Thursday, June 2, 2016

WAFANYABIASHARA 2000 WAANDAMANA KUPINGA ONGEZEKO LA ADA YA UPANGISHAJI MAENEO KWA ZAIDI YA ASILIMIA 40

  Zaidi ya wafanyabiashara 2000 wa masoko tisa ya Halmashauri ya jiji la mwanza wamelalamikia ongezeko la asilimia zaidi ya 400 la ada ya zabuni ya upangishaji wa maeneo mbalimbali ya biashara na kushauri utekelezaji wa sheria hiyo ndogo ya mwaka 2008 isitishwe ili kutoa nafasi ya mashauriano baina ya halmashauri ya jiji la Mwanza na wadau wa biashara kufanyika.

   Wafanyabiashara hai wamebeba mabango yenye ujumbe wa kupinga upandishaji wa ada ya zabuni ya maduka,migahawa na meza kutoka shilingi 10,000 hadi 50,000 kwa migahawa na maduka na shilingi 20,000 hadi shilingi 100,000 kwa maduka, zabuni ambayo imefunguliwa kuanzia mei 10 mwaka huu na itafungwa Juni 7,badala ya Juni 2 ambayo ilikuwa ni tarehe ya mwisho.

    Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Adam Mgoyi anasema sheria hiyo ndogo ya ada na tozo ilipaswa kutekelezwa tangu mwaka 2008 kwa ajili ya kuendesha huduma stahiki za kijamii.

No comments:

Post a Comment