Tuesday, February 14, 2017

MAJALIWA AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUWA WABUNIFU

Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini wawe wabunifu katika kusaidia kutafuta vyanzo vya mapato kwenye jamii inayowazunguka.

Ametoa wito huo leo ofisini kwake mjini Dodoma mara baada ya kupokea mchango wa Sh 5.6 milioni kwa ajili ya kununulia madawati 70 kutoka kwa watumishi wa Tamisemi - Dodoma.

Amesema ubunifu huo uliofanywa na watumishi wa Tamisemi ni mfano mzuri wa kuigwa na watumishi wengine nchini kwani utaisaidia Serikali kuleta maendeleo.

“Hii ni mara ya tatu kwa Tamisemi kuchangia huduma za jamii kwenye maeneo mbalimbali nchini… lakini pia niwashukuru kwa kuchagua jimbo la Ruangwa kuwa miongoni  mwa maeneo ambayo ni wanufaika wa mchango wenu,” amesema.

No comments:

Post a Comment