Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kupitia kamati yake ya mapato na kudhibiti biashara ya magendo imekamata zaidi ya tani tano za kahawa zenye thamani ya shilingi milioni 6 zikivushwa kimagendo nje ya nchi.
Biashara ya kahawa na maharage iliyokuwa ikifanyika katika njia zisizo rasmi na kuacha nchi ikikosa mapato yake, sasa huenda ikaanza kufuata utaratibu mara baada ya serikali katika wilaya ya Kyerwa,
kuunda timu ili kudhibiti hali hiyo iliyokuwa imeota mizizi, ambapo wafanyabiashara walio wengi ukwepa kupita katika mipaka rasmi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo INNOCENT MADUHU ambaye pia ni kaimu afisa mipango wa wilaya hiyo, amesema wananchi walioko mpakani wana mazoea ya kuuza kahawa na mazao mengine kwa wanunuzi wasio rasmi, ambao hutorosha bidhaa hizo nje ya nchi kupitia mto Kagera, unaotenganisha nchini ya Tanzania na Uganda.
Katika zoezi hilo mbali na kukamatwa kwa zaidi ya tani tano za kahawa, pia vitu mbalimbali ikiwemo pikipiki kumi, baiskeli na mitumbwi iliyokuwa ikisafirisha bidhaa hizo,pia vilikamatwa.
No comments:
Post a Comment