Klabu ya Azam FC imewapa mkataba wa miaka miwili makocha waapya wawili Zeben Hernandez na Jonas Garcia kutoka Hispania kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho ambacho kilikuwa na kocha Stewart Hall ambapo klabu hiyo imetangaza kuachana nae rasmi leo.
Zeben Hernandez atakuwa kocha mkuu wakati na Jonas Garcia yeye atakuwa kocha wa viungo huku Denis Kitambi akiendelea kuwepo kama kocha msaidizi na ndiye atakuwa mwenyeji wao nchini wakati watakapoanza majukumu yao mapya.
Ungozi wa Azam FC umekamilisha mazunguzo na makocha kutoka Hispania na umewapa mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu na kibarua chao cha kwanza itakuwa ni michuano inayokuja ya Kagame Cup, amesema ofisa habari wa klabu ya Azam FC.
Makocha hao watarejea kwao Hispania baada ya kushuhudia mchezo wa mwisho wa ligi kati ya Azam FC dhidi ya Mgambo JKT pamoja na ule wa FA Cup dhidi ya Yanga, baada ya hapo watarejea nchini kwa ajili ya kuanza majukumu yao kama makocha wapya wa Azam.
No comments:
Post a Comment