Msanii wa muziki na mtayarishaji, Dully Skyes amesema studio yake ya ‘Dhahabu Record’ anaibadilisha matumizi na kuwa academy ya kufundishia utayarishaji wa muziki.
Akizungumza na Bongo5 Jumanne hii, Dully amesema amefikia maamuzi hayo baada ya kuona kuna vijana wengi wanahitaji kujifunza maswala ya utayarishaji wa muziki.
“Studio ya Dhahabu Record naibadilisha matumizi, anaifanya kuwa academy ya utayarishaji wa muziki,” alisema Dully. Kwa sasa nipo kwenye mchakato wa kufanya hilo, na soon kila kitu kitakuwa wazi,” Muimbaji huyo wa wimbo ‘Tuachie’ aliyowashirikisha Yamoto Band, amesema studio yake ya 4.12 ndiyo studio ambao itakuwa inahusika na maswala ya kuandaa muziki.
No comments:
Post a Comment