Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Boniface Mkwasa leo ametaja kikosi chenye majina ya wachezaji 26 kitakachoingia kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Kenya pamoja na ile ya kufuzu kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri.
Nahodha wa zamani wa Taifa stars, Nadir Cannavaro alitajwa kuichezea timu hiyo kuziba pengo la Kelvin Yondani ambaye anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano licha ya yeye kutangaza kujiuzulu.
Kikosi cha Taifa Stars kitaingia kambini tarehe 23 kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya utakaochezwa tarehe 29 Mei jijini Nairobi Baada ya hapo Taifa Stars itarejea Dar kukamilisha maandalizi ya kuivaa Misri katika mchezo ambao inahitaji ushindi wa angalau mabao matatu kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon mwakani. Kikosi kamili: Kikosi cha Stars: Walinda Milango: Deo Munish ( Yanga), Aishi Manula (Azam) na Benno Kakolanya ( Prisons). Walinzi: Juma Abdul, Haji Mwinyi,Nadir Haroub (Yanga ), Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris ( Azam), Mohamed Tshabalala (Simba) na Andrew Vicent ( Mtibwa Sugar). Viungo: Himid Mao, Farid Mussa ( Azam), Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya ( Mtibwa Sugar ),Hassan Kabunda ( Mwadui ), Juma Mahadhi (Coastal Union) na Ismail Issa Juma ( JKU) Washambuliaji: Elias Maguri ( Stand United), John Bocco ( Azam) Ibrahim Hajib ( Simba), Mbwana Samatta ( Genk GRC, Ubelgiji), na Thomas Ulimwengu ( TP Mazembe)
No comments:
Post a Comment