Mabingwa wa klabu bingwa Afrika Mamelodi Sundowns wameshinda ubingwa wa Super Cup 2017 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya miamba ya DR Congo TP Mazembe.
Mbrazil Ricardo Nascimento ndiye aliyepeleka shangwe kwa mashabiki wa Mamelodi kufatia kujaza kambani mkwaju wa penati dakika ya 83 na kukipa ushindi kikosi cha Pitso Mosimane baada ya kutawala mchezo kwa muda mwingi kwenye uwanja wa Loftus Versveld.
Penati hiyo ilitolewa kufatia nahodha wa Mamelodi Homphela Kekana kuangushwa kwenye box na beki wa TP Mazembe Issama Mpeko.
Licha ya klabu hiyo ambayo ilikuja Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo kutawala game, walipata nafasi nzuri dakika ya 78 ambapo Anthony Laffor raia wa Liberia aliachia shuti ambalo liligonga mwamba baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Percy Tau.
Denis Onyango golikipa wa Mamelodi na timu ya taifa ya Uganda Cranes ambaye pia ni mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, alifanya kazi ya ziada kuiweka timu yake salama baada ya shambulizi kali lililofanywa na Mazembe.
Kikosi cha Pitso Mosimane ambao pia ni mabingwa wa Afrika kimekuwa cha pili kutwaa taji la Super Cup kwa timu za Afrika Kusini wakitanguliwa na Orlando Pirates waliotwaa taji hilo mwaka 1996 walipoifunga JS Kabylie ya Algeria.
Mbali ya kutwaa kombe, wakali hao wa Afrika Kusini wamebeba kitita cha dola 100,000 za Marekani wakati TP Mazembe wao wakichukua dola 75,000.
No comments:
Post a Comment