Serikali ya Saudi Arabia imekabidhi tani 100 za tende kwa lengo kuwasaidia waislam wanaofunga katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani ikiwa ni utaratibu wa serikali hiyo ambao hutekelezwa katika nchi nyingi duniani.
Akizungumza wakati wa makabdhiano hayo kaimu balozi saudi Arabia nchini Tanzania Wajih Alotaibi amesema msaada huu umetolewa na mfalme Salman kupitia kituo chake cha misaada ya kibinadamu ambao ni njia moja ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
Msaada huo ambao umepokelewa na mkurugenzi wa idara ya mashariki na kati katika wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki balozi Abdalah Kiliwa kwa niaba ya serikali
amesema msaada huu ni miongoni mwa misaada mingi inayotolewa na nchi hiyo ambao si wa serikali pekee bali umewalenga zaidi wananchi kuwarahishia kupata futari.
No comments:
Post a Comment