sukariKiwanda cha sukari cha manyara kimeendelea kuhifadhi tani 181 za sukari ambazo zimekutwa mapema mwezi huu kinyume na agizo la mkuu wa wilaya ambapo aliagiza uongozi wa kiwanda hicho kuweka sukari hiyo kwenye mifuko rasmi kwaajili ya kusambazwa kwa wananchi jambo ambalo halijafanyika.
Tani hizo za sukari zimeendelea kuhifadhiwa katika ghala la kiwanda hiki bila kusambazwa kwa wananchi kwa maelezokuwa sukari hii haijawa tayari kwa matumizi ya binadamu huku uongozi wa kiwanda hiki pia ukisema kuwa tani hizi za sukari zitaboreshwa kwaajili ya matumizi ya binadamu pindi kiwanda ktakapoanza uzalishaji kutokana na sasa kusimama kupisha matengenezo.
Aidha agizo la kuutaka uongozi wa kiwanda hiki kuanza uzalishaji mara moja badala ya kusubiri mwishoni mwa mwezi ujao ili kusaidia kuondoa tatizo la sukari linalowakabili wananchi kwa sasa.
Kwa sasa sukari imeendelea kuuzwa kwa bei tofautitofauti ambapo kwa huuzwa kwa bei ya chini kabisa kwa shilingi 3000 wakati baadhi ya maeneo inauzwa kwa shilingi 6000.
No comments:
Post a Comment