Wednesday, July 20, 2016

ALIYEMUUA MKE WAKE KUKATILI ATIWA MBARONI, KAGERA

   Jeshi la polisi mkoani Kagera limefanikiwa kumtia mbaroni Sendon Andrew mkazi wa kijiji cha Byamtemba kilichopo katika kata ya Nsunga iliyoko wilayani Misenyi

     mkoani Kagera aliyekimbilia nchi jirani ya Uganda kwa tuhuma ya kumuua  kikatili mke wake Rosemery Desdery kwa kumpigwa fimbo na mateke katika seheme mbalimbali za mwili wake.

     Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera mrakibu mwandamizi wa jeshi hilo Abel Mtagwa ambaye pia ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa mkoa huo,amesema mtuhumiwa huyo baada ya kufanya

      mauaji hayo kwenye eneo la Sebure ya nyumba yao alimburuza marehemu hadi kwenye chumba chao cha kulala na kumfunika na blanketi na wakati akitoroka aliwambia watoto wao kuwa amemuacha mama yao amelala na anaondoka atarudi kesho yake.

     Kaimu kamanda huyo akitoa wito kwa wananchi amesema jeshi hilo halitawavumilia mtu yoyote atakayejihusisha na vitendo vya mauaji kwa kuwa vitendo  hivyo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

No comments:

Post a Comment