Msanii mkongwe wa maigizo nchini Muhogo Mchungu amelalamikia watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa vijana kwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Muhogo Mchungu ameyasema hayo katika mahojiano na Enews na amewataka wazazi wajiunge na mitandao hiyo ya kijamii ili waweze kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao hiyo kwa kufuatilia matumizi ya watoto wao.
Muhogo alisema kuwa yeye hasapoti kabisa uchafu unaofanyika katika mitandao na hata katika maisha yake ya kawaida hayupo karibu na watu wenye tabia chafu katika jamii.
No comments:
Post a Comment