TAKRIBANI kwa miaka mitatu, wanafunzi wa shule ya msingi Nyantole iliyopo kitongoji cha Nyantole kata ya Ziwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wamelazimika kusomea katika jengo la msikiti kutokana na kutokuwepo kwa vyumba vya madarasa.
Wanafunzi wa shule ya msingi Nyantole ambao wamesoma katika jengo la msikiti kwa sasa wameondokana na adha hiyo mara baada ya kukamilika kwa jengo la msikiti na hivyo jengo hilo kubaki kuwa chuo cha watoto wa kiilsamu wakisoma elimu ya dini huku wanafunzi hao wakilitumia majira ya asubuhi.
Licha ya kuondokana na adha ya kutoka nje kila ifikapo wakati wa ibada lakini pia wanakabiliwa na tatizo la upungufu wa matundu ya vyoo yaliyopo ni matundu mawili yakitumiwa na wanafunzi 184 pamoja na walimu wao jambo linasababisha wanafunzi wengine kujisaidia maporini.
Diwani wa kata hiyo Zuberi Maftaha amekiri kuwepo kwa changamoto hizo na kuiomba jamii kujitokeza kuchangia nguvu zao ili kufikia lengo la uhitaji wa madarasa matano yatakayokidhi mahitaji ya wanafunzi hao.
No comments:
Post a Comment