kama umeme wa upepo,gesi na umeme wa jotoardhi ambao unaweza kuisaidia nchi kuzalisha bidhaa kwa bei nafuu na kuleta ushindani wenye uwiano duniani.

JIKO LA MCHINA LASABABISHA KIFO CHA MTOTO

    Mama mzazi wa mtoto Bahati aliyefariki dunia, Lulu John ( wa pili kushoto) akifarijiwa na majirani baada ya tukio hilo la moto lililogharimu maisha ya mtoto wake. Mwanza.

     Mtoto Bahati John mwenye umri wa miaka minne na nusu amefariki dunia na vifaa vya ndani ambavyo thamani yake haijajulikana kuteketea moto. Tukio hilo limetokea saa kumi jioni katika mtaa wa Kamachumu, Kata ya Kirumba wilayani Ilemela jijini Mwanza.

      Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, Mussa Kaboni amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni jiko la mchina lililowashwa bila kufuatiliwa na muwashaji. Amesema kuwa katika tukio hilo, wakati wahusika wanawasha jiko hilo kulikuwa na watoto wawili Emmanuel John na Bahati John ambao walikuwa wamelala ambapo mkubwa wao Sospeter aliyekuwa anatoka shuleni ndiye aliwemwokoa mdogo wake mmoja Emmanuel.

     “Chanzo ni moto uliosababishwa na jiko la mchina ambalo liliwashwa bila kufuatiliwa, sisi tulipigiwa simu na kufika, lakini bahati nzuri tumekuta wasamaria wameshazima moto na kuokoa baadhi ya vitu,”amesema.

       Mzazi wa marehemu, Lulu John amesema alipata taarifa akiwa kazini na alipofika alikuta mwanaye ameshafariki na baadhi ya vitu kuungua.

       “Hii ni tabia yake mfanyakazi kuacha jiko linawaka anakwenda zake,”amesema John. Diwani wa Kirumba, Alex Ngussa amewataka wazazi na walezi kuwa waangalifu wanapokuwa kwenye shughuli za mapishi.

MADEAMA KUTUA DAR ALHAMISI

  Wapinzani wa Yanga katika michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho barani Afrika, Medeama ya Ghana, itawasili jijini Dar es Salaam, keshokutwa Alhamisi kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ).

  
      Yanga watakuwa wenyeji wa Medeama katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumamosi kuanzia saa 10 jioni. Huu ni mchezo wa tatu kwa Young Africans katika harakati za kuwania Kombe la shirikisho hatua ya makundi.

      Michezo miwili ya awali ilikuwa ni dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria ambako ilipoteza kwa bao 1-0 kabla ya kupoteza tena dhidi ya TP Mazembe, mechi iliyopigwa jijini Dar es Salaam. Mchezo wa Jumamosi utachezeshwa na waamuzi kutoka Misri ambao ni Ibrahim Nour El Din atakayekuwa mwamuzi wa kati; akisaidiwa na Ayman Degaish na Samir Gamal Saad wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Mohamed Maarouf Eid Mansour.

     Kamishna wa mchezo huo atakuwa Pasipononga Liwewe kutoka Zambia na maofisa wasimamizi ni Mfubusa Bernard ambaye atasimamia utendaji wa waamuzi wakati Mratibu Mkuu wa mchezo huo kutoka CAF atakuwa Ian Peter Keith Mc Leod.

TFF YATAFUTA MKURUGENZI WA MASOKO

    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeongeza muda zaidi kuimarisha idara zake ambako imeongeza muda wa wiki moja kwa Watanzania wenye sifa za Idara ya Masoko na Habari ili kuongoza Idara hiyo.

     Awali tarehe ya  mwisho ilikuwa Julai 11, 2016 lakini kwa sasa tarehe ya mwisho itakuwa Julai 19, mwaka huu kwa nafasi ambazo TFF imetangaza ajira. Lengo hasa ni kuendana na hali halisi ya uendeshaji mpira wa miguu duniani ambako masoko, habari na mahusiano ya Kimataifa yamekuwa funguo za kupata rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu popote duniani.

     Pili ni kuhakikisha rasilimali za kuendesha mpira wa miguu zinatokana na soka na vilevile kuhakikisha wadau wanapata habari sahihi kwa wakati mwafaka.

     Kwa nafasi za kazi TFF tembelea tovuti yao www.tff.or.tz au waandikie ili utumiwe tangazo kwa barua pepe tanfootball@tff.or.tz Mbali ya kuboreshwa kwa Idara hiyo ya Masoko, pia TFF imepania kutoa kipaumbele katika masuala ya waamuzi na wanawake kwa kuanzisha madawati ya kudumu katika Kurugenzi ya Ufundi.

     Hapo awali madawati ya wanawake na waamuzi yaliendeshwa na watumishi wa kujitolea (Volunteers) au wa muda (Part timers).

      Akizungumza na Mtandao huu, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliamsha changamoto mbalimbali za soka la wanawake miongoni mwanzo ikiwa ni uibuaji na uendelezaji vipaji, Timu ya Taifa, mafunzo katika taaluma mbalimbali, ligi za wanawake na masoko kwa bidhaaa (products) za soka la wanawake.

      Kuhusu waamuzi, Katibu Mkuu alilielezea eneo hili kama lenye changamoto nyingi hasa hasa katika kupata waamuzi wenye viwango vya Kimataifa.

Dkt. SHEIN AZUNGUMZA NA WAZEE WA ZANZIBAR

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake kwa wazee waliotimiza umri wa miaka 70 katika hafla maalum ya ilyofanyika kumpongeza yeye Rais iliyofanywa na Wazee hao katiika Viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja leo.

     Wazee wa
ya Kusini Unguja nao walihudhuria katika hafla ya kumponheza na kumshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuwawezesha kupata mafao ya kufikia umri wa miaka 70 katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja.

       Msoma utenzi Bw.Mohamed Abdalla Zungu kutoka Kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja akighani Utenzi wake wakati wa hafla ya Shukrani na Pongezi maalum kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein zilizotolewa leo na Wazee wanaopokea pencheni kwa kutimiza umri wa miaka 70 katika Viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja.

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mzee Bi Mtumwa Ali Khamis ambae alishiriki katika mchezo wa kuigiza wakati wa

      Shukrani na Pongezi maalum kwa Rais wa Zanzibar zilizotolewa na Wazee waliotimiza umri wa miaka 70 katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja.

Monday, July 11, 2016

WANANCHI EPUKENI UHASAMA UCHAGUZI UMEKWISHA - MPOTO

   Msanii wa muziki wa dansi, sanaa ya jukwaani (theatre performances), mwandishi wa vitabu vya mashairi na hadithi zenye mafunzo,amewataka watanzania kuepuka uhasama kwani uchaguzi umealizika na kinachotakiwa ni wao kujikita kwenye shughuli za ujenzi Mpoto ameyasema hayo

     alipokuwa akishiriki katika kipindi cha Supa Mix kinachorushwa na East Afrika Radio Jijini Dar es salaam wakati akishiriki usiku wa mapinduzi ambao umelenga vipindi vyote kuwa na watangazaji wenza katika vipindi vyote vya redio.

    Hakuna haja ya kuwa na uhasama , wananchi wanatakiwa washikamane ili kuchapa kazi na kuleta maendeleo ya taifa kwani uchaguzi umemalizika. Mrisho pamoja na kuimba nyimbo zake zenye nasaha kwa jamii pia amewataka madereva bodaboda kuheshimu kazini zao kwani ndizo zinawaingizia kipato.

      ''Kuna baadhi ya bodaboda wapo kama wameingiliwa na pepo, yani ukiwakuta hawathamini kazi yao wachafu na hii inatokana na wengi kupata bodaboda na kuingia mtaani bila mafunzo yoyote''amesema Mpoto.

YANGA HATI HATI KUMKOSA TAMBWE DHIDI YA MADEAMA

    Kuelekea katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika, Klabu ya Yanga iko katika hatari ya kuwakosa baadhi ya wachezaji akiwemo mshambuliaji wa kimataifa Amis Tambwe kutokana kutokana na kusumbuliwa na Maralia.

      Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema,Tambwe alipelekwa hospitali leo kuwekewa dripu ili pate nguvu baada ya kudhoofishwa na Malaria iliyompata wiki iliyopita.

    Tambwe aliukosa mchezo uliopita dhidi ya TP Mazembe kutokana na kuwa anatumikia adhabu ya kadi na sasa anapambana na Malaria.

      Tayari Yanga SC itawakosa beki Mwinyi Hajji Mngwali, viungo Deus Kaseke na Geoffrey Mwashiuya katika mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi.

     Wachezaji ambao Yanga inamatumaini ya kuwatumia katika mchezo wa Jumamosi ni Matheo Antony, Oscar Joshua na Malimi Busungu. Yanga inahitaji ushindi dhidi ya Medeama baada ya kupoteza mechi zote mbili za mwanzo wakifungwa 1-0 mara zote na Mo Bejaia nchini Algeria Juni 19 na TP Mazembe ya DRC Dar es Salaam Juni 28.

WAKULIMA WA UFATA , LINDI NA MTWARA WALIA NA SERIKALI BEI KUSHUKA

Anaandika Mwl Razaq Mtele Malilo. Katika misimu miwili iliyopita zao la ufuta lilinunuliwa kuanzia Tsh 2500 ha   di Tsh 3000  hali iliyopelekea watu wengi kuhamasika kulima zao hili kwa wingi na vijana wengi walihamasika kurudi mjini hasa jiji la Dar Es Salaam baada ya kuvutiwa na ongezeko hilo la bei hali ilyopelekea uzalishaji wa ufuta katika nchi yetu kuongezeka na kuwa ya kwanza barani Afrika na ya tatu duniani.

     Katika hali isiyotarajiwa bei ya ufuta mwaka huu imeshuka kati asilimia 45 hadi 50 na zao hilo limenunuliwa kwa bei ya Tsh 1600 hadi Tsh 1500 katika mikoa hiyo ya Kusini bei ambayo haina tija kwa mkulima hasa ukilinganisha na kupanda kwa gharama za uzalishaji wa zao hilo na gharama za maisha kwa ujumla.

     Ikumbukwe kwamba kutokana na kupanda kwa bei ya zao hilo miaka miwili iliyopita watu walikuwa wakijikiti katika kilimo cha zao hilo la biashara na kupunguza kulima mazao  ya chakula kama mahindi wakitegemea kununua chakula pale wauzapo ufuta.

      Lakini pia mwaka huu katika mikoa hiyo yalitokea majanga ya mafuriko yaliyosababisha kusombwa kwa mazao ya chakula shambani kama mahindi, mihogo na mazao mengine. Hivyo, watu walitegemea zao la ufuta liwe kama mkombozi wao kwani walitegemea bei nzuri kama ya mwaka jana au kupanda zaidi hii ni kutokana na ahidi ya Mh Rais Dr. JOHN POMBE MAGUFULI akiwa kwenye kampeni katika kijiji cha NANGARU, jimbo la Mchinga mkoani Lindi, OKTOBA 13 MWAKA JANA aliwaahidi wakulima wa ufuta kuwa atahakikisha anasimamia bei ya zao la ufuta ili wananchi hao wauze mazao yao kwa bei ya tija ili nao wajikwamue na umasikini.

      Ahadi iliwafanya wakulima hao wahamasike kumpigia kura nyingi na alipopita kuwa Rais walihamasika kulima ufuta kwa wingi wakitarajia bei ya tija zaidi ila hali halisi imekuwa kinyume chake mara dufu.

       Hivyo basi, kutokana na kushuka kwa uzalishaji  wa mazao ya chakula kwa sababu za mazao kusombwa na mafuriko na wakulima kujikita zaidi na mazao ya biashara na hii ni kutokana na kutokuwa na uwezo wa kugharamia mazao yote ya chakula na kilimo kwani wanatumia zana duni za kilimo kama jembe la mkono hivyo kushindwa kumudu kulima mazao yote .

       Anguko la bei ya ufuta ni pigo kwa wakulima hao na uwenda hali hii ikasababisha maisha magumu kwao na pia kukabiliwa na njaa kali kwani wengi wao walitegemea kuuza ufuta ili wakipata pesa wanunue chakula na mahitaji mengine ya msingi.

      Hivyo , kwa sasa wakulima hao wamebaki wakiwa wanyonge wakiwa hawana cha kufanya na wamekosa mtetezi. Wakulima hao wanaiomba licha ya kutowasaidia kipindi cha kilimo, wanaiomba serikali na Rais Magufuli akumbuke ahadi yake kwa wakulima hao kwani wamekula hasara kubwa mwaka huu.

      Wanaitaka serikali iwatafutie soko la uhakika na lenye tija ili nao waweze kujikwamua kimaisha na kuondokana na umasikini. Kwa niaba ya wakulima natumaini ujumbe huu wa wakulima utawafika wahusika na wataufanyia kazi.