Tuesday, February 14, 2017

ASILIMIA 40 HAWAJAJIUNGA SEKONDARI

Dar es Salaam. Imebainika kuwa asilimia 40 ya watoto wanaotakiwa kusoma sekondari wameshindwa kutokana na vikwazo mbalimbali licha ya kuwapo kwa sera ya elimu bure.

Ripoti yenye jina la ‘nilikuwa na ndoto za kumaliza shule’ iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu (Human Rights Watch) Dar es Salaam jana, imetaja vikwazo hivyo kuwa ni pamoja na sera zilizopitwa na wakati na hali ngumu ya maisha.

Mtafiti wa haki za watoto wa shirika hilo, Elin Martinez amesema katika utafiti huo walioufanya mwaka 2016 waliwahoji wanafunzi 220 wa shule za sekondari, vijana ambao hawapo shuleni, wazazi, wataalamu wa elimu, wanaharakati na maofisa wa Serikali na kugundua kuwa zaidi ya watoto milioni 1.5 wamekosa elimu ya sekondari.

No comments:

Post a Comment