Kuelekea katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika, Klabu ya Yanga iko katika hatari ya kuwakosa baadhi ya wachezaji akiwemo mshambuliaji wa kimataifa Amis Tambwe kutokana kutokana na kusumbuliwa na Maralia.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema,Tambwe alipelekwa hospitali leo kuwekewa dripu ili pate nguvu baada ya kudhoofishwa na Malaria iliyompata wiki iliyopita.
Tambwe aliukosa mchezo uliopita dhidi ya TP Mazembe kutokana na kuwa anatumikia adhabu ya kadi na sasa anapambana na Malaria.
Tayari Yanga SC itawakosa beki Mwinyi Hajji Mngwali, viungo Deus Kaseke na Geoffrey Mwashiuya katika mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi.
Wachezaji ambao Yanga inamatumaini ya kuwatumia katika mchezo wa Jumamosi ni Matheo Antony, Oscar Joshua na Malimi Busungu. Yanga inahitaji ushindi dhidi ya Medeama baada ya kupoteza mechi zote mbili za mwanzo wakifungwa 1-0 mara zote na Mo Bejaia nchini Algeria Juni 19 na TP Mazembe ya DRC Dar es Salaam Juni 28.
No comments:
Post a Comment