Serikali ya mkoa wa Ruvuma imetuma boti tatu za Askari kwenda kutafuta miili ya marehemu ikiwa ni Siku moja baada ya serikali ya mkoa huo kubaini Watu kumi na moja wanahofiwa kufa maji baada ya boti walilokuwa wanasafiria kutoka Mbambaa-bey Wilaya ya Nyasa mkoani humo kwenda bandari ya Nkata-bay nchini Malawi kuzama na kufa maji.
Kwa mujibu wa kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bensony Mpesya amesema kuwa watu waliokuwa wanasafiri kwa boti hiyo ni watanzania ambao walioondoka katika bandari ya Mbamba-bey toka mei 21 mwaka huu ambapo walipaswa wameingia Nkata-bey mei 22,ambapo kilomita kumi na tano wakiwa wanakaribia kufika nchini Malawi walipata dhoruba ya mawimbi ambapo wakapiga simu kwa ndugu zao kuomba msaada baada ya boti lao kuingia maji.
Amefafanua kuwa kinachoashiria kuwa watu hao wamepoteza maisha ni kutopatikana kwa mawasiiano yao ya simu na kuonekana kwa baadhi ya mabaki ya bidhaa zilizokuwa zinasafirishwa na wafanyabiashara hao kwenye boti ikiwa ni pamoja na mafuta ya kula boksi mbili yaliyoonekana ufukweni mwa ziwa Nyasa upande wa Malawi.
Aidha Mpesya amesema jitihada za kutafuta miili ya watanzania hao inaendela baada ya kufanya mawasiliano na ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Malawi kuomba kibali cha kuruhusiwa kuanza kutafuta miili na boti iliyozama ambapo kati ya watu hao kumi na moja wamiliki wa boti walikuwa watano na wafanyabiashara walikuwa sita.
Naye mkuu wa wilaya ya nyasa Magreth Malenga amesema kuwa ndani ya boti kulikuwa na mizigo ya vitenge vilivyokuwa vinatoka Tanzania
No comments:
Post a Comment