Tuesday, May 31, 2016

MKUU WA MKOA KUPANDISHWA KORTINI

   Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa, Dadi Faki Dadi ZANZIBAR: Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam (pichani) amesema hivi sasa wanafanya uchunguzi kuhusu madai kwamba aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa, Dadi Faki Dadi aliyedaiwa kufumaniwa na bintiye wa kambo hotelini na pindi upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

   Awali gazeti hili lilipata taarifa kutoka katika vyanzo vyake ndani ya jeshi la polisi kwamba Dadi alikuwa akifuatiliwa na makachero wa polisi baada ya mkewe kumtuhumu ‘kutoka’ na binti yao mwenye umri wa miaka 21.

    Habari zilidai kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita alionekana na makachero akiwa na msichana huyo wakiingia katika Hoteli ya Executive iliyoko Kilimani, Unguja.

   Imeelezwa kuwa mara baada ya kuingia katika hoteli hiyo, Dadi na msichana huyo ambaye jina lake linahifadhiwa, alivamiwa na kufumaniwa na polisi waliokuwa na mama wa mtoto aliyekuwa naye.

     Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kamanda Mkadam alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kisha akasema mtuhumiwa alikamatwa na askari polisi baada ya mkewe aliyemtaja kwa jina moja la Sharifa, ambaye ni mama wa binti anayedaiwa kufumaniwa  naye Dadi kutoa taarifa polisi.

   “Sasa hivi tunafanya upelelezi na utakapokamilika tutampandisha kizimbani,” alisema kamanda huyo na kufafanua kuwa baada ya kukamatwa na polisi Dadi alifikishwa Kituo cha Polisi cha Muembe Madema saa 11 jioni.

    Pia alithibitisha kuwa mtoa habari polisi ni mama wa mtoto ambaye ni mke wa mtuhumiwa huyo, alisema Dadi yupo nje kwa dhamana ya watu wawili.

WANAFUNZI UDSM WAGOMA

   Dar es salaam. Wanafunzi wa chuo kikuu cha cha Dar es salaam mpaka sasa wamegoma wakiishinikiza bodi ya mikopo kutoa fedha kwa ajili ya kujikimu. Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi,
Shamila Mshengema amesema mgomo huo ni matokeo ya taarifa zisizoeleweka zilizo kuwa zikitolewa na bodi juu ya lini fedha hizo zitatolewa.

  Kwa kawaida pesa ya chakula huingiziwa kila baada ya siku 60 na mpaka sasa yapata wiki mbili pasipo kupatikana.

    Mgomo huo unakuja zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Rais Magufuli Kuzulu chuo hicho kwa ajili ya uzinduzi wa jengo la Maktaba.

MESSI ALIVYOMCHOMEA BABA YAKE KWENYE KESI YA KODI

   Lionel Messi amesema hafahamu jambo lolote kwejye mikataba anayosaibi kwa sababu huwa hana utaratibu wa kusoma.

   Kauli hii ya Lionel Messi inakuja wakati kesi yake ya ukwepaji kofi inatarajiwa kuendelea Jumanne ya leo, Katika kesi hiyo Messi na Baba yake Jorge Horacio wanatuhumiwa kukwepa kodi ya kiasi cha 4.1 million euros katika kipindi cha baina ya  2007 na  2009. Kwa mujibu wa gazeti la Catalan la El Periodico, Messi alimwambia jaji mwaka 2013:

 
   “Namuamini baba yangu, ambaye anashughulikia biashara zangu zote. “Chochote anachoniambia nifanye, nafanya.” Alipoulizwa kama huwa anasomaga mikataba yake kabla ya kusaini, nahodha huyo wa Argentina. “Nasaini kila kitu lakini sijawahi kusoma mikataba.

   “Sijui nini nasaini.” Baada ya ratiba ya leo ya kesi Messi anatarajiwa kurudi kujiunga na timu yake ya taifa ya Argentina kwa ajili ya michuano ya Copa America inayotarajiwa kuanza tarehe 4, June.

BAADHI YA WABUNGE WAPONGEZA WENZAO KUSIMAMISHWA

 
   Baadhi ya wabunge wa chama tawala wamepongeza uamuzi wa bunge wa kuwasimamisha wabunge 7 wa upinzani kwa kutofuata sheria za bunge kwa kutaka kushinikiza

  
    kujadiliwa kwa hoja ambayo ilikuwa imeshatolewa maamuzi kuhusu bunge kurushwa live Baadhi ya wabunge hao ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambaye ameupongeza uamuzi wa Bunge na kusema kwamba ni lazima ifike sehemu adhabu itawale bungeni.

  
    Wabunge 7 waliosimamishwa wamepewa kitu wanachostahili kwa kuvunja kanuni. Mbunge wa Geita vijijini Joseph Kasheku Msukuma amesema kwamba adhabu hiyo ni sawa kwa wabunge hao ili iwe fundisho kwa wabunge wapya. Kwa upande wake Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga amesema kwamba kusimamishwa huko kutajenga heshima ya Bunge na kuwa fundisho kwa wengine.

  
    Aidha Wabunge waliosimamishwa ni Tundu Lissu na Ester Bulaya vikao vya mkutano wa tatu na wanne, Godbless Lema, Zitto Kabwe, Paulin Gekul, na Halima Mdee vikao vyote vya mkutano wa tatu na John Heche vikao 10 vya mkutano unaoendelea sasa.

WATUMISHI WA HALMASHAURI WATUPWA JELA

    Geita. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita imewahukumu kutumikia kifungo cha miaka minne jela miaka watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kosa la kughushi na kumdanganya mwajiri.

   Waliohukumiwa adhabu hiyo kila mmoja ni Mhasibu wa Idara ya Afya, Frank Maganga na Mtunza Bohari, Angelina Mhando baada ya kupatikana na hatia ya kutenda makosa hayo kati ya Desemba 13, 2010 na Januari 6, 2011.

   Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Safina Simfukwe alimhukumu Maganga kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka minne au kulipa faini ya Sh6.5 milioni.

 
   Pia, alimhukumu Mhando kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka miwili, au kulipa faini ya Sh2 milioni kwa kosa la kughushi na miaka mingine miwili na faini ya Sh2 milioni kwa kumdanganya mwajiri, adhabu zote zinakwenda sambamba. Hata hivyo, hadi Mwananchi inaondoka mahakamani hapo washtakiwa walikuwa hawajalipa faini hizo.

   Wakati huohuo, Mahakama ya Wilaya ya Chato mkoani Geita, imemhukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh600,000 mgambo wa Mahakama ya Mwanzo Buseresere, Majaliwa Gwakilala baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya Sh300, 000.

    Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Jovith Kato baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwa, mshtakiwa aliomba rushwa kutoka kwa Reuben Ndimila ili asimkamate kwa kesi ya kuruka dhamana iliyokuwa likimkabilia mahakamani.

    Hakimu Kato alisema baada ya kupitia ushahidi wa Takukuru na utetezi wa mshtakiwa, Mahakama imeridhika pasi na shaka kwamba mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo, hivyo hiyo iyakuwa fundisho kwa wengine.

NEEMA KWA WAFANYA KAZI NCHINI YAJA

  Arusha.

Kutokana na kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi kutopata fidia inayotokana na ajali mahala pa kazi,
watumishi kutoka sekta zote wataanza kunufaika na mfuko wa fidia nchini Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Anthony Mavunde alisema jana kuwa fidia kwa wafanyakazi zitaanza kulipwa kuanzia Julai mosi.

    Mavunde alisema hayo wakati wa akifungua semina kuhusu mfuko huo ambao umetokana na Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi ya mwaka 2008. Alisema kwa sasa mfuko umeboreshwa badala ya kutoa fidia elekezi ya Sh10,800, lakini mfanyakazi atalipwa zaidi ya fedha hizo.

    “Mfuko huu hautachangiwa na wafanyakazi, bali waajiri ndiyo watachangia asilimia ambayo itamwezesha mfanyakazi kulipwa fidia atakapokutwa na majanga,” alisema Mavunde. Pia, alisema licha ya mfuko huo kuanzishwa unakabiliwa na upungufu wa madaktari waliobobea juu ya masuala ya ajali na ugonjwa kazini na kuwataka madaktari kuzingatia weledi wa kazi kutoa taarifa sahihi kwenye mfuko huo.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Masha Mshomba alisema tangu mfuko huo uanzishwe mwaka 2015 walipanga kutoa mafunzo kwa zaidi ya madaktari 300 mpaka ifikapo Julai, mwaka huu.

   Alisema lengo ni kuhakikisha mafunzo juu ya mfanyakazi yupi alipwe fidia yanatolewa ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wa sheria hiyo unafanikiwa. “Lengo la semina hii ni kubaini magonjwa yatokanayo na kazi, ajali na vifo vitokanavyo na kazi.

    Hatuwezi kujua bila kuwapo na taarifa ya daktari, tunaamini madaktari ni wadau na watakwenda kutusaidia katika utendaji wa mfuko huu ili uwe na manufaa kwa wahusika,” alisema Mshomba.

    Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa mfuko huo, Emmanuel Humba alisema utajumuisha mifuko yote ambayo ilitangulia kuanzishwa kama mfuko wa pensheni, bima ya afya na mingine na lengo ni kufanya mafao yawe yanatolewa sehemu moja.

   Baadhi ya wafanyakazi wamesema wana imani mfuko huo utasaidia kuondoa ukiritimba uliopo. “Tofauti na zamani, mtu alikuwa analazimika kwenda huku, mara kule mara apigwe kalenda, lakini nadhani hawa watakuwa tofauti.

   Tunawaomba wawe wanafanyia kazi haraka madai,” alisema Lucas Ntumba wa Kampuni ya Tanzania Spread Sheet Ltd.

MBUNGE AMTAJA 'JK' SAKATA LA EPA

   Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete  Dodoma. Mbunge wa Konde Khatibu Said Haji (Cuf), jana aliibua sakata la Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) bungeni akimtaja Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kwamba alikiuka Katiba kwa kutoa msamaha kwa watu waliotuhumiwa.

    Hata hivyo, Serikali kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria Dk Harrion Mwakyembe ilikanusha madai hayo na kusema Rais alikuwa sahihi kwa kuwa viko vifungu ambavyo vinampa nafasi hiyo. Katika swali la nyongeza, mbunge huyo alihoji ni kwa nini Kikwete alitoa msamaha kwa watu hao kabla hawajahukumiwa na Mahakama kama Katiba inavyosema.

   “Kama hivyo ndivyo, basi naomba ukubali kuwa Kikwete (Rais mstaafu) alivunja Katiba ya nchi kwa kuwapa msamaha watuhumiwa wa EPA ambao walikuwa hawajahukumiwa bado, naomba majibu,” alihoji Haji.

   Katika swali la msingi Mbunge huyo alitaka kujua iwapo Rais kwa mujibu wa Ibara ya 45 (1) A hadi D anayo mamlaka ya kutoa msamaha kwa watuhumiwa wa uhalifu wa aina yoyote ambao mashauri yake yapo katika vyombo vya dola kwenye hatua za uchunguzi/upelelezi au mahakamani.

 
   Waziri alisema ibara hiyo ni kweli inampa mamlaka Rais ya kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya Mahakama kupitia kifungu cha kwanza

(1). Dk Mwakyembe alisema kifungu

(ii) kinampa Rais Mamlaka ya kumwachia kabisa au kwa muda maalumu mtu yeyote aliyehukumiwa kuadhibiwa kwa kosa lolote. “Katika kifungu cha

(iii) Rais anaweza kubadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu na kifungu cha

(iv) anaweza kufuta adhabu yoyote au sehemu ya adhabu,” alisema Dk Mwakyembe. Alisema kwa kuzingatia masharti ya Katiba, msamaha wa Rais unatolewa kwa mtu aliyetiwa hatiani na kupewa adhabu na Mahakama lakini watuhimiwa wa uhalifu ambao mashauri yao yako hatua za upelelezi au uendeshaji mahakamani hawaguswi na masharti ya ibara hiyo.

    Alisema Rais hawezi kutoa msamaha kwa watuhumiwa wa uhalifu wa aina yoyote ambao mashauri yao yapo katika vyombo vya dola kwani hatima ya watuhumiwa hao inakuwa bado ipo katika mamlaka za uchunguzi, mashtaka na Mahakama.

14 MBARONI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI

  JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu 14 wakiwamo wanawake wawili na mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwika wilayani Moshi,

  kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha. Miongoni mwa watuhumiwa hao wapo wanaodaiwa kuwa majambazi sugu 10, waganga wa kienyeji wawili ambao walikuwa wakitumika kwa ajili ya kuwapa dawa watuhumiwa hao ili wasikamatwe na polisi na kuzindika silaha zilizokuwa zikitumika katika ujambazi na wanawake wapishi wa watuhumiwa hao wakiwa mafichoni.

    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mtafungwa alisema jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika mikoa ya Tanga na Kilimanjaro kufuatia msako mkali wa askari uliotokana na taarifa za siri.

    Mtafungwa alisema mwanafunzi wa sekondari ya Mwika, Kelvin Shayo (17) miongoni mwa matukio anayotuhumiwa kushiriki ni pamoja na la kumpora bastola yenye namba YP0466 Tz Car aina ya brown, askari mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Elibariki Urio (67). Kamanda alisema silaha hiyo iliporwa Februari 25 mwaka huu baada ya majambazi kumvamia nyumbani kwake na kupora mali pamoja na silaha hiyo kisha kwenda kuificha nyumbani kwa Eleutery Nguma (62) mkazi wa Makami Chini, Tarafa ya Vunjo ikiwa imefukiwa ardhini kwenye mfuko wa plastiki.

   Aidha, Mtafungwa alisema kwa mujibu wa kumbukumbu za polisi mtuhumiwa huyo (Nguma) ilidhaniwa kuwa ameacha vitendo vya ujambazi lakini amebainika kuwa ni mpangaji wa njama za ujambazi, kuficha mali za wizi pamoja na kuficha silaha zinazotumika katika uhalifu.

MWALIMU ATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMKUWADIA MWANAFUNZI WAJE

   Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyaigabo iliyopo Kijiji cha Musati wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara anatuhumiwa kumkuwadia kijana anayemuuzia duka kwa kumpelekea mwanafunzi na kusababisha apate ujauzito.

   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’hazi alisema mwalimu huyo, Agness Matiko amekamatwa na kuhojiwa kwa tuhuma hizo.

   Ng’hanzi alisema binti huyo mwenye umri wa miaka 16 alimaliza darasa la saba mwaka jana kwenye shule anayofundisha mwalimu huyo. Alisema mwalimu huyo alikuwa akimtoa darasani mwanafunzi na kumpeleka nyumbani kwake na kumkutanisha na kijana wake huyo kwa ajili ya kufanya naye ngono.

   Binti huyo alikuwa anasoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Ikorongo kabla ya kufukuzwa baada ya kubainika kuwa na mimba ya miezi sita. “Mwaka jana nikiwa darasa la saba mwalimu alinipeleka nyumbani kwake ili nikamsaidie kukamua ng’ombe maziwa, siku ya pili wakati wa mapumziko alinichukua nikamuoshee vyombo tulimkuta huyo kijana baadaye mwalimu alinisihi nibaki naye ndani,” alidai.

  Alidai licha ya kukataa kufanya naye ngono, lakini mwalimu alimwambia: “Mimi ni mwalimu wako, kama lingekuwa jambo baya nisingekushauri, hivyo wewe kubali, akatufungia kwa nje. Huyo kijana akanipeleka chumbani kwake akanilaza kitandani na kuniingilia.” Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo baadaye mwalimu huyo alikwenda kufungua mlango na kumchukua na kumpeleka darasani na huo ukawa mwendelezo wa kumkutanisha na kijana huyo.

   Alidai kila mara alimpeleka nyumbani kwake na kuwakutanisha huku akimwambia anataka waoane. “Baada ya kubainika nina ujauzito walimtorosha huyo kijana na kudai kuwa walimfukuza kwa madai aliwatia hasara dukani,” alidai.

   Akizungumza baada ya kupata dhamana, licha ya kukiri kukamatwa kwa tuhuma hizo, mwalimu Matiko alisema hajawahi kumfanyia ukuwadi mwanafunzi huyo. Alisema kijana aliyekuwa akiishi kwake walimpata kijijini hapa akiwa anatafuta kazi.

   “Ndipo tulimpatia kazi ya kuuza duka tangu Aprili hadi Oktoba 2015 nilipomfukuza kwa kunisababishia hasara na alisema kwao ni Mabatini mkoani Mwanza,” alisema. Baba wa binti huyo, Marwa Nchama (53) alisema baada ya kubaini ana mimba alifuatilia na kubaini mwanaye alikuwa akifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na kijana huyo.

   Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Turuka Samwel alikana kulifahamu tukio hilo likiwamo suala la walimu kuwafanyisha kazi wanafunzi majumbani mwao.

   Mkuu wa Wilaya hiyo, Maftah Ally, alisema watumishi wanaohusishwa na tuhuma za kuwapa mimba wanafunzi licha ya kufikishwa mahakamani, watawachukulia hatua za kinidhamu.

Monday, May 30, 2016

WANANCHI WAKAMATA PUNDA 200 WANAODAIWA KUIBWA ARUSHA

    Wakazi wa kijiji cha Naberera  kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji wamekamata zaidi ya Punda  Kihongo miambili wanaodaiwa kuibwa kwenye maboma ya  wananchi na  kusafirishwa kwenda  mkoani Dodoma huku sabini kati yao wakiwa kwenye gari aina ya Mitsubishi  Fuso lenye namba za usajili T 983 ABK na hadi sasa watu sita wamekamatwa kwa tuhuma hizo wakiwemo Afisa mtendaji na Bwana mifugo wa kijiji hicho.

   ITV ilifika katika kituo kidogo cha Polisi  cha Naberera na kushuhudia baadhi ya Punda wakiwa kwenye gari aina ya Mitsubushi Fuso wanadaiwa kukamatwa usiku wakipelekwa mkoani Dodoma kunakodaiwa kuwepo soko la wanyama hao huku wananchi wakidai hivi sasa Punda wamekwisha kijiji hapo na hali ya usafirishaji imekuwa mbaya kwani ndiyo tegemeo pekee la kusafirisha mizigo  maji na mazao ya biashara na chakula.

    Uongozi wa Kitongoji cha Kidonge kilichoatharika zaidi na wizi huo  amesema athari za wizi huo kwa wafugaji ni kubwa na jamii ya kifugaji inashangaa mnyama Punda kuwa kutumika kama chakula wakati kwa wafugaji ni usafiri wa kutegemewa.

    Mwenyekiti wa kijiji cha Naberera Jacob Korosi amekiri kuwa baadhi ya viongozi wa kijiji wamekuwa wakihusika na wizi wa punda na hadi sasa zaidi ya punda elfu mbili na mia tano wameshaibwa  na wamefikisha taarifa kwenye ngazi husika bila mafanikio.

CAF YARUDISHA MFUMO WA MTOANO


   Shirikisho la Soka Afrika limetaja mfumo mpya wa mashindano kuanzia mwakani, na sasa limerudisha mfumo wa mechi za mtoano kuanzia hatua ya Robo Fainali.

  Katika kikao cha Jumanne ya Mei 24, mwaka 2016 mjini Cairo, Misri; Kamati ya Mashindano ya Klabu ya CAF ilikubaliana juu ya mfumo mpya wa Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.

   Mabadiliko katika mashindano hayo mawili yalitangazwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou katika Mkutano Mkuu wa 38 wa shirikisho hilo uliofanyika mjini Mexico City, kwamba kuanzia mwakani kutakuwan na timu 16 katika hatua ya makundi.


    Baada ya raundi za awali, timu 32 zitafuzu kuwania hatua ya 16 Bora ya mashindano yote. Watakaofuzu hatua ya 16 Bora kwa Ligi ya Mabingwa wataingizwa moja kwa moja katika makundi manne. baada ya mechi za makundi za nyumbani na ugenini,

   washindi wawili wa juu wa kila kundi wataingia Robo Fainali ambayo itaanza kuchezwa kwa mtoano hadi fainali. Klabu zitakazoongoza makundi zitaanzia ugenini katika Robo Fainali na kumalizia nyumbani.

   Katika Kombe la Shirikisho, timu 16 zitakazofuzu hatua ya makundi zitakuwa ni pamoja na zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa na baada ya hapo, mambo yatakwenda kama yalivyopangwa kwenye Ligi ya Mabingwa.

MADHARA YA KUWEKA SIMU KATIKA MFUKO WA MBELE WA SURUALI NI HAYA:

   Kuna utafiti ulifanyika katika shule ya Technical Medical Haifa, nchini Israel, ambao ulionyesha kwamba uwekaji wa simu katika mfuko wa mbele wa Jeans yako una madhara mabaya katika afya yako.

    Kuweka simu katika mfuko wa mbele wa suruali yako unapunguza nguvu za kiume Katika uchunguzi huu walikuwa wakiwachunguza wanaume 100 ambao walikuwa wana matatizo ya utasa, ambapo waligundua kuweka simu yako katika mfuko wa mbele wa suruali yako itapunguza uwezo wako na nguvu za kiume .

   Wanaume ambao wanapendelea kuweka simu zao katika mfuko wa mbele wa jeans zao, asilimia 47 wameathirika na tabia hii.Wanasayansi wanasisitiza kwamba matatizo yote haya yanatokana na electromagnetic iliyopo katika simu.

    Pia utafiti huu uligundua kwamba watu ambao wanapendelea kuweka simu zao kitandani, karibu au katika usawa wa vichwa vyao wana viwago vidogo sana vya nguvu za kiume tofauti na wale wanaoziweka simu zao mbali wakiwa wamelala.

  Kwa hiyo yakupasa kuwa makini, usipendelee kuweka simu yako karibu na mwili wako ukiwa umelala.

MOURINHO KUMPA SHAVU JIPYA RIO

  Gazeti la Daily Mirror limeripoti kuwa kocha mpya wa Manchester United Jose Mourinho, anataka kumleta mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Rio Ferdinand na kumfanya kuwa kocha wake msaidizi.

 
   Taarifa za awali zinadai kwamba Mreno huyo tayari ameshafanya hatua za awali ili kujihakikishia kama legend huyo wa Man United anaweza kurudi tena Old Trafford kwa kazi hiyo. Kutokana na Ryan Giggs kukataa ofa ya kuwa kocha msaidizi chini Mourinho, Mreno huyo anataka kumleta Rio ili kuhakikisha kuwa anafanya kazi na mtu ambaye anaijua vizuri United ndani na nje.

    Licha ya kumtaka Rio, Mourinho bado atamleta msaidizi wake wa muda mrefu Rui Faria lakini anaamini kufanya kazi na mtu anayejua vizuri United anahisi ni jambo lenye mantiki ili kumsaidia kujenga mahusiano mazuri na mashabiki.

  Rio anaonekana kuwa mtu sahihi Kutokana na historia kubwa aliyonayo katika klabu ya United ikiwemo kutwaa ndoo 12 kwa kipindi chote alichodumu na klabu, Rio anaonekana kuwa mtu sahihi wa kushika nafasi hiyo hasa kutokana na heshima kubwa aliyonayo kwa mashabiki. Kwa sasa Rio ni mchambuzi wa masuala ya soka.

Mc PILIPILI AAMPA SHAVU BARNABA

   MC Pilipili. MKALI wa vichekesho vya majukwaani Bongo anayefahamika zaidi kwa jina la MC Pilipili, hivi karibuni amempa shavu mwanamuziki anayekimbiza kwenye gemu la Bongo Fleva, Barnaba ambaye watakuwa naye kwenye tamasha lake litakalofanyika jijini Mbeya ambalo linajulikana kwa jina la Cheka Vicheko vya Juu Nyanda za Juu.

  Barnaba Akizungumza na mtandao wetu, MC Pilipili alisema, ameamua kumpa shavu hilo Barnaba kwa sababu ni mtu anayefahamu vizuri juu ya uwezo wake na anauhakika atamsaidia sana katika tamasha hilo litakalofanyika Juni 3, mwaka huu katika Ukumbi wa Tugimbe Mafiati ambapo atapiga shoo ambayo haijawahi kutokea.

   “Barnaba ni mwanamuziki mzuri na ninapenda kufanya naye kazi, watu wa Mbeya wategemee kupata vitu adimu kutoka kwa mwanamuziki huyo lakini zaidi mimi maana nimejiandaa kuwavunja mbavu kwelikweli,” alisema MC Pilipili.

KOCHA PLUIJM AANZA KUIFUNGIA KAZI MIKANDA YA TP MAZEMBE

  Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, ameshtukia dili mapema na kuamua kuwaomba viongozi wampatie video za mechi za wapinzani wao kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, hasa TP Mazembe.

   Yanga imepangwa Kundi A ikiwa na timu za MO Bejaia (Algeria), Medeama (Ghana) na TP Mazembe huku Kundi B, likiwa na Kawkab (Morocco), Etoile du Sahel (Tunisia), FUS Rabat na Ahly Tripoli (Libya).

   “Ninahitaji muda zaidi wa kuwaangalia TP Mazembe kwenye baadhi ya mechi za mwisho walizocheza kwa ajili ya kuwaona wachezaji wenye madhara nitakaotakiwa kuwadhibiti mara tutakapokutana nao.

   “Ninaamini hao Mazembe sidhani kama ni wale niliowaona nikiwa naifundisha Berrekum Chelsea ya Ghana, hivyo ninahitaji muda zaidi kwa ajili ya kuwaangalia,” alisema Pluijm.

RAIS WA UTURUKI AWATAKA WAISLAMU KUTOPANGA UZAZI

   Rais Reccep Tayip Erdogan Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan amewataka Waislamu kukataa kutumia vifaa vya upangaji uzazi kwa lengo la kupata watoto wengi.

  Katika taarifa iliorushwa hewani kupitia runinga za taifa hilo,bw Erdogan amesema kuwa hakuna familia ya Kiislamu inayopaswa kupanga uzazi na kwamba ni muhimu kupata watotozaidi.

   Makundi ya wanawake yamekuwa yakimkosoa kiongozi huyo wa Uturuki kwa kufananisha upangaji uzazi na uhaini,huku huku akipinga wto wa usawa wa kijinsia.

WALIOJARIBU KUSHAMBULIA NDEGE WAHUKUMIWA MAISHA JELA

   Mahakama ya kijeshi kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu, imewahukumu kifungo cha maisha wanaume wawili ambao walipatikana na hatia ya kupanga shambulizi dhidi ya ndege ya shirika la Daallo mwezi Februari.

    Bomu lililipuka ndani ya ndege hiyo muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mogadishu ikiwa safarini kwenda nchini Djibouti. Shimo lilitobolewa kando mwa ndege hiyo lakini hata hivyo ndege haikusambaratika.

   Abiria mmoja ambaye alitupwa nje ya ndege hiyo aliaga dunia na wengine wawili wakajeruhiwa. Washtakiwa wengine wanane walihukumiwa vifungo vya kati ya miezi sita na miaka minne. Hao ni pamoja na waliokuwa wafanyikazi wa uwanja wa ndege na maafisa wa ulinzi.

ACHOMWA KISU TUMBONI WAKIGOMBEA MWANAMKE

   Kiteto. Mkazi wa Kijiji cha Ngapepa Kata ya Kijungu wilayani Kiteto Mkoa wa Manyara amenusurika kifo baada ya kuchomwa kisu tumboni na mtu asiyefahamika wakati wakimgombea mwanamke. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Massawe alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku.

    Alisema polisi wanamshikilia mwanamke anayedaiwa kuwa chanzo cha ugomvi huo, mkazi wa Kijiji cha Ngapepa ili aisaidie kumtambua mtuhumiwa aliyetoroka.

   Alisema chanzo cha tukio hilo inadaiwa ni wivu wa mapenzi uliosababishwa na mwanamke huyo kutembea na wanaume wawili kwa wakati mmoja. “Uchunguzi wa awali unaonyesha watu hawa hawafahamiani na wala hakuna ambaye ni mume wa mwanamke huyo na anayewafahamu ni mwanamke aliyesababisha ugomvi,” alidai Massawe. Alisema majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto akipatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

    Hata hivyo, Kamanda Massawe alishauri jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi hasa katika masuala ya mapenzi na kuhamaki bila kujua historia ya mahusiano yoyote kwani wanasababisha matukio ambayo baadaye huja kuyajutia.

  Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, Mariam Abdalah na Julius Lucas walidai kitenda hicho kilichangiwa pia na ulevi.

FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA NYANYA..

  FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA        NYANYA....

Hili ni tunda mashuhuri na lenye virutubisho ambalo kwa kawaida hutumika kama mbogamboga.

Kwa wastani, watu hula takribani kilo 8 za nyanya kwa mwaka. Nyanya zina aina mbalimbali za viasili vya kurutubisha na visivyorutubisha vinavyohusiana na faida kadha wa  kadha za kiafya.

  Hii inajumuisha lycopene, vitamini C,  A na K, potasiamu, na nyuzinyuzi. Nyanya moja yenye ukubwa wa wastani inaweza  kutoa takribani nusu ya kiasi cha kila siku cha vitamini  C anachohitajika kupata mtu.

   Viasili mbalimbali vya  nyanya vinasadikika kufanya kazi pamoja kuleta  manufaa ya kiafya. Hii ni pamoja na kusaidia kujenga afya ya meno, afya  ya mifupa, afya ya ngozi, afya ya nywele, kupunguza  shinikizo la damu (PB) na kupunguza viwango vya  lehemu pamoja na kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na saratani.

    Baadhi ya vionjo vya nyanya kama vile lycopene  hufyonzwa kwa wepesi mwilini pale nyanya  zinapochemshwa, iwe kwa kuzipika au kuzichemsha. Sasa huenda tunazijua faida za kula lishe kamili ya  kuleta afya ikiwa ni pamoja na kula matunda na  mbogamboga.

    Lakini wasichokijua watu wengi ni  kwamba juisi ya mbogamboga ndiyo inayosaidia  kudumisha urari (pH) muhimu wa haidrojeni ya mwili. pH ina maana ya nguvu ya haidrojeni katika mizani ya  kupimia hali-asidi ya vitu mwilini. Ili mwili ufanye kazi  vizuri na kuweza kuendelea kuishi, lazima uwe na  vikemikali vinavyolipuka na vitu vya asidi ili  kutengeneza chumvi na kutoa umajimaji wenye nguvu  ya haidrojeni (ya baina ya 7 na 7.5) na uwe na kipimo  cha haidrojeni chenye urari kamili kwa sababu saba:

1. Kuulinda mwili dhidi ya uharibifu utokanao na  chembechembe za maradhi na kuukinga na uzee wa  kabla ya wakati.

   2. Kuusaidia mwili kudumisha viwango vya lehemu  vyenye kuleta afya bora.

   3. Kuweka msukumo wa damu katika kiwango bora cha afya.

   4. Kuweka katika hali ya kawaida kikemikali cha  kusawazisha sukari ya damu (insulin) na kuzuia  ongezeko la uzito wa mwili linaloweza kuhatarisha afya.

   5. Kuuwezesha moyo kufanya kazi vizuri.

   6. Kuongeza uzalishaji wa nishati

    7. Kudumisha mfumo wa kinga ya mwili, mfumo wa  umeng’enyaji, kudumisha afya ya viungo vya mwili na mifupa

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA MAYAI NA MAMBO MENGINE..

MAYAI SIO CHAKULA TU. YANA FAIDA INGINE HII HPA CHINI.... YAI

limekuwa na matumizi kama chakula kwa muda mrefu, wapo ambao hutumia chakula hicho kwa kukaanga,

kuchemsha, kunywa likiwa bichi na au kuchanganya katika vyakula vingine mbalimbali.Lakini pia kuna matumizi ya Yai zaidi ya chakula,

kwani linauwezo mkubwa wa kurutubisha ngozi, nywele na pia kuondoa uchovu. Jinsi ya kufanya ukitaka kutumia Yai kuboresha muonekano wa ngozi na nywele zako. Chukua Yai,

changanya na asali kijiko kimoja cha chai mafuta ya Olive .Chukua mchanganyiko huo kisha pakaa usoni na shingoni,

kaa nao kwa dakika kumi hadi 15. Hii itasaidia kama una mashimo usoni yatokanayo na chunusi kubana.

Pia itasaidia kulainisha ngozi yako na kuwa nyororo, mchanganyiko huu pia utasaidia kukuondolea michubuko au alama za kuungua na jua,

mafuta au krimu usoni.Unaweza kutenganisha kiini cha Yai na ule ute mweupe, kisha chukua ute weka kwenye kikombe au bakuli, baada ya hapo pigapiga ule ute hadi uwe na mapovu kisha chukua povu,

linawe usoni au paka mwili mzima kisha liache likauke. Baada ya hapo osha na maji ya uvuguvugu, ukifanya hivyo mara kwa mara itakusaidia kufanya ngozi yako iwe anga’avu

.Kama umetoka kazini na unaonekana umechoka na unataka kutoka usiku, chukua ute wa yai na pakaa chini ya jicho na uache kwa dakika 10 hadi 15 kisha safisha, itasaidia kuondoa muonekano wa uchovu katika macho yako. Iwapo unasumbuliwa na kuwashwa ngozi, matumizi ya Yai pia ni njia sahihi kuepuka tatizo.

Maski ya Yai ina utajiri wa ‘Acid’ za Amino ambazo husaidia kupunguza na kuondoa miunguzo au muwasho mwilini kutokana na protini inayopatikana kwenye Yai.

Kama unawashwa mwili mzima, chukua ute wa yai kidogo halafu nyunyiza katika maji utakayoyaoga sambamba na sabuni ya kuogea ndani ya siku chache utaona matokeo. Kwa upande wa nywele wale ambao,

nywele zao hazina afya au ukuaji wao ni hafifu wanaweza kupaka yai kichwani, hakikisha inagusa mizizi inayosaidia kuotesha nywele, kama nilivyoeleza awali protini iliyopo kwenye yai ndio chanzo cha kila kitu.Unaweza kutumia Yai kama ‘Hair Conditioner’,

chukua kiini chake changanya na asali, mafuta ya watoto na maji kidogo. Changanya vizuri kisha paka kichwa kizima acha kwa dakika 20 kisha osha na maji ya baridi chukua ute mweupe changanya na shampoo yako kidogo.

SAUDI ARABIA YACHUKIZWA NA TANGAZO LA IRAN

   Saudi Arabia imejibu tangazo la Iran kwamba raia wake hawataruhusiwa kwenda kuhiji Makka mwaka huu,kwa madai ya kwamba mamlaka ya Saudia imetengeneza vikwazo kwa mahujaji wa Iran kushiriki Hijja hiyo.

   Hata hivyo Waziri wa Mambo ya nje wa Saudia Adel al-Jubeir amesema kuwa waumini hao wa Kiislam kutoka nchini Iran,wanahitaji kupewa idhini pia ya kufanya maandamano wakiwa nchiniSaudia jambo ambalo halikubaliki. Iran inalaumu maafisa wa Saudia kwa vifo vya mamia ya mahujaji wake vilivyotokea mwakajana walipokwenda kuhiji.

   Professor Mohammad Marandi kutoka chuo kikuu cha Tehran,anasema wa hoja ya Iran, ni kutaka kujiridhisha kama Mahujaji wake watakuwa salama katika Hijja ya mwaka huu "Raia wa Iran hawana namna. Maoni ya Wairan ni ya hasira na jazba dhidi ya familia ya Kisaudia. Saudia imewakatalia Wairan matumizi ya Kamera,ambazo ndizo zilizotumika kuonyesha picha za maelfu ya watu waliokufa katika Hijja ya mwaka jana wakiwemo raia wa Iran.

   Na kwa kuwa Saudia haikulezea mazingira halisi ya vifo hivyo na baadaye ikaomba msamaha,Wairan wanaona bado mazingira hayajawa salama kwao kwa ajili ya Hijja ya mwaka''. Professor Marandi amesema vurugu zilizosababisha vifo katika Hijja mwaka jana hazikudhibitiwa vyema na serikali ya Saudia "Saudia ilionyesha bayana kutoheshimu mahujaji,familia zao na kwa miili ya waliokufa, jambo ambalo kwa Wairan halikubaliki.

   Hivyo Wairan wanataka kujua ni maboresho gani yatafanyika mwaka huu ili waweze kuwa salama zaidi,lakini Saudia hawataki kuweka wazi kwamba ni mabadiliko gani yaliyofanyika,na wakati huo huo viongozi wa dini nchini Saudia wanaamini kuwa Wairan si waumini kamili wa dini ya kiislamu''.

WALINDA AMANI WATANO WAUAWA MALI

  Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali umesema kuwa walinda amani wake watano wameuawa na wengine wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi lililotokea katikati ya mji wa Mopti.

   Waathirika wanatokea nchini Togo.Gari lao lilipatwa na moto kabla ya kukanyaga bomu la ardhini,na kisha kulipuka.Waziri wa masuala ya kigeni nchini Mali, Abdoulaye Diop, ametuma salam za rambirambi katika mitandao ya kijamii kwa UN na nchi ya Togo.

   Vifo vyao vimekuja wakati dunia ikiadhimisha siku yawalinda amani.Mwaka uliopita walinda amani 129 kutoka umoja wa mataifa walipoteza maisha katika nchi 16 wanazofanyia shughuli zao.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU POMBE YA VIROBA YA KWENYE MIFUKO YA PLASTIKI

   Mifuko ya plastiki inayofungasha pombe maarufu kama ‘viroba’ imepigwa marufuku na Serikali kuanzia mwakani. Sambamba na hilo Serikali pia, imepiga marufuku moja kwa moja utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini wa mifuko ya plastiki kuanzia mwaka huo.

   Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba aliwaambia wanahabari jana sehemu kubwa ya mifuko hiyo inayotolewa bure imekuwa ikichangia uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubwa. Wakati Makamba akiyasema hayo, Februari mwaka huu Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina aliondoa zuio la matumizi ya mifuko ya plastiki akisema kuwa itaziweka rehani ajira za Watanzania wanaofanya kazi kwenye viwanda vinavyotengeneza mifuko hiyo.

   Pia, Mpina alisema itapunguza kasi ya uwekezaji wa viwanda vilivyowekeza katika bidhaa hiyo. Akizungumza katika siku ya Mazingira Afrika, Mkurugenzi wa Mazingira, Dk Julius Ningu alisema maamuzi hayo yamelenga kulinda viwanda vilivyoajiri mamia ya Watanzania, tofauti na nchi nyingine zinazotegemea wazalishaji wa nje ya nchi.

   Makamba akizungumzia uamuzi mpya wa kuzuia mifuko ya plastiki, alisema matumizi ya mifuko inayofungashia vileo na inayotumika katika matumizi mengine husambaa na kuchafua mazingira. Alisema mifuko ya plastiki inatajwa kuziba mifereji na kusababisha mafuriko na athari nyingine za mazingira.

    “Leo (Jana), tumeamua kutangaza ili kuwaanda wahusika wasiendelee kuwekeza katika mifuko hii badala yake wasubiri utaratibu mwingine utakaowekwa na Serikali,” alisema Makamba na kuongeza kuwa:  “Asilimia kubwa ya uchafu kwenye nyanzo vya maji, mito, maziwa na fukwe za bahari ni mifuko ya plastiki.” Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, alisema Serikali inakamilisha majadiliano ya ndani na baadaye itawahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku ya moja kwa moja mifuko hiyo.

   Alifafanua kwamba Serikali itatoa muda kwa walioajiriwa, kujiajiri na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko hiyo ili kujiandaa kuacha shughuli hizo na badala yake itawezesha mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungashio mbadala. “Kwa wanaotengeza mifuko hii na kuiuza katika soko la nje hatuna tatizo nao waendelee. Ila kwa soko la ndani hawataruhusiwa kufanya hivyo.Zuio hili litakuwa la kisheria siyo kwa maneno,” alisisitiza Makamba.

   Aliongeza kuwa katika kuonyesha Serikali imedhamiria kupambana na hali hiyo wizara yake imeamua kutuma timu ya watu watano kwenda Rwanda kujifunza namna bora ya kudhibiti matumizi na kuzuia mifuko hiyo tangu mwaka 2008. Waziri huyo alitoa wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa mifuko hiyo kujiandaa na zuio hilo na katika siku zijazo Serikali itatoa utaratibu na maelekezo ya tarehe ya kuanza zuio huku taratibu nyingine za kina zikifuata ili kuondoa mkanganyiko.

    Katika hatua nyingine, Makamba alisema maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika Juni 5 kila mwaka hayatafanyika kitaifa badala yake wizara imewaelekeza wakuu wa mikoa kufanya maadhimisho katika maeneo yao.  “Tumewapa miongozo kuhusu utekezezaji wa shughuli hizo za maadhimisho zinazolenga kutoa hamasa ya hifadhi ya mazingira hususan nyanzo ya maji amabayo ni muhimu kwa viumbe hai,” alisema Makamba. Kwa mujibu wa Makamba, kauli mbiu ya mwaka huu kitaifa juu ya maadhimisho hayo ni ‘ tuhifadhi vyanzo vya maji kwa uhai wa taifa letu’aliwashauri na kuwataka Watanzania kutumia siku hiyo kupanda miti, kudhibiti uchomaji wa misitu Ofisa Mwandamizi Mazingira wa Nemc, Arnold Kisagala alisema nusu ya mifuko ya plastiki nchini inazalishwa na kuingizwa kutoka nchi jirani ya Kenya. Alisema agizo la Waziri Makamba litawezekana, lakini linahitaji ushirikiano kutoka kwenye sekta zingine kwa kuwa viwanda vingi vya mifuko ya plastiki vipo Kenya.

   "NEMC tayari tulishaanza mazungumzo na wazalishaji kuhusu mifuko ya plastiki,” alisema.

KAULI YA JPM KUJITOA SADAKA YAZUA MJADALA

  Dar es Salaam. Kauli ya Rais John Magufuli kwamba yuko tayari kuutoa mwili wake sadaka katika kupambana na rushwa na ufisadi uku kuwasaidia wanyonge, imeibua mjadala huku wanasiasa wakitofautiana.

 
   Akizungumza katika Mkutano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema: “Unapoona watu wanashangaashangaa sana (ni) kwa sababu hawakuzoea haya. Na walifikiri nitakuwa part of them (sehemu yao), never (haitatokea), not me (si mimi). “Ni mara 10 nisiwe rais, nikachunge hata ndege, nikakae kijijini kuliko niwe Rais halafu nivumilie uozo huu unaofanyika.

  I’m saying never (nasema haitatokea).” Rais Magufuli amekuwa akizitoa kauli kama hizo mara kwa mara, hasa anapowawajibisha baadhi ya watendaji wa Serikali, huku ikidaiwa kuna upinzani mkali ndani ya chama chake cha CCM, hali inayohisiwa kusababisha kauli hiyo. Mkurugenzi wa Fordia, Bubelwa Kaiza alisema kauli hizo za Rais Magufuli zinaonyesha uzalendo wa kweli na amefanikiwa kufanya mambo yaliyowashinda marais waliomtangulia.

  “Ndani ya CCM kuna upinzani mkali kutoka kwa makada. Kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita watendaji wa Serikali wamekuwa na mikakati ya kusaidia wezi na utapeli, hivyo anachofanya ni ‘revival strategy (mkakati wa kufufua),” alisema Kaiza. “Watendaji wa Serikali waliosimamishwa kwa kipindi kifupi cha Rais Magufuli ni wengi kuliko waliosimamishwa na Rais Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kwa pamoja.

   Haogopi na wala hana upendeleo,” alisema Kaiza. Kaiza alisema tabia ya muda mrefu ya kubebana ndani ya CCM imesababisha kuwapo kwa ufisadi uliokithiri, ukiwamo uingizwaji wa dawa za kulevya na ujangili wa meno ya tembo. Hata hivyo, msemaji mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka alisema hakuna upinzani wala mpasuko ndani ya chama hicho kuhusu utendaji wa Rais. “Sidhani kama kuna kuvutana na watu ndani ya CCM.

   Rais Magufuli ni mwana-CCM, kwa tafsiri yangu, amekataa kuungana na wakwepa kodi, wabadhirifu wa mali ya umma ambao baadhi yao wamo ndani ya chama na wengine wako nje,” alisema. “Rais Magufuli anatekeleza mipango ya chama kwa asilimia 100 na hakuna mpasuko. Anachokifanya ndicho kinachotakiwa na chama. “Unapojiunga na CCM unaapa kwamba binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

  Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote, nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma. Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa. Sasa asiyeyafuata haya ameingia kwenye chama kwa bahati mbaya.

  
   Alisema Magufuli hawezi kuwa kama rais wa zamani wa Malawi, Bingu wa Mutharika (marehemu) aliyejitoa chama tawala cha Democratic Progressive Party na kuanzisha Peoples Party baada ya kutoelewana na wenzake. “Haiwezekani akajitoa CCM kwa sababu anachokifanya ndicho msingi wa CCM.

   Kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ ilikuwapo hata zamani, Uhuru ni Kazi, Kazi ni kipimo cha utu,” alisema mbunge huyo wa zamani wa Simanjiro. “Kwa kweli amejitoa sadaka katika taifa hili ambalo rushwa imetamalaki na kuna mafisadi wamekuwapo. Si kazi ndogo.” Alipoulizwa kuhusu kauli hiyo, Dk Benson Bana, mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema Rais Magufuli amejitoa mhanga kupambana na ufisadi, japo hataki kukitumia chama chake kwa sababu kitamharibia.

“Rais amejitoa mhanga kupambana na ufisadi, kusafisha Serikali ni ajenda yake. Tunaona yanayotokea. Yeye kama Rais alikuwa anauambia umma kwa sababu watu wanaweza kusema ni nguvu ya soda, si unajua tena watu wenye nguvu ya pesa, watafanya kila wawezalo,” alisema. “Suala la chama kuchafuka si la leo, CCM ilishachafuka, ndiyo maana wakati wa kuomba kura, Rais Magufuli hakuwa akiitanguliza chama, na yeyote mwenye busara, huwezi kujitambulisha na CCM.

    “Wilson Mkama alijitahidi akavua magamba yakakumbatiwa kwingine, akaja (katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman) Kinana na (katibu mwenezi) Nape Nnauye wakazunguka nchi nzima kujaribu kukirudisha chama kwenye mstari, lakini hiyo si kazi ya siku moja.

  “Tena mimi ningekuwa mshauri, ningewashauri wamwache Rais Magufuli aongoze Serikali. Watafute mtu mwingine aongoze chama kwa sababu ukijitambulisha na CCM huwezi kuwa popular (kupendwa na wengi). Sisi tunaopita mitaani tunajua.” Kwa upande wake, George Shumbusho kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, alisema ujumbe huo wa Rais Magufuli unatoa tahadhari kwa wafanyabiashara kuwa baadhi yao wabadilike na kuanza kutumia njia zisizokuwa na ujanja wa kukwepa kodi, vinginevyo atakuwa na uwezo wa kuwashughulikia bila kuhofia jambo lolote.

   Profesa Shumbusho alisema imekuwa kawaida baadhi ya wafanyabiashara kutumia nafasi zao kushawishi viongozi wanaoingia Ikulu. “Hata Hayati Mwalimu Julius Nyerere alisema Ikulu ikiingiliwa na wafanyabiashara, Rais hawezi kukusanya kodi.

   Sasa labda (Rais Magufuli) ameona wanajaribu kumshawishi,” alisema profesa huyo huku akicheza. Emmanuel Mallya, mhadhiri kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), alisema si jambo geni na baya kwa kundi la wafanyabiashara kutoa mchango wao kwa mgombea wa urais wanayempenda aingie madarakani.

   Alisema duniani kote kumekuwa na makundi mbalimbali yaliyo na lengo la kushawishi mgombea fulani kuingia Ikulu, yakiamini ana uwezo wa kushughulikia masilahi yao. “Makundi haya huitwa ‘lobby groups’. Hii si kwa nia mbaya hata waandishi huonyesha mrengo wao kushawishi ili mgombea akiingia Ikulu, awasaidie kufanikisha masilahi yao. Lakini yapo makundi ambayo hutumia nafasi hiyo kwa lengo la kupata unafuu wa kujinufaisha maslahi yao.

   Hata hivyo, makamu mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari alisema endapo Rais Magufuli ataiacha kauli hiyo bila ufafanuzi, atakuwa amewakebehi marais wastaafu waliomtangulia. Profesa Safari alisema hakuna chama chochote cha upinzani kilichowahi kuongoza taifa hili hivyo, kauli hiyo ina maanisha wafanyabiashara ndiyo waliowaweka madarakani viongozi hao waliomtangulia. “Kauli hiyo ni kuwabeza wenzake hao waliomtangulia kwa sababu upinzani hauhusiki na haujawahi kuongoza nchi hii.

   Sasa akiacha kauli hii kama ilivyo, hiyo ndiyo maana yake,” alisema. Kwa upande wake mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alisema kauli hizo za Rais Magufuli hazina dhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi nchini.

   “Kwa ajenda ya ufisadi, Rais Magufuli kashindwa kuwawajibisha wale watu ambao hata jamii inawajua, lakini anasema anatumbua jipu hata likiwa kwenye kwapa, mbona kashindwa kuwatumbua,” alisema Mchungaji Msigwa bila ya kutaja watu ambao Rais hajawachukulia hatua.

MWANAMKE ALIWA NA MAMBA AUSTRALIA

  Mamba Polisi kaskazini mwa Australia wanasema kuwa mwanamke mmoja hajulikani aliko, baada ya kushambuliwa na mamba alipokwenda kuongelea usiku.

  Mwanamke huyo na rafiki yake walikuwa katika kidibwi chenye kina kifupi katika hifadhi ya kitaifa ya wanyama pori ya Daintree. Hifadhi hiyo ya taifa ipo katika maeneo ya Queensland, nchini humo.

   tukio hilo ni limetokea Jumapili jana, ambapo hadi sasa inahofiwa kuwa huenda ameliwa na Mamba.

ALEXANDER GAULAND ADAIWA KUTOA MATAMSHI YA KIBAGUZI

   Jerome Boateng adaiwa kutolewa matamshi ya kibaguzi Naibu kiongozi wa Chama cha kupambana na uhamiaji nchini Ujerumani amezungumza maneno ya kibaguzi dhidi ya mchezaji nyota wa Ujerumani Jerome Boateng ambaye baba yake ni raia kutoka Ghana.

  Alexander Gauland,aliliambia Gazeti la Ujerumani la (the Frankfurter Allgemeine) kuwa watu wanafikiri Boateng ni mchezaji mzuri lakini kamwe hatomuhitaji kama rafiki yake.

    Gauland alilaaniwa vikali na wachezaji mbalimbali,Waziri wa mambo ya ndani pamoja na Rais wa shirikisho la soka nchini Ujerumani ,Reinhard Grindel amesema maneno yake kuwa hayana maana. Gauland baadaye alijibu kuwa hakumaanisha

    kumdhalilisha Jerome Boateng ambaye amekuwa nguzo muhimu kwa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani.

MUFTI MKUU ZANZIBAR ALITAKA BARAZA LA MAULAMAA KUTAFUTA NJIA YA KUTATUA MIGONGANO ILIYOPO

  Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Swalehe Omar Qaabi amelitaka baraza la Maalamaa  kutafuta  mbinu ya kuongea na wananchi katika baadhi ya maeneo kisiwani pemba kugomeana katika huduma za kijamii na kutafuta njia ya kutatua hali hiyo isiendelee miongoni mwao.

    Hayo ameyasema hapa ukumbi wa kiwanja cha michezo Gomban  alipo kuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa siku moja kwa wajumbe wa baraza la malamaa na viongozi wa dini kisiwani Pemba. Kwa upande wao  baadhi ya maulamaa walisema hali hiyo ni kero na kuitaka serikali kuu kuliona no kushiriki kufanya kwa upande wao kuiweka jamii iweze kuishi bila ya migogoro miongoni mwao.

  
   Akisoma maazimio ya mkutano huo wa baraza la maulamaa mbele ya Mufti Mkuu wa Zanzibar afisa mdhamini afisi ya Rais katiba na utawala bora Omari Khamis amesema maalumaa wamekubaliana kuchukua hatua za kumaliza migogoro hiyo miongoni mwa jamii  iliyosababishwa na siasa.

WAMACHINGA MKOANI MWANZA WACHANGIA MADAWATI 30 KATIKA JITIHADA ZA KUPUNGUZA UHABA WA MADAWATI

   Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ametoa siku tano kwa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza kuondoa dampo la uchafu lililopo mtaa wa Makoroboi, maarufu kama ‘City park’ kutokana mlundikano wa taka hizo kutoa harufu kali na kusababisha kero kwa baadhi ya wafanyabiashara waliopo katika eneo hilo.

  Mongella ametoa agizo hilo wakati akipokea Madawati thelathini yaliyotolewa na shirika la umoja wa Machinga mkoa wa Mwanza, (SHIUMA) kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika kumaliza uhaba wa madawati nchini, baada ya machinga hao kuguswa na kilio cha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari cha kusoma wakiwa wamekaa  chini.

    Pamoja na changamoto zinazowakabili wamachinga, ikiwemo uhaba wa maeneo ya kufanyia biashara, ukosefu wa mitaji na elimu ya ujasiriamali, bado wameamua kuchangia sekta ya elimu kwa kila kizimba kuchangia shilingi elfu kumi na nne kwa ajili ya kuchonga madawati hayo yatakayopelekwa katika shule ya msingi Nyashana.

   Mwenyekiti wa shirika la umoja wa machinga mkoa wa Mwanza Ernest Matondo anaeleza sababu zilizopelekea shule ya msingi nyashana inayokabiliwa na upungufu wa madawati 236 kupewa kipaumbele cha kukabidhiwa madawati hayo licha ya kuwepo kwa shule nyingine za wilaya ya Nyamagana zenye upungufu wa madawati.

Sunday, May 29, 2016

KIONGOZI WA KIDINI NCHINI SAUDI APIGA MARUFUKU KUPIGA SELFIE NA PAKA

  Paka ni moja ya viumbe maarufu sana katika mitandao ya kijamii baada ya binadamu. Na uhakika ushakutana na picha na video kadhaa za paka katika pitapita zako.

   Kiongozi mmoja wa kidini nchini Saudi apiga marufuku watu kupiga picha za selfi na viumbe hao. Kiongozi huyo (Cleric) bwana Saleh bin Fawzan al-Fawzan ni mmoja wa wajumbe wa baraza la kidini lenye nguvu sana nchini humo – Saudi Council of Senior Scholars. Bwana Fawzan amesema ‘kupiga picha na paka ni tabia inayosambaa sana kwenye watu wanaopenda kuwa kama wazungu’ (alitumia neno ‘westerners’, yaani watu wa mataifa ya magharibi – Ulaya na Marekani.

   Kiongozi huyo aliliongelea jambo hilo baada ya kuulizwa swali kuhusu mtazamo wako juu ya jambo la upigaji picha za selfi alipokuwa anahojiwa katika kipindi cha televisheni. Baadaye alipanua zaidi tafsiri yake akisema upigaji picha wa aina yeyote kama hauna maana si wa lazima.

    Alisema isiishiye kwenye paka tuu bali ata na mbwa au kingine chochote kisicho cha ulazima/maana. Watu wengi wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii wakipinga katazo hilo, wengi wanaonesha kupinga kwao kwa kupiga picha za selfi na paka wao.

WANAJESHI 5 WA UKRAIN WAUAWA MASHARIKI MWA NCHI

  Wanajeshi wa Ukrain Jeshi la Ukrain linasema kuwa wanajeshi watano wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa kwa muda wa saa 24 zilizopita wakati wa mapigano na waasi wanaoiunga mkono Urusi mashariki mwa nchi hiyo.

   Hiyo ndiyo idadi ya pili ya vifo vingi vya kila siku vinavyo wakumba wanajeshi wa Ukrain Kila upande unamlaumu mwingine kwa kukiuka usitishwaji mapigano uliotiwa sahihi mwezi Februari mwaka uliopita.

    Karibu watu 9000 wanaripotiwa kuuawa kwenye mzozo huo ambao ulifuatia hatua ya Urusi ya kuimega rasi ya Crimea mwaka 2014

HII NI MAALUMU KWA MADEREVA WA MAGARI MAKUBWA YA MIZIGO.

  Malori yajiendeshayo yenyewe yakamilisha safari Ulaya Msafara wa malori yajiendeshayo yenyewe (kwa kiasi kikubwa) yamekamilisha safari katika mji wa bandari wa Rotterdam nchini Uholanzi, hii ni safari ya kwanza ya magari kama hayaa kuweza kuvuka mpaka wa nchi  yakitokea nchi za Sweden na pia kusini mwa Ujerumani.

   malori yajiendeshayo yenyewe Malori haya yanatoka katika kampuni za untengenezaji wa malori ambayo kwa pamoja zinatengeneza kundi la malori ambayo yanasafiri pamoja,

   tukio hili linaitwa platooning challenge na linahusisha malori yajiendeshayo yenyewe kwa kupokea taarifa juu ya kuongeza mwendo ama kupunguza mwendo kutoka katika gari lililombele kabisa.

   Tofauti ya magari haya na magari yajiendeshayo kama yale ya Google ni kwamba malori haya yanakuwa na gari moja ambalo limetangulia na linaendeshwa na binadamu na lori hili lililo mbele linatuma taarifa kuhusu breki na kuongeza mwendo  kwa kutumia njia ya Wi-Fi kwenda gari la nyuma. Waandaji wa shughuri hii nzima wanasema kwamba kufanikiwa kwa safari hii kunamaana kubwa hasa kwa sekta ya usafirishaji wa mizigo katika bara hilo la ulaya.

    Inasemekana kwamba kwa kuwa ajari nyingi zinatokana na makosa ya binadamu basi malori yajiendeshayo yenyewe yatasaidia kupunguza ajari kaitka barabara za bara hilo. Tafiti zinaonesha kwamba matumizi ya mafuta yanapungua iwapo Malori yatatumia mfumo uliotumiwa na malori hayo, pamoja na hilo pia imegundulika kwamba njia hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa foleni za magari.

   Njia hii inahusisha magari mawili ama matatu ambayo yanakuwa yanalifuata gari moja ambalo ndilo linalotoa taarifa zinazotumika kuendesha mengine ambayo yanafuata.

WALIOHAMISHWA KUPISHA UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE 2012 WAMEENDELEA KULALAMIKA

Wakazi 174 kati ya 864 waliohamishwa na halmashauri ya manispaa Ilala kupisha Upanuzi wa Uwanja wa ndege mwaka 2012 wameendelea kulalamikia manispaa ya Ilala kwa madai ya kuwapatia viwanja hewa 174 ambayo wamiliki wa meneo hayo wamegoma kuwaruhusu kuingia kwa madai kuwa hawajalipwa fidia mashamba hayo.

   Wakazi hao waliopelekwa katika viwanja hivyo vilivyopimwa katika maeneo ya Pugu kinyamwezi,Kigogo fresh,zavala na Nyeburu wamesema pamoja na kukabidhiwa hati za umiliki wa maeneo waliyopelekwa baada ya nyumba zao kuvunjwa kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege lakini wamiliki wamegoma kuachia maeneo hayo kwa madai ya kutolipwa fidia .

   Wakizungumza na chanel ten ambayo ilitembelea maeneo hayo yenye Mgogoro wananchi hao wakiongozwa na kamati ya wananchi walioondolewa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege,wamesema mpaka sasa wamekuwa katika maisha ya shida huku mamlaka zinazohusika zikishindwa kuingilia kati mgogoro huo. Aidha wakazi hao wamedai kuwa baadhi yao walipewa viwanja

   vilivyoitwa alama T ,lakini walipotaka Kuviendelea walielezwa kuwa maeneo hayo ni ya wazi ambayo ni ya huduma za kijamii ikiwemo ya Makaburi,shule zahanati na viwanja vya wazi na kubaki njia panda na kumuomba Mkuu wa mkoa wa dsm paul makonda kuingilia kati baada ya kudai manispaa ya ilala imeshindwa kutatua mgogoro huo.

AZMA YA KUIFANYA TANZANIA KUWA YA VIWANDA

    oil-and-gas-investments

    Halmashauri nchini zimetakiwa  kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji ili kuiwezesha serikali ya awamu ya tano kufikia azma yake ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

  Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charlles Mwijage  wakati akifungua maonyesho ya nne ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga .

   Amesema Serikali  imeazimia kutumia rasilimali ya ardhi iliyopo ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi kupitia uzalishaji wa viwanda kwa kushirikisha wananchi katika fursa ya uwekezaji ambavyo itawawezesha kumiliki hisa badala ya kusubiri Ajira za mikataba .

   Awali akimkaribisha waziri Mwijage mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela amesema mkoa umejipanga ki mkakati katika kutumia fursa za miundombinu iliyopo ili kujiletea maendeleo ya kiuchumi.

   Maonyesho ya nne kimataifa ya biashara mkoa wa Tanga yanayofanyika kwa siku kumi yanashirikisha wajasiriamali na wafanyabishara wa ndani na nje ya nchi.

IRAN HAITAPELEKA RAIA WAKE KUHIJI MECCA

  Mecca Waziri wa utamaduni nchini Iran anasema kuwa nchi hiyo haitawatuma raia wake kwenda kuhiji mwaka huu nchini Saudi Arabia. Ali Jannati alisema kuwa sio vizuri kwa Saudi Arabia kuwawekea vizuizi raia wa Iran wanaotaka kuhiji.

    Wakati wa hija ya mwaka uliopita, mamia ya mahujaji waliuawa wengi wao raia wa Iran wakati wa kisa kibaya cha mkanyagano. Msukosuko kati ya Iran na Saudi Arabia umekuwa ukiongezeka wakati pande hizo mbili zinaunga mkono makundi tofauti yanayopigana nchini Syria na Yemen.

    Mamia ya watu waliuawa kwenye mkanyagano mwaka uliopita

BURUDANI GOOD NEWS KWA MUZIKI WA AFRIKA CHRIS BROWN KAMPOST WIZKID NA KUANDIKA HIVI..

    Najua jina la Chriss Brown sio geni masikioni mwa watu wanaopenda muziki, basi leo May 29 2016 huenda ikawa ni good news kwa muziki wa Afrika, baada ya msanii kutoka Marekani Chriss Brown kumpost msanii Wizkid kutoka Nigeria.

  Katika ukurasa wake wa Instagram Chriss Brown amempost Wizkid na kuandika maneno machache sana, lakini yanatafsirika kama kumualika mkali huyo wa Nigeria katika tour yake ya One Hell Of Nite Tour kwa mwaka 2016 atakayoifanya bara la Ulaya katika nchi za Uholanzi, Ujerumani na Denmark.

   Muda mchache baada ya Chriss Brown kupost picha ya Wizkid, staa huyo kutokea Nigeria alipost nae picha kama hiyo na kuthibitisha kuwa kuanzia June 5 hadi June 11 2016 atakuwa katika Tour pamoja na Chriss Brown.

SAMATTA AIPELEKA GENK EUROPA LEAGUE

   Samatta-ushindi Leo May 29, Mbwana Samatta ameandika historia mpya kwenye maisha yake baada ya kuisaidia timu yake ya Genk kushinda mchezo wa fainali ya play off na hatimaye kufu kucheza michuano ya Ulaya (Europa League).

   Samatta ambaye alianza kwenye kikosi cha kwanza cha Genk ameisaidia klabu yake kupata ushindi wa magoli 5-1 kwenye uwanja wao wa  nyumbani (Cristal Arena) dhidi ya Sporting Charleroi. Katika ushindi huo wa magoli 5-1,

  BSamatta amefunga goli moja ambalo lilikuwa ni goli la pili kwenye mchezo huo. Nikolaos Karelis ambaye amfunga hat-trick kwenye mchezo huo alianza kuifungia Genk goli la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 17 kisha Samatta akazamisha bao la pili dakika ya 27 kabla ya Sandy Walsh kupiga bao la tatu dakika ya 45 na kuipeleka Genk mapumziko ikiwa mbele kwa magoli 3-1.

ANYAMA AINYIMA USHINDI STARS

Stars vs Algeria 1 Mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kujipima nguvu kati ya timu ya taifa ya Tanzania dhidi ya Kenya ‘Harambee Stars umemalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

   Elias Maguli alianza kuipa Stars bao la kuongoza kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi nzuri iliyopigwa na Juma Abdul. Lakini baadaye Kenya walisawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penati iliyopigwa na Victor Wanyama anayecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Southampton inayoshiriki ligi kuu nchini England.

    Mechi hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya vikosi hivyo kujipima nguvu kabla ya mechi zao kuwania kushiriki fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2017. Stars itakuwa mwenyeji wa Misri June 4, kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

WAKUREGENZI WATAKIWA KUANZISHA MIRADI YA NG'OMBE

    Serikali ya Tanzania imetoa agizo kwa wakurugenzi nchini kuanzisha miradi ya ufugaji wa ng’ombe ili kuwasaidia wanafunzi kupata maziwa shuleni na kuwajengea tabia ya unywaji wa maziwa wakiwa bado wadogo.


    Agizo hilo limetolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe na Mkuu wa wilaya ya Ludewa, Anatory Choya, wakati akizindua wiki ya unywaji wa maziwa kitaifa ambayo inaadhimishwa mkoani Njombe kitaifa wakati kukiwa na asilimia 52 ya udumavu mkoani humo.

   kuwa serikali kama itataka kila shule kuwa na maziwa kama halmashauri hazita weza kifedha basi zianzishe miradi ya ufugaji wa ng’ombe mashuleni. Katika maadhimisho hayo Ofisa Mifugo Mkuu Wizara ya Kilimo,
   Mifugo na Uvuvi Abdallah Temba amesema selikali inasambaza madume Bora ya Ngombe ya Mbegu ili kuwasaidia wafugaji kupata Ng’ombe wa Mbegu kwa urahisi.

     Mbali na hayo, Zena Issa Ofisa Viwango wa Shirika la Viwango Nchini TBS na Debora Haule Afisa Masoko TBS wanasema wameshiriki maadhimisho hayo ili kutoa elimu kwa jamii ili kutumia bidhaa zilizo sindikwa na kuthibitishwa na shiriki la viwango nchini TBS.

Friday, May 27, 2016

JINO KUBWA LA NYANGUMI LAPATIKANA AUSTRALIA

  Jino kubwa la nyangumi limepatikana ufukweni Australia, na kuwa thibitisho la kwanza kwamba nyangumi wakubwa hatari sana waliishi mbali na Amerika.

    Mkusanyaji wa visukuku Murray Orr alipata jino hilo lenye urefu wa sentimeta 30 (inchi 12) ufukweni Beaumaris Bay karibu na mji wa Melbourne mwezi Februari. Alilikabidhi kwa makumbusho ya Victoria, ambayo yalianza kulionesha kwa umma Alhamisi. Inakadiriwa kwamba nyangumi mwenye jino hilo aliishi zaidi ya miaka milioni tano iliyopita.

    Alitoka kwa aina ya nyangumi ambao siku hizi hawapatikani duniani. Nyangumi hao wanaaminika kuwa watangulizi wa nyangumi wakubwa wa sasa wajulikanao kwa Kiingereza kama "sperm whales".

BENKI YA DUNIA IMEWEKA MSISITIZO WA HILI NCHINI TANZANIA

  Benki ya dunia imesisitiza nia yake ya kuendelea kuimarisha ofisi ya takwimu nchini NBS ili iwe na uwezo wa kuisaidia serikali kupunguza gharama za utafutaji na uhifadhi wa takwimu mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

   Nia ya Benki ya dunia ni kuijengea uwezo taasisi hiyo kukusanya takwimu ili kufikia maendeleo na kulingana na dira ya taifa ya mwaka 2025 ambapo itatoa dola milioni 2.

   Mkurugenzi mkazi wa benki ya dunia, kwa Tanzania,Burundi, Malawi na Somalia BELLA BIRD ametoa kauli hiyo alipofanya ziara kwenye ofisi kuu ya takwimu ya taifa ambapo amesema pamoja na benki hiyo kusaidia ofisi ya takwimu ya taifa, msaada huo ulenge kutoa hamasa ya uchapaji kazi itakayoisaidia nchi kufikia malengo ya kutokomeza umaskini kama dunia ilivyokubaliana ifikapo mwaka 2020.

 
   Mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu,Dk.ALIBINA CHUWA, kwa niaba ya serikali ameshukuru kwa msaada huo utakaowawezesha kuharakisha juhudi za ofisi hiyo za kutoa takwimu sahihi kwa ajili ya maendeleo ya taifa katika mradi wa uboreshaji na uimarishaji takwimu nchini, yaani TANZANIA STATISTICAL MASTER PLAN ambao awamu ya kwanza itakamilika mwezi juni mwaka 2018.

KENYA YASISITIZA KUZIFUNGA KAMBI ZA WAKIMBIZI

   Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa hatobadili uamuzi wake wa kuifunga kambu kuu ya Dadaab,makao ya zaidi ya raia 300,000 wa Somalia.

   Taarifa kutoka afisini mwake inasema kuwa amemuambia naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson kwamba hatua hiyo haitabadilishwa. ''Treni imeondoka kituoni .Kwa hivyo ni wale wanaotaka kuona ufanisi wa safari hiyo wangie ndani'',aliongezea.

    Makundi ya msaada na shirika la wakimbizi katika Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea wasiwasi wake kuhusu kufungwa huko. Bw Kenyatta amesema kuwa kufungwa kwa kambi hizo kutashughulikiwa kwa njia inayofaa.Matamshi yake yanajiri siku moja tu baada ya rais wa Somalia Kuonya kuusu kufungwa kwa kambi hiyo.

MADEREVA WA NWENDO KASI WAOMBA MIKATABA IWEKWE WAZI

   Mapema jana Madereva wa mabasi yaendayo haraka jijini dar es salaam walimwomba mwajiri wao kuweka wazi juu ya mikataba yao kutokana na jambo hilo kutotekelezwa kama walivyokusudia jambo ambalo linawatia wasiwasi.

   Wakizungumza na channel ten kwa masharti ya kutotajwa majina yao wala kupigwa picha wamesema tangu waanze kazi wamekuwa wakilipwa posho shilingi elfu 10 kwa siku na wakati mwingine hawapewi, huku suala la mishahara wakishindwa kulitambua kutokana na kutosainishwa mikataba ya ajira zao.

   Channel ten imemtafuta mwajiri wa madereva hao UDA-RT ambapo mkurugenzi mtendaji wake David Mgwassa ametolea ufafanuzi suala hilo kuwa hali hiyo imetokana na kutokamilika kwa baadhi ya masuala ikiwemo kufunguliwa kwa akaunti benki kuu na vibali ambavyo endapo vitapatikana zoezi la kusainishwa mikataba yao litafanyika mara moja.

WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA 'NIDA' WASHINIKIZWA UONGOZI KUWALIPA STAHIKI ZAO

   Waliokuwa wafanyakazi wa mkataba wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA ambao ajira zao zilisitishwa wamekusanyika katika ofisi za mamlaka hiyo Kinondoni jijini Dar es salaam kushinikiza uongozi kuwalipa stahiki zao ikiwemo

    mishahara ya miezi mitatu ambayo wanadai hawajalipwa pamoja na fidia ya usitishwaji wa mkataba Wakizungumza na Channel Ten iliyofika katika ofisi hizo wafanyakazi hao wameendeleza malalamiko yao dhidi ya mamlaka hiyo madai ya kufanya uamuzi ghafla wa kusitisha mikataba yao na kuutaka uongozi kuwalipa stahiki zao Aidha wameiomba serikali kuangalia upya na kuingilia kati usitishwaji wa mkataba huo uliofanywa na NIDA kutokana na waathirika wengi kuwa ni vijana.

    Channel Ten hata hivyo haikuweza kufanikiwa kuzungumza na uongozi wa NIDA ili kupata ufafanuzi kuhusu malalamiko hayo baada ya kuelezwa wahusika wapo kwenye kikao

WANANCHI WA KIBUNDUGULU RUNGWE WALAZIMIKA KUVUKA MTO KWA KAMBA

  Kukosekana kwa daraja katika mto Mbaka unaotenganicha kitongoji cha Kibundugulu na kijiji cha Mbaka wilayani Rungwe kumekuwa

    kukisababisha maafa ya mara kwa mara kwa wananchi ambao hulazimika kuvuka mto huo kwa kamba na wengine kupiga mbizi kwa ajili ya kufuata huduma muhimu za kijamii ng’ambo ya mto huo. Kero ya kukosekana kwa kivuko kwenye mto Mbaka

    imesababisha athari kubwa kwa wananchi wa kitongoji cha Kibunduguru, hali ambayo imemlazimu mbunge wa jimbo la Rungwe Sauli Henry Amon kutoa taarifa katika ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa ili serikali iweze kuchukua hatua za kuwasaidia wananchi hao.

     Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia maafa, Mheshimiwa Jenesta Joachim Mhagama amelazimika kutembelea eneo hilo na kutoa agizo kwa mwenyekiti wa kamati ya maafa mkoa wa Mbeya, kufanya tathimini ya athari za mto huo na kupeleka taarifa ofisini kwake ili serikali iwezi kuchukua hatua za haraka.

    Hata hivyo afisa mipango wa wilaya ya Rungwe, William Makufwe amesema kuwa tayari halmashauri yake imeanza kuchukua hatua za kujenga kivuko cha miguu kwenye mto huo, mradi ambao hata hivyo haujawahi kupata fedha za kuukamilisha.

WANAWAKE WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUBADILI FIKRA ZA MFUMO DUME

Waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe Angela Kairuki amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika kubadili fikra za mfumo dume na kujiendeleza kielimu kwani ndio njia pekee itakayofanikisha malengo yaliyowekwa na serikali ya kufikia uwiano wa asilimia 50 kwa 50 katika utendaji kazi kwa wanawake na wanaume kwenye sekta mbalimbali ifikapo mwaka 2030.

     Waziri Kairuki anatoa rai hiyo kwa wanawake katika uzinduzi wa katiba na mkutano mkuu wa chama cha makatibu mahususi Tanzania Tapsea ambapo amesema licha ya serikali na wadau wa maendeleo kupambana kuhakikisha mfumo dume

    unatokomezwa nchini jitihada hizo zitagonga mwamba endapo kundi hilo litashindwa kutambua umuhimu wao katika jamii kwa kujiendeleza hasa kielimu. Mhe Mary Nagu mbunge wa Hanang akizungumza katika mkutano huo amewataka wanawake kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali na kuvisajili ili viweze kufikiwa kwa urahisi na serikali huku mwenyekiti wa Tapsea Zuhura Maganga akieleza kuwa chama hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011 kimerejesha heshima na utu kwa makatibu mukhtasi ambao walikuwa wakidharaulika na kuonekana watu wa mwisho maofisini.

   Nao baadhi ya makatibu mahsusi wameelezea changamoto zinazowakabili katika utendaji wao huku wakisikitishwa na hatua ya baadhi ya wakubwa wao kuwataka au kuwadhalilisha kingono huku wakikosa mahala pa kusemea kwa hofu ya kukosa ajira.

SERIKALI VUNJENI BODI YA SUMATRA -MBUNGE MTOLEA

  Mbunge wa Temeke Jijini Dar es salaam Abdallah Mtolea (CUF) ameitaka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuivunja bodi ya SUMATRA kwa kutosimamia sheria inayotaka watanzania theluthi mbili kuajiriwa wakati meli zinapotia nanga bandarini.

    Mtolea amebainisha Bungeni kwamba watu wanaofanya kazi katika meli nyingi zinazoingia nchini siyo watanzania ambapo sheria inataka watanzania theluthi mbili waweze kuajiriwa meli zinapoingia nchini, hivyo kwa kuwa jukumu hilo ni la SUMATRA na imeshindwa kusimamia sheria hiyo bodi yake ivunjwe na kuwekwa watendaji watakaosimamia sheria ili watanzania waweze kunufaika na ajira.

    Aijibu swali hilo Naibu Wazirin wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani amesema kwamba ni kweli kuna malalamiko kutoka kwa mabaharia wengi pamoja na wafanyakazi wa meli juu ya ajira hizo ila sheria hiyo kuna namna inatafsiriwa vibaya.

     Naibu Waziri Ngonyani amesema kwamba serikali itapitia upya sheria hiyo ili iweze kutoa nafasi kwa pande zote mbili.