oil-and-gas-investments
Halmashauri nchini zimetakiwa kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji ili kuiwezesha serikali ya awamu ya tano kufikia azma yake ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charlles Mwijage wakati akifungua maonyesho ya nne ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga .
Amesema Serikali imeazimia kutumia rasilimali ya ardhi iliyopo ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi kupitia uzalishaji wa viwanda kwa kushirikisha wananchi katika fursa ya uwekezaji ambavyo itawawezesha kumiliki hisa badala ya kusubiri Ajira za mikataba .
Awali akimkaribisha waziri Mwijage mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela amesema mkoa umejipanga ki mkakati katika kutumia fursa za miundombinu iliyopo ili kujiletea maendeleo ya kiuchumi.
Maonyesho ya nne kimataifa ya biashara mkoa wa Tanga yanayofanyika kwa siku kumi yanashirikisha wajasiriamali na wafanyabishara wa ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment