London.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Theresa May ameshinda katika awamu ya kwanza ya kuwania uongozi wa Chama cha Conservative kwa kupata kura nyingi.
Kiongozi huyo mpya atachukua hatamu za uongozi kutoka kwa Waziri Mkuu aliyeko madarakani David Cameron, ambaye alisema atajiuzulu baada ya nchi yake kupiga kura ya maoni ya kujiondoa uanachama wa Umoja wa Ulaya (EU). May alizungumzia matokeo na ushindi wake kuwa alikuwa ni yeye pekee anayeungwa mkono zaidi na chama chake cha Conservative.
May alikuwa akiipigia kampeni Uingereza kubakia Umoja wa Ulaya, huku mpinzani wake wa karibu Andrea Leadsom akiita kujiondoa.
No comments:
Post a Comment