Wednesday, February 15, 2017

CHINA KUJENGA UWANJA WA KISASA CHALINZE

China kujenga uwanja wa kisasa Chalinze

Halmashauri ya Chalinze, Mkoani Pwani, ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na Serikali ya China, ili kujenga uwanja wa kisasa wa michezo katika eneo la kijiji cha Msoga.

Akizungumza na East Africa Radio, Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema ujenzi wa uwanja wa kisasa katika jimbo hilo, ni kuboresha miundombinu na kukuza michezo jimboni humo.

Ufadhili wa ujenzi wa uwanja huo wa michezo kwa watoto wa Msoga ni muendelezo wa ufadhili wa China katika kijiji cha Msoga baada ya kujenga shule ya msingi Msoga.

No comments:

Post a Comment