Mwanza. Wakulima wa pamba kutoka mikoa mbalimbali nchini wameiomba Serikali kuingilia kati sekta hiyo ili iwanufaishe.
Wakizungumza katika kikao cha wadau wa pamba kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Waziri wa Biashara na Viwanda, Charles Mwijage wamesema kumekuwa na ngonjera kwenye zao hilo jambo linalokatisha tamaa kuendelea na kilimo hicho.
Mkazi wa Kishapu Mkoa wa Shinyanga, Joshua Kalando amesema umefika wakati Serikali kutekeleza wajibu na katiba ya kilimo cha pamba. Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Pamba (Tacoga), Godfrey Masaga amesema kilimo kimeingiliwa na watu wasio waaminifu ambao huharibu zao hilo. Mwenyekiti wa Chama cha Wanunuzi wa Pamba (TCA), Mohamed Sharifu amesema lawama na hasara zote za wakulima ama mbegu kutoota au kuharibiwa kwa mizani ya kununulia, wanazipata wao.
No comments:
Post a Comment