Monday, June 13, 2016

BABATI HAJAKOMA TU

  Mkuu wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Crispin Meela.  Unaweza kusema hawajakoma. Hii ni baada ya kutolewa taarifa za ubadhirifu wa Sh1.4 bilioni kwenye Halmashauri ya Mji wa Babati katika mradi wa ujenzi wa barabara.

    Mkuu wa Wilaya ya Babati koani Manyara, Crispin Meela amesema hayo wakati akitoa taarifa ya uchunguzi wa  kamati aliyounda kuhusu matumizi ya fedha katika mradi wenye thamani ya Sh12 bilioni uliofadhiliwa na Benki ya Dunia.

   Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, Meela amesema katika mradi huo wa kilometa 10.2;  Benki ya Dunia imetoa Sh2 bilioni kwa ajili ya kuanza kwa mradi huo lakini zimetafunwa na wajanja wachache, hivyo kukwamisha mradi huo. Baada ya kupokea taarifa hiyo, Bendera ameikabidhi kwa vyombo vya dola, ambavyo ni polisi,

    Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na usalama wa Taifa kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kubaini ukweli na kuwachukulia hatua waliohusika.

No comments:

Post a Comment