Songwe. Polisi mkoani Songwe inawashikilia wahamiaji haramu 13 raia wa Ethiopia ambao wamekamatwa wakiwa katika harakati za kutaka kuvuka mpaka kwenda Afrika Kusini.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ambwene Mwanyasi amesema wahamiaji hao walikamatwa juzi saa 12 jioni eneo la Mlowo wilayani Mbozi. Mwanyasi alisema wahamiaji hao walikuwa wakisafirishwa katika gari aina ya Toyota Noah lililokuwa likiendeshwa na mkazi wa Tunduma wilayani Momba na baada ya kuhojiwa walidai walikuwa wakienda Afrika Kusini kutafuta ajira.
Ofisa Uhamiaji na Mwanasheria kutoka Ofisi ya Uhamiaji Kituo cha Tunduma, Mashaka Manyamabunini amesema wahamiaji hao wamekiri kuwa lengo lao lilikuwa ni kupita Tanzania, huku akiwataka wananchi kuacha biashara ya usafirishaji wa binadamu.
No comments:
Post a Comment