IDADI ya watumishi hewa waliobainika mkoani Morogoro, imefikia 252 na watu hao tayari wamelipwa Sh bilioni 1.2 kupitia mishahara.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe, alisema hayo juzi wakati wa kuapisha wakuu wa wilaya, walioteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli. Alisema uhakiki bado unaendelea kufanywa na timu ya wataalamu. Taarifa kamili itatolewa baada ya timu hiyo kukamilisha uhakiki.
Alisema licha ya kuchukua hatua za awali kubaini watumishi hewa, pia mkoa uliunda timu ya wataalamu iliyoanza uhakiki Mei 13, mwaka huu. Alisema hadi sasa timu hiyo imeshahakiki halmashauri nane za mkoa huo za Ulanga, Malinyi, Manispaa ya Morogoro, halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Gairo, Mvomero, Kilombero na Mji Ifakara. “ Mpaka sasa idadi ya watumishi hewa iliyopatikana ni watumishi 252,” alisema Dk Kebwe na kwamba timu hiyo ya uhakiki, inakamilisha kazi katika halmashauri ya wilaya ya Kilosa.
No comments:
Post a Comment