Tuesday, June 7, 2016

KATA YA KIZARA HAINA MAWASILIANO YA SIMU

  Dodoma. Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani amekiri kuwa Kata ya Kizara katika Wilaya ya Korogwe haina mawasiliano ya simu.

   Ngonyani amesema kwa kulitambua hilo, Serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote ilikiingiza kijiji cha Majimoto kutoka Kata ya Kizara kutekeleza mradi wa mawasiliano vijijini wa awamu ya pili ‘B’.

   Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani (CCM) ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itapeleka mawasiliano ya simu kitika kata hiyo. Naibu Waziri amesema mradi huo unatekelezwa na kampuni ya simu ya MIC (Tigo) kwa ruzuku ya Dola 105,920 za Marekani na ulianza kutekelezwa Mei 23,2015.

    Amesema hadi sasa, MIC wamekwishafanya tathmini ya kiufundi ya eneo la kujenga mnara na mradi unategemea kukamilika ifikapo Juni 30.

No comments:

Post a Comment