Dar es Salaam. Awamu ya kwanza ya ugawaji wa mashine za bure za kielektroniki za kutolea risiti (EFD) umeanza jana jijini Dar es Salaam. Mashine hizo zinatarajiwa kuwafikia wafanyabiashara wadogo 5,703.
Taarifa hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata. Kamishna huyo alisema lengo la mchakato huo ni kutaka kuhakikisha wafanyabiashara wote wanashiriki kulipa kodi.
Awali, wakati akiingia madarakani Rais John Magufuli aliweka msisitizo wa kuhakikisha Serikali inakusanya mapato kikamilifu ili kuiwezesha nchi kujiendesha na kukidhi huduma mbalimbali za kijamii.
No comments:
Post a Comment