Afisa Mtendaji wa Azam Rhys Torrington (kushoto) akikabidhiana hati ya makubaliano na Mratibu wa mashindano ya Sports Extra Ndondo Cup Shafii Dauda kwa ajili ya kuonesha mechi hizo.
Pembeni (Kulia) ni mwakilishi wa Azam Tv Charles Hilary na kushoto ni kutoka Clouds Media Alex Lwambano. KAMPUNI ya Azam Media imeingia makubaliano na kampuni ya Clouds Media kupitia kipindi cha Sports Extra Kuonyesha mechi za kombe la Dr Mwaka Sport Extra Ndondo Cup ambapo itakuwa ni endelevu kuanzia hatua ya 32 mpaka fainali na itakuwa ikionyesha moja kwa moja.
Hatua hiyo inakuwa ni baada ya kila mwaka kampuni ya Azam kuonyesha mechi nne za mwisho kuanzia hatua ya nusu fainali pamoja na mshindi wa tatu na fainali yenyewe. Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya Azam Mediai, Afisa Mtendaji Mkuu Ryhs Torrington amesema kuwa kupitia chaneli ya Azam HD watanzani wote wataona michuano hiyo ya Ndondo Cup na baadhi ya mechi nyingine zitakuwa zinaonekana Azam Two ambayo inaonekana Afrika Mashariki.
"Tumeingia mkataba na Clouds kupitia kipindi cha Sports Extra na huu utakuwa ni endelevu kwani tumeshawahi kuonyesha michuano hiyo na kwa mwaka huu tumeamua kuingia makubaliano haya kwanza kwa kuwapa vijana kuonyesha fursa zao kupitia mpira wa miguu,"amesema Torrington.
Naye Mratibu wa kipindi cha Sports Extra na Ndondo Cup, Shafii Dauda na kusema kuwa wamefurahi kuweza kupata fursa hiyo na watahakikisha wanaibua vipaji huku ukizingatia wameweka sheria ya timu shiriki kutumia wachezaji watano wa ligi kuu.
Huu ni mwaka wa tatu toka kuanza mashindano hayo na kuanzia Jumapili wataanza na mechi ya ufunguzi kati ya Faru Jeuri ambao na mabingwa na Temeke Market utakaochezwa uwanja w Bandari. "Tumewekeza kuibua vipaji na hatua hii tumedhamiria kuonyesha soka la ushindani hasa kwani tumeweka sheria kuwa timu inatakiwa kutumia wachezaji watano wa ligi kuu na wengine wote wawe vijana,"amesema Dauda.
No comments:
Post a Comment