Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk Philip Mpango ametangaza hatua 10 za kupunguza na kudhibiti matumizi ya Serikali bila kuathiri ubora wa huduma zinazotolewa. Hatua hizo ni pamoja na:
Kuhakikisha mikutano yote ikiwa ni pamoja na mikutano ya bodi, mafunzo na semina inatumia kumbi za Serikali na Taasisi za Umma; Kutoa kipaumbele kwa Taasisi za Umma katika kutoa huduma kwa Serikali kama vile bima, usafirishaji wa barua, mizigo na vifurushi, matangazo na usafiri;
Kudhibiti matumizi ya umeme, simu na maji ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara; Kudhibiti ulipaji wa mishahara kwa watumishi ili kuepuka malipo yasiyostahili. Aidha, Serikali itaendelea kufanya sensa ya watumishi wote; Kudhibiti utoaji wa mikopo ya elimu ya juu ili kuepuka utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wasio stahili;
Kuendelea kufanya ununuzi wa magari kwa pamoja na bidhaa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji ili kupata unafuu wa bei; Kuendelea kudhibiti gharama za uendeshaji wa magari ikiwa ni pamoja na matengenezo, mafuta na vilainishi; Kupunguza na kuondoa matumizi yasiyo na tija katika maeneo
mbalimbali ikiwemo maadhimisho na sherehe za kitaifa, matamasha, machapisho na safari za ndani na nje ya nchi zisizo na tija; Kuhimiza matumizi ya nakala laini (soft copy) za machapisho mbalimbali hususan
yanayozidi kurasa 50 ili kupunguza gharama za uchapishaji na kutunza mazingira; na Kudhibiti matumizi ya Taasisi na Mashirika ya Umma yasiyowiana na majukumu yao ya msingi na yasiyo na tija.
No comments:
Post a Comment