Saturday, February 18, 2017

RIPOTI YA UGUNDUZI MPYA WA BARA LA 8 DUNIANI

Ripoti ya Ugunduzi mpya wa bara la 8 Duniani

Wanasayansi wafahamisha kuwa bara la 8 lawezekana kuwa lipo chini ya bahari ya Pasifiki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika jarida la Marekani la 'Geological Society of America' ni kwamba bara hilo limepewa jina la Zealandia .

Bara hilo lililokubalika na wanasayansi linasemekana kupatikana katika upande wa Kusini Magharibi mwa bahari ya Pasifiki.

Liko na ukubwa wa kilomita milioni 5 za mraba sawa na thuluthi ya ardhi ya bara la Australia .

Wanasayansi wamesema kuwa bara hilo limefinikwa na maji ya bahari .

No comments:

Post a Comment