Jeshi la polisi mkoani Dodoma linawatafuta watu watatu wanaoshukiwa kuwa majambazi baada ya kutoroka na wengine wawili kuuwawa na wananchi katika kijiji cha Michese, Kata ya Mkonze kwenye Manispaa ya Dodoma.
Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari mjini Dodoma, kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Lazaro Mambosasa amesema majambazi hao walifanya tukio Juni 11, mwaka huu kwa kuvamia duka la mfanyabiashara Boniface Fidelis na kupora shilingi milioni tano.
Kamanda Mambosasa amefafanua kuwa majambazi hao walikuwa bastola mbili zilizotengenezwa kienyeji na moja ya iliyotengenezwa kiwandani, ambapo majambazi wawili walizingirwa na wananchi na kuchomwa moto na miili yao bado haijatambulika, na ipo kwenye chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa Dodoma.
VAmeongeza kuwa uchunguzi wa silaha zilizokamatwa utafanyika kitaalam, ili wahusika wote wa tukio hilo waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua, na akawaomba wananchi waendelee kutoa taarifa kwa jeshi hilo, katika kuwafichua wahalifu wanaoishi ndani ya jamii.
No comments:
Post a Comment