Tuesday, July 12, 2016

HII NDIYO SABABU YA MAENDELEO KUCHELEWESHWA AFRIKA

    Upatikanaji hafifu wa nishati kwa nchi nyingi za barani Afrika ndio chanzo kimojawapo cha kuchelewesha maendeleo barani humo nandio pia sababu kuu ya kutofikiwa kwa malengo ya milennia na kusababisha bara hilo kutofikia malengo yake ya maendeleo inayohitaji.

      Hayo yalisemwa na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais anaeshughulikia muungano na mazingira,JANUARY MAKAMBA,alipokuwa anafungua mkutano wa  upatikanaji wa nishati na tabia nchi unaoshirikisha jopo la wataalam wa nishati unaofanyika jijini DAR ES SALAAM.

     Amesema hata kama kutafanyika juhudi za kufikia malengo hayo ikiwa hakutafanyika sambamba na kurekebisha hali ya tabianchi na huduma za nishati,ni wazi juhudi za upunguzaji wa umaskini zitashindwa. Mkurugenzi mkuu wa shirika la hifadhi ya wanyama duniani WWF nchini,Dr.AMANI NGUSARU,

      amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kuja na mapendekezo ya namna ambavyo nchi inaweza kukabiliana na tabianchi kwa kuendeleza vyanzo vya nishati mbadala kama umeme wa upepo,gesi na umeme wa jotoardhi ambao unaweza kuisaidia nchi kuzalisha bidhaa kwa bei nafuu na kuleta ushindani wenye uwiano duniani.

No comments:

Post a Comment