FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA NYANYA....
Hili ni tunda mashuhuri na lenye virutubisho ambalo kwa kawaida hutumika kama mbogamboga.
Kwa wastani, watu hula takribani kilo 8 za nyanya kwa mwaka. Nyanya zina aina mbalimbali za viasili vya kurutubisha na visivyorutubisha vinavyohusiana na faida kadha wa kadha za kiafya.
Hii inajumuisha lycopene, vitamini C, A na K, potasiamu, na nyuzinyuzi. Nyanya moja yenye ukubwa wa wastani inaweza kutoa takribani nusu ya kiasi cha kila siku cha vitamini C anachohitajika kupata mtu.
Viasili mbalimbali vya nyanya vinasadikika kufanya kazi pamoja kuleta manufaa ya kiafya. Hii ni pamoja na kusaidia kujenga afya ya meno, afya ya mifupa, afya ya ngozi, afya ya nywele, kupunguza shinikizo la damu (PB) na kupunguza viwango vya lehemu pamoja na kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na saratani.
Baadhi ya vionjo vya nyanya kama vile lycopene hufyonzwa kwa wepesi mwilini pale nyanya zinapochemshwa, iwe kwa kuzipika au kuzichemsha. Sasa huenda tunazijua faida za kula lishe kamili ya kuleta afya ikiwa ni pamoja na kula matunda na mbogamboga.
Lakini wasichokijua watu wengi ni kwamba juisi ya mbogamboga ndiyo inayosaidia kudumisha urari (pH) muhimu wa haidrojeni ya mwili. pH ina maana ya nguvu ya haidrojeni katika mizani ya kupimia hali-asidi ya vitu mwilini. Ili mwili ufanye kazi vizuri na kuweza kuendelea kuishi, lazima uwe na vikemikali vinavyolipuka na vitu vya asidi ili kutengeneza chumvi na kutoa umajimaji wenye nguvu ya haidrojeni (ya baina ya 7 na 7.5) na uwe na kipimo cha haidrojeni chenye urari kamili kwa sababu saba:
1. Kuulinda mwili dhidi ya uharibifu utokanao na chembechembe za maradhi na kuukinga na uzee wa kabla ya wakati.
2. Kuusaidia mwili kudumisha viwango vya lehemu vyenye kuleta afya bora.
3. Kuweka msukumo wa damu katika kiwango bora cha afya.
4. Kuweka katika hali ya kawaida kikemikali cha kusawazisha sukari ya damu (insulin) na kuzuia ongezeko la uzito wa mwili linaloweza kuhatarisha afya.
5. Kuuwezesha moyo kufanya kazi vizuri.
6. Kuongeza uzalishaji wa nishati
7. Kudumisha mfumo wa kinga ya mwili, mfumo wa umeng’enyaji, kudumisha afya ya viungo vya mwili na mifupa
No comments:
Post a Comment