Wakazi wa kijiji cha Naberera kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji wamekamata zaidi ya Punda Kihongo miambili wanaodaiwa kuibwa kwenye maboma ya wananchi na kusafirishwa kwenda mkoani Dodoma huku sabini kati yao wakiwa kwenye gari aina ya Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T 983 ABK na hadi sasa watu sita wamekamatwa kwa tuhuma hizo wakiwemo Afisa mtendaji na Bwana mifugo wa kijiji hicho.
ITV ilifika katika kituo kidogo cha Polisi cha Naberera na kushuhudia baadhi ya Punda wakiwa kwenye gari aina ya Mitsubushi Fuso wanadaiwa kukamatwa usiku wakipelekwa mkoani Dodoma kunakodaiwa kuwepo soko la wanyama hao huku wananchi wakidai hivi sasa Punda wamekwisha kijiji hapo na hali ya usafirishaji imekuwa mbaya kwani ndiyo tegemeo pekee la kusafirisha mizigo maji na mazao ya biashara na chakula.
Uongozi wa Kitongoji cha Kidonge kilichoatharika zaidi na wizi huo amesema athari za wizi huo kwa wafugaji ni kubwa na jamii ya kifugaji inashangaa mnyama Punda kuwa kutumika kama chakula wakati kwa wafugaji ni usafiri wa kutegemewa.
Mwenyekiti wa kijiji cha Naberera Jacob Korosi amekiri kuwa baadhi ya viongozi wa kijiji wamekuwa wakihusika na wizi wa punda na hadi sasa zaidi ya punda elfu mbili na mia tano wameshaibwa na wamefikisha taarifa kwenye ngazi husika bila mafanikio.
No comments:
Post a Comment