Thursday, February 16, 2017

VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA VYAKAMATA MASHAMBA MAKUBWA YA BANGI WILAYANI TARIME

Vikosi vya ulinzi na usalama vyakamata mashamba makubwa ya bangi wilayani Tarime.

Vikosi vya ulinzi na usalama katika kanda maalum ya Tarime na Rorya, vimefanikiwa kakamata mashamba makubwa ya bangi ambayo yamelimwa katika ardhi ya nusu ya kijiji cha Nyarwana ikiwa ni mara ya kwanza kwa mashamba hayo makubwa kukamatwa katika wilaya ya Tarime mkoani Mara.

 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Tarime Bw. Glorious Luoga,amesema licha ya oparesheni hiyo ya siku mbili kufanyika katika kata za Matongo na Kibasuka,lakini mashamba makubwa yamekamatwa katika kijiji cha Nyarwana huku wakulima wa zao hilo haramu wakilinda mashamba hayo kwa kutumia silaha za jadi.

Kwa upande wake kamanda wa polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya,kamishina msaidizi wa jeshi la polisi ACP Andrew Satta,amesema watu kumi na nne wamekamatwa kwa kumiliki mashamba 37 ya bangi, yakiwemo magunia 20 ya bangi kavu sawa na tani moja iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya kuingizwa sokoni.

No comments:

Post a Comment