Tuesday, July 5, 2016

BI CHEKA ARUDI UPYA KWA KISHINDO

   BAADA ya kimya cha muda mrefu msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, aliyewahi kutamba akiwa ndani ya Kundi la Wanaume Familiy, Cheka Haji ‘Bi cheka’ ameibuka upya kwenye tasnia hiyo baada ya kutoa ngoma kali inayokwenda kwa jina la Mapenzi ya Kale Siku Hizi Hakunaga

     aliyomshirikisha mkali kwenye gemu la Muziki wa Singeli, Marick Thadei ‘DJ Mack’. Akichonga na Uwazi Showbiz, kwa niaba ya Bi Cheka, DJ Mack amesema wimbo huo umepikwa na prodyuza kutoka Natal Records aitwaye G Max na anaamini utafanya vizuri  hata kumrudishia Bi Cheka mashabiki waliokuwa wanamfuatilia.

      “Wimbo ni mzuri kiukweli, ninatumaini utafanya vizuri na kumrudisha Bi Cheka kwenye reli maana ni kimya sasa kimepita tangu asikike kutokana na matatizo ya hapa na pale yanayoweza kumpata binadamu yeyote,” alisema DJ Mack. Source: Global Publisher

No comments:

Post a Comment