Friday, June 10, 2016

MSIRI WA TRA KUTINGA IKULU

Moshi.  

  Msiri wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) aliyestahili kulipwa Sh210 milioni, baada ya kufichua ukwepaji wa kodi ya Sh7 bilioni ameamua suala hilo kulifikisha Rais Magufuli TRA imekuwa ikitangaza kuwa inatoa asilimia tatu ya thamani ya kodi iliyokwepwa kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa mhusika.

    Hata hivyo, imebainika kuwa kiwango cha juu cha asilimia tatu kinachotolewa hakitakiwi kuzidi Sh20 milioni, hata kama msiri atakuwa amefichua ukwepaji wa kodi ya mabilioni ya fedha.

   Akizungumza na gazeti hili jana, msiri huyo alisema ameamua kumwandikia Rais Magufuli baada ya jitihada za kufuatilia malipo yake kugonga mwamba.

No comments:

Post a Comment