Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango Dodoma. Serikali imezifungia kampuni 21 na wakurugenzi wake, kushiriki zabuni zinazohusu ununuzi wa umma kwa mwaka mmoja.
Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango alipokuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti kwa ajili ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/17. Alisema asilimia 90 ya kampuni zilizofungiwa ambazo ni 19, ilisababishwa na kutotimiza masharti ya mkataba katika utekelezaji wa miradi husika,
asilimia 10 iliyobaki ambazo ni kampuni mbili zilifungiwa kutokana na kuwasilisha nyaraka zisizo halali. “Serikali imefanikiwa kuokoa Sh16.61 bilioni kwa kununua magari 551, kwa kutumia utaratibu huu,” alisema.
No comments:
Post a Comment