Monday, February 27, 2017

ZINGATIA HAYA KABLA YA KUFANYIA USHAURI WA KIBIASHARA UNAOPEWA

Zingatia Haya Kabla Ya Kufanyia Kazi Ushauri Wa Kibiashara Unaopewa

Kama kuna kitu ambacho kila mtu anaweza kushauri kadiri ya utashi wake, basi ni ushauri wa kibiashara. Watu wengi wamekuwa wakipokea ushauri wa biashara unaotolewa na kila mtu, tena kwa bure, lakini wanapoufanyia kazi ndipo wanagundua haukuwa ushauri mzuri.

Kila kipindi kuna aina za biashara ambazo huwa zinashabikiwa na watu wengi, biashara ambazo kila mtu anaongelea na wale wanaozifanya kuonekana waipata faida. Hapa ndipo unakuta kila mtu anashauriwa kuingia kwenye biashara hiyo, kwa sababu ndiyo ‘habari ya mjini’ kwa wakati huo na hivyo wengi wanakimbilia kuchukua hatua kabla fursa haijawapita.

Changamoto nyingine kubwa inayowafanya watu kupewa ushauri ambao siyo makini kwenye biashara ni kutokuwa tayari kulipa gharama za ushauri. Wengi wamekuwa wakichukulia ushauri kama kitu kidogo ambacho hakipaswi kulipiwa. Hivyo wanachukua ushauri wa bure ambao unawaumiza sana.

Leo tutakwenda kujifunza mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kufanyia kazi ushauri wowote unaopewa kibiashara. Kwa kuzingatia mambo haya utaepuka kufanya maamuzi ya msukumo ambayo yatakuingiza kwenye hasara.

Jambo la kwanza; fanya utafiti wako mwenyewe.
Usipokee maneno ya watu na kuyaamini kwa asilimia mia moja. Fanya utafiti wako kujua kama kweli biashara unayoambiwa inalipa kama ni kweli. Angalia ukubwa wa soko la biashara hiyo, ona ni kwa kiasi gani bado wateja hawajafikiwa. Pia angalia uwezekano wa kukua zaidi kwenye biashara hiyo. Fanya utafiti wako mdogo kulijua soko na hata kuwajua wale waliopo kwenye biashara hiyo kwa sasa.

Jambo la pili; ongea na wale wanaofanya.
Kwa kuwa umesikia biashara inalipa, usifikiri kwamba haina changamoto zake. Na ili kujua changamoto za biashara yoyote, angalia wale ambao wanafanya biashara hiyo. Ongea nao au wafuatilie ili kuona changamoto yao hasa ni nini. Ni vyema ukazijua changamoto za biashara yako mapema kabla hata hujaingia ili uweze kupambana nazo.

Wengi wa wanaoshindwa kwenye biashara mpya ni kutokana na kukutana na changamoto ambazo hawakuzitegemea hapo awali.

Jambo la tatu; mwangalie yule anayekupa ushauri wa biashara.
Watu wengi wamekuwa wakitaka kusikia tu ushauri mzuri wa biashara, hivyo wakiusikia hawajali anayewaambia ni nani. Hivyo unakuta mtu kasikia wengine wanasema biashara fulani inalipa, na yeye anatoka na taarifa hizo kuja kukupa wewe. Hajafanya utafiti wowote na wala hana utaalamu wa biashara, ila amesikia inalipa na anakuambia na wewe ukafanye kwa sababu inalipa.

Hakikisha mtu unayechukua ushauri wa biashara kwake ana utaalamu wa biashara au anafanya biashara hiyo anayokushauri ufanye. Kama na yeye amesikia inalipa ila hajui kwa kina kuhusu biashara hiyo, ni vyema ukaokoa muda wako au kufanya utafiti zaidi kabla hujaingia kwenye biashara hiyo.

Ni rahisi kushauri kuliko kufanya, hivyo mara zote unapopokea ushauri chunguza kwa makini kabla hujachukua hatua. Usiharakishe kufanyia kazi ushauri unaopewa kwa sababu tu unaonekana ni biashara itakayokulipa. Fanyia kazi ushauri unaopewa na utoke na mpango ambao unaweza kuupigania mpaka kufanikiwa kwenye biashara yako.

RAIA WA UJERUMANI AKATWA NA WANAJIHAD

Raia wa Ujerumani akatwa kichwa na Wanajihad

Jurgen Kantner ni raia wa Ujerumani aliyekatwa kichwa na wanajihad

Wapiganaji wa Kiislamu nchini Ufilipino wamechapisha kanda ya video inayoonyesha mateka mmoja wa Ujerumani akikatwa kichwa.

Jurgen Kanther alitekwa nyara katika jahazi lake pwani ya Malaysia jimbo la Sabah mnamo mwez Novemba.

Mwili wa mtu aliyekuwa naye baadaye ulipatikana katika mashua hiyo.

Siku ya mwisho ya kulipa fidia ya dola 483,000 ilikamilika siku ya Jumapili.

Bw Kantner mwenye umri wa miaka 70 na bi Merz walikuwa wamewahi kutekwa nyara awali.

Walizuiliwa kwa siku 52 mwaka 2008 na maharamia wa Kisomali na waliachiliwa huru baada ya kikombozi kutolewa.

Video hiyo ilioripotiwa na wapiganaji wa SITE inamuonyesha bwana Kantner akikatwa shingo na mtu aliyeshika kisu.

Mjumbe wa serikali Jesus Dureza alithibitisha mauaji hayo.

Hadi wakati wa mwisho sekta tofauti ikiwemo jeshi zilishindwa kuokoa maisha yake.

''Sote tulijaribu uwezo wetu lakini hatukufanikiwa'',alisema.

Abu Sayyaf ni kundi dogo na lenye ghasia kubwa kusini mwa Ufilipino, likijulikana kwa unyama wake ikiwemo kukata watu vichwa.

Kundi hio linatii wapiganaji wa Islamic State na limefanya utekaji nyara mwingi wa wageni na raia wa Ufilipino.

Wengine wamewachiliwa kwa kutoa kikombozi lakini idadi kubwa bado inaendelea kuzuiliwa.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO NAPE NNAUYE ATUMA SALAMU ZA POLE SHIRIKISHO LA RIADHA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye atuma salamu za pole shirikisho la riadha

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ametoa salamu za pole kwa Rais wa Shirikisho la  Riadha  nchini, Anthony Mtaka kufuatia kifo cha mshiriki kutoka nchini Kenya, Charles Rioba (36) aliyefariki  katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika Februari, 26 mkoani Kilimanjaro.

Rioba alishiriki kwa hiari mbio zijulikanazo kama ‘run for fun’ za Kilometa 21, zilizohusisha wananchi mbalimbali wakiwemo pia viongozi wastaafu.

Lakini akiwa katika mbio hizo alianguka na kupatiwa huduma ya kwanza kisha  kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) na baadae kufariki dunia.

Waziri Nape ametoa pole pia kwa waandaaji wa mashindano hayo na wote ambao wameguswa na msiba huo

BARNABA APATA MPENZI MPYA BAADA YA KUACHANA NA MKEWE

Barnaba Apata mpenzi mpya Baada ya Kuachana na Mkewe

Haya sasa Barnabas Naye ameanza taratibu kutuonyesha MTU wake ama Nene? Kama wengi mjuavyo Mwanamuziki Barnaba alizenguana na mkewe na kuachana ambapo aliyekuwa mkewe Siku ya Valentine day alionyesha ulimwengu kuwa AME move on kwa picha iliyosambaa akiwa na mwanaume mwingine..

Sasa Barnaba na yeye amekuja na kupost picha akiwa na msichana mwingine huku akituachia kitendawili...
.

#Repost #barnabaclassic
・・・
Pale Crush brother anapokutaka na crushe sister #iam_just_rakel 😘🌺🔥🗽☀️ Doll metalick Moshi Moshi -Classic Yuko Njiani Jesus is my Power 😊☕️Asante mzazi #@Regrann from @crazyvoicess - Follow @crazyvoicess (me) for more videos like this! ❤😄
Amazing 😍
Tag a friend 👇
🎤
#crazyvoicess #amazing #vocals

RASMI WIZARA YA MAMBO YA NJE YAHAMISHA OFISI ZAKE DODOMA

Walio keti ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katika), Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi (wa kwanza kulia) Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bw. Nigel Msangi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bw.Hamid Mbegu wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara Mjini Dodoma

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kuwa tayari imeshahamia Dodoma kuanzia tarehe 17 Februari, 2017. Hatua hiyo imehusisha Awamu Mbili, Awamu ya kwanza imetekelezwa tarehe 28 Januari, 2017 na Awamu ya Pili imetekelezwa tarehe 17 Februari, 2017.

Miongoni mwa Watumishi waliohamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza (Awamu ndogo ya kwanza tarehe 28 Januari, 2017) nipamoja na Viongozi Wakuu na Watumishi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine P.Mahiga na Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba pamoja na Watumishi Kumi (10) waliofuatana nao. Awamu ndogo ya kwanza ilifuatiwa na (Awamu ndogo ya Pili tarehe, 17 Februari, 2017) iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Dkt. Aziz P.Mlima na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan M.Mwinyi wa kiongozana na Watumishi 33 wa Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Katika Uhamisho huo wa Awamu ya Kwanza, jumla ya Watumishi 43 wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameungana na Viongozi wao Wakuu.

Mawasiliano ya Wizara yatakayotumika kuanzia sasa nikama ifuatavyo:

Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Barabara ya Makole,
S.L.P 2933,
Jengo la LAPF, Ghorofaya6,
DODOMA.

Namba za Simu: +255 (0) 262323201-7,
Nukushi : +255-26-2323208,
Barua pepe : nje@nje.go.tz Tovuti : www.foreign.go.tz

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dodoma, 27 Februari, 2017.

RASMI 'JUUKO' ATUA MSIMBAZI

BEKI wa kimataifa wa Uganda Juuko Murshid amewasili Dar kukiongezea nguvu kikosi cha Simba SC kwa mechi zilizobaki za kombe la shirikisho na zile mechi saba za ligi kuu.

Juuko ambaye alikuwa na matatizo ya kifamilia kwa kufiwa na watoto wake watatu (mapacha) akiwa anaitumikia timu ya taifa ya Uganda kwenye michuano ya AFCON nchini Gabon amewasili jana.

Shaffidauda.co.tz imezungumza na meneja wa Simba Mussa Hassan Mgosi amedhibitisha kumpokea Juuko na kumwambia awasili leo Jumatatu kwenye mazoezi ya timu hiyo uwanja wa Polisi baada ya wachezaji wote wa Simba kupewa mapumziko ya siku moja (jana).

Kurudi kwa Juuko kunaweza kuwa faraja kwa wanachama na wapenzi wa Simba kutokana na beki wao Method Mwajale kuwa majeruhi na bado hawana imani na beki Novalty Lufunga.

Simba imeshuka dimbani mara 23 na kuhhjikusanyia alama 54, huku ikikabiliwa na mchezo ugumu dhidi ya Mbeya City March 4.

ZITTO KABWE AANDIKA UJUMBE HUU BAADA YA GODBLESS LEMA KUNYIMWA DHAMANA

Zitto Kabwe Aandika Ujumbee Huu Baada Ya Godbless Lema Kunyimwa Dhamana

Baada ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania iliyokaa Arusha kutupa Rufaa zote mbili zilizofunguliwa na Serikali dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuhusiana na dhamana ya mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amezungumza.

Kiongozi huyo wa ACT ametumia Facebook kutoa malalamiko yake:
Mnamkamata mtu kwa kosa lenye dhamana. Mahakama Kuu inaruhusu dhamana. Serikali inakataa rufaa kuzuia dhamana. Mtu anakaa jela miezi 4, tena mwakilishi wa watu. Siku ya hukumu kuhusu dhamana Serikali inaondoa shauri mbele ya jopo la majaji 3. Lengo? Kumkomoa mtu. Siasa za ukomoaji zinajenga chuki kwenye jamii na chuki inazaa visasi. Haitoshi majaji kukemea Ofisi ya DPP. Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa. Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa makusudi dhidi ya wananchi.











NAPIGANIA KUACHIA ALBAMU MWAKA HUU, IKISHINDIKANA NITAIUZA DUKANI KWANGU

Napigania kuachia albamu mwaka huu, ikishindikana nitauzia dukani kwangu - Cyrill Kamikaze

Rapper Cyrill Kamikaze amefunguka juu ya mpango wake wa kuachia albamu kama walivyofanya Navy Kenzo na baadhi ya wasanii walioahidi kufanya hivyo mwaka huu.

Akiongea katika kipindi cha Flavour Express cha Maisha FM, Silver Touchez, Rapper huyo amesema anapigania kuachia albamu mwaka huu japo kwenye swala la uuzaji ndio tatizo lakini ikishindikana atauzia hata dukani kwake.

“Mimi nini ngoma nyingi sana zipo studio. Actually nina ngoma nyingi mpaka nyingine zimekuwa outdated kwa sababu nimekuwa nikirekodi sana. Situation ya kutoa albamu Bongo imekuwa tatizo kidogo nikisema nitoe nitajuliza nitaanzia wapi kuiuza?,” amesema Cyrill.

“Lakini kuanzia mwaka jana, mwaka juzi ilikuwa ni ndoto yangu lakini kunakuwa na mambo mengi yanaingiliana. Lakini mwaka huu ninataka kupigania hili suala niwe na albamu mkononi na ikishindikana basi nitaiuza hata dukani kwangu,” ameongeza.

'IFM ' KUWA CHUO KIKUU

IFM kuwa chuo kikuu


SERIKALI imesema imepokea ombi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) la kutaka kupandishwa hadhi na kuwa Chuo Kikuu, kutokana na kukidhi vigezo. Imeahidi kufanyia kazi ombi hilo kwa kushirikiana na wadau wengine ili kufanikisha jambo hilo, bila kupindisha utaratibu wa serikali.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Dk Anthony Mavunde wakati akizindua Baraza la Tisa la Wafanyakazi la chuo hicho.

"Sishangazwi na ombi lenu la kuwa Chuo Kikuu, nimelichukua na ninaahidi kuwasiliana na wadau wengine wa serikali tunone njia bora ya kuliendeza bila kupindisha taratibu," alisema Mavunde.

Mavunde ametaka Baraza hilo jipya kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatekeleza mipango waliyojiwekea ambayo inaendana na utekelezaji wa wa mipango ya serikali.

Amesema mabaraza mengi ya wafanyakazi yanaykumbana na changamoto, ikiwemo ya kuikosa kuaminiana kati ya menejimenti na wafanyakazi hatua ambayo husababisha kila pendekezo linalowasilishwa kwenye baraza kukataliwa na wafanyazi.

"Lakini nimeelezwa kuwa kwenu hakuna Tatizo hili, naomba muendelee na kuaminiana katika kusukuma maendeleo ya Chuo na Taifa kwa ujumla," amesema.

Awali, Mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Profesa Taadeo Sata alisema, chuo hicho kwa sasa kinatekeleza mradi wa upanuzi wa chuo hicho katika eneo la Msata, Bagamoyo mkoani Pwani.

Alisema pamoja na kwamba chuo hicho kinatafuta pesa kupitia vyanzo mbalimbali lakini kinahitaji msaada wa serikali ili kukamilisha ujenzi huo.

"Baraza la wafanyakazi wa chuo ni muhimu kwa maendeleo ya chuo chetu. Kwa sasa tumedahili wanafunzi zaidi ya 8,000 katika fani mbalimbali na tuna wahadhiri 152," alisema.

Mwenyekiti wa Baraza la IFM, Letticia Rutashobya alisema chuo hicho kinatekeleza mikakati mbalimbali ya kuoberesha chuo hicho. Waziri Mavunde pia alitembelea eneo litakalojengwa Chuo cha IFM lililopo Msata ambalo lina ukubwa wa ekari 1,500.

Saturday, February 25, 2017

HII NDIO SIMU INAYOUZWA TSH 8184

hii ndio Simu inayouzwa Tsh 8,184

Kampuni moja ya India inatarajiwa kuzindua kile kinachojulikana kuwa simu aina ya smartphone ya bei rahisi.

Kampuni ya Ringing Bells imesema kuwa simu hiyo kwa jina Freedom 251 itagharimu Rupee 500 sawa na dola 7.3, lakini vyombo vya habari nchini India vimesema kuwa itauzwa kwa Rupee 251 pekee ambazo ni sawa na dola 3.67.

Ripoti zinasema simu hiyo ina ukubwa wa 8GB na ina kamera mbele na nyuma.

India ni soko la pili kwa ukubwa la simu na lina wateja bilioni moja wanaomiliki simu. 

Freedom 251 inatarajiwa kulenga soko ambalo tayari linatawaliwa na simu za bei ya chini.

“Hii ndio modeli yetu ya kwanza na tunafikiri kwamba inaleta mabadiliko katika soko la simu,” shirika la habari la AFP,lilimnukuu msemaji wa kampuni hiyo .

Aliongeza, “Kwa sasa kampuni hiyo inanunua vifaa vya kutengezea simu kutoka nje kabla ya kuviunganisha nchini India,lakini ina mpango wa kutengeza vifaa hivyo nchini India katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.,”





JE WAJUA SIGARA HUHARUBU DNA NA KUONGEZA HATARI YA KUPATA KENSA

je wajua Sigara huharibu DNA na kuongeza hatari

Kemikali za sumu zilizoko katika tumbaku ya sigara huharibu DNA za mwili wa binadamu dakika chache tu baada ya mtu kuanza kuvuta sigara. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni, kemikali hizo zinazoitwa Polycylic Aromatic Hydrocarbons (PAHs) husababisha DNA ziharibike na kuongeza uwezekano wa mtu kupata kensa.

Katika uchunguzi huo watalamu walichukua kemikali hizo katika miili ya wavuta sigara na kuzifanyia uchunguzi, ambapo waligundua kuwa, kemikali za PHA hubadilika haraka mwilini na kuwa sumu ambayo huharibu DNA baada ya kupita dakika 15 hadi 30 tangu kuingia tumbaku katika mwili wa binadamu. Sumu hiyo hubadilisha seli mwilini au kufanya mutation, kitendo ambacho huweza kusababisha kensa.

Wataalamu hao wanasema, kitendo hicho hufanyika kwa haraka sana kama vile inavyoingizwa mada ya sumu kwenye damu kwa sindano. Habari hii ni tahadhari kwa watu wanaotaka kuanza kuvuta sigara, kwani takwimu zinatuonyesha kwamba, watu 3,000 hufariki dunia kila siku umwenguni kutokana na kensa ya mapafu, maradhi ambayo husababishwa kwa asilimia 90 na uvutaji sigara.

Madhara ya kuvuta sigara kwa muda mrefu yanajulikana na wengi, ambayo ni pamoja na magonj
wa ya moyo na kensa mbalimbali, lakini wataalamu wanatuasa ya kuwa, madhara ya sigara huanza pale tu mtu anapoanza kupiga pafu ya kwanza na kuingiza moshi wa sigara mwilini. Hivyo bado hujachelewa na unaweza kuacha sigara hii leo!

MACHANGUDOA KUANZA KUSHUGHULIKIWA

Machangudoa kuanza kushughulikiwa

MKUU wa wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Ali Hapi, ametoa onyo kwa wamiliki wa baa wanaowahifadhi watu wanaojihusisha na biashara ya ngono ‘Machangudoa’ kuwa watafutiwa leseni.

Ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata ya Kijitonyama waliodai kuwa kuna baadhi ya baa zimekuwa zikiwahifadhi wanaouza miili, hali ambayo ni hatari kwa mazingira na makuzi ya watoto.

Hapi amesema haiwezekani serikali iwe inapambana na biashara hiyo haramu lakini kuna baadhi ya baa zinawafuga machangudoa.

"Tutashughulika na changudoa na tutashughulika na wenye baa zinazowahifadhi machangudoa, kwa sababu hili ni suala lililo kinyume cha sheria, serikali inapambana na hili tatizo halafu mwingine analikumbatia, hilo haliwezekani, tutawachukulia hatua za kisheria," amesema.

Awali, akitoa malalamiko yake kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete, mkazi wa Kijitonyama alidai kuna baa zilizogeuka kero kwao.

Ameitaja baa iitwayo Kona ya Sinza imekuwa ikiwahifadhi machangudoa hivyo kuhatarisha makuzi ya watoto kwa kuwa wanaweza kuiga tabia zisizofaa.

"Hii baa iko hapo Afrika Sana, machangudoa wako pale wanajiuza hadharani, sasa kwa kweli hii ni kero kubwa kwetu, watoto wanaweza kuiga na matokeo yake tutakuwa na kizazi kibaya ," amesema mwananchi huyo.

MAJALIWA ATAKA JAMII YENYE MAADILI

Majaliwa ataka jamii yenye maadili

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema ili kuwa na taifa lenye ustawi, jamii haina budi kuwekeza kwenye makuzi mema ili kuepuka kuwa na taifa la vijana wasio na maadili.

Aidha, amesema serikali inapopambana na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, matumizi holela ya pombe za viroba, mimba za utotoni na mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ili kuboresha huduma za jamii, lengo lake ni kujenga kesho iliyo bora kwa vijana.

Waziri Mkuu aliyasema hayo juzi usiku katika hafla ya chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangia maadhimisho ya siku ya Skauti Afrika na miaka 100 ya Uskauti Tanzania, iliyoandaliwa na Chama cha Skauti Tanzania.

Alisema nusu ya Watanzania ni vijana, hivyo ni muhimu kuweka mazingira mazuri kwa ajili yao. Chama cha Skauti kama moja ya taasisi kongwe nchini ni wadau muhimu katika malezi ya vijana.

"Tunaposhuhudia makundi kama Panya Road, ongezeko la vijana wenye uraibu wa dawa za kulevya na ongezeko la mimba za utotoni, sanjari na kuhoji nafasi ya wazazi kwenye malezi ya watoto wetu, tunadhani ni wakati mwafaka pia kwa Chama cha Skauti nacho kujitathmini endapo bado kina ushawishi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na endapo kuna jambo linaweza kufanyika ili kurekebisha hali hiyo," amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Alisema serikali inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa kwa ajili ya kuhakikisha kila mtoto mwenye uwezo wa kwenda shule anafanya hivyo, bila kikwazo.

Alifafanua kuwa serikali imekuwa ikitoa Sh bilioni 18.7 kila mwezi ambazo zimesaidia kuondoa ada na michango yote kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

Pia alishauri kamati inayoandaa shughulli hizo kubuni njia mbalimbali za kupata michango kama kuwa na mechi za soka, mabonanza ya muziki, bahati nasibu na kampeni za uchangiaji kupitia makampuni ya simu za mkononi.

Aidha, alishauri kamati hiyo kuona uwezekano wa kuunganisha matukio ya maadhimisho ya Miaka 100 ya Skauti Tanzania na Siku ya Skauti Afrika kuyafanya kwa pamoja na kwa bajeti ndogo, ili fedha zitakazookolewa zitumike katika shughuli mbalimbali za kuhamasisha uskauti nchini.

Awali, Rais wa Chama cha Skauti nchini na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema, chama hicho kimekuwa msaada mkubwa katika kuwajenga vijana katika mazingira bora. Alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuwahamasisha vijana kuwa raia bora wenye kuwajibika ipasavyo.

Alisema maadhimisho hayo yanahitaji Sh milioni 600 ili yaweze kukamilika, kwani yatashirikisha na nchi nyingine mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika.

Katika chakula hicho cha hisani, fedha zilizopatikana kwa ahadi na taslimu ni Sh milioni 265.1, hivyo wananchi kuombwa kuendelea kuwasilisha michango yao kwa ajili ya maadhimisho hayo.

WANAFUNZI KIGAMBONI WADAI UMBALI NDIO SABABU YA KUFELI KWAO

Wanafunzi Kigamboni wadai umbali ndio sababu ya kufeli kwao

Dar es Salaam. Wakati wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakiendelea kujiuliza kwanini shule sita za mwisho katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana zimetoka katika jiji hilo, imeelezwa kuwa umbali kwenda shuleni ni moja ya sababu za matokeo hayo kuwa mabaya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Kimbiji, Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile ambaye shule mbili kati ya sita zilizopata matokeo mabaya zinatoka jimboni kwake, alisema mkakati wa kujenga mabweni kila sekondari utasaidia kuondoa tatizo hilo.

Bweni hilo limejengwa na Kampuni ya Lake Cement kwa gharama ya Sh65 milioni ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya ushiriki wa maendeleo ya jamii (CSR).

Akizungumza kwenye makabidhiano hayo, Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo, Afroz Ansari alisema mbali na bweni, tayari wamejenga madarasa mengine mawili.

RAIS MAGUFULINNA MUSEVENI WAKUBALIANA KUTOSAINI MKATABA WA EPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017 .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni kwa pamoja wamekubaliana kutosaini mkataba wa mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Ulaya (EPA).

Makubaliano hayo yamefanyika jana Ikulu, Jijini Dar es Salaam ambapo  Rais Yoweri Museveni yuko nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 25 – 26  Februari, 2017.

Akiongea na waandishi wa habari Rais Magufuli amesema kuwa mkataba wa EPA hauna faida bali ni aina nyingine ya ukoloni ambao unataka kurejeshwa kwa nchi za Afrika.

“Nimeongea na Rais Yoweri Museveni amekubali kutosaini mkataba wa EPA, nitawaagiza wataalamu waliosaidia kutupa maelezo juu ya madhara ya mkataba huo kwenda pia Uganda kuwapa maelezo ambao waliyatoa kwa Tanzania,” alifafanua Dkt. Magufuli.

Kwa upande wake, Rais Yoweri Museveni amesema kuwa ameongea na Rais Magufuli na wamekubaliana kutosaini mkataba huo na kuongeza kuwa suala la EPA ni lazima lijadiliwe na nchi zote za Afrika Mashariki ili kuwepo na msimamo wa pamoja kwa nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha Rais Museni amempongeza Rais Magufuli kwa kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua ndege mpya Sita, hivyo amekaribisha shirika hilo kutoa huduma za usafiri wa anga nchini Uganda kutokana na nchi hiyo kuwa na uhitaji wa huduma hiyo.

Vilevile amempongeza Rais Magufuli kwa ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway) kutoka Dar es Salaa mpaka Mwanza na Isaka mpaka Rwanda ambapo itapelekea ujenzi wa bandari kavu katika mkoa wa Mwanza hivyo wafanyabiashara wa Uganda kunufaika na bandari hiyo ambayo itakuwa karibu zaidi kuliko ilivyo kwa Dar es Salaam.

Wakati huohuo Mawaziri wa Nje kutoka Tanzania na Uganda Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Oryem Henry Okello wamesaini makubaliano ya uhusiano katika mambo ya Diplomasia baina ya nchi hizo mbili.

Museveni yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo atatembelea baadhi ya maeneo kadhaa ikiwemo kiwanda cha Juice cha mfanyabiashara Mtanzania Said Bakhressa ambaye pia amewekeza nchini Uganda.

ATIMULIWA UCHUNGAJI KWA KUWAPA MIMBA WAUMINI

Atimuliwa uchungaji kwa kuwapa mimba waumini

Geita. Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo katika Kijiji cha Bukondo, Peter Msopela amefukuzwa kazi hiyo baada ya kukiri kuwapa mimba waumini wake wawili katika kipindi cha mwaka mmoja.

Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kikao cha ngazi za juu za kanisa hilo kilichofanyika juzi, Askofu mkuu wa kanisa hilo, Herryabwana Majebele alisema amemsimamisha kazi mchungaji huyo kwa kuwa amechafua kanisa la bwana.

Mchungaji Msopela amekiri kufanya kosa hilo na amejitetea kwamba alipitiwa na shetani, hivyo kuwataka waumini wamsamehe. Pia amemsihi Askofu Majebele asimfukuze kanisani.

Hata hivyo, Askofu Majebele alisema mchungaji huyo licha ya kulitumikia kanisa kwa kipindi cha miaka sita, kitendo alichokifanya ni kuvunja Amri 10 za Mungu.

“Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa waumini wakimtuhumu Msopela kuwabebesha mimba wanawake wawili wa kanisa lake na kuwaahidi kuwaoa. Ushahidi upo kutoka kwa waliotendewa vitendo hivyo, nimemfukuza kazi ya uchungaji ili akaendelee na starehe zake huko kwingine,” alisema Majebele.

Baada ya kumvua wadhifa huo, Askofu Majebele alisema kanisa hilo sasa litakuwa chini ya uangalizi wa Mwinjilisti Malisafi Damasi hadi pale atakapoletwa mchungaji mwingine.

Mmoja wa waumini waliopewa mimba na mchungaji huyo, Sarah Muhayiwa alisema alianza uhusiano wa kimapenzi naye tangu mwaka jana na kwamba baada ya kubeba ujauzito, alianza kumshauri asiseme jambo hilo kanisani akiahidi atamuoa.

“Baada ya hapo alinipangishia chumba mjini Katoro tangu Januari 3 lakini akanitelekeza, muda mfupi nikasikia ametangaza kumchumbia mwanamke mwingine ambaye naye alikuwa na ujauzito wake,” alisema Sarah.

Mzee wa kanisa hilo, Penina Thomas alisema mchungaji huyo amekuwa akifumaniwa mara kwa mara na hivyo anapaswa kuondolewa kwenye nafasi hiyo.

Mwinjilisti Damasi alisema kutokana na tabia hizo, waumini wengi wamekata tamaa ya kuendelea kuhudhuria ibada.

SITOKUBALI UZEMBE KATIKA UJENZI WA BOMBS LA MAFUTA KUTOKA TANGA HADI HOIMA

Sitokubali uzembe katika ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Hoima - Magufuli

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli amesema hatavumilia uzembe wa aina yoyote katika ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Hoima nchini Uganda bali anataka ujenzi wa bomba hilo ufanywe katika hali inayotarajiwa ili wananchi wa Uganda na Tanzania wanufaike nalo.

Dr.Magufuli ametoa onyo hilo Ikulu jijini Dar es salaam  mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda uliofanyika mbele yake na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta museveni ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Aidha Rais DKt.magufuli amemweleza mgeni wake Rais Museveni kuwa Tanzania imeanza kujenga reli kutoka Dar es Salaam hadi mkoani Mwanza kwa kiwango cha kisasa yaani Standard Gauge ambapo itakapofika mkoani Mwanza atajenga bandari kavu maalum kwa ajili ya kuhudumia wafanyabiashara wa Uganda pekee.

Naye Rais Museveni amesema nchi ya Uganda inaitambua Tanzania kama rafiki wa kweli na kwamba atashirikiana na Rais Dr.Magufuli katika nyanja zote lengo kuu likiwa ni kuwafanya watanzania na waganda waweze kuishi maisha bora zaidi ya hivi sasa.

Baadhi ya nyanja ambazo Tanzania na Uganda wamekubaliana ni kuimarisha biashara miongoni mwao,kushirikiana katika usafiri wa anga,mawaziri wa mambo ya nje kukutana mara kwa mara na kujadiliana jinsi ya kuboresha uhusiano baina ya mataifa.

ANTHONY LUSEKELO AMUONYA NAY WA MITEGO KUFUNGUA KANISA

Anthony Lusekelo amuonya nay wa mitego kufungua kanisa...adai anamchezea mungu kama ana mama amkanye

Baada ya hivi karibuni msanii wa hip hop, Nay wa Mitego kutangaza kuwa atafungua kanisa lake ambalo litakuwa si la biashara bali ni la kumuabudu Mungu aliye hai, Mchungaji maarufu nchini, Lusekelo Anthony aka Mzee wa Upako amemuonya kutomchezea Mungu

Mzee wa upako ameyasema hayo alipotafutwa na E-News ya EATV baada ya kuulizwa maswali juu ya kauli hiyo.“Kama unakuja kanisani kwa maana kuna biashara, nakupa miaka hii mitatu sio utatembelea ndala utatembelea kucha, ni mtoto mdogo sana hana akili.

"Mungu hataniwi, anafanya kufuru, kama ana mama yake amemzaa amuonye. Mimi biblia nimesoma na hizo lugha zake nyepesi zitamtokea puani, asithubutu kufanya kanisa kama biashara.

"Baada ya miaka hii mitatu atajua kwamba kuongoza watu sio kama kuongoza ngo’mbe hakuna jambo gumu kama kuongoza watu wenye akili kama wewe wenye ufahamu kama wewe, wapo watu wengi walianzisha makanisa kwanini walifunga, ujinga hujui ni ujinga ni utoto,” alisema Mzee wa Upako.Nay amedai kuwa kanisa lake litajengwa Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam.

Friday, February 24, 2017

DAWA ZA NYWELE ZINAZOSABABISHA UVIMBE WA KIZAZI KWA WANAWAKE

Dawa Za Nywele Zinazosababisha Uvimbe Wa Kizazi Kwa Wanawake

Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.

Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.

“Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids,” anasema.

Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi.

Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika.

“Zipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone,” anasema.

Dk Chipata anasema madhara yanayopatikana katika kemikali za vipodozi ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali nyingine husababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury).

“Dawa za nywele zina madhara si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi,” anasema.

Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi badala ya kujibadilisha.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.

Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.

Dk Wise anasema aliwafanyia uchunguzi wanawake wanaotumia dawa za kulainisha nywele na kuangali umri walioanza kutumia dawa hizo, mara ngapi, waliungua kiasi gani na walikaa na dawa hizo kichwani kwa kipindi gani.

Aliwafuatilia wanawake 23,580 wanaotumia dawa za kulainisha nywele na baada ya kipindi fulani walipimwa. Kati yao, 7146 waligundulika kuwa na uvimbe kwenye kizazi baada ya kupimwa kwa mionzi na wengine kufanyiwa upasuaji.

Kwa nini relaxer ni hatari kwa wanawake?
Dk Wise anasema mchanganyiko ulio kenye dawa za nywele hasa zilizoandikwa “Lye Relaxer” ni sodium hydroxide wakati makopo ya dawa yaliyoandikwa “No Lye Relaxer” yana calcium hydroxide na guanidine carbonate.

Bidhaa za kulainishwa nywele zilizoandikwa ‘no lye relaxer’ zinadaiwa kusababisha majeraha kwa kiasi kidogo ukilinganisha na zile zilizoandikwa “Lye Relaxer”.

JINSI YA KUTENGENEZA TOMATO SAUCE

Jinsi ya kutengenza Tomato Sauce

Mara kadhaa nimekuwa nikileta Makala mbalimbali ambazo zinakupa hamasa tu ila Makala ya leo ni pesa mkononi. Pesa mkononi ndiyo ambayo kila mtu anahitaji. Pia nimeamua kukuletea makala haya ili tuendane sawa na Tanzania ya viwanda.

Najua inawezekana kabisa kila mtu kuwa na kiwanda, unashangaa wala usishangae maana huo ndio ukweli maana kila kitu kinapatikana kiurahisi katika mazingira yetu.

Unajua kuwa mikono yako ndiyo itakayokupa pesa? Kama hufahamu basi nimekuja kukujuza ni kivipi utatumia mikono yako ili uweze kuwa tajiri.

Yafuatayo ndiyo mahitaji ya kutengeneza tomato source.
1. Nyanya kilo 1.
2. Vitunguu maji viwili.
3. Vinegar vijiko 3 vya chai.
4. Sukari vijiko 2 vya chai.
5. Chumvi kijiko kimoja cha chai
6. Maji ya moto kikombe kimoja cha chai.
7. Mafuta ya kula vijiko 7 ya vyakula.

Haya ndiyo mahitaji ya kutaka kutengeneza tomato souce, hata hivyo kama unataka kutengeneza zaidi ya hapo unatakiwa kuongeza uwiano wa mahitaji hayo.

JINSI YA KUTENGENEZA TOMATO SOURCE.

HATUA YA KWANZA.
A) Menya nyanya na vitunguu kisha vikate vipande vidogo vidogo.
B) Tumia Brenda kusaga mchanganyiko wako.
C) Anza kuweka malighafi namba 1 hadi namba 4 katika brenda yako kutokana na ratio (uwiano ) uliopewa hapo juu. Saga kwa dakika kadhaa hadi uone imetokea rojo laini.

HATUA YA PILI.
A) Tumia sufuria yenye nafasi kupika mseto huu.
B) Weka sufuria yako jikoni tia mafuta ya kula acha yachemke kisha mwagia mseto wako na kisha uanze kukoroga kwa dakika 30 kuelekea upande mmoja huku ukichemka.
C) Baada ya hapo epua mseto huo utakuwa tayari imeshakuwa tomato funga vizuri na kisha peleka sokoni.

Mpaka kufikia hapo wewe Tajiri, na mafanikio makubwa ambayo yatakuwa upande wako endapo utakuwa umeamua kuondokana na umaskini kwa njia ya kutengeneza vitu mbalimbali kwa ajili ya kuuza.

Nikusihi uendelee kufuatana nami katika Makala zijazo ili tuweze kufika mahali ambapo tunatamani kufika.? Endelea kufuatana nasi hapa dira ya mafanikio kwa masomo mengine yanayokuja.

KARAFUU KIUNGO KWA VYAKULA NA TIBA YA MAGONJWA

Karafuu Kiungo kwa Vyakula na Tiba ya Magonjwa mengi

Karafuu ni zao linalotokana na  mkarafuu, ingawa karafuu hazimo katika kundi la vyakula wala vinywaji lakini ni kiungo na dawa  muhimu sana kwa maisha ya binadamu.                                                                                     
Mikarafuu ilianza kupandwa kwenye visiwa vya Shelisheli, Mauritius na sehemu nyinginezo katika karne ya 19. Miche ya mikarafuu ililetwa Zanzibar kutoka Indonesia, mashariki ya mbali mwaka 1818.

Mikarafuu inastawi zaidi Visiwani vya Unguja na Pemba ambapo katika miaka 30 iliyopiata Zanzibar ilikuwa inazalisha asilimia 80 ya karafuu zote zinazohitajika duniani ambapo uchumi wake ulitegemea sana zao la karafuu.

Karafuu zina matumizi mengi, ambapo hutumika kama kiungo katika vyakula na vinywaji, dawa kwa maradhi ya tumbo, meno na misuli vile vile hutumika katika kuleta harufu nzuri ya kinywa, mwili na mazingira ya nyumbani.

Pia karafuu zinatumika katika uzalishaji wa bizaa nyengine ikiwemo sigara, mafuta ya karafuu ambayo hutumika kwa kuchulia misuli inayouma, kutengezea dawa za meno na perfume kwa ajili ya manukato.

Karafuu zinatumika sana kwenye mapishi ya vyakula mbali mbali ikiwemo nyama, biriani, pilau, mchuzi wa masalo na vyakula vikavu kama vile vileja, beskuti na donas na kwa ubande wa vinywaji karafuu hutumika katika chai na maziwa .

Kama vilivyo viungo vyengine karafuu nazo zina utamu, ladha na harufu nzuri ya kuvutia na kupendeza katika vyakula hivyo ambapo watu wengi hasa katika bara la Asia, Mashariki ya kati na ulaya hupenda sana kiugo cha karafuu katika vyakula vyao.

Karafuu inasaidia usagaji mzuri wa chakula tumboni na ni nzuri  kwa matibabu ya maumivu ya tumbo, tumbo kujaa gesi na kiungulia. Hivyo karafuu ni miongoni mwa kiungo muhimu katika vyakula kutokana na vinasaba vya aina ya eugnol vilivyomo ndani ya karafuu.

Aidha karafuu hutumika katika utengenezaji wa mafuta (Mafuta ya karafuu) ambapo mafuta hayo husafisha damu, tafiti zinaonyesha kuwa visanaba vilivyomo katika karafauu vinapunguza sumu katika damu. Vinasaba aina ya eugnol vilivyomo ndani ya karafuu vinasaidia mzunguko mzuri wa damu.

Kutokana na ukuaji wa viwanda duniani kumekuwa na mahitaji makubwa ya karafuu pamoja na kuongezeka kwa nchi zinazozalisha ambapo karafuu hutumika sana kwa utengenezeji wa sigara katika nchi za Ulaya, Asia na Marekani.

Sigara zinazotengenezewa karafuu kutoka Zanzibar zina thamani na ubora zaidi duniani kuliko sigara zinazotengezewa karafuu kutoka nchi nyengine kutokana na ubora wa karafuu za Zanzibar.

Pia karafuu hutumika katika viwanda kwa ajili ya kutengezea dawa za meno kwa ajili ya kutunza meno na kuondosha maumivu ya meno na ufidhi, kung’arisha meno na kuleta harufu nzuri ya kinywa, harufu iliyomo katika karafuu inasaidia kuondosha harufu mbaya mdomoni.

Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa mwaka 2011katika Jarida la Asia Plant Science and Research toleo namba 1 (2) karafuu husadia kutibu vidonda vya mdomo na kuimarisha Afya ya fizi pamoja na kuzuia meno kuoza.

Aidha Mafuta ya karafuu yamekusanya vinasaba vya eugnol ambavyo vimekuwa vikitumiwa na Madaktari wa meno kwa miaka mingi kutibu matatizo ya meno na ufizi.

Karafuu inatumika katika urembo ambapo hutumika kusugulia mwili (scrub) kwakuchanganya unga wa karafuu kavu iliyosagwa na mafuta ya nazi na liwa ambapo husuguliwaa mwili mzima kuondoa uchafu.

Mbali na hayo pia karafuu hutengenezewa sabuni ambazo ni nzuri kwa kuondosha maradhi ya ngozi kama vile harara, vipele na chunusi na kuifanya ngozi iwe nyororo na yenye kuvutia. Sio hayo tu lakini pia karafuu hutumika kutengenezea mafuta mazuri kwa sababu karafuu ina harufuu ya kipekee inayovutia.

Hivyo karafuu na mafuta ya karafuu ni mazuri kwa ajili ya kutunza ngozi hasa kwa ngozi yenye mabaranga, mba na kuchakaa ambapo huifanya ngozi kuwa nzuri na yenye kung’ara.

Matumizi ya karafuu na mafuta ya karafuu kwa kawaida humfanya mtu kuwa mchangamfu kwa kuondoa uchofu kwa vile karafuu inaiweka akili katika hali nzuri na kufanya ubongo ufanye kazi vizuri. Pia husadia kuondoa matatizo ya kusinzia, kupoteza kumbukumbu na wasiwasi.

Mafuta ya karafuu husaidia kuondosha maumivu ya kichwa kwa kuchanganganywa na chumvi na kupakaa kwenye paji la uso hupoza maumivu. Pia huondosha matatizo katika mfumo wa upumuaji na kusafisha koo na hutibu kikohozi, mafua na pumu.

Mchanganyiko wa mafuta ya karafuu na mafuta ya ufuta (sesame oil) ni mazuri kwa kuondsha maumivu ya sikio.​​​

MAGEREZA KUJENGA KIWANDA CHA SUKARI

Magereza kujenga kiwanda cha sukari

JESHI la Magereza limetiliana saini na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF na NSSF ili kufufua kilimo cha miwa na kiwanda cha sukari mkoani Morogoro kitakachozalisha zaidi ya tani za sukari 30,000 kwa mwaka.

Aidha, kiwanda hicho cha sukari kitaondoa tatizo la uhaba wa sukari nchini ambalo linatokea kila mwaka sambamba na kuondoa utegemezi wa sukari ambayo huagizwa kutoka nje ya nchi wakati ambao hakuna sukari ya kutosha nchini.

Akizungumza baada ya tukio hilo Dar es Salaam jana, Mkuu wa jeshi hilo, Juma Malewa alisema Machi Mosi mwaka huu kilimo cha miwa kitaanza katika eneo la gereza Mbigiri lililopo Morogoro.

Alisema kufufuliwa kwa kilimo cha miwa na pia kiwanda hicho cha sukari kinaendana na kauli ya Rais wa awamu ya tano, John Magufuli ya kuifanya Tanzania ya viwanda.

“Moja ya ahadi zake Rais ni kuifanya nchi yetu kuwa yenye uchumi wa viwanda, katika utekelezaji wa agizo hilo tulikutana na PPF na NSSF kwa mazungumzo ya kufufua kiwanda hiki,” alisema Malewa.

Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Pensheni wa NSSF, Godias Kahyaara alisema kiwanda hicho kitazalisha tani 30,000 za sukari kila mwaka na kwamba tani zaidi ya 400,000 zitazalishwa katika kilimo cha miwa kwenye shamba hilo linalomilikiwa na Jeshi la Magereza.

“Mbali na kuzalisha sisi wenyewe, pia wakazi wa Dakawa watapata fursa ya kuuza miwa yao kiwandani, tunachowashauri wakae mkao wa kula kwa kuzalisha miwa ya kutosha kwaajili ya kuuza katika kiwanda hicho,” alisema Kahyarara.

Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio alisema kiwanda hicho kitaokoa fedha za kigeni ambazo hutumika kila mwaka kwa ajili ya kuagiza sukari nje ya nchi.

Alitoa wito kwa wakazi wa maeneo jirani na kiwanda hicho kuongeza uzalishaji wa miwa kwaajili ya kuuza kiwandani ili kuchochea uchumi wao na pia kuongeza uzalishaji wa sukari kuhakikisha kwamba hakuna sukari inayoingizwa kutoka nje ya Tanzania.

Alisema ukarabati wa kiwanda hicho unaendelea na pia wanaendelea kusafisha mashamba ya miwa kwaajili ya kuanza kilimo Machi mosi mwaka huu.

Kwa mujibu wa Malewa, kiwanda hicho cha sukari kilianzishwa mwaka 1978 lakini kilifungwa mwaka 1996 kutokana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchakavu wa mitambo na pia soko la sukari.

WATANO MBARONI KWA MAUAJI

Watano mbaroni kwa mauaji

POLISI mkoani Rukwa inawashikilia watu watano wakituhumiwa kuwaua kikatili watu watatu wa familia moja ambao ni wakazi wa kijiji cha Mfinga kilichopo katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga kwa kwa kucharangwa na mapanga na mashoka kwa kile kilichoelezwa kuwa ni imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando, aliwataja marehemu hao kuwa ni Joachim Kayanda (60), mkewe Evelina Mwanakatwe (47) na mtoto wao wa kiume aitwaye Emanuel Kayanda (27) .

Kwa mujibu wa Kamanda Kyando, watuhumiwa hao ambao hakuwa tayari kutaja majina yao kwa hofu ya kuvuruga upelelezi wa kipolisi unaoendelea, wanaendelea kuhojiwa na polisi ambapo watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa awali wa shauri lao kukamilika .

Alisema mauaji hayo yalitokea Februari 22, mwaka huu usiku wa manane katika kijiji cha Mfinga kilichopo katika Tarafa ya Mtowisa iliyopo katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga.

Akisimulia mkasa huo, Kamanda Kyando alisema kuwa usiku huo wa tukio watu wasiofahamika wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mapanga, mashoka na marungu walifunga mlango wa nyumba walimolala wanafamilia hao na kuwaua kikatili kwa kuwakata kata kwa mapanga na mashoka.

Alidai kuwa watu hao walifanikiwa kutoroka katoka eneo hilo la tukio muda mfupi baada ya kutenda unyama huo.

“Chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina kwani familia hiyo ilikuwa inatuhumiwa kuwa ni washirikina,” alisisitiza.

MKE WA BILIONEA MSUYA ASHITAKIWA TENA KWA MAUAJI

Mke wa bilionea Msuya ashitakiwa tena kwa mauaji

KWA mara ya pili, mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Mariam Mrita (41) na mfanyabiashara Revocatus Muyela (40), wamesomewa mashitaka ya mauaji. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam juzi iliwaachia huru kwa kuwa upande wa mashitaka ulishindwa kurekebisha hati ya mashitaka.

Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi amedai kuwa washitakiwa hao wanakabiliwa na kosa moja la mauaji mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Kuna madai ya kuwepo utata kuhusiana na uamuzi huo wa upande wa mashitaka.

Akiwasomea mashitaka, Kishenyi amedai kuwa washitakiwa hao wanakabiliwa na kosa moja la mauaji ambalo walilitenda Mei 25, mwaka jana.

Amedai kuwa washitakiwa hao walimuua dada wa bilionea Msuya, Aneth ambaye walimchinja nyumbani kwake Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuwasomea kosa hilo, Hakimu Simba alisema kuwa washitakiwa hawapaswi kujibu kitu chochote kwa sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Kishenyi aliiomba Mahakama iahirishe kesi hadi siku nyingine kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Utata ulitokea baada ya Wakili wa utetezi, Peter Kibatala kudai kuwa hati ya mashitaka ipo kinyume na sheria na kwamba Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Alidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kinyume na sheria kwa sababu ilishatolewa uamuzi Februari 23, mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa ambapo aliwaachia huru washitakiwa wote.

Alidai kuwa, alimsikia Hakimu Mwambapa aliyetoa uamuzi huo akisema washitakiwa wameachiwa huru na si kwamba wamefutiwa mashitaka.

"Maneno aliyoyatumia Hakimu katika uamuzi wake ni amewa-set free washitakiwa na si kuwa-discharge, hivyo hawa washitakiwa wapo huru na hawakupaswa kukamatwa na kuletwa mahakamani kusomewa kosa hilo la mauaji," alidai Kibatala.

Pia alibainisha kuwa hatua ya Mahakama hiyo kukosa mamlaka inatokana na kosa ambalo wamesomewa washitakiwa tayari limeshatolewa uamuzi.

Alidai kuwa kitendo cha upande wa mashtaka kuwakamata washtakiwa hao na kuwasomea kosa lile lile la mauaji ni sawa na uchonganishi baina ya Hakimu mmoja na mwingine.

Alieleza kuwa awali kabla ya washtakiwa hao kuachiwa huru upande wa mashtaka ulipewa nafasi zaidi ya tatu na Mahakama ili kubadilisha hati ya mashtaka lakini walishindwa.

Akijibu, Kishenyi amedai kuwa washitakiwa hao wamepandishwa kizimbani jana na kusomewa kosa hilo kwa mujibu wa sheria.

Amedai kuwa uamuzi uliotolewa juzi na Mahakama hiyo ilikuwa ni kuwafutia mashitaka ambapo Jamhuri ina uwezo wa kuwakamata tena washitakiwa na kuwasomea kosa hilo la mauaji.

Alieleza kuwa kwa namna yeyote ile uamuzi uliotolewa mahakamani hapo, ulikuwa na athari za kuwafutia mashtaka washtakiwa, ndio maana wamekamatwa tena.

Amebainisha kuwa haoni sehemu yeyote ambayo inaonesha kosa walilosemewa washitakiwa lipo kimakosa mahakamani hapo.

Kutokana na mvutano huo wa kisheria, Hakimu Simba amesem, anajua mzizi wa fitina wa kuibuka kwa hoja hizo ni uamuzi uliotolewa juzi mahakamani hapo.

"Ili kukata mzizi huo wa fitina na kuondoa utata, itabidi uamuzi huo uletwe kwa ajili ya kuuangalia sehemu ambazo mnabishania, tena kwa vile umetolewa na mahakama hii...hakuna kitakachoharibika," amesema Hakimu Simba.

Aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 7, mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi kama washtakiwa waliachiwa huru ama walifutiwa mashtaka. ends

Tuesday, February 21, 2017

WATU WANNE WAFA MGODINI WAKIPORA DHAHABU

Watu wanne Wafa mgodini wakipora dhahabu

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA, DHAHIRI KIDAVASHARI.

WATU wanne wamefariki dunia na idadi kama hiyo kujeruhiwa baada ya kufukiwa kwenye machimbo ya dhahabu eneo la Nanyuki, wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari alisema ajali hiyo ilitokea jana asubuhi baada ya zaidi ya wanananchi 50 kuvamia shimo la dhahabu linalomilikiwa na Vincent Minja, mkazi wa jijini Dar es Salaam.

Kamanda Kidavashari alisema wananchi hao walivamia shimo hilo baada ya kupata taarifa kuwa linatoa dhahabu nyingi.

Hata hivyo, alisema wananchi hao walianza kuchimba bila kuchukua tahadhari, hali iliyosababisha shimo hilo kuporomoka na kuwafukia watu 11.

Kamanda Kidavashari aliwataja watu wanne waliofariki dunia ndani ya shimo hilo kuwa ni Andrew Paulo (26), Mark Frederick (22) na Isaack Mwanjale (30) wakazi wa kijiji cha Itumbi, na Hamis Mailosi (25), mkazi wa kijiji cha Mapogoro.

Aidha, aliwataja waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni Saimon Majaliwa (25), mkazi wa Itumbi, Mazoea Mahona (25), mkazi wa Mkoa wa Tabora, Benny Bahati (23), mkazi wa Kijiji cha Mapogoro na James Alinanuswe (26), mkazi wa Tukuyu wilayani Rungwe.

Alisema kilichosababisha shimo hilo kuporomoka ni wananchi hao kuchimba eneo hilo bila utaratibu na kwamba hawakuchukua tahadhari yoyote kutokana na hali ya mvua inayonyesha mara kwa mara.

“Wananchi wale tunawachukulia kuwa ni wezi kwa sababu walivamia eneo lenye leseni ya mtu mwingine. Taarifa za awali ni kwamba waliobainika kuwa wamefariki dunia ni wanne na wengine wanne wamejeruhiwa, lakini watatu walitoka wakiwa hai na walikimbia,” alisema Kamamda Kidavashari.

Alisema baada ya uokoaji, miili ya marehemu ilipelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya huku majeruhi wakiwa wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Diwani wa Kata hiyo ya Matundasi, Kimo Chogga, alisema wananchi hao walianza kuvamia eneo hilo Jumatatu ya wiki iliyopita na kwamba walizuiliwa na mwenye leseni ya eneo hilo, lakini walikaidi.

Alisema ilipofika Alhamisi, walielimishwa vizuri na kukubali kusimamisha uchimbaji baada ya mwenye eneo kuwaeleza kuwa kufikia jana, atakuwa ameweka utaratibu mzuri wa namna ya kuchimba.

Hata hivyo, Chogga alisema wananchi hao jana asubuhi walivamia tena shimo moja wakidai mmiliki wa leseni ya eneo hilo naye aliendelea kuchimba.

Alisema baada ya kufukiwa, juhudi zilianza kufanyika za uokoaji na katika harakati hizo ndipo walipokuta watu wanne kati ya 11 waliokuwa wamefukiwa wameshafariki dunia, wanne wamejeruhiwa na wengine watatu walitoka wazima na kutoroka.

“Baada ya waliokuwa wamefukiwa kuokolewa, bado wananchi waliendelea kung’ang’ania waendelee kuchimba, hali iliyolifanya Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi na kuwataka wananchi hao waondoke waelekee ofisi ya kijiji kwa ajili ya mazungumzo," alisema Chogga.

Hata hivyo, alisema wananchi hao walianza kufanya fujo kwa kuzuia barabara kwa kutumia miba, magogo na mawe wakidai miili ya wenzao waliofariki dunia ili waendelee na maziko.

Nipashe lilimtafuta Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Dk. Stanford Mwakataghe, ili kuelezea hali ya majeruhi na miili iliyopokelewa katika Hospitali ya Wilaya, lakini simu yake ilikuwa haipokelewi.

DONALD NGOMA HATACHEZA MECHI YA SIMBA VS YANGA

Donald Ngoma hatacheza mechi ya Simba Vs Yanga


Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma amewathibitishia mashabiki wa klabu hiyo hatacheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ngoma amewambia mashabiki mubashara kupitia mtandao wake wa Facebook alipokuwa akifafanua habari kwamba amegoma kucheza.

"Wengi wanauliza kuhusiana na hali yangu, ukweli ni kwamba mimi ni majeruhi na sitacheza mechi ya Jumamosi, siwezi kucheza kwavile bado nina majeraha."

Kuna watu wanazusha kwamba nimegoma kucheza, hakuna kitu kama hicho hayo ni maneno tu, mimi ninaumwa ntachezaje? mnatakiwa kuelewa afya ya mchezaji ni kitu muhimu kwenye maisha ya mpira.

"Nitakuwa nje ya uwanja kama wiki sita, wala mashabiki wasiwe na wasiwasi kuna Chirwa(Obrey) na Tambwe (Amissi) ni wanajeshi watapambana. Timu itafanya vizuri."


Monday, February 20, 2017

SHERIA YA KUZUIA WANAUME KUOA WAKE WENGI KUTANGAZWA NIGERIA

Sheria ya kuzuia wanaume kuoa wake wengi kutangazwa Nigeria

Mmoja wa viongozi wakuu wa kiislamu nchini Nigeria anasema kuwa atatangaza sheria ambayo itawazuia wanaume kuoa zaidi ya mke mmoja.

Kiongozi huyo kutoka jimbo la Kano Lamido Sanusi, anasema kuwa tamaduni ya kuoa wake wengi imechangia kuwepo ugaidi kaskazini mwa nchi.

Dini ya kiislamu inamruhujsu mwanamume kuoa hadi wake wanne.

Lakini kiongozi huyo anasema kuwa baadhi ya wanaume wa kiislamu hawana uwezo wa kutunza familia kubwa.

"Wanazaa watoto ishirini, watoto hawapati elimu na huishia kuwa wahalifu na magaidi." Alisema Sanusi.

Umaskini unaonekana kuwa sababu kuu ya kuibuka kwa kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Sanusi anasema kuwa sheria hiyo itakuwa sehemu ya sheria ya kifamilia ambayo itaharamisha ndoa za lazima.

Vita dhidi ya dawa za Kulevya Waathirika wajitokeza kwa wingi kupata dawa ya Methadone

Vita dhidi ya dawa za kulevya inayoendelea imeanza kuzaa matunda baada ya idadi ya waathirika wa dawa hizo kujitokeza kwa wingi kwenye clinic za waathirika wa dawa za kulevya zinapopatikana dawa za METHADONE.

Hata hivyo changamoto iliyopo kwa vituo hivyo inadaiwa kuwa ni uwezo mdogo wa kuhudumia idadi hiyo kubwa ya waathirika inayozidi kuongezeka siku hadi siku nchini kote hali ambayo inatoa chanagmoto kwa mamlaka husika kuangalia namna ya kujenga uwezo kwa vituo kama hivyo ili viweze kutoa huduma kwa waathirika .

Katika mahojiano maalum na Channel Ten Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dr Aziz Msuya amesema kuwa vituo vya vya matibabu ambavyo ni vitatu tu kwa nchi nzima ni Kliniki ya METHADONE ya Muhimbili, Mwanyamala na Temeke hali ambayo bado ni kikwazo katika kuwasaidia waathirika wa dawa za kulevya walioamua kuacha matumizi ya dawa hizo, na wameamua kwa hiyari yao kwenda kwenye vituo hivyo kupata matibabu.

Wakielezea madhara ya dawa za kulevya kwa watumiaji wa dawa hizo Mganga Mkuu Manispaa ya Kinondoni pamoja na msimamizi wa kituo cha kuwasaidia waathirika hao katika Hospitali ya Mwananyamala wanasema.

Channel ten imefanikiwa kuzungumza na baadhi ya waathirika wa dawa za kulevya ambao tayari wameshaanza kupata matibabu kwenye vituo hivyo.






DC ROMBO AMSWEKA RUMANDE MWALIMU

DC Rombo amsweka rumande mwalimu

Rombo. Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Agnes Hokororo amemweka rumande mwalimu wa Shule ya Sekodari Matolo baada ya kukutwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo.

Hokororo amesema tukio hilo limetokea (leo Jumatatu saa 12 asubuhi) baada ya mwalimu huyo kuwekewa mitego na wazazi wa mwanafunzi huyo  ambapo mwanafunzi huyo alitoroka nyumbani usiku na kwenda kulala nyumbani kwa malimu huyo.

Amesema baada ya wazazi na baadhi ya majirani walizingira nyumba ya mwalimu huyo na kunipigia simu ili akashuhudie wakifanya kitendo hicho.

“Kwa kweli ni jambo la kusikitisha  nilifika katika nyumba ya mwalimu  asubuhi  majira ya saa 12:00 na kukuta akiwa na mwanafunzi huyo huku  mwanafunzi akikiri kuwa amekuwa akitoroka mara kwa mara  na kuja kulala kwa malimu wake,”amesema Hokororo.








Sunday, February 19, 2017

MAMELODI SUNDOWNS IMETWAA SUPER CUP YAIPIGA TP MAZEMBE

Mabingwa wa klabu bingwa Afrika Mamelodi Sundowns wameshinda ubingwa wa Super Cup 2017 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya miamba ya DR Congo TP Mazembe.

Mbrazil Ricardo Nascimento ndiye aliyepeleka shangwe kwa mashabiki wa Mamelodi kufatia kujaza kambani mkwaju wa penati dakika ya 83 na kukipa ushindi kikosi cha Pitso Mosimane baada ya kutawala mchezo kwa muda mwingi kwenye uwanja wa Loftus Versveld.

Penati hiyo ilitolewa kufatia nahodha wa Mamelodi Homphela Kekana kuangushwa kwenye box na beki wa TP Mazembe Issama Mpeko.

Licha ya klabu hiyo ambayo ilikuja Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo kutawala game, walipata nafasi nzuri dakika ya 78 ambapo Anthony Laffor raia wa Liberia aliachia shuti ambalo liligonga mwamba baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Percy Tau.

Denis Onyango golikipa wa Mamelodi na timu ya taifa ya Uganda Cranes ambaye pia ni mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, alifanya kazi ya ziada kuiweka timu yake salama baada ya shambulizi kali lililofanywa na Mazembe.

Kikosi cha Pitso Mosimane ambao pia ni mabingwa wa Afrika kimekuwa cha pili kutwaa taji la Super Cup kwa timu za Afrika Kusini wakitanguliwa na Orlando Pirates waliotwaa taji hilo mwaka 1996 walipoifunga JS Kabylie ya Algeria.

Mbali ya kutwaa kombe, wakali hao wa Afrika Kusini wamebeba kitita cha dola 100,000 za  Marekani wakati TP Mazembe wao wakichukua dola 75,000.

SIMULIZI YA MTOTO WA UNGA ALIYEIBULIWA NA RC MAKONDA

Simulizi ya Mtoto wa Unga Aliyeibuliwa na RC Makonda inasikitisha


DAR ES SALAAM: Mtoto Zuhura Athuman (16), mmoja kati ya wawili waliosimamishwa mbele ya kamera na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitaja awamu ya tatu ya wanaodaiwa kujihusisha na madawa ya kulevya, amesimulia mambo mazito yaliyosababisha kuanza kuvuta unga na kujihusisha na ngono akiwa katika umri mdogo.

Akizungumza na Risasi Jumamosi akiwa katika kituo cha uangalizi wa waathirika wa madawa ya kulevya, Pederef kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, alisema ndoto zake zote zimezimika baada ya kuanza kuvuta unga akiwa na umri wa miaka 11, ingawa kwa sasa ameachana na tabia hiyo.

ALIANZA NA ‘MSUBA’

Mtoto huyo ambaye hakupata bahati ya kumfahamu mama yake mzazi kutokana na kufariki, alizaliwa kwa baba aliyekuwa mvuta bangi na mnywa pombe kupita kiasi, hali iliyosababisha naye kuanza ‘kula msuba’ akiwa na umri wa miaka tisa tu, wakati huo wakiishi Kinondoni Manyanya.


“Nilikuwa nikikuta baba kaacha kipisi cha bangi nachukua na kwenda kuvuta, wakati huo nikiwa na miaka tisa tu na kuanzia hapo ukawa ndiyo mchezo wangu. Ilikuwa kama nikikosa hela, bora niibe

ilimradi ninunue bangi ili nijisikie vizuri,” alisema.

BABA YAKE AANZA KUUMWA, AFARIKI

Zuhura anasimulia kuwa maisha yao hayakuwa mazuri kutokana na tabia mbaya za baba yake, lakini hali ilizidi kuwa tete baada ya mzazi huyo kuanza kuumwa, kitendo kilichosababisha achukuliwe na shangazi yake, aliyekuwa akiishi Mbagala kwa uangalizi zaidi.

Muda mfupi baadaye, baba yake alifariki, kitu kilichoyafanya maisha yake yawe mabaya zaidi, akalazimika kuacha masomo katika Shule ya Msingi Kibondemaji akiwa darasa la pili, kwani bangi nayo ilikuwa imeshamkolea kichwani.

“Nilikuwa sitaki tena shule, nilikuwa nikiwatukana walimu na mtaani nilikuwa mtata, sikumuelewa mtu yeyote,” alisema.

AANZA KUJIUZA MBAGALA

Akiwa bado kwa shangazi yake, alianza tabia ya kuondoka na kukaa siku mbili au tatu bila kurudi nyumbani, akisema alikuwa akienda kujiuza Mbagala Zakhem ili aweze kupata hela ya kununulia bangi na mara kwa mara ndugu zake walikuwa wakimkamata na kumrejesha nyumbani ambako alifungwa kamba.

“Nilivyoona kila siku ndugu zangu wananikamata na kunifunga kamba, niliamua kutoroka na kwende Kariakoo, ambako ndipo maisha yangu yalipozidi kuharibika.”

AKUTANA NA MBABA MBWIA UNGA

Akiwa na tabia yake ya kuvuta bangi, hapo Kariakoo alikutana na kijana mmoja mwenye miaka 40, ambaye alianza naye uhusiano wa kimapenzi, siku moja akiwa anavuta bangi zake, ndipo kijana huyo akamwambia ili ajisikie vizuri zaidi, yampasa kuchanganya na unga kidogo.

“Mimi huyo kaka alikuwa akinipa hela ya kununua bangi, akanidanganya kuwa nikitaka niione nzuri, anichanganyie na unga kidogo na nilipojaribu nilijisikia vizuri sana, ndio ukawa mwanzo wangu wa kubwia unga.” 

KUMBE JAMAA ALIKUWA NA NGOMA!

Zuhura aliendelea kusema kuwa alipoanza uhusiano na kijana huyo, watu wakaanza kumuasa kuachana naye kwa madai kuwa alikuwa na Ukimwi, lakini hakusikia kwa vile alikuwa akipewa shilingi elfu sita ambazo alizitumia kununulia unga.

“Huyo mbaba alikuwa ni mkubwa sana kwangu lakini sikujali kwa sababu aliniwezesha kupata hela ya unga, nilikuwa naombwa sana niachane naye kwa vile alikuwa mwathirika, lakini ndiyo hivyo.”

AKAMATWA, ATUPWA SOBER

Akiendelea kutumia madawa na mpenzi wake mitaa hiyo ya Kariakoo, ghafla siku moja alijikuta akikamatwa na watu asiowafahamu, ambao walimbeba msobemsobe hadi katika kituo hicho cha Pederef kilichopo Kigamboni, ambako walimpatia mahitaji yake yote na baadaye akabainika kuwa ni mwathirika.

“Nilipoambiwa nimeathirika sikushtuka sana kwa kuwa niliyoyafanya ni mengi, ila niliumia kwa kuwa ndoto zangu zote zimezima kabisa kwa kuwa sijasoma, nimekuwa teja na Ukimwi juu ila nashukuru kitu kimoja kwa sasa nimeacha unga ila naumia kwenye huu ugonjwa inawezekana nimeambukiza wengi naumia sana,” alisema.

  AHARIBIKA VIDOLE, MIGUU

Zuhura ambaye bado anahitaji kusoma, chakula na matunda kwa ajili ya kuuweka mwili wake sawa kutokana na ugonjwa huo, pia ameharibika vidole vyake vya mikononi, kwa kile alichodai ni kwa sababu ya vigae, alivyokuwa akitumia katika ubwiaji unga.


Licha ya vidole hivyo vinavyoonekana kuharibika ngozi yake, pia miguu yake nayo inaonekana kuathirika na ugonjwa wa ngozi ambao unafanana na fangasi.

BAADA YA UWOYA KUSEMA ANAPENDA WANAUME WAGUMU, FID Q AMJIBU

Baada ya Uwoya kusema anapenda wanaume wagumu, Fid Q amjibu


Baada ya malkia wa filamu nchini Irene Uwoya kutoa kauli yake ya kuwa anapenda wanaume wagumu na kumtolea mfano Fid Q, rapper huyo amefunguka na kuzungumzia kauli ya muigizaji huyo.


Fid Q amedai yeye siyo mwanaume mzuri lakini ana good look.

“Mimi wakiitwa wanaume wabaya siwezi kwenda lakini pia wakiitwa mahandsome boy siwezi kwenda, lakini najijua mimi ni good look,” alisema Fid Q.

Pia rapper huyo amempongeza muigizaji huyo kwa jicho lake la kumuona na kumtolea mfano

AFYA YA MANJI IKO FITI, SASA MAPAMBANO YANAENDELEA

Afya ya Manji iko fiti, sasa mapambano yanaendelea


Dar es Salaam. Afya ya mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji inaendelea vizuri baada ya jopo la madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), kuendeleza matibabu yake baada ya kupata dhamana akitokea mahakamani.

Hii ni mara ya pili kwa Manji kuugua ghafla na kulazwa hospitalini hapo, mara ya kwanza ilikuwa polisi alipokuwa akihojiwa ambako aliugua ghafla jioni na alipelekwa JKCI.

Mkurugenzi wa Tiba wa JKCI, Dk Peter Kisenge alisema walimpokea Manji akitokea mahakamani na kwamba anaendelea na matibabu na afya yake inazidi kuimarika.

“Tunaendelea kumpatia matibabu yanayohitajika kwake kwa sasa na anaendelea vizuri,” alisema Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya moyo katika taasisi hiyo.

Taarifa za ndani zaidi zilidai kuwa Manji kwa sasa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo. Hata hivyo, madaktari wa JKCI bado wameendelea kusita kuzungumzia tatizo linaloisumbua afya ya Mwenyekiti huyo wa klabu ya Yanga.

Hata hivyo, mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo, Manji alikutana na wingi wa wagonjwa kiasi cha kumfanya alazwe na wagonjwa wengine baada ya vyumba vya wagonjwa mashuhuri kujaa.

Vita dawa za kulevya

Vita dhidi ya dawa za kulevya imeendelea kupamba moto nchini hasa baada ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kukabidhiwa majina 97 ya wauzaji wakubwa, pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzindua Baraza la Taifa kukabiliana na uhalifu huo.

Ni vita ambayo haipiganwi Tanzania pekee, Kenya kuna watuhumiwa wamefikishwa mahakamani nchini Marekani, Rais Donald Trump ameanza mapambano hayo huku nchini Ufilipino Rais wake, Rodrigo Duterte aliishaanza kwa kuwapiga risasi watumiaji na wauzaji.

Kinachotokea sasa nchini ni mwendelezo wa kilichoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyeanza na wasanii na baadaye akataja watu 65 na hivi karibuni alikabidhi majina 97 kwa Kamishna Mkuu Rogers Sianga akisema wanaweza kuwa na taarifa zinazoweza kusaidia katika vita hiyo.

Pia, wakati Makonda akikabidhi majina 97 kwa Kamishna Sianga, alitoa amri ya kukamatwa Chid Mapenzi (Rashid Said) na kesho Jumatatu kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro watuhumiwa watatu wa dawa za kulevya, Agnes Gerald ‘Masogange, Chid Mapenzi na Walid Nasher watafikishwa mahakamani.

Wakati Makonda akikabidhi majina hayo, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima alitangaza vita dhidi ya Makonda baada ya kumtaja kwenye orodha ya wanaojihusisha na uhalifu huo.

Askofu Gwajima alisema hayo katika ibada ya Jumapili iliyopita iliyofanyika kanisani kwake Ubungo, baada ya kuachiwa na polisi, alitumia fursa hiyo kuwaeleza waumini wake na Watanzania kilichotokea tangu aliporipoti polisi.

Ilivyokuwa Jumatatu

Akizungumza katika kikao alichokiita cha awamu ya tatu ya kutaja majina wanaojihusisha na dawa za kulevya, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Makonda alisema ana majina mengine 97 baada ya majina ya wasanii na yale 65.

Awamu ya kwanza ilikuwa mapema mwezi huu, Makonda alitangaza hadharani majina ya wasanii aliodai wanajihusisha na dawa za kulevya akiwataka wafike kituo cha polisi cha kanda maalumu kwa ajili ya mahojiano huku awamu ya pili akiwataja wanasiasa na viongozi wa dini akiwataka pia wafike katika kituo hicho.

Makonda alisema kundi hilo la tatu, limewahusisha baadhi ya watu ambao wako ndani ya nchi aliodai wana mtandao na watu wa nje ambao kuingiza kilo 2,000 au 5,000 siyo jambo gumu kwao.

Siku hiyo hiyo, Kamishna Sianga alitumia fursa hiyo kusema kuwa atawaagiza maofisa wa Serikali waliopitisha tani 21 za viuatilifu vya kutengeneza dawa za kulevya kukamatwa na kuhojiwa na wakibainika watachukuliwa hatua.

Jumanne

Jina la Makonda lilitawala kila kona nchini ikiwamo kutajwa katika mkutano wa Bunge uliomalizika hivi karibuni na kujadiliwa zaidi katika mitandao ya kijamii, ikiwamo makundi ya WhatsApp na mingine.

Wakati mkuu wa mkoa huyo akitawala kila kona, mfanyabiashara Manji aliyekuwa yupo hospitali kwa ajili ya matibabu akiwa chini ya ulinzi, alikumbwa na mkasa mwingine baada ya Kampuni ya Quality Group kudaiwa kuajiri wageni 25 wasiokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.

Ofisa Uhamiaji wa Dar es Salaam, John Msumule aliwaeleza wanahabari kuwa uchunguzi uliofanywa na idara hiyo ulibaini watu 128, waliajiriwa katika kampuni tofauti ambazo ni miongoni mwa kampuni 20 zilizo chini ya Quality Group.

Msumule alisema kutokana na hali hiyo, wamepanga kumshtaki Manji kama mmiliki wa Quality Group kutokana na tuhuma za kuajiri raia wa kigeni wasio kuwa vibali, na kutoa wito kumtaka kuripoti uhamiaji baada ya kutoka polisi

Jumatano

Manji alitoka hospitali Jumatano saa 10.00 jioni baada ya kupatiwa matibabu kwa siku tatu, ingawa haikufahamika alikwenda nyumbani au polisi. Mbali na hilo, siku hiyo vyombo vya habari viliripoti kukamatwa kwa mwanadada anayetamba katika video za nyimbo mbalimbali za bongo fleva, Agnes Gerald ’Masogange’ kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya.

Alhamisi

Manji alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu, akitokea hospitalini alikokuwa amelezwa baada ya kuugua ghafla akiwa katika kituo cha polisi.

Manji alipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kutumia dawa za kulevya aina ya heroin, hata hivyo mfanyabiashara huyo alikana shtaka hilo.

Katika kesi hiyo, Manji aliwakilishwa na mawakili watatu ambao ni Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Jeremiah Mtobeya wakati upande wa Serikali uliwakilishwa na Osward Tibabyekoma , Kishenyi Mutalemwa (Wakili Mwandamizi wa Serikali) na Shedrack Kimaro.

Tibabyekomwa alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na akaomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika.

Wakili Mgongolwa kwa niaba ya jopo la mawakili wa Manji aliomba Mahakama kumpa dhamana mteja wao kwa sababu shtaka linalomkabili kisheria linadhaminiwa na kwamba apewe masharti nafuu.

Hata hivyo, Tibabyekoma aliiambia mahakama hiyo kuwa hawana pingamizi kwa sababu shtaka hilo linadhaminika kisheria.

Baada ya maelezo hayo, Manji alitakiwa kutimiza masharti ya dhamana kwa kuwa na mdhamini mmoja anayeaminika ambaye atasaini hati ya dhamana ya maneno ya thamani ya Sh10 milioni.

Manji alidhaminiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ambaye aliikamilisha kazi hiyo na Manji kuachiwa huru.

Ijumaa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliwataka wakuu wa mikoa nchini na wilaya kutotangaza majina ya watuhumiwa kabla ya kufanyika uchunguzi na kujiridhisha.

Majaliwa alitoa kauli wakati akizindua Baraza la Taifa la Dawa za Kulevya, hafla iliyofanyika ofisini kwake Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wakuu wa mikoa mbalimbali wakiwamo wakuu wa majeshi ya ulinzi na usalama. Aliwataka wakuu wote wa mikoa kushiriki vita hiyo kwa kuwa wao ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama kwenye maeneo yao ya kazi, pia kwa kuzingatia sheria na kanuni wana uwezo huo.

MASOGANGE NA CHIDI MAPENZI TUMEWAKUTA NA MADAWA PIA WANATUMIA

Masogange na Chid Mapenzi Tumewakuta na Madawa pia Wanatumia- Kamanda Sirro


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Simon Sirro amesema  watuhumiwa watatu Agnes Masogange, Rashid Idd au Chid Mapenzi na Wallis Latif Nasher ambaye ni muuza magari katika eneo la mikocheni watapandishwa kizimbani Jumatatu kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya lakini pia walibainika wanatumia dawa hizo baada ya kupelekwa kwa Mkemia Mkuu

Katika kupambana na Askari feki, jeshi limemtia mbaroni aliyekuwa askari Magereza wa cheo cha Koplo Peter Elias Msigwa aliyekuwa mtumishi katika gereza la keko, ambaye alifukuzwa kazi Desemba mwaka jana, lakini alikamatwa jana akiwa na mavazi ya kiaskari tena akiwa amejipandisha cheo kutoka koplo hadi Sajenti wa Polisi

Jeshi hilo pia limesema limewatia mbaroni watu 65 kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya pamoja na watuhumiwa 73 wa wizi na ujambazi wa kutumia silaha, mita

UMEIPATA HII YA FLORA MBASHA KUTAMBULISHA WACHUMBA WAWILI KANISANI

Umeipata hii ya Flora Mbasha kutambulisha Wachumba Wawili Kanisani?


DAR ES SALAAM: Mwanamuziki wa Injili Bongo, Flora Mbasha amezua gumzo la aina yake baada ya kudaiwa kuwatambulisha wachumba wawili tofauti katika Kanisa la Mchungaji Paul Bendera wa Kanisa la Ufunuo, Kimara- Bonyokwa.

Chanzo makini kilichopo kwenye kanisa hilo, kimeeleza kuwa, Flora ambaye sasa anatarajiwa kuolewa na jamaa anayefahamika kwa jina la Daud Kusekwa, awali alidaiwa kumtambulisha Peter Elias kama mchumba wake hivyo kuzua tafrani kwa waumini kuhoji kulikoni atangaze uchumba kwa watu tofauti ndani ya muda mfupi.

“Unajua tatizo linakuja ni kama Flora aliamua kubadili gia angani, awali alikuja kanisani kwetu na yule Peter ambaye pia mwanzoni watu walikuwa wakijua ni mlinzi wake, ghafla tukashangaa amemleta mtu mwingine na kusema ndiye atakayefunga naye ndoa.

“Huwezi amini hili suala litakuwa limempasua sana kichwa mchungaji. Watu hawawezi kukubali kwa lengo la kujenga nidhamu watataka kusimamia haki, kama ni yule wa awali ndiyo halali kutambulika kanisani au huyu mpya,”  kilisema chanzo hicho ambacho kilijitambulisha kuwa kinasali kanisani hapo.

Mwanahabari wetu alimwendea hewani Mchungaji Bendera ambapo alikiri kuwafahamu Flora, Daud na Peter lakini akasema Peter alimtambulisha tu kama muumini hivyo hakuona sababu ya kumkataa Daud pindi alipotambulishwa na Flora kama mchumba wake wanayetarajia kuoana.

“Peter na Flora walikuja kama waumini. Lakini kama umesikia tofauti, nitawaita wote ili kuliweka sawa,” alisema mchungaji huyo.

Hata hivyo, chanzo kilichopo kanisani hapo kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, mbali na uchumba huo kuzua tafrani kanisani hapo, kuna taarifa kuwa Flora anamtishia Peter kwamba amuache na asiingilie maisha yake na mpenzi wake wa sasa.

“Nasikia Flora anamtishia sana Peter hususan baada ya Peter kuwa anamtaka mwanaye ambaye amemnyang’anya. Sasa anamchimba kweli mkwara hadi jamaa imebidi atoe taarifa kituo  cha polisi,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kunyaka ubuyu huo, mwanahabari wetu alimvutia waya Peter ambapo alipopatikana alikiri kupokea vitisho hivyo na kwamba ametoa taarifa katika Kituo Kidogo cha Polisi Tabata- Kisiwani.

“Ni kweli ananitishia lakini mimi siwezi kukubali mwanangu alelewe na mtu ambaye sina imani naye. Nitaenndelea kudai haki yangu,” alisema Peter huku akimtumia mwandishi wetu RB iliyosomeka, TBK/RB/37/2017 TAARIFA.

Alipoulizwa kama ameitwa na Mchungaji Bendera ili wakazungumzie suala lake akasema hajaitwa.

Kwa upande wake Flora, alipoulizwa kuhusiana na madai hayo, alisema hataki kabisa kuzungumzia habari za Peter.

Flora ambaye ameimba nyimbo nyingi nzuri za Injili ikiwemo Jipe Moyo, kabla ya kumuacha Peter na kuingia kwenye uchumba na Daud, aliolewa na Emmannuel Mbasha ambaye walitengana mwaka 2014.